Yaani ni baada tu ya Lowasa kuja Chadema ndo ukagundua Richmond ni ya nani? seriously? Mbona tangu yuko CCM kwenye vikao vya kuvuana magamba Lowasa alikuwa anasema maazimio yote ya Richmond aliyatekeleza kwa kushirikiana na Rais wa wakati huo? Kwa nini haukumwamini wakati huo uje umwamini baada ya kuhamia Chadema?
By the way, kashfa ya Lowasa haikuwa richmond peke yake, amekuwa akituhumiwa kuwa na pesa zisizo na maelezo (Ref Mwl Nyerere); amekuwa akituhumiwa kuwa na uhusiano wa karibu na wapiga dili wa nchi hii (Rostam, Chenge etc); amekuwa akituhumiwa kuwa na mtandao unaosimamia upigaji dili na kuweka watu kwenye nafasi nyeti serikalini (ambao pia ndo ulimweka Kikwete); Je haya yote aliyatolea maelezo gani?