Mjue tapeli aliyekubuhu John Alex | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjue tapeli aliyekubuhu John Alex

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rwabugiri, Jan 6, 2009.

 1. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nimesimuliwa na jamaa yangu ambaye ni mmoja wa wahanga wa tapeli huyu!

  Huyu jamaa Jonh Alex ana vijiduka vitatu ambavyo hujifanya anauza vifaa vya ujenzi kutengeneza computer pamoja na mabati. maduka yako sehemu ya Kinondoni, Mbezi beach karibu na mateoclub opposite na njia ya kwenda St. marys, pamoja na bunju. Kaandika nembo nzuri kabisa Jonh Alex Enterprises. Anacho fanya ni kukusanya order ya vifaa hivyo na down payment baada ya hapo hulala mbele. Wanao lizwa sana sana ni hasa wale wanao taka mabati ya South africa (aka. mabati ya Ando') kwani huchukuliwa kwa order.

  Mshtuko mkubwa alo upata jamaa yangu baada ya kugundua kwamba jamaa anamzengua alipo enda polisi ni pale alipo kuta kila polisi akimfahamu fika huyo jamaa kwamba ni tapeli aliye kubuhu, ana kesi zaidi ya nne mahakamani, na alisha wahi kumtapeli hadi afande Tibaigana! kwahiyo jamaa yangu aliishia kuambiwa Pole na polisi kwamba ndo umeisha lizwa! na kwa maelezo yake ni kwamba pale polisi anafahamika kama vile ndo nyumbani kwake!

  Nikiwa nakupa onyo ndugu unaye soma hapa usije lizwa kama jamaa yangu, nabaki kushangaa hivi inawezekanaje jamaa tapeli anaye sumbua jamii polisi wote wanamjua lakini anaendelea kupeta mtaani na kuendelea sumbua jamii kwa kuwaibia vipesa vyao wanavyo vihangaikia na pengine kuwa wamevikopa?

  Hivi yawezekana Tanzania hii hii mtu anaweza amua tunisha kifua akaishi juu ya sheria akiendelea wanyanyasa raia wenzake ili hali vyombo vya usalama vikimjua fika?
   
  Last edited: Jan 7, 2009
 2. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rwabugiri, neno sahihi ni TAPELI na si TAPERI....Be blessed mkuu
   
 3. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ni rahisi kuleta taarifa hapa ya kusema bwana John Alex ni tapeli lakini ni vigumu kuleta uthibitisho pasi na shaka (beyond reasonable doubt) kwamba mtu huyu kweli ni tapeli.naogopa kuleta mambo ya kumchafua mtu na biashara yake kama hakuna uthibitisho wa kutosha wa haya madai. Naamini kama huyu mtu alifikia hatua ya kumtapeli kamanda wa polisi wa kanda malumu basi asingeachwa aendelee kufanya utapeli wake tena! kidogo hii hainiingii akilini.
   
 4. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Hiyo story aliyotoa Rwabugiri si ndio ushaidi wake kuhusu hicho anachokisema au ulitaka akuwekee video hapa inayoonyesha jamaa yake akitapeliwa?
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kinyamana ni hiari yako kutoamini mada hii,
  Lakini ukweli ni kwamba binafsi hata John simfahamu wala sina faida yoyote ya kumchafua hapa!, Nimeleta habari hii kwa nia njema ya kujuvyana kama kawaida yetu ili na nyie wenzangu msije ingizwa mjini kama jamaa yangu. Hata hivo wana bodi naamini wapo wengi wenye uwezo wa kufika maeneo ya polisi Kawe, tafadhali ulizieni stori hii huko kwani jamaa yangu kanihakikishia kwamba pale anajulikana kama vile ni nyumbani kwao, na wanajua habari yote ya utapeli wake!

  Na hata wanao weza fika maeneo ya Kinondoni na mbezi kwenye maduka yake ukiongea na majirani wema watakueleza ukweli wote juu ya tapeli huyu.

  Lakini pia kanipatia hadi namba yake (John) ya simu kama mna ihitaji naweza wawekeeni hapa ama ni PM nitakutumia ili kama waweza kuwa mpelelezi mzuri waweza ongea na kumuuliza habari zote hizi na hata kesi kibao alizo nazo mahakamani.

  tafadhali wanao weza fika maeneo hayo kupata data zaidi juu ya huyu jamaa zimwageni hapa ili tusaidiane kujua ukweli huu na kujihadhari naye. Lakini pia wanasheria saidieni ni kwa vipi mtu kama huyu aweza dhibitiwa ili asiendelee inyanyasa jamii.
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Kinyamana, hujalizwa weye.Nenda pale Kinondoni karibu na Biafra sehemu yoyote ukiona vigae vinauzwa, muulizie huyu jamaa na utampata.Ukitaka utibitisha muagize vifaa vyovyote vya kuezeka na utaupata uthibitisho unaouhitaji.
  Tumshukuru Mkuu Rwabugiri,John Alex ,ni tapeli wa siku nyingi sana mjini hapa.
   
 7. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Nafikiri kuna umuhimu wa kuanzisha kajigazeti/journal katako orodhesha makampuni, pamoja na wahusika wakuu, ambayo yanahusika katika biashara za kitapeli.

  Itasaidia wateja kupata fursa ya kupitia kigazeti hiki kabla ya kushiriki kwenye mkataba na makampuni yoyote - iwe ya ujenzi, uhandisi, ukandarasi, fundi umeme, n.k.

  Nafikiria kitu kama Better Bureau Business (bbb.com), ambapo watu mbalimbali watapata fursa ya kuripoti makampuni (na contact zao) ya kitapeli yaliyowahi kuwatapeli kwa namna fulani.
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Wakati wa kuripotiwa lazima kuwa na ushahidi wa kutosha ili kusiwe na uwezekano wa sabotafe btn businesses.
   
 9. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu Gwakisa asante kuwa shuhuda, nawasihi na wengine wenye data zake zileteni jamaa huyu anatisha, huyo jamaa yangu kanieleza kwamba pia anatembea na mguu wa kuku ambao anadhani anaumiliki kihalali kwani akikamatwa na polisi huwa anausalimisha kwanza! na anasema yuko smart muda wote na ukimuona huwezi amini, mbaya zaidi anadai eti hata mkewe anashiriki katika biashara hiyo chafu katika mojawapo ya viduka vyake, huyo mama hukaa na kupokea order na kuchukua hiyo down payment!

  Kuanzisha hicho kijarida ni jambo jema japo ndo hivo utata utakuja kwa kutaka udhibitisho wa kutosha wa jinsi gani ulitapeliwa, na kama ujuavyo hiyo yaweza leta uhasama pia katika jamii hasa ukizingatia kwamba vyombo vyetu vya dola ndo hivo vinamjua fika tapeli anaye tesa watu na vinabakia kumuhadithia ( kama simulizi kwamba alisha mliza na huyu na yule nayule kama hadithi) na kutoa pole kwa walio tapeliwa naye!
   
 10. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #10
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
   
 11. C

  Chief JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Unataka ushahidi? Kampe advance ya kununua mabati ya Ando halafu utuletee feedback hapa au kaulize polisi Kawe kama ulivyoambiwa.
   
 12. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Lakini kwa tahadhari tu ni kwamba sumu haionjwi
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Unaweza ipika kwenye nyama na kukaonjesha Kambwa ka-jirani.
  Shiiiii Shiiiiiii, jirani akijua, basi na wewe una hali mbaya.
   
Loading...