Allah's Slave
JF-Expert Member
- Mar 14, 2008
- 562
- 45
Bravo Michuzi,
My brother in blood, I grew up with the guy, ni mmoja wa vijana makini sana waliotulia niliowahi kuwaona katika maisha yangu wakichacharika na maisha, wakati sisi tukienda nje kutafuta meli, yeye ni mmoja wa wale waliobaki home "wakisotea meli za nyumbani", yeye ninamuweka kundi moja na Kuo, Bob Rich, Choggy, Chris Phaby, Shebby, Franco, Gibbson, Ray Abdu, Marcochella, Wandiba, Gerry Kotto, na wengineo.
Kwa kweli ni heshima kubwa kwangu kumuona kwamba kati ya wale tuliosota sana na waya mkali enzi za Mwalimu, na yeye ni mmoja wa wale walio-make it, ninamuona Michuzi akihangaika, hasa enzi zile za Disco Toto YMCA, chini ya DJ Kali Kali na Nigger Jay, I mean sijawahi kusikia Michuzi amemuibia mtu wala kuvunja sheria za jamhuri, huyu ni role model kwa vijana wengi wa kisasa wasioelewa namna ya ku-struggle, na ninakumbuka zamani jinsi sometimes tulivyokuwa tunakwama yaaani umepiga picha kwake hela za kulipia huna, mkulu Michuzi atacheka tu na kukwambia kazana lakini atakupa picha zako,
Bravo michuzi, na Mungu akubariki mkuu uendelee na uhangaikaji wa maishaa maana bado mwisho, sio siri kuwa mafanikio yako ni mwiba kwa wengine, maana maoni hapa juu yanajisema yenyewe, weka pamba mkuu, hapo juu ni clear kuwa hakuna anyejua ulikotoka kimaisha na hasa background yako, wanafikiri na wewe ni mtoto wa kibosile,
Mungu Akubariki Bro, A luta Continua!
Huyu bwana ni kibaraka wa wakubwa na kwa ujumla ni mtu mwenye kujipendekeza kwa waheshmiwa na vigogo. Alishapigwa mkwara kabla kuwa aangalie watu wanachochangia kwenye blog yake au wataanza kumnyima safari za nje, akafyata. Je safari za nje ni za maana zaidi kuliko maslahi ya taifa?
"Mwangalia pande zote za shilingi" -FD
lakini wanaomjua tangu enzi hizo za 'Robot na Breakdance' kina Mwamvita, Shalamar, Diga diga et al -Ushirika Club, YMCA, Rungwe Oceanic na 'mjini dar', jamaa ni mtu poa sana.
la kujiuliza ni kuwa yuko vipi sasa? Mnaomsifia kupita kiasi huenda mlimuona mara ya mwisho miaka kumi iliyopita. Jamani tunataka mtuambie sasa hivi yuko vipi sio alikuwa akawa hadithi za abunuasi, yaliyopita simbele tugange yajayo.
Inaonekana kweli michuzi enzi zake alikuwa mwema na mtafutaji au hata sasa hivi lakini la kujiuliza ni kuwa yuko vipi sasa?
Me370, hebu tupe upande wa pili wa michuzi, naona hapa anaelekea kupambwa tu..na misifa kibao...kama wamjua zaidi tafadhali tuambie..
ushi
Ni kushusha hadhi hapa JF kujadili akina Michuzi, eti nilicheza naye disco sijui wapi nikiwa na diga diga, Chris Phabby Bob Rich, Choggy, Chris Phaby, Shebby, Franco, Gibbson, Ray Abdu Michuzi ni 'Robot na Breakdance' kina Mwamvita, Shalamar, nilikuwa naye miaka hiyo -Ushirika Club, YMCA, Rungwe Oceanic na 'mjini dar', jamaa ni mtu poa sana.
...ujinga huu tujadili mambo ya maana!!! Tumwache na blog yake.....tujadili mambo ya taifa letu jamani...wengine hapa nilikuwa naheshimu sana michango yao...lakini hili mmmmhhh laninitia shaka...huu ni mtazamo wangu, si lazima niwe sahihi...
nafikiri hizi quotes zako mbili hapo juu zinajisema wazi, nini nia yako kwa Michuzi, maana inaonekana wazi kwa watu kama mimi tunaoweza ku-read between the lines,
Otherwise, nilikuwa ninakuheshimu sana mkuu, mpaka nilipoona hizo quotes zako mbili hapo juu,
By the way, have a nice day bro!