Picha inazungumza maneno elfu moja

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,263
Picha hiyo hapo chini kaiweka Emmanuel "Jenkins" Muganda.

Nimemwandikia maneno haya:
Jenkins,

Hapo mna historia ya uhuru wa Tanganyika ya kuandikwa kwa wino wa dhahabu.

Kwanza Chief Edward Makwaia na Daisy Sykes.

Ni 1950s nyumbani kwa kina Daisy Chief David Kidaha Makwaia kila alipokuja Dar es Salaam kuhudhuria kikao cha LEGCO Abdul Sykes atamwalika nyumbani kwake kwa chakula cha jioni.

Nyumba hii ilikuwa Mtaa wa Stanley na Sikukuu na ndipo alipozaliwa Daisy na ndipo alipowajua viongozi wengi wa harakati za kudai uhuru pamoja na Mwalimu Nyerere baba wa taifa letu

Mama Daisy ananihadithia niko nyumbani kwake Ali Hassan Mwinyi Road.
Hivi niandikapo ni kama vile namuona.

Anasema Abdul Sykes na Chief Kidaha mazungumzo yao yalikuwa kila wakikutana ni hali ya baadae ya Tanganyika kama nchi huru.

Abdul Sykes akimtaka sana Chief Kidaha achukue uongozi wa TAA waunde chama cha TANU wadai uhuru wa Tanganyika.

Kwa nini Abdul alimtaka sana Chief Kidaha?

Jibu lipo katika moja ya Nyaraka za Sykes nilizosoma.

Dr. Wilbard Mwanjisi ameandika makala aliyotaka ichapwe kwenye gazeti la Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) na anaeleza mchango mkubwa wa Chief Kidaha ndani ya LEGCO anapochangia masuala ya Waafrika.

Abdul Sykes kapanda meli Mwanza anatokea Dar es Salaam anakwenda Nansio Ukerewe kuzungumza na Hamza Mwapachu kuhusu hali ya ofisi ya TAA HQ New Street, Rais wa TAA Vedasto Kyaruzi hayuko kapewa uhamisho na serikali Abdul Secretary kapwelewa ofisi haina mtu kwa kuwa na yeye Hamza Mwapachu pia kaondolewa Dar-es-Salaam yuko kisiwani.

Hii ilikuwa team ya TAA Political Subcommittee iliyokuwa inapanga mikakati ya kuunda TANU na kudai uhuru.

Wafanye nini mambo yaende?

Ndani ya meli ile Chief Michael Lukumbuzya yumo anatoka Makerere anarudi likizo nyumbani.

Hamza Mwapachu kawaleta wananchi bandarini kumpokea Secretary na Act. President wa TAA Abdul Sykes.

Ngoma zinapigwa bandarini wakati meli inafunga gati wananchi wamekuja kumlaki Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy.

Chief Lukumbuzya ameshangaa huyu anaepokewa hivi kwa magoma na shangwe ni nani?

Amesema John Iliffe historia nyingi ya TANU iko mikononi mwa watu binafsi.

Jenkins,

Hiyo picha yenu ni maktaba tosha ya historia ya uhuru wa Tanganyika.
Screenshot_20230924-174822.jpg
 
mazungumzo yao yalikuwa kila wakikutana ni hali ya baadae ya Tanganyika kama nchi huru.
Kwa muktadha huo, Je, Tanganyika ni Nchi huru?

Zanzibar Je?

Ni vizuri kuona Picha za wakongwe. Itapendeza zaidi wakiwa wanatokeza kuelimisha Vijana na kukemea upotoshaji wa Historia ya Tanganyika Nchini.
.
 
Picha hiyo hapo chini kaiweka Emmanuel "Jenkins" Muganda.

Nimemwandikia maneno haya:

Jenkins,

Hapo mna historia ya uhuru wa Tanganyika ya kuandikwa kwa wino wa dhahabu.

Kwanza Chief Edward Makwaia na Daisy Sykes.

Ni 1950s nyumbani kwa kina Daisy Chief David Kidaha Makwaia kila alipokuja Dar es Salaam kuhudhuria kikao cha LEGCO Abdul Sykes atamwalika nyumbani kwake kwa chakula cha jioni.

Nyumba hii ilikuwa Mtaa wa Stanley na Sikukuu na ndipo alipozaliwa Daisy na ndipo alipowajua viongozi wengi wa harakati za kudai uhuru pamoja na Mwalimu Nyerere baba wa taifa letu

Mama Daisy ananihadithia niko nyumbani kwake Ali Hassan Mwinyi Road.

Hivi niandikapo ni kama vile namuona.

Anasema Abdul Sykes na Chief Kidaha mazungumzo yao yalikuwa kila wakikutana ni hali ya baadae ya Tanganyika kama nchi huru.

Abdul Sykes akimtaka sana Chief Kidaha achukue uongozi wa TAA waunde chama cha TANU wadai uhuru wa Tanganyika.

Kwa nini Abdul alimtaka sana Chief Kidaha?

Jibu lipo katika moja ya Nyaraka za Sykes nilizosoma.

Dr. Wilbard Mwanjisi ameandika makala aliyotaka ichapwe kwenye gazeti la Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) na anaeleza mchango mkubwa wa Chief Kidaha ndani ya LEGCO anapochangia masuala ya Waafrika.

Abdul Sykes kapanda meli Mwanza anatokea Dar es Salaam anakwenda Nansio Ukerewe kuzungumza na Hamza Mwapachu kuhusu hali ya ofisi ya TAA HQ New Street, Rais wa TAA Vedasto Kyaruzi hayuko kapewa uhamisho na serikali Abdul Secretary kapwelewa ofisi haina mtu kwa kuwa na yeye Hamza Mwapachu pia kaondolewa Dar-es-Salaam yuko kisiwani.

Hii ilikuwa team ya TAA Political Subcommittee iliyokuwa inapanga mikakati ya kuunda TANU na kudai uhuru.

Wafanye nini mambo yaende?

Ndani ya meli ile Chief Michael Lukumbuzya yumo anatoka Makerere anarudi likizo nyumbani.

Hamza Mwapachu kawaleta wananchi bandarini kumpokea Secretary na Act. President wa TAA Abdul Sykes.

Ngoma zinapigwa bandarini wakati meli inafunga gati wananchi wamekuja kumlaki Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy.

Chief Lukumbuzya ameshangaa huyu anaepokewa hivi kwa magoma na shangwe ni nani?

Amesema John Iliffe historia nyingi ya TANU iko mikononi mwa watu binafsi.

Jenkins,

Hiyo picha yenu ni maktaba tosha ya historia ya uhuru wa Tanganyika.View attachment 2760933
Hiyo picha mmeificha wapi?
 
Picha hewa, haifunguki
Livan,
Ungesema tu picha haionekani tafadhali irushe tena ingependeza.

JamiiForums118371170.jpg

Picha hii ina kumbukumbuku muhimu katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mwanamke pekee katika picha hiyo ni Aisha ''Daisy'' Sykes na pembeni yake ni Chief Edward Jonathan Makwaia mtoto wa Chief David Kidaha Makwaia ambae Abdul Sykes Sykes alimtaka sana ajiunge na TAA waunde TANU.

1700796554559.png

Kulia waliosimama ni Chief Edward Anthony Makwaia na kushoto ni Kleist Sykes.
 
Livan,
Ungesema tu picha haionekani tafadhali irushe tena ingependeza.

View attachment 2822819

Picha hii ina kumbukumbuku muhimu katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mwanamke pekee katika picha hiyo ni Aisha ''Daisy'' Sykes na pembeni yake ni Chief Edward Jonathan Makwaia mtoto wa Chief David Kidaha Makwaia ambae Abdul Sykes Sykes alimtaka sana ajiunge na TAA waunde TANU.

View attachment 2822829
Kulia waliosimama ni Chief Edward Anthony Makwaia na kushoto ni Kleist Sykes.

Asante Mzee wangu, Sorry kwa utata wa lugha nilotumia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom