Mjue Issa Michuzi

Status
Not open for further replies.

Allah's Slave

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
562
45
Sikiliza Mahojiano baina ya Michuzi na radio butiama. Michuzi anaeleza aliingiaje kwenye Uandishi wa habari na lini. Pia anasema kabla ya kuwa mpiga picha alikuwa nani.
Historia ya blog yake na nani na nini kilichomfanya aanzishe blog.

Click Here
 
MUHIDIN ISSA MICHUZI NINAYEMFAHAMU MIMI SIKU ZA NYUMA ALIKUWA AKIKAA MAGOMENI MTAA WA IDRISSA(?)....PIA WAKATI ULE KWENYE ITV KULIKUWA NA KIPINDI CHA KITIMOTO KILICHOKUWA KIKIENDESHWA NA RAFIKI YAKE PASCAL MAYALA....(ambaya naye toka siku nyingi huwa anaendesha racing motocycle bila helmet....stimes kukiwa na wasichana warembo tofauti)).........!
MORE ABOUT MICHUZI.....?
 
Huyu bwana ni kibaraka wa wakubwa na kwa ujumla ni mtu mwenye kujipendekeza kwa waheshmiwa na vigogo. Alishapigwa mkwara kabla kuwa aangalie watu wanachochangia kwenye blog yake au wataanza kumnyima safari za nje, akafyata.

Je safari za nje ni za maana zaidi kuliko maslahi ya taifa?
 
Mie Issa Michuzi ninayemfahamu ni yule tarehe mosi aprili ya mwaka 2008 (siku ya wapumbavu) aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Tegeta iliyopo Wilayani Ilala.
 
Nilishawahi kusikiliza hayo mahojiano yake. Michuzi ni mtupu, mwandishi mdosho.

Kwanza, hajui nini cha kusema au kutosema hadharani. ‘Niko dedicated kwenye Blog yangu kuliko kazi yangu Daily News.’ Kwa kauli hii, angekuwa nchi zenye uwajibikaji, bosi wake angemfukuza kazi. Huyu ni Mhariri Mkuu wa Daily News anasema hivi!

Pili, hajui Kiswahili hata kidogo. ‘Bahati mbaya ama nzuri nilikuwa na Mwalimu mmoja alinifundisha kupiga picha.’ Sasa, kwa nini bahati mbaya? Alipoulizwa aliingiaje kwenye ku-blog: “Namsifu au namlaumu ndugu Ndesanjo kwa kunitia moyo, kunisaidia kuingia kwenye ku-blog.’ Sasa kwa nini umlaumu? Pia, kasema ‘Daily News ina autononomy, sijui nisemeje Kiswahili.’ Kumbuka, huyu ni mwandishi wa habari, tena aliyeishi Magomeni, hawezi kujifanya anashindwa kutafsiri au kuelezea neno ‘mamlaka’ au ‘kujitegemea.’

Mwisho lakini sio mwisho kabisa, haelewi nini kinaendelea kisiasa. Alipoulizwa kuhusu ubora wa Kikwete, akaanza kummiminia sifa kama: ‘Kikwete ana mvuto, ni handsome boy.’ Lakini, Kikwete alisifika kwa ujana, sio uzuri wa sura. Na pia, mtu mzima hawezi kuwa ‘handsome boy’ kwa sababu sio boy. Labda angesema ana ‘baby face.’ Angekuwa hajajifanya hajui kujieleza kwa Kiswahili nisingemkosoa kwa sababu sio lugha yake. Akizidi kumsifu Handsome boy Kikwete, kasema huwezi kumshinda kwa wanawake. Tatizo la huyu Handsome boy ni kwamba anadhani matatizo ya nchi ni ‘Mungu kapanga.’

Mwisho kabisa, hata kwenye fani yake hiyo hiyo ya upiga picha anachemsha. Blog yake ina picha ambazo zinaorodhesha majina ya walioko kwenye picha bila kusema ni mtu ni wa kushoto au kulia.

Michuzi na Kikwete wote mdosho.
 
Bravo Michuzi,

My brother in blood, I grew up with the guy, ni mmoja wa vijana makini sana waliotulia niliowahi kuwaona katika maisha yangu wakichacharika na maisha, wakati sisi tukienda nje kutafuta meli, yeye ni mmoja wa wale waliobaki home "wakisotea meli za nyumbani", yeye ninamuweka kundi moja na Kuo, Bob Rich, Choggy, Chris Phaby, Shebby, Franco, Gibbson, Ray Abdu, Marcochella, Wandiba, Gerry Kotto, na wengineo.

Kwa kweli ni heshima kubwa kwangu kumuona kwamba kati ya wale tuliosota sana na waya mkali enzi za Mwalimu, na yeye ni mmoja wa wale walio-make it, ninamuona Michuzi akihangaika, hasa enzi zile za Disco Toto YMCA, chini ya DJ Kali Kali na Nigger Jay, I mean sijawahi kusikia Michuzi amemuibia mtu wala kuvunja sheria za jamhuri, huyu ni role model kwa vijana wengi wa kisasa wasioelewa namna ya ku-struggle, na ninakumbuka zamani jinsi sometimes tulivyokuwa tunakwama yaaani umepiga picha kwake hela za kulipia huna, mkulu Michuzi atacheka tu na kukwambia kazana lakini atakupa picha zako,

Bravo michuzi, na Mungu akubariki mkuu uendelee na uhangaikaji wa maishaa maana bado mwisho, sio siri kuwa mafanikio yako ni mwiba kwa wengine, maana maoni hapa juu yanajisema yenyewe, weka pamba mkuu, hapo juu ni clear kuwa hakuna anyejua ulikotoka kimaisha na hasa background yako, wanafikiri na wewe ni mtoto wa kibosile,

Mungu Akubariki Bro, A luta Continua!
 
FM,
BRAVO!
Katika angle hiyo uliyo plot Michuzi hakuna shaka Mtu mzima NI BONGE la role MODAL vijana tunastahilikuiga tena,Ningependa kutoa ushauri kwa Michuzi kufanya japo kamkutano Kila mkoa kuwaambia vijana jinsi ya KU-struggle katika hari hii ngumu ya maisha haya pia asisahau kuwapa ukweli kwamba "when it comes a time to wrench feet"unaramba kweli ili yako yafanikiwe.

Mimi nilikua nikimwona Michuzi akitoka kwenye Hari ngumu yani Completely poverty mpaka akio girl friend wa rafiki yake (mcheza mpira) kama mke wake wa kwanza (LATE IT BE NOTED THAT,HAYA NI MAMBO YAKE BINAFSI,ILA I COULDnt HELP TO PUT IT HERE!
i am really sorry MTU MZIMA)
mpaka sasa Mtu Mzima ni kamillionea furani mwenye UJIKO MWINGI hapa bongo.

Nakufagiria sana,ila kama vp ni PM ili nikupe ushauri wakizushi kimjini mjini si unajua!?
 
Huyu bwana ni kibaraka wa wakubwa na kwa ujumla ni mtu mwenye kujipendekeza kwa waheshmiwa na vigogo. Alishapigwa mkwara kabla kuwa aangalie watu wanachochangia kwenye blog yake au wataanza kumnyima safari za nje, akafyata. Je safari za nje ni za maana zaidi kuliko maslahi ya taifa?

Me370, hebu tupe upande wa pili wa michuzi, naona hapa anaelekea kupambwa tu..na misifa kibao...kama wamjua zaidi tafadhali tuambie..

ushi
 
Michuzi ni mtafutaji, sio mwanasiasa, sasa kuna tofauti kati ya hizo shughuli mbili, huyu sio mbunge wala mjumbe wa NEC, ni simply mtafutaji, na baharia wa nchi kavu, unaweza kumrushia anything you want lakini tunaomjua vizuri tupo, na kama kawaida yetu tutamsimamia,

Mimi ninamuombea tena watokee wabongo zaidi wenye jitihada kama zake, huyu sio PHD, wala Masters, kama nyinyi, just leave the man alone!

Mkulu Michuzi, Bravo and keep it up!
 
...jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, duh! watu bwana, wamejaa roho ya "korosho"!

kama historia ndio inayomhukumu mtu, basi kuna wakati miaka ile 'wakubwa' walikuwa wanaikimbia hiyo kamera ya michuzi! tatizo wanaomhukumu michuzi humu 'bila haki' ni wale walomjua issamichuzi via his blog!,

lakini wanaomjua tangu enzi hizo za 'Robot na Breakdance' kina Mwamvita, Shalamar, Diga diga et al -Ushirika Club, YMCA, Rungwe Oceanic na 'mjini dar', jamaa ni mtu poa sana.

"Mwangalia pande zote za shilingi" -FD
 
lakini wanaomjua tangu enzi hizo za 'Robot na Breakdance' kina Mwamvita, Shalamar, Diga diga et al -Ushirika Club, YMCA, Rungwe Oceanic na 'mjini dar', jamaa ni mtu poa sana.

Sasa sisi tuliobugi Pango Disco kwa muziki wa Sunburst tutaseme nini!

Jamaa anastahili pongezi kwa vyovyote vile.
 
Inaonekana kweli michuzi enzi zake alikuwa mwema na mtafutaji au hata sasa hivi lakini la kujiuliza ni kuwa yuko vipi sasa? Mnaomsifia kupita kiasi huenda mlimuona mara ya mwisho miaka kumi iliyopita. Jamani tunataka mtuambie sasa hivi yuko vipi sio alikuwa akawa hadithi za abunuasi, yaliyopita simbele tugange yajayo.
 
la kujiuliza ni kuwa yuko vipi sasa? Mnaomsifia kupita kiasi huenda mlimuona mara ya mwisho miaka kumi iliyopita. Jamani tunataka mtuambie sasa hivi yuko vipi sio alikuwa akawa hadithi za abunuasi, yaliyopita simbele tugange yajayo.

Mkuu heshima mbele, sasa basi ianonekana kuwa wewe unamjua vizuri alivyo sasa, kuliko sisi wengine kwa maneno yako mwenyewe hapo juu, sasa vipi ukituwekea? Hatuwezi kuganga ya yajayo iwepo hatujui ya sasa kama ni mazuri au ni mabaya, weka dataz hapa mkuu tuone jinsi Michuzi alivyoiba hela kule BOT, au EPA, au labda aliwapiga picha sana kule Richimonduli wakamkatia, au na yeye alikuwa Butiama, kula nchi?

Mkulu Michuzi, hawa ndio walitaka ukale polisi hawa, wakati wao wanakula majumbani mwao duh! yaaani sisi Afrikans sina hamu, ukipata kidogo tu basi noma!
 
Inaonekana kweli michuzi enzi zake alikuwa mwema na mtafutaji au hata sasa hivi lakini la kujiuliza ni kuwa yuko vipi sasa?

Michuzi bado mwema na mtafutaji mpaka leo. Jamaa hii ni personality yake. Mimi nimekuwa nasikia tu jina la Michuzi bila ya kumfahamu. Nimekutana naye kwa mara ya kwanza mwezi wa kwanza nilipokuwa nyumbani. Kutokana na blog yake kuwa maarufu, nilipata hamu ya kumwona huyu jamaa kwa karibu (well ukweli ni kwamba kuna favor nilikuwa nataka anisaidie). Basi nilipofika nyumbani nikamtafuta. Tukapanga tukutane pale opposite na ilipokuwa Motel Agip kwenye mgahawa mmoja wanauza ugali na samaki bomba sana. Kwa jinsi tulivyobadilishana mazungumzo siku ile niliamini kuwa jamaa ni mtu mzuri sana. Michuzi ni mcheshi sana. Na ukimsikiliza kwa makini utagundua ustaharabu na hekima aliyokuwa nayo.

Kuna rafiki yangu mmoja nilishawahi kumwambia, kama michuzi angekuwa marekani basi angekuwa mtu wa kucheza na red carpet kwa sana. Jamaa ni celebrity type...at the wrong side of the World.
 
Nilishawahi kusikiliza hayo mahojiano yake. Michuzi ni mtupu, mwandishi mdosho.

Kwanza, hajui nini cha kusema au kutosema hadharani. ‘Niko dedicated kwenye Blog yangu kuliko kazi yangu Daily News.’ Kwa kauli hii, angekuwa nchi zenye uwajibikaji, bosi wake angemfukuzilia mbali. Huyu ni Mhariri Mkuu wa Daily News anasema hivi!

Pili, hajui Kiswahili hata kidogo. ‘Bahati mbaya ama nzuri nilikuwa na Mwalimu mmoja alinifundisha kupiga picha.’ Sasa, kwa nini bahati mbaya? Alipoulizwa aliingiaje kwenye ku-blog: “Namsifu au namlaumu ndugu Ndesanjo kwa kunitia moyo, kunisaidia kuingia kwenye ku-blog.’ Sasa kwa nini umlaumu? Pia, kasema ‘Daily News ina autononomy, sijui nisemeje Kiswahili.’ Kumbuka, huyu ni mwandishi wa habari, tena aliyeishi Magomeni, hawezi kujifanya anashindwa kutafsiri au kuelezea neno ‘mamlaka’ au ‘kujitegemea.’

Mwisho lakini sio mwisho kabisa, haelewi nini kinaendelea kisiasa. Alipoulizwa kuhusu ubora wa Kikwete, akaanza kummiminia sifa kama: ‘Kikwete ana mvuto, ni handsome boy.’ Lakini, Kikwete alisifika kwa ujana, sio uzuri wa sura. Na pia, mtu mzima hawezi kuwa ‘handsome boy’ kwa sababu sio boy. Labda angesema ana ‘baby face.’ Angekuwa hajajifanya hajui kujieleza kwa Kiswahili nisingemkosoa kwa sababu sio lugha yake. Akizidi kumsifu Handsome boy Kikwete, kasema huwezi kumshinda kwa wanawake. Tatizo la huyu Handsome boy ni kwamba anadhani matatizo ya nchi ni ‘Mungu kapanga.’

Mwisho kabisa, hata kwenye fani yake hiyo hiyo ya upiga picha anachemsha. Blog yake ina picha ambazo zinaorodhesha majina ya walioko kwenye picha bila kusema ni mtu ni wa kushoto au kulia.

Michuzi na Kikwete wote mdosho.
 
Ni kushusha hadhi hapa JF kujadili akina Michuzi, eti nilicheza naye disco sijui wapi nikiwa na diga diga, Chris Phabby Bob Rich, Choggy, Chris Phaby, Shebby, Franco, Gibbson, Ray Abdu Michuzi ni 'Robot na Breakdance' kina Mwamvita, Shalamar, nilikuwa naye miaka hiyo -Ushirika Club, YMCA, Rungwe Oceanic na 'mjini dar', jamaa ni mtu poa sana.
...ujinga huu tujadili mambo ya maana!!! Tumwache na blog yake.....tujadili mambo ya taifa letu jamani...wengine hapa nilikuwa naheshimu sana michango yao...lakini hili mmmmhhh laninitia shaka...huu ni mtazamo wangu, si lazima niwe sahihi...
 
Me370, hebu tupe upande wa pili wa michuzi, naona hapa anaelekea kupambwa tu..na misifa kibao...kama wamjua zaidi tafadhali tuambie..

ushi

Ni kushusha hadhi hapa JF kujadili akina Michuzi, eti nilicheza naye disco sijui wapi nikiwa na diga diga, Chris Phabby Bob Rich, Choggy, Chris Phaby, Shebby, Franco, Gibbson, Ray Abdu Michuzi ni 'Robot na Breakdance' kina Mwamvita, Shalamar, nilikuwa naye miaka hiyo -Ushirika Club, YMCA, Rungwe Oceanic na 'mjini dar', jamaa ni mtu poa sana.
...ujinga huu tujadili mambo ya maana!!! Tumwache na blog yake.....tujadili mambo ya taifa letu jamani...wengine hapa nilikuwa naheshimu sana michango yao...lakini hili mmmmhhh laninitia shaka...huu ni mtazamo wangu, si lazima niwe sahihi...

Mkuu wangu,

Uzuri na ubaya wa bina-adam, against bina-adam wenziwe, huonyeshwa kwanza kwa maneno, halafu baadaye kwa vitendo,

nafikiri hizi quotes zako mbili hapo juu zinajisema wazi, nini nia yako kwa Michuzi, maana inaonekana wazi kwa watu kama mimi tunaoweza ku-read between the lines,

However:-

1. Hiii ni section ya matangazo madogo madogo, kwa hiyo kujadili anything hapa ni fair deal, hata iwe Michuzi.

2. Ninarudia tena na tena, kuwa mwenye ushahidi wa Michuzi kuhusika na EPA, BOT, IPTL, NSSSF, Kutuletea mikataba ya BUZWAGI, aziweke hizo dataz hapa tuzichambue.

Otherwise, nilikuwa ninakuheshimu sana mkuu, mpaka nilipoona hizo quotes zako mbili hapo juu,

By the way, have a nice day bro!
 
nafikiri hizi quotes zako mbili hapo juu zinajisema wazi, nini nia yako kwa Michuzi, maana inaonekana wazi kwa watu kama mimi tunaoweza ku-read between the lines,

Otherwise, nilikuwa ninakuheshimu sana mkuu,
mpaka nilipoona hizo quotes zako mbili hapo juu,

By the way, have a nice day bro!

Hahahah mkubwa wangu, duu nadhani unajikweza kidogo hapo, "watu kama mimi" mtani wangu ES, kwani wewe ni Shekhe Yahaya hahahaha...mimi nitaendelea kukuheshimu as a personal ila pale ambapo nadhani tutapisha kimitizamo sintoacha kufanya hivyo. Simjui Michuzi, kabisa zaidi ya mara chache chache sana kuangalia blog yake...kama wewe uliyekuwa ukiruka naye majoka ...isitoshe nahisi pia mumenizidi umri.....sina nia mbaya na huyo bwana....nashangaa mzee badala ya kujadili issue tuanahangaika na mpiga picha...anyway kama nimekukwaza na mcheza disco mwenzako wa enzi hizo sisi waungwana huomba msamaha na sintochangia tena hii Mjue mzee wa Mchuzi

Enjoy your week ends

Ushi
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom