godson Lomayani
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 538
- 711
Haukustahili kuwa jiji
Kwa nini nitoke nje ya mji ,wakati mipaka ya eneo iliyopewa hadhi feki ya jiji inajulikanaEti haikustahili kuwa jiji. Ndio maana nina recommend utoke nje ya mji. Umeishia mjini unasema unaijua arusha.
Ni sawa niende dar niishie kawe, ubungo , kariakoo.. niseme niafahamu dar.. no. There is more than that.
Waliokuwepo kuliita jiji si wajinga, ime qualify thats why. Labda ww uwe na vipimo vyako mwenyewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini nitoke nje ya mji ,wakati mipaka ya eneo iliyopewa hadhi feki ya jiji inajulikana
Hivi Mji wenye Mlima Meru, mlima wa pili kwa urefu Tanzania baada ya Kilimanjaro, Mji wenye Ngorongoro crater, Mbuga ya Tarangire, Mbuga ya Arusha National Park, Madini pekee Dunia nzima, madini ya Tanzanite...utajiri huu unaupata tena Mkoa gani hapa TZ? sasa sijui ulitarajia nini haswa
Mkivuta kijiti ndio mnadanganyana Ar ni zaidi ya Dar?we ntu m1 hutuumizi kichwa mana dunia inaitambua Arusha na mazuri yake zaidi ya Dar.
Arusha home sweety home of mans
Nakaa moshi lakin siwezi jifananisha na Arusha maisha yangu yoteArusha ni mji mzuri ila ni wa kawaida sana.Nimekuwa nikisikia sifa inazopewa Arusha,lakini nilichokishuhudia ni tofauti na nilichokuwa nakisikia.
Nimekaa Arusha Kwa zaidi ya wiki 4 nimefanikiwa kuzunguka maeneo yote ya muhimu sijaona kitu cha ajabu.
Nimeona hata mji wa Moshi ni mzuri sana zaidi ya Arusha,ni sifa tu zisizo na miguu inapewa Arusha.
Hitimisho: Arusha ni mji mzuri Ila wa kawaida sana isipewe sifa zilizopitiliza.Moshi licha ya udogo wa eneo ni mji mzuri zaidi ya Arusha.
Wewe unaishi Olmatejoo.Acha ukuda hamna cha ziada ukiacha vibaka na wanywa pombe na mbege na bangi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo hayo maeneo sio ArushaUmetembelea wapi na wapi?
Isije ukawa umetembelea kule unga limited,chekereni na moshono mwisho halafu unadai Arusha mji wa kawaida.
Nimekaa chuga na kusomea uko advance pako vizuri sana.
Kasoro kubwa ya Arusha ni udogo wa stendi yao.
Kwanza kwenu wapi? isijekuwa ni mtu wa nyanda za juu kusini halafu unaipondea Arusha.
Live long Chuga.
Upo nje ya madaHivi Mji wenye Mlima Meru, mlima wa pili kwa urefu Tanzania baada ya Kilimanjaro, Mji wenye Ngorongoro crater, Mbuga ya Tarangire, Mbuga ya Arusha National Park, Madini pekee Dunia nzima, madini ya Tanzanite...utajiri huu unaupata tena Mkoa gani hapa TZ? sasa sijui ulitarajia nini haswa
Sina shida na vivutio vya utalii,nasisitiza tena mji wa Arusha ni wa kawaida sana,licha za kuzungukwa na vivutio vya utalii mji umeshindwa kukua Kwa Kasi ya maanaHahaa ni huna nauli jonbaa? Nina gari nitafute nikutembeze kwa gharama zangu.
Kwann utoke sababu hapo bado ujaimaliza arusha yenyewe. mjini ni part ndogo tu. And for the record kama unaita feki.. serikali litambua kama jiji.. labda serikal ya kichwa chako ndio haitaki. Anyway your too late. Huwez badilisha chochote mkuu.
Arusha ni pana sana, kama nivyosema imezubgukwa na vivutio vya utalii.. so huwez kutarajia mazingira yake yafanane na ya dar. Kama bi feki hiyo ni ww
Sent using Jamii Forums mobile app
Umemaliza mkuu, Nami nakazi hapa hapa.Mimi nawacheki mnavyobishana tu kuhusu Arusha.Mimi naishi hapa na nimekulia Arusha ila asili ya wazazi wangu ni Upareni-Usangi.Arusha zamani ilikuwa nzuri kwa sababu miji mingi ilikuwa bado haijakua tofauti na sasa.Hali ya hewa ni nzuri lakini mji ni wa kawaida sana.Watalii ni wengi wanaoenda kwenye vivutio vya utalii lakini hakuna impact ya moja kwa moja kwa sisi vijana tusiojishughulisha bali tumebaki tuna suka rasta tukisubiri zali la kuolewa/kuoa ajuza wa kizungu.Mzunguko wa fedha sasa hivi ni mdogo na vijana wengi wa Arusha wamepigwa doro tu,mikwara kibao,bangi,mirungi,mbege,viroba vya pombe na kujisifia kuoa au kuolewa na wazungu.Eti kijana wa kiume "kuolewa"na mwanamke wa kibongo ni michosho,afadhali "ajuza wa kizungu"hawa vijana ni wapuzi kabisa kwa sababu ninayosema yapo kwenye vinywa vya vijana hawa,hata ukijaribu kutembelea vijiwe vyao utayasikia na kushuhudia katika mazungumzo yao ninayoyasema.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakikujibu utujuze na sisiHivi jiji la Arusha inajumuisha na mbuga za wanyama,wilaya zilizopo mbali huko au Arusha city centre na vitongoji vyake?
Hizo sijui Geneva ya Africa ndiyo sifa za kijinga inazopewa Arusha,kumbe hakuna kituNakaa moshi lakin siwezi jifananisha na Arusha maisha yangu yote
Utakua umelishwa cha Arusha sasa wenge limekushika ww sio bure
Hiyo ni GENEVA of Africa
Sent using Jamii Forums mobile app