Mjeshi afunguka kuhusu Arusha

Mjeshi afunguka kuhusu Arusha

Mtoa maada hana lolote lenye uhakika yote aloyosema yapo hewan tu! Sawa kabisa na umbea wa magazeti ya ijuma na mengine ya udaku! Kwani ni lazima kila mtu akipiga stor na rafki yake ambae ni mwanausalama wataweza jua ukweli juu ya serikali?

hawa ndo waleee ndugu lawama wanaotuma viji sms kujenga chuki kwa wananch! kama kweli unayoyasema sa waogopa nini hapa jamvini hakuna anaekujua wewe mbugira, bila shaka huo ni umbea tu tena wa jinsia ke,.

Nyie watu wa elfu 7, 7 leo mmejazana humu si mchezo ama mmeongezeka nini?
 
Sina hakika na nilicho soma na kukiona ktk picha ila niwazavyo mm, tanzia tunahitaji amani na utulivu sana na kujazana chuki, udini, ukabila na uchama huu utatugawa na kutuacha tukimwaga damu kila kukicha, tuache kuposhana, na wala sipo tayar kw mtu yoyote aliye changia au kuandika mada kumuita mtu msenzi, muongo, mpuuz na majina mengine M/mungu ibariki tanzania tubaki kuwa wa1 ni hivyo tu mm napita.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mungu saidia CDM na UDHALIMU wa CCM ubakie uchi.
 
Usitake kulipaka jeshi matope kama ni kweli na jamaa anchosema anauhakika nacho akatoe ushahidi mahala panapo stahili siyo kutaka kujaza chuki kwa wananchi. Mzalendo wa kweli hajifichi na kusema kinafiki.
 
Hivi hao wanajeshi huwa hawatumii akili, au wako kama mbwa wa kufuga, wakiachiwa minyororo wanang'ata tu.
Kwani kama wangalikwenda halafu wakabaki watulivu, kunatokea nini, wote hawana akili....

Narrow thinking! wewe ndo huna akili
 
Ndugu zangu tuangalie Mbele na Nyuma , what about hizi shutuma za Mtwara, hasa ukiangalia Jinsi Mh. Prof. Lipumba anavyo lalamika kuhusu Mtwara wanajeshi wanavyotumika. Nina wasiwasi nafikiri mtoa maada yupo sawa.hiyo habari itakuwa ya uhakika.
 
Habari wakuu,
Tarehe 25/06/2013 nilimtembelea Rafiki yangu mmoja ambaye ni mwanajeshi Huko mkoa (kapuni) jina la kambi (kapuni). Jamaa aliniambia mambo mengi kuhusu Arusha, hasa kwenye harakati za chadema. anasema yeye alikuwa mkoa wa Arusha kabla hajahamishiwa Kigoma, alikuwa kikosi no(kapuni). aliniambaia kwamba chadema wakifanya maandamano au mikutano walikuwa wanapewa sale za asikari polisi kuja kudeal na chadema, ili ionekane kwamba ni polisi wanaotuliza ghasia kumbe ni wanajesshi wa JWTZ. Jamaa akasema hili suala lilikuwa linawauma sana, kuna siku pale arusha zilitokea fujo kati ya ccm na chadema wakaambiwa waende kuwadhibiti chadema, jamaa wakaenda na uniform za polisi, badala ya kuwapiga chadema wakawapiga ccm, vunjavunja. baada ya fujo kumalizika ikaonekana watu walioumia sana na kuvunjika ni wa ccm. Serikali ikaamua kuwahamisha wote na kuwapeleka pembeni mwa nchi (mipakani huko). akaniambia kwa sasa serikali inachukua wanajeshi wa Morgoro kuja kutuliza fujo Arusha,wakiwa wamevaa gwanda la polisi.
Hii ni hatari sana kutumia Jeshi kuwakandamiza wananchi.


Hii taarifa itakuwa ya Ukweli. Wakati wa Chaguzi karibia zote zinazotarajiwa kuipa CCM shida walinzi huwa JWTZ katika magwanda ama ya Polisi, au ya Mgambo. Hii taarifa nilipewa na Mwanajeshi ambaye huwa hana sababu ya kunidanganya.
 
Hadithi yako nzuri sana mkuu

Njiwa, hiyo sio hadithi. Kwa tuliokuwa Zenji 2005 tuliona hilo. Askari wote wa kutuliza ghasia, wanajeshi na mambo mengine walikuwa imported kutoka bara. Sishangai hilo la Arusha. Kwa mantiki ni kwamba, askari polisi mnaeishi nyumba moja uraiani hawezi kuua majirani zake ambao anajua baadhi yao atakutana nao jioni kwenye nyumba hiyo ya mtaani anakoishi. Kwa hiyo basi, ili kupunguza chuki, kwa wananchi majirani wanachukuliwa wajeda kutoka mbali ili kuja kushusha kipondo hapo mahali. Kumbuka kwamba kota za polisi hazitoshi, wengi tupo nao mtaani.
 
Back
Top Bottom