Ralphryder
JF-Expert Member
- Nov 16, 2011
- 5,599
- 1,798
Habari wakuu,
Tarehe 25/06/2013 nilimtembelea Rafiki yangu mmoja ambaye ni mwanajeshi
Huko mkoa (kapuni) jina la kambi (kapuni). Jamaa aliniambia mambo mengi
kuhusu Arusha, hasa kwenye harakati za chadema. anasema yeye alikuwa
mkoa wa Arusha kabla hajahamishiwa Kigoma, alikuwa kikosi no(kapuni).
aliniambaia kwamba chadema wakifanya maandamano au mikutano walikuwa
wanapewa sale za asikari polisi kuja kudeal na chadema, ili ionekane
kwamba ni polisi wanaotuliza ghasia kumbe ni wanajesshi wa JWTZ. Jamaa
akasema hili suala lilikuwa linawauma sana, kuna siku pale arusha
zilitokea fujo kati ya ccm na chadema wakaambiwa waende kuwadhibiti
chadema, jamaa wakaenda na uniform za polisi, badala ya kuwapiga chadema
wakawapiga ccm, vunjavunja. baada ya fujo kumalizika ikaonekana watu
walioumia sana na kuvunjika ni wa ccm. Serikali ikaamua kuwahamisha wote
na kuwapeleka pembeni mwa nchi (mipakani huko). akaniambia kwa sasa
serikali inachukua wanajeshi wa Morgoro kuja kutuliza fujo Arusha,wakiwa
wamevaa gwanda la polisi.
Hii ni hatari sana kutumia Jeshi kuwakandamiza
wananchi.
Una ushahidi? mtu mzima kusutwa aibu! peleka majungu na masulupwete yako huko!