Kamanda Sirro atakuwa bonge la IGP

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,197
4,376
Nimekuwa nikimsikiliza huyu jamaa, akiwa anafanya mahojiano mbalimbali. Iwe na BBC, DW, na pia vyombo vya habari vya hapa nyumbani. Uongeaji wake huwa wanikosha sana.

Jamaa ametulia, anaongea 'point' tu, kila mtu hutamani kumsikiliza. Ninaamini haya matukio ya ujambazi Dar es Salaam yataisha kabla hakujacha.

Watu kama hawa tukiwa CCP walikuwa wana pass out angalau na kirungu kimoja, hususani cha ukakamavu.

Ukiwaacha Thobias Andengenye na Diwani Athumani, Sirro atakuwa Bonge la IGP.

I Second you.
CP Simon Sirro sio tu kuwa ni Bonge la RPC but also ni Bonge la Askari.
Namkumbuka akiwa RPC Mwanza kwenye uchaguzi Mkuu 2010.
Namkumbuka kwenye issue ya Ikwiriri.
CP Sirro ametulia,hatumii ubabe na Msuli,huyu jamaa hata watu wakigoma akija anaongea nao Dakika kadhaa wanatawanyika wakiwa Mioyo safi pasi kurushwa hata baruti wala bomu la Machozi.
Kuna Jamaa wawili katika jeshi la Polisi ambao Binafsi hunikosha sana.
CP Sirro na CP Diwani Athumani

Aliwahi sifiwa hadi na Gazeti la Mwanahalisi, kwa kuzima mapigano ya wakulima na wafugaji huko Ikwiriri.

Kamanda wa polisi huyu si wa Tanzania
picture-73.jpg

Na Nyaronyo Kicheere - Imechapwa 30 May 2012

296
Waraka wa Wiki
Features
siro.jpg

MKUU wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Simon Siro, labda si Mtanzania. Nina maana anaweza kuwa raia wa kigeni. Nitaeleza.

Kwa vitendo vyake na kwa kauli zake, SACP Siro si raia kabisa au kwa maneno mengine si polisi wa Tanzania. Haiwezekani askari Polisi Mtanzania tena mwenye cheo kikubwa kama cha Kamishna akaliaibisha na kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa namna alivyofanya Kamanda Siro.

Akiwa mji mdogo wa Ikwiriri wilayani Rufiji katika mkoa wa Pwani, wiki iliyopita, Kamanda Siro, alifanya yale ambayo askari Mtanzania aliyehitimu ukuruta katika chuo maarufu cha Polisi Moshi (CCP) hawezi kuyafanya wala kufikiria kuyafanya.

Nimesoma kwenye vyombo vya habari na kushuhudia Kamanda Siro akisema kwamba askari wa Kituo cha Ikwiriri walikosea na kwamba ndio chanzo cha vurugu zilizohusisha mapigano ya wakulima na wafugaji!

Gazeti moja liliandika: “Lakini hali hiyo tete ilibadilika ghafla jana (Jumanne wiki iliyopita) wakati Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi nchini, Simon Siro, alipotumia busara na kuingilia kati siyo tu kwa kuamuru kuachiwa kwa watuhumiwa hao, bali pia kuwalaumu polisi na kusema wao ndio wamekuwa chanzo cha tatizo kutokana na kuwapendelea wafugaji. Hatua hiyo ndiyo iliyorejesha amani na utulivu katika eneo hilo.”

Hapa nilipo nahema kwa hasira. Kamanda anayeongoza kikosi cha Polisi wa Fanya Fujo Uone (FFU), anawagwaya wakulima? Kamanda mkubwa wa Polisi anawanyenyekea wakulima badala ya kuwapiga mikanda, kuwakanyaga mateke ili wakome kulalama na wawaogope Polisi!

Kamanda gani huyu? Ama kweli Jeshi la Polisi nalo limeingiliwa. Nchi yetu sasa ipo hoi bin taaban. Tunakotoka, tunakokwenda, hatukujui, tunakwenda hobelahobela tu.

Zamani watu walisema uandishi wa habari umeingiliwa na makanjanja; wahandisi nao wameingiliwa na sasa wanajenga barabara inabomoka kesho yake; wanasiasa wameingiliwa sasa hawajui kudanganya ndiyo maana wanafukuzwa kazi kwa wizi; wao wanadai wameonewa na kuandaa maandamano ya kuwapokea.

Hata mashushushu nao wameingiliwa, tofauti na zamani. Waliopo sasa hawajifichi; hebu fikiria shushushu wa chama fulani anapomwalika Mwenyekiti wa chama kingine kuja kuwa mpambe wake atakapoomba urais kupitia chama chake! Si kila mtu atamgundua kuwa ni shushushu aliyetumwa kukiangamiza chama hiki?

Na tuache haya ya kuingiliwa kwa sababu hata mameya nao wameingiliwa na sasa wanafikiri kwa namna tofauti sana kwa kutumia kiungo nyeti anachokifahamu mwenzao wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi, peke yake.

Turudi kwa Kamanda Siro, polisi mwoga anayetofautiana na makamanda wenzake na askari wenzake. Tabia ya Kamanda Siro itafanya raia wasiwaogope polisi tena na hii ni hatari sana kwa jeshi letu la Polisi.

Sisi Watanzania tumezoea na tunawapenda polisi na makamanda wa Polisi katili, wanaopiga raia ili kuwanyoosha waweze kutawalika vema. Tunataka makamanda wa polisi kama Venance Tossi aliyewanyoosha watuhumiwa wa ujangili.

Tumezoea makamanda wa Polisi kama Michael Kamhanda wa Mkoa wa Ruvuma, aliyewakomesha wakazi wa Songea wakakoma kabisa hadi leo hatusikii maandamano wala mikutano ya kupinga mauaji ya kishenzi mkoani humo.

Tunataka Polisi kama Kamanda Andengenye wa Arusha na IGP Said Mwema wenye intelijensia kali na uwezo wa kupiga marufuku maandamano na kutawanya mikutano ya wabishi wanaotumia kisingizio cha siasa za upinzani.

Hatujamsahau kiboko ya njia, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja. Huyu ndiye aliyetumwa na IGP Mwema kuongoza maofisa kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda Songea kufanya uchunguzi wa ghasia hizo.

Tunataka makamanda kama Chagonja aliyeshirikiana vema na wenzake wakawatwanga wakazi wa Nyamongo, wakaua sita au saba hivi na walipoendelea kuleta vurugu wakipewa kichwa na CHADEMA wakatupa maiti barabarani na kuyatelekeza huko. Tarime na Nyamongo wakanyooka hadi leo.

Viongozi kadhaa wa CHADEMA wakiwamo wabunge Esther Matiko na Tundu Lissu, walipoleta za kuleta, nao wakaswekwa ndani na kufunguliwa mashitaka na hadi leo kesi ipo mahakamani. Yes, tunataka makamanda wa Polisi kama hawa.

Yeye Kamanda Siro analeta lele mama? Hakuna kukamata wala kusweka ndani? Eti leo anasamehe na kuamuru wakulima 53 wakorofi wa Ikwiriri waliokamatwa kwa kudiriki kupiga wafugaji wa Kimasai na Kisukuma. Wakulima watawapa Polisi nini hadi wanasikilizwa na Kamanda Siro?

Wafugaji wanawanunulia askari wa Polisi saa, simu, redio, televisheni, nyama kilo mbilimbili, maziwa kwa bili chupa moja kila askari na hivyo watoto wa askari hawapati kwashiorkor na hata nauli wafugaji wanawalipia askari kwenda Utete na Dar es Salaam! Leo watu wanaobughudhi wafugaji wanaachiwa?

Hapana, huu si utamaduni wetu Watanzania. Kamanda Siro achunguzwe uraia wake isije ikawa ni Mrundi, Mkongo, Mmalawi, Mzambia au Mnyarwanda.

Haiwezekani Kamanda wa Polisi wa Tanzania aliyeiva hasa mafunzo ya ukakamavu, aonyeshe ulegelege kama huyu Kamanda Siro.

Kule kwetu nilikozaliwa, polisi hasa tunawafahamu. Kwa upande wa Kenya wanaitwa “machoni’ au kwa jina lao maarufu la GSU au General Service Unit.

Hawa ndio wanaokaribia kulingana na askari wa kwetu FFU – Fanya Fujo Uone. Hawa FFU kule kwetu tunawaita “motoroisi” nasikia Kingereza chake ni Motorized Police.

Kwetu hatujui FFU bali tunajua “motoroisi” ambao wakiingia kijijini au kufika kwako, hutasikia wanapiga hodi, bali utasikia mbwa akilia kapigwa teke, kuku wanaruka na kilio juu, paka na mbuzi hata kondoo wakikanyagwa mabuti na kupigwa mikanda. Hao ndio askari wanaoogopwa Ukuryani.

Mliona askari wale waliokuwa wakipiga raia Zanzibar hadi wakaua zaidi ya 20 na wengine wanasema waliouawa ni karibu 100. Wale askari waliokuwa wanapiga raia na wakimkosa wanakanyaga baiskeli yake! Hamkuona kwenye video? Wale ndio askari wetu Tanzania. Siro siye.

Hivi Kamanda Siro anayefyata mkia kwa Wandengereko atafanya kazi mkoani Mara kweli? Mie napendekeza avuliwe madaraka maana ameonyesha udhaifu mkubwa. Hatutaki askari narenare katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa huku raia wakikiasi chama tawala.

Sasa raia wanaikimbia CCM na Polisi nao, tena Kamanda mkubwa anatetemeka na kuonyesha woga kwenye eneo la tukio na anarudi nyuma eti anawalaumu Polisi wake kuwa ndio chanzo cha vurugu? Kamanda gani huyu, haraka fukuzilia mbali kabla mambo hayajaharibika.

Bila hivyo Polisi watakosa heshima.

Historia ya Sirro

Simon Nyakoro Sirro alizaliwa eneo la Kiabakari wilaya ya Butiama mkoani Mara mwaka 1963.
Kuhusu elimu yake, Simon Sirro alisoma Shule ya Sekondari ya Ilboru jijini Arusha na Tosamaganga kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu kusoma Shahada ya awali katika Sheria.
Sirro amesoma pia seminari (masomo ya upadri) na kufikia ngazi ya juu kabla ya kuacha na kujiunga na Jeshi la Polisi.
Kamanda Sirro alisema kuwa kama isingekuwa baba yake basi leo yeye angekuwa ni Padri wa Kanisa Katoliki kwani ndiyo ndoto yake kubwa, lakini baada ya wazazi wake kumkatisha ndipo alipojiunga na jeshi hilo.
Unajua wazazi kule kwetu Musoma walikuwa hawakuelewi usipooa. Mzazi aliona mimi ni kijana mkubwa akasema haiwezekani,” alisema Sirro alipofanya mahojiano na Mwananchi kipindi cha nyuma.
Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Kituo cha Polisi Buguruni mwaka 1998, Mkuu wa Upelelezi Tarafa ya Magomeni kwa miaka 5 na Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Tabora.
Mwaka 2002 alikuwa Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam akiwa ni msaidizi wa Abdallah Zombe.
Sirro ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam wa tatu ambapo aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli Februari 15 mwaka 2006 akichukua nafasi ya Suleiman Kova aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2008. Kabla ya Kova aliyekuwa akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni Alfred Tibaigana.
Wakati Suleiman Kova akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sirro alikuwa msadizi wake ambapo baadae alirithi mikoba yake.
Kabla ya kuongoza Kanda Maalum Dar es Salaam, Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Tanzania. Moja ya opersheni kubwa alizowahi kuongozi ni Operesheni Kimbunga dhidi ya wahamiaji haramu mwaka 2012.
Lakini pia, Simon Nyakoro Sirro amewahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Mikoa mbalimbali ambayo ni Tanga, Mwanza na Shinyanga.
Wakuu wengine wa Jeshi la Polisi ni;
1.Elangwa Shahidi (1964-1970), alistaafu.
2.Hamza Azizi (1972-1973), aling’olewa na Mwl. 3.Nyerere kwa matumizi mabaya ya madaraka.
4.Samwel Pundugu (1973-1975).
5.Philemon Mgaya (1975-1980), aliachishwa kazi kwa manufaa ya umma.
6.Solomoni Liani (1980-1984), alihitimisha kipindi cha mwisho cha Mwl. Nyerere.
7.Harun Mahundi (1984-1996), alistaafu.
8.Omari Mahita (1996-2006), alistaafu.
9.Said Mwema (2006-2013), alistaafu.
10.Ernest mangu (2013-2017), atapangiwa kazi nyingine, na
11.Simon Sirro (2017-) yupo madarakani.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Nyakoro Sirro ameoa mke mmoja na ana watoto wanne
 
Hivi mangu amekosa nini fasta,nadhani Mangu si mbaya sana ila wana siasa hasa ccm wamemyumbisha sana na kupelekea kuchuja ghafla na ma rpc makada wamelifanya jeshi kuchukiwa sana
 
Akiwa Mwanza alifanya kazi yake vizuri sana hata kuletwa Dar kusaidia intelijensia, baada ya Kova kuwa kovu na kuondoka na Siro kupewa nafasi ya Kova naona kama ule uweledi wake ameanza kuuweka pembeni na kuwa na muhemko wa kisiasa zaidi, Siamini kama atastahili kuwa IGP maana ameonekana sasa yeye kuwa kada wa chama fulani na kufuata amri za wana siasa.
Tabia pia ya kukimbilia press kila saa nayo inampunguzia heshima anatakiwa awe na msemaji wake sio kila jambo kwenye press ni kamanda Siro, aende site, atumikie Wananchi na sio kuwatisha kwamaba atawashughulikia. Sio kauli nzuri kwa msomi kama Kamanda Siro.
 
Akiwa Mwanza alifanya kazi yake vizuri sana hata kuletwa Dar kusaidia intelijensia, baada ya Kova kuwa kovu na kuondoka na Siro kupewa nafasi ya Kova naona kama ule uweledi wake ameanza kuuweka pembeni na kuwa na muhemko wa kisiasa zaidi, Siamini kama atastahili kuwa IGP maana ameonekana sasa yeye kuwa kada wa chama fulani na kufuata amri za wana siasa.
Tabia pia ya kukimbilia press kila saa nayo inampunguzia heshima anatakiwa awe na msemaji wake sio kila jambo kwenye press ni kamanda Siro, aende site, atumikie Wananchi na sio kuwatisha kwamaba atawashughulikia. Sio kauli nzuri kwa msomi kama Kamanda Siro.
Jamaa yuko vizuri sana.
 
mfumo uliopo si mzuri watumishi wa umma wana jihusisha na siasa katika masuala ambayo hayahitaji siasa kuwe na utengano kazi za chama zibaki kwa wanachama na siasa zibaki kwa wanasiasa .
 
I hope so too
Simoni Siro ni performer yule hategemei kuteuliwa alipo sasa anaridhika anachotaka ni kutumikia nchi na kuacha legacy. Amekulia shule zenye heshima kuu ya kinidhamu hapa nchini(mmeelewa), hawezi kuwa na tamaa alichofundishwa ni OBIDIENCE AND PERSEVERANCE
 
Nimekuwa nikimsikiliza huyu jamaa, akiwa anafanya mahojiano mbalimbali. Iwe na BBC, DW, na pia vyombo vya habari vya hapa nyumbani. Uongeaji wake huwa wanikosha sana.

Jamaa ametulia, anaongea 'point' tu, kila mtu hutamani kumsikiliza. Ninaamini haya matukio ya ujambazi Dar es Salaam yataisha kabla hakujacha.

Watu kama hawa tukiwa CCP walikuwa wana pass out angalau na kirungu kimoja, hususani cha ukakamavu.

Ukiwaacha Thobias Andengenye na Diwani Athumani, Sirro atakuwa Bonge la IGP.
Na kuongoza Polisi kuwakamata wabunge wa CDM kwa zuio feki la mahakama? kwenda kumsearch Mdee home kama kibaka? kumsafirisha Bulaya mpaka Dar toka Mwanza nadhani navyo vyapasa kumpa credit
 
HUYUUU WA SASA ANAITWA KIRAHISIII N A MSTAAFU NYUMBANII KWA HOMESOPPING CENTRE WANAPIGA PICHA NA DOGO KAMA WATOTO WADOGO AISEE NI SHIDAAAA AEND E NA MWENZAKE KOVA
 
Hivi kuna IGP ambaye huwa haegemei upande wa CCM? Hilo la kuegemea upande wa CCM imekuwa ni tabia ya Ma- IGP wetu utadhani kama ni sifa ya ziada ndani ya Jeshi la Polisi inayotakiwa ili mtu apande vyeo haraka haraka!!
 
Na kuongoza Polisi kuwakamata wabunge wa CDM kwa zuio feki la mahakama? kwenda kumsearch Mdee home kama kibaka? kumsafirisha Bulaya mpaka Dar toka Mwanza nadhani navyo vyapasa kumpa credit
Hayo makandokando ni ya kawaida. Tupime mazuri na mabaya.
 
Hivi kuna IGP ambaye huwa haegemei upande wa CCM? Hilo la kuegemea upande wa CCM imekuwa ni tabia ya Ma- IGP wetu utadhani kama ni sifa ya ziada ndani ya Jeshi la Polisi inayotakiwa ili mtu apande vyeo haraka haraka!!
Nadhani ukiacha udhaifu wao, lakini nadhani katiba ya sasa ni ya mfumo wa chama kimoja katika vyama vingi. Taratibu tutafikatu.
 
Simoni Siro ni performer yule hategemei kuteuliwa alipo sasa anaridhika anachotaka ni kutumikia nchi na kuacha legacy. Amekulia shule zenye heshima kuu ya kinidhamu hapa nchini(mmeelewa), hawezi kuwa na tamaa alichofundishwa ni OBIDIENCE AND PERSEVERANCE
Uko sahihi kabisa mkuu.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom