Msanii,Kama hamjui baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 niliacha kabisa kusoma makala zake.
amebakia kuupamba uchafu kuuita uzoefu.
Lakini kwa kuwa ni mtanzania ana uhuru wa kutoa maoni yake. na kwa kuwa anaijua media vyema sana na ni rafiki mzuri wa mr. Mkumbwa anajua kilichopangwa na kupangika. na kwa kuwa bado ni mfuasi mwema wa Muungwana anajua how to play salva's tricks. Huwa anafanya trips nyingi sana mikoani na alizidisha sana hivi karibuni kabla ya kampeni. Mnajua alikuwa anafuata nini huko mikoani? nani aligharimia safari zake? Namhurumia Jenerali Ulimwengu kwa kuzungukwa na mamluki wanaomchunguza kila move yake wakisaka weak link yake.
Ametoa maoni na sisi ndo wapiga kura. je tulazimishwe kupiga kura kwa mtazamo wake? Ina maana yeye hataki chadema ishinde? amefanya nini kupromote demokrasia na elimu ya uraia kamammdau zaidi ya makala za kuzungumzia watu na soka?
Hawa ndio wanaoitwa establishment journalists ambao wako comfortable na status quo na hawataki kuona inabadilika. Nilishangazwa na hamaki ya Mkumbwa Ally, lakini baadaye nikafikiria nikaona u-CCM wake ulivyomweka ndani ya box. Pili kuna njama pia za chama tawala za kuonyesha kwamba juhudi za Dr. Slaa hazitamfikisha kokote na sasa zinaanza kuandikwa makala kuonyesha hivyo ili ifikapo Oktoba 31 CCM ifanye mipango yake ya kuchakachua. Hawataki kuona CHADEMA inakuja juu. Wako comfortable na Lipumba kwa sababu huyu wanajua limits zake. Ushindi wa Slaa utakuwa revolutionary na hawa establishment types watajikuta nje ya mapinduzi na comfort zone yao imetobolewa.