Mjengwa atishia kujidhuru sababu ya JF

Status
Not open for further replies.
Mwanahabari gwiji kwa njia ya blog Tanzani Mr Maggid Mjengwa amewatolea uvivu wanachadema waliojazana JF kwa tabia yao ya kushambulia kwa ushabiki na kejeli bila kufikiri wala kujadili mambo kwa hoja na logic...............BIG UP MJENGWA

monkeyspank.gif
 
kaahidiwa ukuu wa wilaya zilizoanzishwa mwaka huu ndo maana anaongea ushirooooooooooo mtupu
stupid maggid
 
nimemfata kule kwenye blogu yake nimemnanga kwamba ugomvi wa nyumbani asiupeleke kwa jirani.
 
Zawadi nono mnayoweza kutupa ni Katiba mpya

lC.gif
Maggid Mjengwa​
Oktoba 6, 2010
rC.jpg

KWENYE moja ya matangazo ya uchaguzi kwenye luninga anaonekana bwana anayewauliza wapiga kura kama watakwenda kupiga kura. Kila mmoja anatoa sababu za kutokwenda kupiga kura. Kisha bwana yule anahitimisha kwa kusema: “Na matokeo yakitangazwa msilalamike kuwa kura zimebwa!” Nadhani tangazo lile lina walakini; maana kilichopaswa kutafutiwa jibu ni swali la kwa nini watu hawataki kwenda kupiga kura. Stalin wa Urusi aliwahi kutamka: "Anayepiga kura hana anachoamua, anayehesabu kura ndiye anayeamua kila kitu".
Na hapa lipo tatizo la msingi. Watu kukosa imani na wenye kusimamia uhesabuji wa kura zenyewe. Kuna wanaojisikia kuwa kura zao hazina umuhimu; kwani, mwisho wa yote, kura zitaibwa.
Katika nchi zetu hizi, kukosa imani na wenye kusimamia mchakato wa uchaguzi hadi kuhesabu kura ndio chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani. Tumeona hayo kwa jirani zetu kule Kenya.
Wakenya walishiriki mchakato wa kujiandikisha na hata kupiga kura bila matatizo makubwa. Kazi ikaja kwenye kuhesabu kura. Ndipo hapo hesabu zikaanza kuwa ngumu. Kukawa na kufuta hapa na pale. Kukawa na kushinikizana na kadhalika. Hatimaye damu ikamwagika.

Kila mwenye kufikiri alielewa kuwa kiini cha vurugu za Kenya ni Tume ya Uchaguzi ambayo haikuwa huru. Wakenya wale leo wana Katiba mpya. Katiba ya watu wa Kenya.
Hivyo basi, dawa ya kuepuka au kupunguza shari kama iliyotokea Kenya ni kwa nchi zetu hizi kuangalia upya Katiba zetu hizi na hususan inapohusu uchaguzi na Tume ya Uchaguzi.
Nasi kama taifa, tuanze sasa kuangalia uwezekano wa kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba mpya. Zawadi kubwa kwetu Watanzania tukaposherehekea miaka hamsini ya uhuru wetu iwe ni kwa viongozi wetu kutuanzishia mchakato huo. Na huo ndio utakuwa urithi muhimu na wa maana kubwa tutakaoviachia vizazi vijavyo.
Kwamba siasa ni jambo jema na la kuvutia tunalishuhudia katika nchi za wenzetu zenye kuzingatia utawala wa sheria na zenye katiba zenye kulinda maslahi ya nchi zao.
Kwa mfano, tunaona jinsi mchakato wa kutafuta wagombea urais nchini Marekani unavyofanyika. Ndani ya chama kimoja watu wanashindana kwa hoja.
Kule Marekani tuliona Hillary Clinton na Barrack Obama wa chama cha Democrat wakichuana kwa karibu kutafuta nafasi ya kuchaguliwa kugombea urais kupitia chama chao.
Hillary na Obama hawakuwa na chuki binafsi kati yao. Walishindana kwa hoja. Ikifika siku mmoja wao akachaguliwa na mwingine akashindwa. Ustaarabu kwao ikawa ni kupongezana kwa kushikana mikono na baadae kushirikiana katika kufanikisha ushindi wa chama chao.
Na hata Obama aliposhinda Urais, akamfanya Hillary Clinton kuwa Waziri wake wa Mambo ya Nje.

Kama ni mitandao, wenzetu yao huisha siku ile mshindi anapotangazwa. Hakuna kutafutana na kufanyiana hila baada ya hapo. Hiyo ndio maana halisi ya ushindani. Hiyo ndio siasa, si mchezo mchafu.
Ikumbukwe kuwa kila matokeo ya uchaguzi yana tafsiri zake. Kama ni uchaguzi huru na wa haki kuna mawili; kushinda au kushindwa. Katika hilo la mwisho, kiongozi au chama kinashindwa uchaguzi, kuna kusikitika, lakini wakati huo huo kuwepo na furaha kuona demokrasia inafanya kazi yake.

Mgombea au chama kikubali kuwa wapiga kura wamewakataa, hamkuwafanyia mengi waliotarajia, au hawaamini kuwa mtawatekelezea wanayotarajia, hivyo basi, wamewachagua wengine. Mkubali kuchukua nafasi ya wapinzani, mwangalie kasoro zenu, mjipange upya. Siasa haiishii kwenye uchaguzi, kila siku ni siasa, kuna uchaguzi mwingine unakuja.

Katika nchi zetu hizi tunaona ni jinsi gani hilo la kukubali kushindwa linakuwa gumu kwa baadhi ya wanasiasa. Ukweli tu kuwa katika nchi zetu hizi Tume Huru za Uchaguzi hukataliwa na walio madarakani unathibitisha dalili za kutokuwa na utayari wa kuendesha ushindani wa kisiasa katika mazingira ya tambarare kwa pande zote zinazoshindana.

Lakini, ushindani wa kisiasa mara nyingi unahusu vyama. Tatizo kuna wanaoingia katika ushindani wa kisiasa kupitia vyama na bila kujua dhana ya chama ina maana gani.
Na tuanze kwa kujiuliza: Je, chama cha siasa ni nini? Katika harakati za kisiasa kuna aina mbili za vyama; Chama cha Ukombozi na Chama cha Uongozi. TANU, FRELIMO, ANC ni mifano ya vyama vya ukombozi vilivyokuja kugeuka kuwa vyama vya uongozi. CCM, CUF, CHADEMA ni mifano michache ya vyama vya uongozi.

Chama imara cha ukombozi kinatakiwa kijenge uwezo wa kuwa chama cha uongozi mara ile kitapotwaa madaraka. Hufanya hivyo kwa kuweka mkazo juu ya mafunzo kwa makada wake. TANU, FRELIMO na ANC viliweza kujenga uwezo huo.
Kielelezo cha nguvu na umakini wa chama cha kisiasa ni uwingi na ubora wa makada wake. Chama ni makada kwa vile chama ni itikadi, malengo na shabaha na wala si nasaba na umaarufu wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama.

Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma.
Chama hicho hujiamini. Edward Mondlane, kiongozi wa kwanza wa Frelimo alipouawa kwa bomu la barua, Frelimo walijua watafanya nini, walijua mchakato gani utumike katika kumpata mrithi wake. Na hata Samora Machel, alipotoweka ghafla kwa ajali ya ndege, FRELIMO walijua watafanya nini.
Na kama Nyerere angekufa wakati wa TANU, bila shaka, TANU walikuwa wamejiandaa vema na cha kufanya. TANU haikuwa na ukame wa jeshi la makada. Nguvu ya Frelimo kama ilivyokuwa kwa TANU zilikuwa ni makada wake.
Na ieleweke, kuwa makada ni roho ya chama. Chama kikianza kupungukiwa na idadi ya makada wake wakereketwa, basi, chama hicho hakina mustakabali ulio salama, kitayumba na pengine kuangukia kaburini.

Tuangalie basi mfano wa chama kisichokuwa na nguvu ya makada. Wakati John Garang wa SPLM alipokufa kwa ajali ya ndege, hakuna ndani ya SPLM aliyekuwa na hakika ya nini kifanyike.
Kwamba ni mke na mtoto wa John Garang waliosimama mbele ya kamera za waandishi wa kimataifa kujaribu kuelekeza nini John Garang angependa kifanyike kilidhihirisha udhaifu wa SPLM. Kwamba SPLM ni John Garang na kinyume chake. SPLM ilikuwa ni chama mtu.
 
kuendelea kumjadili mjengwa na mpango wake huo ni kumpa umaarufu asiostahili
huyu sijawahi kumfikiria hat kuwa ni mwandishi sana sana ni mwandikaji
sijawahi ona lolote katika uandishi wake:llama:
 
Neno La Leo: Ng'ombe kipofu, na ng'ombe aliyevunjika mguu!

Ndugu zangu,

Wahehe wana msemo; Isenga imbofu na isenga indenyeefu.
Kwamba ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu, wote
watakufa njaa. Ng'ombe kipofu hawezi kuyaona majani, na yule
aliyevunjika mguu naye hawezi kujikokota kwenda kutafuta nyasi za kula.

Tunavyoenenda kama jamii wakati mwingine ni sawa na ng'ombe
kipofu na yule aliyevunjika mguu. Unaweza kuliona hilo nyumbani kwako,
katika ukoo wako na hata mahala pako pa kazi.

Leo kuna wanaotafuta visingizio vya kuingia vitani. Kuna wanaodai
wanapigana kuwatetea wanyonge walio gizani. Walio gizani nao wameanza
kuona katika giza hilo hilo, maana wamekuwa gizani kwa muda mrefu.
Wameshtuka. Wanahoji mantiki ya vita vinavyopiganwa kwa niaba yao.

Na walioamua kuingia vitani nao wanaonekana kutojiandaa vema na vita
hivyo, wanaelekea kushindwa, maana wanapigana vita vya kinafiki. Na
kamwe usiingie kwenye vita kama hujajiandaa.
Mwingine atasema; vita vingine havina budi kupiganwa hata kama
hujajiandaa kupigana na kushinda. Hapana, huendi vitani ili mradi tu
unakwenda vitani , kama vile unakwenda harusini. Vita si lelemama.

Katika dunia hii inasemwa; chagua vita vyako. Haina maana uchague vita
kama unachagua mashati ya mitumba Kariakoo. Ina maana kubwa. Pima
kwanza, soma alama za nyakati. Chagua vita inayoshindika, iliyo ya
muhimu kupiganwa na unayokuwa na hakika ya kuwa umejiandaa vema kulipa
gharama ya ushindi. Kwamba unachokipigania si cha kinafiki.

Angalia kwanza kwenye kabati lako, kabla hujaanza kutangaza kwa watu, kuwa kabati la jirani yako lina mzoga unaonuka, huenda nawe unao, umeanza kutoa harufu, lakini unahisi tu harufu ya mzoga wa jirani yako!
Wengi wetu tumekutana na hali ya kuwaona jogoo wawili wakipambana. Kawaida ya mpambano wa majogoo wawili ni kuvutia watazamaji. Na kila mtazamaji huwa na hulka ya kuchagua jogoo wake wa kumshangilia; kama ni jogoo mweusi na mwekundu, basi, kutakuwa na mashabiki wa jogoo mweusi na wale wa mwekundu. Yahitaji ujasiri kuamua kuwa katikati, kutochagua jogoo wa kumshabikia.
Na hutokea, kwa yule ambaye jogoo wake ameshindwa pambano, basi, atatoka mahali hapo kwa masikitiko, akiwa na unyonge, kisa? Jogoo wake kashindwa! Ni hulka ya mwanadamu. Yahitaji ujasiri kuamua kuwa katikati, kutochagua upande. Kutochagua jogoo wa kumshabikia. Wapo wanadamu wenye ujasiri huo. Pambano linapoendelea au linapomalizika, basi, huweza kutoa tathmini isiyoegemea upande mmoja.

Ndio, tunapaswa pia kutumia bongo zetu katika kutoa hukumu, na si kuongozwa na mapenzi ya moyoni tu. Hivyo ndivyo wafanyavyo mahakimu na majaji wanapoamua mashauri mahakamani. Usiishie tu kumlaani jogoo mwekundu anayeonekana kuwa na maumbile makubwa kwa kumtwanga jogoo wako mweusi mwenye maumbile madogo. Ukiumiza kichwa, unaweza kubaini , kuwa jogoo mwekundu alikuwa na sababu na haki za kumtwanga jogoo wako mweusi. Unatakiwa kuwa na ujasiri wa kuyaangalia mapungufu ya jogoo wako mweusi. Si wengi wenye kutaka kuifanya kazi hii ya kuumiza vichwa, kutafakari mapungufu yao na yale ya wanaowashabikia.
Naam. Maisha ni mapambano, kuna kushinda na kushindwa. Ushindi una gharama.
Mwanadamu jiandae na gharama ya ushindi. Ushindi waweza kuwa ghali mno.
Unaweza kupambana ukashinda, lakini gharama ya ushindi yaweza kuwa jamaa na
marafiki wa wote uliowashinda watageuka kuwa maadui zako, yawezekana
watakuwa maadui kwako kwa muda mrefu tu. Watakukasirikia, watafanya yote
nawe upate maumivu.

Hivyo, mwanadamu usifikiri tu gharama ya kushindwa, fikiri pia gharama ya
ushindi. Na wakati mwingine, ni gharama inayostahili kulipwa. Franklin
Roosevelt alikuwa Rais wa zamani wa Marekani. Alifahamu faida na hasara za
kuwa na maadui. Waliompinga katika sera zake za kiuchumi aliwaita " Watiifu
wa Kiuchumi" Na akasema; wamejiunga kwa pamoja kunichukia na nakaribisha
chuki zao kwangu!

Kama unapigana vita ya muhimu, kama vita hivyo vyaweza vikawa vya kushinda (
winnable). Na kwamba umejiandaa kulipa gharama ya chuki ya muda mrefu ya
utakaowashinda, basi, ingia vitani, na kama la, tafuta suluhu au rudisha
majeshi nyuma kimpangilio ( tactical retreat).

Swali ni hili; utafikiaje uamuzi wa ama kuingia vitani au la?
Miaka mingi iliyopita alitokea Mfalme wa Epilus aliyeitwa Pyrrhic.
Mfalme huyu aliamua kuingia vitani kulikabili jeshi kubwa na lenye
nguvu nyingi, ni jeshi la Warumi. Lakini kabla ya Mfalme kuingia
baharini na vikosi vyake kuitafuta Italia ya Warumi, msaidizi wake wa
karibu, Cineas, aliomba mazungumzo ya faragha na Mfalme. Alitaka
kumwuliza maswali na kumshauri.
Cineas alimtamkia Mfalme; " E bwana Mfalme, Warumi wanasadikika kuwa
na jeshi kubwa , lenye nguvu na lenye mashujaa wengi. Ndio maana
wameteka nchi nyingi. Je, Mungu akitusaidia, tukaja kuwashinda Warumi,
tutafanya nini na ushindi wetu?

Mfalme akajibu: " Mbona hilo ni swali jepesi sana. Mara ile
tukiwashinda Warumi, hakutatokea jeshi kutoka mji wowote wa Italia
litakaloweza kupambana nasi."

Cineas alitulia kidogo, kisha akamwuliza Mfalme: " Tukishaikamata
Italia ya Warumi, kipi kitafuatia?"
Mfalme akajibu: Sicily ni kisiwa chenye hazina za thamani kubwa,
itakuwa rahisi sana kukiteka kisiwa hicho."
Cineas aliendelea kuuliza: " Bwana Mfalme, unaongea juu ya mambo ya
kusadikika, lakini una maana kukitwaa kisiwa cha Sicily kutakuwa na
maana ya kukoma kwa vita?"

Mfalme akajibu: " Hapo tutakuwa tumeikaribia Afrika. Na tukishaikamata
Afrika ni nani hapa duniani atathubutu kutukabili kivita?"
" Hakuna" Alijibu Cineas, kisha akauliza; " Na baada ya hapo tutafanya
nini?"
Mpaka hapo Mfalme hakujua Cineas alikuwa anampeleka wapi kwa lojiki ya
kifikra. Mfalme akajibu:
" Baada ya hapo, tutapumzika, tutakula raha. Tutakula na kunywa .
Tutabaki tukichekeshana na kucheka, siku nzima."
Kama ni hivyo, alisema Cineas; " Ni kitu gani kinachotuzuia kufanya
hayo yote sasa bila kwenda vitani?

Mfalme hakuielewa mantiki ya Cineas. Akakaidi ushauri. Akavipeleka
vikosi vyake kupambana na Warumi. Baada ya vita ngumu, jeshi la mfalme
liliwashinda Warumi. Hata hivyo, lilipata hasara kubwa ya kupoteza watu
na kuwa na majeruhi wengi. Jeshi lake likadhohofika sana. Likajaribu
kuitwaa Sparta, likashindwa vibaya sana. Mfalme aliwindwa na hatimaye
akakakamatwa kama kuku na kuawa kwa kupigwa mawe kwenye mitaa ya Argos.

Isenga imbofu na isenga indenyeefu. Ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe
aliyevunjika mguu. Na hilo ndilo ‘Neno Leo.'

Maggid,
Iringa.
 
tingisha we kama unawezaaa....aaahaaaah..aahhaaa
mjengwa ni nai haswa?? mana awa watu wenye blog uwa wanatumiwa na CCM ili wapewe hela, mchekini mwenzie MICHUZI
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom