Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 61,678
- 37,863
11 October 2010
' Mwenyekiti' wenu naandamwa na maneno kule Jamii Forums ( JF). Nimeishi Iringa na Wahehe kwa miaka sita sasa. Mkisikia nimechukua kamba na kujinyonga, basi, ni JF!
Yafuatayo ndio yanayoandikwa kuhusu mimi, nimewajibu pia:
Quote Originally Posted by Kichuguu:
Nadhani hii ni dhana potofu sana kutolewa na Mjengwa, huenda ni kwa vile amekulia ndani ya CCM huku kaka yake, Colonel Mjengwa, akiwa DC wa muda mrefu sana chini ya CCM. Sidhani kama kweli Tanzania tunahitaji misitu ya marais, tunahitaji rais mmoja tu. Kumkataa mtu mwenye uwezo eti kwa vile chama chake hakina miti mingine ni makosa sana kwa vile rais huyo ana mamlaka ya kuunda serikali yake akichukua wasaidizi wake kutoka sehemu yoyote ya nchi ambao ni pamoja na wanachama na wasiokuwa wanachama wa chama chake. Kwa mfano sishangani kuona kuwa Slaa akimfanya Mwakyembe kuwa waziri wa sheria na mambo ya Katiba"
Majibu yangu:
Kichuguu,
Unachoandika si sahihi. Sitamzungumzia Colonel Mjengwa. Sijakulia kwenye CCM, bali nimekulia kwenye siasa. Na wengine wanadhani tukiandika haya tunafikiria vyeo. Asubuhi hii nimetoka kumjibu mwenzetu huyu;
Quote Originally Posted by Sir R:
JK akishinda Mjengwa utakuwa DC
Majibu yangu;
Hata nikipewa dhamana ya U-RC nitasema; " Mheshimiwa, Asante sana, lakini HAPANA kwa sasa". Ndio, nina mke, na watoto wanaonihitaji zaidi katika makuzi yao. Kibarua ninachokifanya sasa na kipato changu, japo kidogo, kinaniwezesha kujikimu. Mimi ni mjamaa, na kamwe sijawahi kuupenda ubepari. Tatizo letu Watanzania ni hulka yetu ya kuangalia ' vyeo' na vyote vyenye kuambatana na vyeo hivyo, kama vile gari la fahari, safari za ndani na nje na posho. Badala ya kuangalia zaidi dhamana inayoendana na vyeo hivyo.
Ni ujinga pia, kudhani kila mtu anayefikiri tofauti , basi, ni fisadi au kanunuliwa na mafisadi.
CHANZO: Mjengwa Blog