Mjadala wa Mafuta na Suala la Muungano

Mjadala wa Mafuta na Suala la Muungano

Zanzibar ni lazima wakubali kwamba Muungano hauko hiari kama wenyewe wanavyofikiria hakuna nchi inapenda kugawanywa tena pale ambazo watu wengi wameshajichanganya kama Tanzania hivyo hizo ndotto hazitatimia kizazi hiki wala kijacho. Dunia huko mbele itakuwa moja hata kuliko sasa na soini kama Tanzania itakuja kujitenga hata siku moja ni maneno. Ni lazima tujiulize kabla ya Muungano na waarabu ni nani walikuwa wa Zanzibari?. Ni Wabara waliokuwa wanafanya biashara za utumwa na Zanzibar ilikuwa kituo kikubwa na Waarabu walivyokuja wakaoana na jamii za Tanganyika na ndiyo maana wanzanzibar wana asili ya kiarabu. Hivyo wanaojiita wa Zanzibar ni mchanganyiko wa wa Tanganyika na Waarabu. Wanzibar hivyo basi ni ndugu kabisa wa watanganyika na mipaka iliyowekwa na waingereza na waarabu haiwezi kuzuia watu kuwa ndugu. Miaka zaidi ya 4o sasa viongozi waligundua hilo na kuja na muungano na zanzibar walipewa baadhi ya haki lakini sio haki zote kwani sasa nchi ilikuwa moja ya Tanzania na sio mbili. Hakuna mtu mwenye akili yake anayetambua zanzibar kama nchi hii ni jina tu kuna nchi moja ya Tanzania na kisiwa cha Zanzibar na wanamwita kiongozi wao raisi lakini hatambuliki duniani. Kupunguza migongano hii Zanzibar ingefuta serikali na kuwe na serikali moja tu ingewasaidia zaidi ya sasa.
Mkuu.
Ni vyema ukajiunge tu na CCM..si unaelewa wao wana sera ya serikali mbili kuelekea moja?

CHADEMA na CUF wana sera ya serikali tatu.

Au uanzishe chama na platform ya kuleta serikali moja, nchi moja Tanzania.
Mkuu, Tanzania si jina la nchi...ni jina la kisanii tu.

Nchi zipo mbili Tanganyika na Zanzibar....au tafuta katika kutoka popote na kokote kumbukumbu za bunge la Tanganyika liliposema linaifuta nchi ya Tanganyika. Chombo hiki ndio chenye mamlaka ya kufanya hivyo au vipi?

Tafuta kumbukumbu katika sijui baraza la mapinduzi au baraza la wawakilishi sheria iliyofuta nchi ya Zanzibar..Wao ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo, au vipi?

Mkuu..Tanzania ni kiini macho tu cha Mwalimu na CCM. Hata muungano wenyewe uliitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kama Zanzibar ilibaki baada ya Muungano kwa muda wote huu huoni ni mwallimu tu ndio alibadilisha jina la Tanganyika kuwa Tanzania?

Tanga ipo, Arusha ipo, Mafia ipo, Mtwara ipo...ambalo halisikiki ni Tanganyika tu.

Kama bongo zetu zinafanya kazi vizuri yatupasa tufikiri, tusiendeleze unafiki wala usanii.
 
Wajitenge kutoka wapi? wajitenge na nchi ipi? wakati wao ndio wana nchi! wewe nchi yako inaitwaje? usiseme Tanzania, Tanzania ni Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, sasa Tanganyika iko wapi? Rais wake nani? Mawaziri wake wako wapi? Bunge lake liko wapi?

Imgekuwa kuna nchi nyingine basi Zanzibar "wangejitenga", ukweli ni kwamba hakuna pa kujitenga na tusijidanganye, wa Zanzibar walistaarabika zamani sana na wametuzidi ujanja wameififirisha Tanganyika na haipo. Na tutafanya na tutatimiza wayatakayo tukitaka tusitake kwani sisi ndio yatima. Huo ndio ukweli.
Mkuu.
Mengi hapa katika post yako ni challenge kwa sisi tunaoitaka Tanganyika irudi, isikike na itambulike kama ilivyokuwa kabla ya Muungano.
CCM wametutupia changa la macho kali lenye kuzifanya akili zetu zione marue rue.
Watu tunashindwa kuona usanii ndani ya jina hili Tanzania.
Tan(ganyika)Zan(zibar) na -ia zawadi kutoka kwa muhindi wa Tanga.
Leo imekuwa kosa la uhaini kuitaja Tanganyika.
Kwa sababu gani? Mwalimu na CCM walitufanya mazezeta ili tuamini kuwa hakuna muungano wa nchi mbili...
Nani anakubali kuwa kuna nchi inaitwa European Union? je kuna nchi inaitwa East African Community? je kuna nchi inaitwa AU?

Hata nchi ya UK wana muungano wa territories zenye majina yake...jikumbushe.

Tanzania kuna , "Tanzania bara" na Zanzibar..Are we that stupid?

Kama sote tunafahamu na kuona mantiki ya EU na EAC ..napata tabu kuwafahamu watu wanaosema Tanzania ni nchi moja...Usahihi ni kusema Tanzania ni muungano wa nchi Mbili...sasa vipi mbili zinageuka moja?

Ili tusichanganyikiwe, inabidi tuelewe pia kuwa Tanganyika na Zanzibar waliunganisha mambo kumi na moja tu na kuyaita mambo ya muungano na Tanganyika ilibakiza mambo kibao katika mamlaka yake na vile vile Zanzibar walibakiza mambo mengi tu katika mamlaka yao... Sasa hii nchi moja inawezekana kivipi?

Au ndio tunakubali mantiki (Changa la macho) ya Nyerere ya moja na moja ni moja au mbili?
Mwalimu alisema haiwezekani kuwa tatu!!!

Kwa wale wataalamu wa mambo ya mazingaombwe na kiini macho tafadhalini nisaidieni kuelewa vipi Tanganyika imepotea? kwa nini Zanzibar imebaki?
Na kwa vipi Tanzania inakuwa ni nchi moja?

Katika maelezo utakayonipa ,jaribu kuweka jazba pembeni na unafiki usiupe nafasi.
 
Who cares? waende tu!

Mkuu.
Wao wanataka waende ninavyofahamu mimi lakini sisi huku tumeshikilia kuwa Tanzania ni nchi moja.
Sisi tukitaka waende basi ni kama "kumsukuma mlevi ".
Inaonekana "viongozi" wetu wana siri yao ambayo hawataki sisi tuijue!
 
nauliza jamani kwanini watanganyika wengi ndo wanaoupenda muungano kuliko wazanzibar?
 
nauliza jamani kwanini watanganyika wengi ndo wanaoupenda muungano kuliko wazanzibar?
Mandi.
Sisi watanganyika wa JF majority hatuutaki Muungano huu CCM.
Huu ni Muungano ambao CCM ndio wameung'ang'ania at any cost ni kuwa umewasaidia na unawasaidia kubaki Madarakani.

Wananchi wengi kwa sasa wa "Tanzania bara" hata hawaelewi hizi habari za Muungano. Ugumu wa maisha hautupi huo muda kama wa wanaJf. Sisi tunajua tu CCM ndiyo inayotuadhibu.
Na wanaona CHADEMA ndio kwa sasa inayopiga "mdundiko" unaovutia masikioni mwao. Na CHADEMA ina sera ya Serikali tatu.

Muungano, mkuu Mandi ,ni bussiness ya CCM. Wananchi wala hawajui kama kuna Muungano. Sisi tunajua tuna nchi yetu inayoitwa Tanzania bara na karibuni hivi tutasherehekea miaka 50 ya uhuru wa "Tanzania bara".

Haya ya Muungano ni mchezo wa kuigiza baina ya CCM na Zanzibar.
 
Mkuu.
Mengi hapa katika post yako ni challenge kwa sisi tunaoitaka Tanganyika irudi, isikike na itambulike kama ilivyokuwa kabla ya Muungano.
CCM wametutupia changa la macho kali lenye kuzifanya akili zetu zione marue rue.
Watu tunashindwa kuona usanii ndani ya jina hili Tanzania.
Tan(ganyika)Zan(zibar) na -ia zawadi kutoka kwa muhindi wa Tanga.
Leo imekuwa kosa la uhaini kuitaja Tanganyika.
Kwa sababu gani? Mwalimu na CCM walitufanya mazezeta ili tuamini kuwa hakuna muungano wa nchi mbili...
Nani anakubali kuwa kuna nchi inaitwa European Union? je kuna nchi inaitwa East African Community? je kuna nchi inaitwa AU?

Hata nchi ya UK wana muungano wa territories zenye majina yake...jikumbushe.

Tanzania kuna , "Tanzania bara" na Zanzibar..Are we that stupid?

Kama sote tunafahamu na kuona mantiki ya EU na EAC ..napata tabu kuwafahamu watu wanaosema Tanzania ni nchi moja...Usahihi ni kusema Tanzania ni muungano wa nchi Mbili...sasa vipi mbili zinageuka moja?

Ili tusichanganyikiwe, inabidi tuelewe pia kuwa Tanganyika na Zanzibar waliunganisha mambo kumi na moja tu na kuyaita mambo ya muungano na Tanganyika ilibakiza mambo kibao katika mamlaka yake na vile vile Zanzibar walibakiza mambo mengi tu katika mamlaka yao... Sasa hii nchi moja inawezekana kivipi?

Au ndio tunakubali mantiki (Changa la macho) ya Nyerere ya moja na moja ni moja au mbili?
Mwalimu alisema haiwezekani kuwa tatu!!!

Kwa wale wataalamu wa mambo ya mazingaombwe na kiini macho tafadhalini nisaidieni kuelewa vipi Tanganyika imepotea? kwa nini Zanzibar imebaki?
Na kwa vipi Tanzania inakuwa ni nchi moja?

Katika maelezo utakayonipa ,jaribu kuweka jazba pembeni na unafiki usiupe nafasi.

Tunaitaka Tanzania yetu irudi, la sivyo tunarudi kwetu Uingereza, sisi tuliozaliwa kabla ya Uhuru ni British subject, mimi cheti changu cha kuzaliwa kinaonesha nimezaliwa Tanganyika, sasa Tanganyika yangu siioni, ina maana sina asili, na asie na asili ni mtumwa, kwa hiyo sisi ni watumwa wa Zanzibar. Wao wana nchi yao, bendera yao, na wakiwa nje ya Tanzania huwasikii hata siku moja kusema mimi nimetoka Tanzania. Wao husema nimetoka Zanzibar na dunia nzima wanawatambuwa. Nenda wewe mwenzangu na mie ukaseme mimi nimetoka Tanganyika.

Kweli kabisa, m-Scotch anasema katoka Scotland, M-Irish anasema katoka Ireland ingawa wote hawa wako katika himaya moja. MZanzibar akisema anatoka Zanzibar, hafanyi makosa, ana haki zote, mpaka vitambulisho vya uZanzibari wameshatoa na wanavyo. Sisi Jee?
 
Hivi sasa Viongozi wa Tanganyika wanafanya kila hila lakini mafuta ya Zanzibar yabakie kuwa ni mali ya Muungano huku gus ya songo songo na mineral yingine za Tanganyika zibakie kuwa za Tanganyika kutokana na kisingizio cha mafuta ya Zanzibar yamo kwenye Muungano hata kama yalingizwa kimakosa.

Hii ni yale maswala ya mivutano ktk kutatua kero za Muungano kwa kuingiza mambo kutoka 11 mpaka 22 bila ya kukaa pande mbili za Muungano kujadili mambo yaliomo ktk (Article of Unio) nimangap.

Kwa nini wenzetu wanakuwa wazido kuondocha mambo yenye utata ktk Kero za Muungano ili kuimirisha Muungano wenyewe? jawabu la hili nikuwa wenzetu hawakuwa na nia safi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ispokuwa ni kujifanya wajanja wa kunyakuwa rasilimali za Zanzibar na kuitawala Zanzibar kwa kutumia upepo wa sera za chama tawala na itikadi za chama.

Tunawaomba viongozi wetu wa smz hususani ccm/smz washe tafauti za chama na wajali maslahi ya ndugu zao na watoto wao wzanzibar ili kulinusuru taifa la watu wa Zanzibar lisinakamia ktk jindamizi la Sera na itikadi za chama ambazo ndio zenye kulinda Muungano Zanzibar hivi sasa. Zanzibar hivi sasa inahitaji Wazanzibar wenyewe wazalendo na wenye mchikamano wa kuokowa Zanzibar yetu tuipendayo na kizazi chetu cha badae kukijengea mazingira mazuri na kuwashia urisi endelezi kwa vijukuu vyao vya badae.

Hii wanayo tufanyia wenzetu sio haki na sio udugu wa Muungano hii nikuuwa Muungano kutokana na Zanzibar nchi yenye watu kidogo na ardhi ndogo kubebeshwa mzigo mkubwa na kila siku bada ya kupungua gero za Muungano basi zinazidi kukuwa tunatoka katika Bad na kwenda katika Warst.

Mimi sioni sababu kwa jinchi kubwa la Tanganyika lenye uchumi mkubwa na ardhi kubwa yenye watu millioni 44 kungagania uchumi mdogo wa Zanzibar kama vile Bandari na ukuchanyaji wa mapato ya Zanzibar, hii ni choyo tu na roho mbaya ambayo wenzetu wanayo.
Kama kweli walikuwa na nia safi ya kuendeleza Muungano udumu na kuimarika ilikuwa wenzetu waisaidie Zanzibar kimaendeleo na kiuchumi sio wafanye ujanja ujaja wa kuibana koo Zanzibar isikuwe kiuchumi na kimaendeleo hichi ni choyo na husda, kama sio hivyo basi wasingali uwa Bandari ya Zanzibar ambayo ndio uti wa mgongo wa Wzanzibar.

Tunawaoba Wawakilishi wetu na Baraza lake ambalo ndio Bunge la Zanzibar na sauti ya Wanyonge Zanzibar washe tafauti zao na panapokuja swala la haki za Zanzibar kuwa kitu kimoja na kulinda rasilimali za zanzibar.

Hivi sasa Tanganyika wanafaidika kwa menaral Zao na Zanzibar hawafaidiki chochote na mineral hizo sasa vipi leo tukubali ku-sacryfy rasilimali zetu na power ya nchi yetu kwa jindamizi la Tanganyika yenye kuvaa Koti la Tanzania?.

Vipi tuendelee kukumbatia bomu lililokwishwa tolewa fuse, hivi sasa Tanganyika inaomba misada mingi tu kwa jina la Tanzania, zanzibar ikifanya hivyo huombiwa wanaingilia mambo ya Muungano swala la mambo ya kigeni ni la Muungano? mbona wao huomba misada kwa jina la Tanzania lakini ikifika nchini hutumika kwa jina la Tanganyika? sio misada yote Zanzibar hupewa %4.5, kuna misada mingi tu huombwa kwa jina la Tanzania lakini Zanzibar haiambukii kitu.

Sasa kusema Samuel sita kuwa Serekali 3 sio solution au kurudi kwa Tanganyika kutaleta ushindani hii mimi nasema sio kweli na ni unafiki na roho mbaya tu yakuzani bado viongozi wa SMz niwatu wa kuburuzwa na kuwaburuza Wzanzibar,tunasema Generatio hio haipo tena hivi sasa, tutazisimamia haki zetu zote kikamilifu.

Jee hafahamu sita kuwa Zanzibar imeungana na Tanganyika? vipi leo aseme Tanganyika ikija itakera, hii nikuonyecha kuwa Muungano ni jindamizi la ujanja wa kuitawala Zanzibar ki-imla kwa hio wajibu wa Viongozi wetu na Wzanzibar kwa jumla nikusimama kidete na kutetea ardhi yetu kwa vizazi vyetu vya baadae.

Mimi nasema kama viongozi wa Tanganyika watakaataa mfumo wa Serekali tatu basi kuendelea na Muungano SMz nikujizonga na itafika hadi tutashindwa kujizongowa.

Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote popote pale walipo.
 

Attachments

  • tanzania1.jpg
    tanzania1.jpg
    25.3 KB · Views: 64
Tanganyika kufanya biashara ya kutamani mafuta ya Zenj ni sawa na tembo kufanya mapenzi na mbu!!!
 
Watu wengine sijui akili zenu ziko wapi...

Kuna post kibao hapa zinaelezea tatizo la Muungano na hadi sababu za huo Muungano, sasa sijui toka ujiunge na JF hujawahi kuzisoma au? Hakuna mtu mwenye mzuka na huo Muungano, namaanisha kwa sie watanganyika. Kama ulimsikiliza Lissu wiki iliyopita utakuwa umeelewa nini nasema. Kwa taarifa yako hakuna mwananchi wa kawaida ambaye ukimuuliza Muungano wetu na Zanzibar unatusaidia nini akasema tuna kitu gani cha maan atunapata zaidi ya kwamba "Nyere alisema tuuenzi Muungano"

-Kwanza tukija kwenu mnatubagua, mnatuita majina ya ajabu ajabu,
-hatuwezi kumiliki ardhi na hata tukimiliki mali siku zote mnakuwa wa kwanza kutuita wezi.
-Hamtaki tuoe mabinti zenu (hasa wapemba).
-Mna ubaguzi wa kidini kila siku hamuachi kupiga vita ukristu zanzibar
-Mnajihisi nyie kama vile ni waarabu, cha ajabu hata waarabu halisi wanawaona mambwiga tu.
-Wavivu, hampendi kufanya kazi mnataka kuishi mko arabuni vile mnasahau wenzenu wako level nyingine.

Hizo sababu chache na ukichanganya kuwa nyinyi kwa nyinyi mnadharauliana (Pemba vs Unguja) zinanifanya niamini siku tukiamua tupulize baragumu Muungano uvunjike tutaanza kuhesabu siku kadhaa kabla hakijalipuka na tutaanza kupokea wakinbizi kadhaa toka visiwani.


 
Ni kweli kabisa Mkuu twatowa denda - TUKILALA bungeni na kuota mafuta ya Zanzibar.

Mrema%2Bchapa%2BUsingizi%2B3%2B%25282%2529.jpg
 
Muungano waliingia makubaliano Nyerere na Karume sisi wengine hatujui kwa nini huu muungano upo. Km vipi si mtmie peoplez power iliyomtoa sultani? mkibaki mnalalamika tuuu hakuna atakayewasikia wakati wenzenu wanajaza matumbo yao tuu. tena sidhani km mnatutendea haki mnaposema wa bara wananufaiki raia hatunufaiki na Zenji sababu hata tukija huko kwenu hatutapeewa ardhi, tukifungua biashara mnatuchomea moto lkn nyie wenzenu walioko huko wana ardhi kubwa tu wana majumba washajenga, wana miradi mikubwa tu huku, washaOA huku, kwa hiyo nadhani hayo mafuta yenu(ya Kufikirika) sijui km sisi tunanufaika/Tutanufaika nayo zaidi ya nyie mnavyonufaika huku bara sasa hivi au tuseme tu TANGANYIKA inawale vizuri sana kuliko dhana yenu potofu ya kujivunia mafuta ambayo hatujajua km yapo ni ndoto tu na kujipa matumaini.
 
Zanzibar hakuna mafuta hata ya taa!. Mimi nimeona study hapa Texas za TZ kuna mafuta maeneo ya Mtwara, Lindi na gas maeneo ya Tanga na siyo Zanzibar
 
Zanzibar hakuna mafuta hata ya taa!. Mimi nimeona study hapa Texas za TZ kuna mafuta maeneo ya Mtwara, Lindi na gas maeneo ya Tanga na siyo Zanzibar
Wazanzibari wanaota ndoto za mchana na wamekuwa wanapayukapayuka ovyo kuhusu mafuta hewa utafikiri wameshayachimba!
 
Muungano waliingia makubaliano Nyerere na Karume sisi wengine hatujui kwa nini huu muungano upo.
Kwani Wazanzibari waliulizwa kwanza kama wanataka Mapinduzi au la, watu walipindua utawala wa Sultani uliokuwepo kwa zaidi ya karne moja? Mbona hata EAC wananchi hawajaulizwa kuwa tuingie au la? Unapokuja Muungano watu hukimbilia hoja ya kushirikishwa wananchi ili mradi tu wapinzani wa Muungano wana lao jambo, ie ulevi wa madaraka!
 
Ni kweli kabisa Mkuu twatowa denda - TUKILALA bungeni na kuota mafuta ya Zanzibar.
Mrema%2Bchapa%2BUsingizi%2B3%2B%25282%2529.jpg
Huyu ni Mrema pekee aliyelala na kutoa denda Bungeni! Sasa hizi kauli za "twalala," "twatowa denda," zinatoka wapi?
 
Zanzibar hakuna mafuta hata ya taa!. Mimi nimeona study hapa Texas za TZ kuna mafuta maeneo ya Mtwara, Lindi na gas maeneo ya Tanga na siyo Zanzibar
Si wanasiasa wala wataalam wa Zanzibar waliowahi kutoa data za kuaminika kuhusu hayo mafuta ya Zanzibar. Sehemu nyingi za nchi hii zina dalili za mafuta lakini inabidi ujue yako kiasi gani (makisio ya reserves), yanaweza kudumu kwa muda gani, je, yanaweza kuchimbwa kibiashara? (mafuta ya baharini yanahitaji uwekezaji mkubwa mno wa teknolojia). Vile vile msisahau kuwa Zanzibar yenyewe iko kwenye maji ya Tanganyika kwa sheria za kimataifa (national territorial waters laws). Hivyo mafuta yaliyo karibu na Pemba yako karibu na Tanga vile vile. Tunaweza na sisi kudai ni ya kwetu. Kwa hiyo suluhisho ni kuzungumza na ku-share. Halafu kuna wajinga wanasema Zanzibar haifaidiki na gas ya Songo Songo na maliasili zingine. Hivi huo umeme mnaoupata kwa dezo unatokana na nini? Halafu kuna formula ya kugawana mapato kati ya Zanzibar na Muungano. Hivyo Zanzibar inapata share ya mapato yanayotokana na raslimali za Bara. Pamoja na yote hayo mimi binafsi sitasikitika hata kidogo muungano ukivunjika. Tumepata viongozi wabovu na maamuzi mabovu kutokana na wingi wa wajumbe wa Zanzibar ndani ya vikao vya CCM na katika Bunge.
 
Back
Top Bottom