Kwanza kabla ya yote, nakupongeza kwa kuiweka mada hii ambayo ni nzuri na inastahiki kujadiliwa, na inajadilika. Tattizo lake ni kuwa "font" pamoja na "paragraphing" - unaweza kusoama na kurejea bila kutaka sehemu moja mara tatu kwa jinsi aya zilivyokaliana. Inakuwa shida kuisoma.
Kuhusu "kuwapa nchi yao"
Hapa Wakuu,
Saint Ivuga na
EMT mnazungumza lugha moja ya hapo kwenye red. Mimi sioni kama ni hivyo mnavyosema, na kama ni kweli haijathibitika kama kweli "idadi kubwa ya Wazanzibari hawataki Muungano". Tusichukulie kelele za Muamsho kuwa ni kauli ya Wazanzibar wote.
Imani yangu ni kuwa, hakuna Mzanzibari na akili yake timamu, anayekataa Muungano kwa kuzingatia pros na cons za kuwepo au kuvunjika kwake. Wale wanaojidanganya na kudanganyika kuwa "Zanzibar
ikipata mafuta ndio itakuwa ukombozi wao kimaisha", wanapaswa kuangalia mifano hai ya majanga yanayozikumba nchi za Kiafrika kutoka na mafuta na maliasili. Tanganyika ni mfano hai - kwenye malighafi ndiko umasikini ulikokithiri -. Kwengine ni Guienea Equatorial, Sudan, Libya (kwa sasa baada ya Wazungu kuingilia kati). Malighafi zisiposimamiwa vyema (na si rahisi kusimamia kwa kuwa hatuna teknolojia), badala ya kuwa neema inakuwa nakama.
Kuhusu suala la kutotaka Muungano, naamini kuna sehemu ya Watanganyika wana msimamo sawa na hawa jamaa wa Muamsho...hawautaki Muungano...lakini zaidi kwa jazba au bila ya kufikiri. Watu wowote watakaokuwa, wawe muamsho au mchemsho, wakipiga kelele hawa, hatupaswi kuwaona wanawawakilisha Wazanzibari wote, kama ambavyo wale wanaodai "Kusini na Kaskazini yao au Mashariki na Magharibi yao" hawawawakilishi Watanganyika wote.
Kwa kufupisha hadithi, ili kujua kama kweli Watanzania (Watanganyika na Wazanzibari) wanataka au hawataki Muungano sio kuachia vikundi vya akina muamsho kuwa mdomo wa watu wote. Naamini kama kutaitishwa kura ya maoni ya MUUNGANO NDIO au HAPANA, WATANZANIA waliowengi wataamua HAPANA. Lakini kama kutakuwa na kura ya maoni yenye options za Mambo yanayotakiwa yawemo kwenye Muungano na Serikali ngapi ziwemo kwenye Muungano huo, WATANZANIA wengi wataukubali.
Kwa ufupi, naamini wanautaka Muungano, wanachokataa ni mizengwe, kutokuwepo kwa uwazi na kero ziazotokana na aina ya Muungano uliopo.