Mjadala wa Mafuta na Suala la Muungano

Mr.Froasty said:
Hizo report na data nilizotoa hapo juu ni za january 2010.Ukitupia macho vizuri utaona kuwa company imesuspend activity kutokana na SMZ/BLW kuweka mguu.

Hivyo kero za muungano zimekuwa kizingiti za kupatikana nishati hiyo, na hilo ni jukumu la JK alituahidi kuzitatua...hadi sasa haijaondolewa hata kero moja!

Mr.Froasty,

..nadhani ripoti ya yule Mshauri Mwelekezi itakuwa na majibu ya maswali tunayojaribu kuyapatia ufumbuzi hapa. sijui kama unakumbuka ile thread ambayo tulianza kudadisi masuala ya sheria za bahari. naamini thread ile ilikuwa inakwenda vizuri sana.

..Baraza la Mapinduzi tayari limeishapitisha uamuzi wa kuondoa mafuta ktk masuala ya Muungano. kutokana na uamuzi huo Zenj sasa hivi wako ktk process ya kuanzisha ZPDC, shirika lao la mafuta. kwa msingi huo shughuli zote za exploration zinasubiri kuanzishwa kwa shirika hilo Zenj.

..kuhusu JK kilishughulikia suala hilo ilipaswa upelekwe mswada wa marekebisho ya katiba kwenye bunge la Jamhuri Dodoma. lakini kama JK hajafanya hivyo bado wabunge toka Zenj walikuwa na nafasi ya kupeleka hoja binafsi kwamba mafuta yaondolewe kwenye muungano. sasa unaweza kudai JK is dragging his feet kwasababu hana nia njema na Zenj, lakini what about wabunge wazawa wa Zenj ndani ya bunge la Jamhuri? ni kitu gani kinawazuia kuwasilisha hoja binafsi?
 
Hao wabunge wazenj mie nilishawahi kusema kwenye forum fulani kama ningekuwa na uwezo ningekwenda na kuwazaba vibao kama alivyopata Mwinyi...

Well kuhusiana na report ya Director wa Opec sina....ila nilifuatilia video alivyokuwa akitoa hoja yake.Report hiyo kwangu haiwezi kuwa na ukweli sana, kwa vile research hiyo wazenj hawakushiriki inavyotakiwa.

Hivyo mimi nimeshatake stand kwa kutumia research za kitaalamu nilizosoma, na stand yangu nadhani utakuwa unaijua kuwa Mafuta si suala la muungano kama ilivyo dhahabu/almasi na mafuta iwe hivyo hivyo....

The matter of fact, mie nataka mjadala mzima wa muungano upelekwe kwa wananchi wakautolee maumuzi...Unfortunately, really sorry bout that...But this is what I stand for, and I dont really think the union as it is right now has any benefit to my country nor to my people.
 
Saturday, 03 July 2010 07:18

Habel Chidawali, Dodoma

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, amesema mafuta hayawezi kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, kama ilivyotamkwa na Rais Jakaya Kikwete na Amani Abeid Karume.

Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na shinikizo la Wazanzibari kutaka mafuta, yaondolewe katika orodha ya mambo ya chombo hicho.

Jaji Werema amesema hakuna jambo lililoko juu ya sheria na kwa msingi huo, mafuta bado yako katika orodha ya Muungano hadi hapo mchakato utakapopitia hatua zote muhimu.

Mwanasheria huyo alizitaja hatua zinazopaswa kufikiwa kuwa ni pamoja na kupitia katika chama kinachongoza serikali ambacho kitatoa mapendekezo na kuingiza katika mjadala wa Bunge.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyasema hayo jana bungeni, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mohamed Rajabu Soud (Jang'ombe-CCM),aliyetaka tamko serikali kuhusu kauli za viongozi wawili hao mafuta yataondolewa katika orodha ya Muungano kabla ya kufikishwa bungeni.

"Mambo hayo hayategemei wala hayaangalii ukubwa wa kambale wala sharubu zake, ni lazima yafikishwe katika Bunge kwa kuwa ni masuala ya kisheria na yatafika bungeni baada ya mchakato kupitia kwenye vyama," alisema Werema.

Katika swali lake la msingi, Hafidh Ali Tahir (Dimani-CCM) alitaka kujua majibu ya serikali kuhusu suala la mafuta kuondolewa katika orodha ya Muungano.

Mbunge huyo pia alitaka kujua msimamo wa kuhusu maneno makali yaliyotolewa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wa kupitisha muswada kuhusu suala hilo.
.
Akijibu swali hilo , Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mohamed Seif Khatibu alisema serikali haina jibu la ndiyo au hapana kuhusu suala la mafuta kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano.

Kuhusu kauli za maneno makali yaliyotolewa na wajumbe wa baraza la wawakilishi, waziri alisema hana taarifa hizo na wala serikali haijui kama maneno hayo yalitolewa huko Zanzibar .
 
Saturday, 03 July 2010 07:18

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, amesema mafuta hayawezi kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, kama ilivyotamkwa na Rais Jakaya Kikwete na Amani Abeid Karume.

Inatisha, mwanasheria mkuu wa serikali anabishana na mwajiri wake tunaenda wapi?

Ina maana hakuna consultation kati yao au vipi.

Ikienda mahakamani mahakama itasema hilo suala la kisiasa liende bungeni.

Leo ikitokea njaa au maafa walahi waziri atasema hilo ni suala la kisiasa ilikliende bungeni.

Hukumu ya kesi ya mtikila tusiifurahie sana itatuweka pabaya sana, leo, kesho na kesho kutwa.
 
Kwani katika katiba ya Jamhuri ya Muungano kuna Suala linalohusu (Mafuta)? Nataka munieleweshe na ikiwa hakuna kwanini Seriakali ya CCM inaliingiza Hili Suala la Mafuta na Mambo yanyohusu Muungano wa Nchi hizi mbili? Mbona hiyo inaonyesha Serikali ya CCM inataka kufanya mambo ya Kudhulumu?
 
Wewe unasema hayawezi kuondolewa wewe kama nani? Hizo sarakasi zenu za ghilba (wenyewe mnaita sheria) zisiwape kichwa cha kutaka kuamua mambo yasiyowahusu.
 
serikali yetu sasa kama mnara wa babeli... eniwei, nategemea sheria zitabadilishwa mafuta yasiwe suala la muungano. nadhani werema amesema aliyosema kutokana na katiba ilivyo sasa
 
Kwani katika katiba ya Jamhuri ya Muungano kuna Suala linalohusu (Mafuta)? Nataka munieleweshe na ikiwa hakuna kwanini Seriakali ya CCM inaliingiza Hili Suala la Mafuta na Mambo yanyohusu Muungano wa Nchi hizi mbili? Mbona hiyo inaonyesha Serikali ya CCM inataka kufanya mambo ya Kudhulumu?

Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa mabadilko inabainisha katika Ibara ya 4 kama ifuatavyo:

" 4-(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenyen mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.

(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.

" (3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa katika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyoko mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na Mambo yasiyo ya Muungano ambayo ni mambo mengine yote yasiyo Mambo ya Muungano.

Mambo ya Muungano:

Orodha ya mambo ya Muungano yamebainishwa katika Nyongeza ya Kwanza kwenye Katiba ambayo inarejea Ibara ya 4 ambapo katika kifungu cha 15 inasomeka kama ifuatavyo:

" 15. Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia."

Uamuzi Juu ya Mambo ya Muungano

Uamuzi juu ya mamno ya Muungano kwa mujibu wa ibara ya 98 ya Katiba umeachwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuondoa suala la mafuta katika orodha ya mambo ya Muungano, Katiba inataka hoja hiyo iwe imeungwa mkono na theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Visiwani. Katiba inasome kama ifuatavyo Katiba Ibara ya 98 (1)(b) ikisomwa pamoja na Nyongeza ya Pili:

" 98.-(1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii kwa kufuata Kanuni zifuatazo:-

(b) Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba hii au masharti yoyote ya Sheria yoyote yanayohusika na jambo lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika Orodha ya Pili kwenye Nyongeza ya Pili iliyoko mwishoni wa Katiba hii, utapitishwa tu iwapo utaungwa mkono kwa kura za Wabunge ambao idadi yao haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Zanzibar.

ORODHA YA PILI
(Imetajwa katika ibara 98 (1) (b))

Mambo ambayo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono na
theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi
mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Visiwani.
1. Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano.
2. Kuwapo kwa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.
3. Madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
4. Kuwapo kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
5. Madaraka ya Serikali ya Zanzibar.
6. Mahakama Kuu ya Zanzibar.

7. Orodha ya Mambo ya Muungano.

Hili suala ni miongoni mwa mambo yanayotia wasi wasi. Mimi sitajadili kuhusu werema maana huyo ni mteule wa rais na kazi yake kubwa ni kulinda maslahi yake binafsi na bosi wake. Hakuthibitishwa au hapaswi kuwajibishwa na chombo chochote kile. Kwani Hosea si amefanya madudu ya kulinda wezi, si bado yupo na anapeta tu,tena ni yeye anakamata walimu na wauguzi wanaochukua sh 200 kukimu njaa.
Hivi si huyu werema alimpelekea rais mswada fake wa uchaguzi,amefanywa nini. Huyu bwana anadhalilisha sana taaluma ya wanasheria.
JF kwani hamkumbuki hata jaji mkuu amepeleka kesi iamuliwe na bunge, alifanya vile kwasababu hukumu original ingemuumbua bosi wake,sasa baada ya october si bosi angemteua mtu mwingine!!!!

Ok,suala la mafuta mimi nasema ni ya wazanzibar kama hawataki kuwepo katika muungano. Lakini mafuta yapo katika ardhi[kama yapo] na ardhi ni ya muungano ndio maana wamejenga bara. Wakiondoa mafuta, good! lakini waambiwe ardhi si suala la muungano pia!
Pia waambiwe ajira si ya muungano, waondoke kule wizara ya afya na fedha,tena wanavyeo tu. Warudi wakashughulikie mafuata watuachie tangnayika yetu.
Wasiruhusiwe kugombea ubunge bara kama Dr mwinyi.
Wabunge wa zbar ndani ya bunge la muungano wagharamiwe na SMZ na si kodi zetu.
Mwisho wazanzibar watuambie wanachangia kiasi gani katika muungano maana bajeti yao ni Billion 500 sawa na wizara ya elimu ya bara.
Wa zenji watuambie hivi idadi ya 1.8 M haioni inafaidika na soko la watu milioni 40. Leo wafanyabiashara wote wa zenj soko lao ni bara sasa wakiweka mtimanyongo nani ataumia. Nasema hivi kwasababu mfanyabiashara wa bara kwenda kufanya kazi zenji si afadhali aende Morogoro mjini 2 M people.
Wana JF let us tell these people black and white,they are the most beneficiary of the union.Period.
 
Sio kweli kwamba Znz inafaidike saaana na muungano, umaskini uliopo kule sioni kama unajustify hiyo 'faida'.

In actual sense, nadhani Znz ikiendelea na trend za sasa za kuwasikiza hawa mafisadi wa CCM huko bara, hali itakuwa mbaya zaidi siku za usoni. Heri viongozi wa Znz waweke pembeni hoja za hawa mabwana, kikulacho ki nguoni mwako. Mafuta ni yenu, nyie na vizazi vyenu, nafasi ya kuitumia ndio hiihii, hamtopewa nyingineyo.
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NYONGEZA YA KWANZA
_________
(Imetajwa katika ibara ya 4)
Mambo ya Muungano
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
simu.
12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya
malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja
mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;
fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika
na fedha za kigeni.
13.Leseni ya viwanda na takwimu.
14.Elimu ya juu.
15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya
motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za
mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote
yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
18.Utafiti.
19.Utafiti wa hali ya hewa.
20.Takwimu.
21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine
yanayohusiana navyo.
 
Mbona wanasema katiba ya muungano haina power visiwani? Na ndiyo maana hata waziri mkuu mnayedai ni wa tanzania hana kazi ya kufanya unguja lazima amwangukie waziri kiongozi?

This whole thing is myth-I mean muungano.
We are just running and living in someone's figments of imagination.
 
Mbona wanasema katiba ya muungano haina power visiwani? Na ndiyo maana hata waziri mkuu mnayedai ni wa tanzania hana kazi ya kufanya unguja lazima amwangukie waziri kiongozi?
[/COLOR][/B]

Soma vizuri Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sio kukurupuka tu!
 
Na Mwinyi Sadallah | 16th March 2011

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kimeshangazwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuwa wazito katika kuliondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano, wakati Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshaamua kuliondoa suala hilo.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Ismail Jussa Ladhu, katika mkutano wa kukabidhi milango ya vyuma itakayowekwa katika nyumba za maendeleo Michezani kwa ajili ya kuzilinda nyumba hizo na wahalifu.

Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliamua suala la mafuta na gesi asilia kuliondoa katika mambo ya Muungano baada ya kupata baraka za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka vyama vya CCM na CUF.

"Inashangza serikali ya Muungano hadi sasa wamekuwa wazito kuwasilisha muswada wa sheria wa kulindoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano," alisema Jussa ambaye pia ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe.

Alisema kitendo hicho kinachelewesha harakati za Zanzibar kufanya utafiti na uchimbaji wa mafuta katika eneo la mwambao wa bahari ya kisiwa cha Pemba, sehemu ambayo inapewa matumaini makubwa ya kuwepo mafuta na gesi.

Alieleza kwamba hivi sasa ni mwaka wa pili tangu hatua hiyo kufikiwa na serikali tangu wakati wa uongozi wa Rais mstaafu, Amani Abeid Karume.
Hata hivyo, alisema wakati suala la mafuta na gesi asilia likiwa halijapatiwa ufumbuzi, Serikali ya Muungano imekuwa ikiendelea kufanya utafiti na gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara kupitia Shirika la Maendeleo ya Mafuta nchini (TPDC).

CHANZO: NIPASHE

MY TAKE:
Kwanini CUF ndio wanaokamalia saula hili kuliko serikali ya mapinduzi ya Zanzibar? Ina maana CUF hawataki muungano?

Wanajamvi hebu toeni maoni yenu.
 
Hii ndio inaitwa SIASA Burudan

Sauti gani ya CUF sasa hivi ambayo ikiongea itasikika angalau Znz kwenyewe tu??
Wana mpango gani na hayo mafuta??? Hali ngumu za maisha hawazioni???
Serikali ya Muungano si ndio hao hao Thithiem "walioolewa" nao Znz??

Au ni kwamba wamekosa hoja za kuongea ambazo zina maslahi kwa wananchi???
 
Cuf imeshinda Pemba zaidi ya CCM; kwahiyo Watu wa Cuf Pemba wanataka kujiendeleza kwa Mafuta hayo na Unajua Zanzibar sidhani wana Mafuta; kama ni Pemba sioni Tatizo kwa Tanzania Bara; Wapemba wengi wanaipenda Bara na Wanaishi Bara na Biashara zao.

So more Power to Pemba's sijui Wazanzibar watajisikiaje???
 
lAKINI KWA NINI CCM HAITAKI KUKUBALIANA NAO NADHANI KUNAHAJA YA KUWAACHIA MAFUTA YAO!
 
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Ismail Jussa Ladhu
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kimeshangazwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuwa wazito katika kuliondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano, wakati Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshaamua kuliondoa suala hilo.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Ismail Jussa Ladhu, katika mkutano wa kukabidhi milango ya vyuma itakayowekwa katika nyumba za maendeleo Michezani kwa ajili ya kuzilinda nyumba hizo na wahalifu.
Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliamua suala la mafuta na gesi asilia kuliondoa katika mambo ya Muungano baada ya kupata baraka za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka vyama vya CCM na CUF.

“Inashangza serikali ya Muungano hadi sasa wamekuwa wazito kuwasilisha muswada wa sheria wa kulindoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano,” alisema Jussa ambaye pia ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe.
Alisema kitendo hicho kinachelewesha harakati za Zanzibar kufanya utafiti na uchimbaji wa mafuta katika eneo la mwambao wa bahari ya kisiwa cha Pemba, sehemu ambayo inapewa matumaini makubwa ya kuwepo mafuta na gesi.
Alieleza kwamba hivi sasa ni mwaka wa pili tangu hatua hiyo kufikiwa na serikali tangu wakati wa uongozi wa Rais mstaafu, Amani Abeid Karume.

Hata hivyo, alisema wakati suala la mafuta na gesi asilia likiwa halijapatiwa ufumbuzi, Serikali ya Muungano imekuwa ikiendelea kufanya utafiti na gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara kupitia Shirika la Maendeleo ya Mafuta nchini (TPDC).
Suala la mafuta na gesi asilia liliondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano kufuatia maamuzi
 
Back
Top Bottom