Mjadala wa DOWANS ITV waibua mapya!

KAMA UMEANGALIA ITV, MKINGA ANATOJA MAJINA YA WATU BILA YA KUWA NA EVIDENCE
je kwanini ITV wanamualika MKinga mchochezi? kwanini anawachonganisha viongozi na wananchi?

what if Jk akiwafungia ITV na JF kwa kuleta uchochezi?

Hizo ndo habari ulizonazo za ki-intelijesia?
 
OOh! Please! Ametoa speech ya mwaka mpya he said nothing zaidi ya Gharama za umeme ni lazima zipande nakutupa story za Sudan etc etc. Kwani hakujua hilo la umeme wakati wa kampeni? mbona alidanganya wananchi? Raisi gani hana vision!!! He is suppose to see at least a little bit further asiishie on the tip of his nose. Unaweza mtetea sana lakini it wont help, watanzania wasio na umeme ni wengi, walioahidiwa pembejeo ni wengi na hawajapata, waliohaidiwa barabara za juu kwa juu ni wengi etc etc. Oh I forgot na wingi wa magari ndio kipimo cha maendeleo I guess itabidi yanunuliwe mengi zaidi, kwa kasi zaidi. Ha ha ha !!! He need to address issues that are important to Tanzania people no excuse!!

He will speak when he has something to say, not speaking because you want him to say something.

Anasubiri taarifa toka kwa watendaji wake ili awe na cha kusema.

Serikali haiendeshwi kwa pressure toka kwa anonymous mtandaoni.


 

Kama unataka rais afanye haya yote, basi hakuna sababu ya kuwa na baraza la mawaziri, makatibu wakuu wa wizara na wakurugenz wa idara za serikali na mashirika ya umma pia. Rais aliye madarakani atekeleze kila kitu, mwenyewe, ndio unavyotaka. If you know the concept ya delegation.

Halafu, kwa taarifa yako, usipende kumpa mtu side. Wengine hatuna vyama humu wala hatufuati mkondo wa wengi bali ukweli wa issue yenyewe.
Achana na hizo kauli za kutetea.

I am around.
 
He will speak when he has something to say, not speaking because you want him to say something.

Anasubiri taarifa toka kwa watendaji wake ili awe na cha kusema.

Serikali haiendeshwi kwa pressure toka kwa anonymous mtandaoni.

Acha uzushi.Anasubiri taarifa kutoka kwa watendaji wake ilhali kila asubuhi anapewa taarifa na TISS?Au unataka kusema akina Othman na Zoka sio Watendaji wake?

Na labda wewe si Mtanzania ndio maana unaropoka kuwa "serikali haiendeshwi kwa pressure kutoka kwa anonymous mtandanoni".Ina maana hujawahi kusikia vilio vya mamilioni ya Watanzania kuhusu mwelekeo wa nchi yetu na sintofahamu ya Kikwete na serikali yake?
 
KAMA UMEANGALIA ITV, MKINGA ANATOJA MAJINA YA WATU BILA YA KUWA NA EVIDENCE
je kwanini ITV wanamualika MKinga mchochezi? kwanini anawachonganisha viongozi na wananchi?

Kalale wewe hili jukwaa sio lako. Ng'ombe we!
 

Utetezi wa kibabaishaji huwa na lifespan fupi.Awali ulimtetea Kikwete kuwa anasubiri taarifa kutoka kwa watendaji wake.Sasa unadai kuwa Rais hawezi kufanya "yote hayo".Jinsi unavyo-present utetezi wako ni kana kwamba Kikwete alishikiwa mtutu wa bunduki kuteua watendaji wazembe ilhali ukweli ni kuwa uteuzi wake umeelemea zaidi kwenye ushkaji badala ya uwezi wa kiutendaji.

Haya tuambie basi,hiyo delegation ya madaraka ya Urais kakabidhiwa nani?ROSTAM AZIZ?

Halafu una utani mbaya sana wewe.Unakemea kwa kusema "achana na hizo kauli za kutetea" ilhali na wewe unatetea pia.And worse still,unatetea a bag full of empty air!
 
He will speak when he has something to say, not speaking because you want him to say something.

Anasubiri taarifa toka kwa watendaji wake ili awe na cha kusema.

Serikali haiendeshwi kwa pressure toka kwa anonymous mtandaoni.

Kumbe yeye si kiongozi mkuu au pilot wa nchi hii? wengine waseme ye ndio apate cha kusema? Huna hoja...
 

Katika issue nzito na inayogusa maisha ya watanzania wengi kama hii kauli au muongozo wa Rais ni muhimu.Ndio maana ya kuwa na kiongozi mkuu wa nchi.We vipi? Kama rais anaenda kumpokea mwendesha baiskeli mmoja kutoka shinyanga, Kutoa ufafanuzi wa fidia ya bilioni 94 sio muhimu? Are you thinking right?
 

Kwa vile mipaka ya nchi yetu iko so porous kiasi kwamba yeyote anayejiskia kuingia Tanzania anaweza kufanya hivyo- na hapo tukiweka kando ufisadi wa maafisa uhamiaji-inatuwia vigumu kuelewa kama baadhi ya wenzetu wanaotetea mambo ya kiuendawazimu ni Watanzania kweli au Banyamulenge!

Unasema nchi ina sheria!Unamaanisha sheria hizi zinazobagua kati ya wenye nacho na wasio nacho?Hizi zinazotofautisha adhabu kati ya Deus Mally na Chenge?
 

Fanya tafakari ya haya maoni yako kwa kurudia kusoma uliyoandika, utaona mwenyewe ulipo miss point
 
Siku yatakapoitishwa maandamano ya nchi nzima kuandamana kwenda kwenye ofisi za serikali ndipo Rais Mwizi atafahamu zipi ni mbivu. Tunisia leo wameweza, SA tuliwasaidia, Zimbabwe, Musumbiji, Angola nk. Chacha tumebaki menyewe. Hata Uganda na Congo tuliwawezesha.
 
2011 sijui kama tutaumaliza salama. Mungu tusaidie
 

Jamani wanaotaka kuangalia Mahojiano ya ITV gonga hapo juu kwenye link .. kila inapomalizika moja gonga ya pili nk. safi sana. Post ya Mzozaji hapo juu. Mods mnaweza kuweka hiyo link kwenye first post ... .... Thanks.
 
He will speak when he has something to say, not speaking because you want him to say something.

Anasubiri taarifa toka kwa watendaji wake ili awe na cha kusema.

Serikali haiendeshwi kwa pressure toka kwa anonymous mtandaoni.
Basi inavyoonekana hiyo taarifa kutoka kwa watendaji wake ataisubiri sana. Kwa hiyo huenda asiwe na chochote cha kusema.
 
Namsikia Rugemeleza akitaja JF kama source yake ya ripoti ya Dowans.

Kumbe tunayoyaandika hapa yanawafumbua macho Watanzania wengi katika sakata hili la ufisadi wa Richmond/Dowans. Hongera sana WanaJF. Mpaka kufikia kutajwa katika majadiliano makubwa kama haya si kazi ndogo na umaarufu wa JF ndiyo utazidi kuongezeka popote pale walipo wabongo duniani.

 
KAMA UMEANGALIA ITV, MKINGA ANATOJA MAJINA YA WATU BILA YA KUWA NA EVIDENCE
je kwanini ITV wanamualika MKinga mchochezi? kwanini anawachonganisha viongozi na wananchi?

unajua ni suala la kujiamini tu. Ndugu yangu kama una evidence za kutosha unaweza kumtaja yeyote na ukabaki na amani yako. Unaowataja hawatakufuata kamwe maana wanajua ukweli wa jambo unaloongelea. Mbona Dr. Slaa ameshawataja watu wazito akiwemo jk mwenyewe lakini mpaka leo kimya!!
 
Aaah ilikuwa balaa,JK avunje baraza au ajiuzulu.


Siyo tu avunje baraza la Mawaziri na yeye mwenyewe ajiuzulu maana ukimya wake katika sakata hili unatisha. Ukimya huu sijui unasababishwa na woga aliuonao kwa Rostam, dharau kwa Watanzania kama vile hajui kinachoendelea nchini kuhusiana na sakata hili la Richmond/dowans au ndiyo nini? Maana kakaa kimya kabisa inaudhi mno kiongozi wa nchi kuwa kimya kiasi hiki wakati kuna mjadala mzito ndani ya nchi yako unaendelea kuhusu malipo makubwa sana yaliyojaa ufisadi wa hali ya juu.

Akisha vunja baraza la Mawaziri na yeye mwenye ajiuzulu maana uongozi wa nchi ulishamshinda tangu awamu yake ya kwanza. Hatuihitaji kuendelea kuwa na kiongozi kama huyu kwa miaka mingine mitano.
 
Tanzania iko mbioni kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Wana JF tafadhali nisaidieni katika hili. Ni suala la ufisadi ndilo litakalotufikisha huko ama udini?. Na tufanyenini ili kuweza kuepuka janga hilo?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…