Mi nafikiri we ndo mchochezi, jamaa alisema mambo yako obvious na kama asingekuwa na uhakika asingesema. Pia mdogo wake mnyika alisema kama hao jamaa wanaona wamechafuliwa majina mbona hawaendi mahakamani?! Hivyo we ndo mchonganishi na ushindwe kabisa ulegeeKAMA UMEANGALIA ITV, MKINGA ANATOJA MAJINA YA WATU BILA YA KUWA NA EVIDENCE
je kwanini ITV wanamualika MKinga mchochezi? kwanini anawachonganisha viongozi na wananchi?
what if Jk akiwafungia ITV na JF kwa kuleta uchochezi?
kama umeangalia itv, mkinga anatoja majina ya watu bila ya kuwa na evidence
je kwanini itv wanamualika mkinga mchochezi? Kwanini anawachonganisha viongozi na wananchi?
What if jk akiwafungia itv na jf kwa kuleta uchochezi?
Sijakuelewa, umeshindwa kuweka hoja zako kwa maneno machache?Baada ya kufuatilia mjadala huu wa ITV yafuatayo ni machache niliyoyang'amua....
Ni wazi mjadala ulikuwa wa kichochezi zaidi kuliko elimishi.
Rugemeleza amejaribu kuwa mkweli zaidi na kuepuka siasa nyingi lakini pia hulka yake ya hamasa tele imemfanya kuwa anajichanganya mambo mengi. Mojawapo ni hili suala la mikataba kwenda bungeni huku akitambua kuwa mkataba unaongelewa hapa ni wa Dowans Vs Tanesco na sio wa nchi na nchi. Lakini zaidi ameshindwa kuonyesha ni jinsi gani serikali inaweza kuingia katika kesi hii. Vile vile Rugemeleza amejichanganya katika suala la mikataba kuingia bungeni kwa hoja ya kuwa hiyo itasaidia kuepuka mikataba mibovu wakati ambapo katika maelezo yake anakiri kuwa mkataba huo hauna tatizo katika vipengele vyake isiopokuwa uhalali wake na pia makosa ya serikali kukubali suala hilo kupelekwa katika mfumo wa sheria wa nje ambao ukweli ni kuwa unakiuka hata vipengele vya mkataba huo.
Hata hivyo ni wazi kuwa wakati wenzake walishadadia sana katika upande wa kisiasa wa suala hilo, ni yeye pekee aliyeweza kutuelimisha upande wa kisheria ambao ndio muhumu zaidi wakati huu tunajitahidi ujinusuru na janga hili.
Mkinga was just being Mkinga lakini ni wazi kuwa ushabiki wake katika siasa za makundi ya MTANDAO umemfanya ajichanganye kupita kiasi hivyo kufanikiwa kuhemusha hisia za watu wa kawaida na washabiki wa kisiasa lakini kushindwa kuwaelimisha wale wenye weledi na busara.
Kibamba ameendelea kujikuta akitumia kauli mbiu na ajenda za chama chake huku akijinasabisha na uanaharakati. Ukweli ni kuwa wakati hawa wote wamejitambulisha kuwa ni wanaharakati lakini maoni yao yameonyesha wazi jinsi gani mitizamo yao ilivyoathiriwa na uanachama, ufuasi na ushabiki wa vyama vyao zaidi ya maslahi ya Tanzania.
Kibamba ni mwanachama hai wa Chadema na pia Michael Dalali ambae naambiwa ni mdogo wa damu wa mbunge wa Chadema Mheshimiwa John Mnyika wakati Mkinga ni kada mfu wa CCM ambaye maslahi yake yameegemea katika kundi za Membe na Samweli Sitta dhidi ya Lowassa na Rostam Azizi.
Ni wazi kutokana na mchanganyiko huo ukijumuishwa na hulka ya kugubikwa na hamasa zinazozidi busara za Rugemeleza zimesababisha kukosekana na hoja makini ambazo zinngeweza kuwaelimisha watanzania zaidi ya kuhemusha hisia zao tu. Mchanganyiko huo pamoja na tabia ya muongoza kipindi Chuwa ya kuwa mshiriki wa kipindi kama ile ya Mzee Mwakwaia wa Kuhenga wa Channel Ten umekosesha haki ya watanzania kujua ukweli wa ndani wa sakata hilo ingawa umefanikisha kuongeza nguvu hoja na maslahi ya kisiasa katika sakati hili huku watanzania wakiendelea kukosa umeme na uchumi kuendelea kuzama. Ni wazi kuwa hiyo ni dhumuni kuu la wengi wa wanasiasa wetu nchini lakini ni wazi si kwa faida ya watanzania katika mizania ya maslahi ya muda mrefu
Nyie watu mbona mmeshindwa kupiga simu kutetea hoja zenu? wazungumzaji wamezungumza hoja zao na walisubiri mpige simu kupeleka hoja zenu na mkanyamaza kimya. AlaaaaaaaaaaMnatumia theory za relativity kumhukumu Rais. Hata kama kuna blunders zimefanyika hapa, lakini nchi ina sheria, kanuni na taratibu katika maamuzi.
Je, mwanasheria mkuu au ngeleja wana mamlaka ya kupitisha ulipwaji wa DOWANS? Nani ana uhakika kama DOWANS watalipwa au hawatalipwa bila kupitishwa na Bunge?
Nyie watu mbona mmeshindwa kupiga simu kutetea hoja zenu? wazungumzaji wamezungumza hoja zao na walisubiri mpige simu kupeleka hoja zenu na mkanyamaza kimya. Alaaaaaaaaaa
Tumewashika na tunawapeleka kwa watanzania sasa! wasitudanganye kwamba uchaguzi umekwisha tunyamaze wakati wanakomba pesa yetu wakati sisi twaendelea kukaa gizani. Eboooo enzi za ujinga kwisha tulipojua ile kauli mbiu ya HATUDANGANYIKIWamiliki wa DOWANZI wanaingia JF kimtindo
Theoretically inawezekana lakini practically Jk hawezi kugomea amri ya Rostam.Jamaa wanataka JK eti agome kulipa dowans!!! Hii imekaaje? Waziri mwenye hiyo dhamana anaemuwakilisha rais kashakubali tulipe!!??
Mkinga namaliza kwa kauli kali anasema NENO USIOGOPE LIMEANDIKWA MARA 350 KWENYE BIBLIA ,KIKWETE NA SERIKALI YAKE WASIOGOPE WAWATOE MAFISADI NA KUWACHUKULIE HATUA.KIKWETE ATAENDA JEHANAMU AKIENDELEA KUOGOPA MAFISADI
NAHISI ANAFAIDIKA AU MNAONAJE WADAU?????????
Kama mchochezi. Rostam ambaye alisema anaingiza Dola 64,000 per hour anaweza kuwajiri mawakili 128 kama kina Mkono ambao wanacharge dola 500 kwa saa,around the clock.KAMA UMEANGALIA ITV, MKINGA ANATOJA MAJINA YA WATU BILA YA KUWA NA EVIDENCE
je kwanini ITV wanamualika MKinga mchochezi? kwanini anawachonganisha viongozi na wananchi?
what if Jk akiwafungia ITV na JF kwa kuleta uchochezi?
KAMA UMEANGALIA ITV, MKINGA ANATOJA MAJINA YA WATU BILA YA KUWA NA EVIDENCE
je kwanini ITV wanamualika MKinga mchochezi? kwanini anawachonganisha viongozi na wananchi?
Mnatumia theory za relativity kumhukumu Rais. Hata kama kuna blunders zimefanyika hapa, lakini nchi ina sheria, kanuni na taratibu katika maamuzi.
Je, mwanasheria mkuu au ngeleja wana mamlaka ya kupitisha ulipwaji wa DOWANS? Nani ana uhakika kama DOWANS watalipwa au hawatalipwa bila kupitishwa na Bunge?
Kwanini Rais anakimbia ku-address issues zinazosumbua watu vichwa? Kwanini anakwepa zile issue zilizo na mijadala mikali kama ya DOWANS, RADA etc. Raisi ndio anatakiwa arudishe mindset za watu ziwe kwenye line moja, ukiona baraza lako linatofautiana kwenye sensitive issues solution sio kukaa kimya. Uongozi sio kuhudhuria sherehe ni pamoja na kuwa tayari na constructive arguments na kuweza kuzi-settle, ili wananchi wako wakuelewe na wawe na imani na wewe. Kama ni haki DOWANS walipwe aje atueleze kwanini: na pia apeleke shauri hilo kwenye baraza la mawaziri ili lizungumzwe! Mimi huyu mtu ananishangaza kabisa yaani ni kama vile watoto wanabishana kuhusu kitu alafu mzazi anaingia mitini then who is incharge of the house?