Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mkuu Imany John tumeshalisema hapa kuwa hizi ni data tuu za kwenye karatasi
Hapa inatakiw atuambiwe mafanikio halisia sio data ambazo wanapika kuwaambia wafadhili oneni tunavyotoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo
Oneni tunavyoboresha sekta ya afya (kwa kutoa vyandarua)
Oneni tulivyotenga budget kwa ajili ya kuongeza majaji na mahakimu
Nenda kwenye uhalisia umuone huyo judge au hakimu aliteuliwa anahudumia wilaya zaidi ya mbili na usafiri hana
Hospitali zipo hakuna dawa na madaktari wenyewe ndio hao wako kwenye mgomo baridi

Kuhusiana na swala la shule ni uwongo mtupu,yani hata chaki mashuleni ni kitendawili kinachosubiri mwekezaji aje kukitegua.

Maji safi yapo?
Umeme wa kuaminika umepatikana lini toka mjomba aingie madarakani?
 
Last edited by a moderator:
lakini Matola nae majibu yake yamekuwa Shallow sana.
angejibu categorically kama mwenzake alivyofanya ila kwa kifupi.
nafikiri swala la internet limemzingua kwa kiasi fulani.
 
Mjadala huu unafurahisha sana maana naona kama Zomba kaamua kwenda kwa mtindo wa Faiza Foxy
mkuu kumbe hicho umekiona.....amezitaja failure za nyerere na mkapa,halafu anawasifu mwinyi na kikwete......this guy is not serious with his data,sources zake hazina new version.
 
swali 1. ni kwa nini utawala wa raisi kikwete umegubikwa na hsutuma za rushwa na ufisadi? na je kwa mtizamo wa zomba ni kweli kikwet kama raisi hana makucha ya kuwadhibiti hawa wala rushwa? kama anayo kwa nini hali iko hivi na kama hana kwa nini asiachie ngazi

swali la 2. raisi kiwkte kwa kiwango kikubwa ameshindwa kuboresha sekta ya afya na kwa kuzingatia mvutano uliopo na na madaktari na hivyo wengi wameamua kuondoa na kwenda nje ya nchi. Nini maoni ya zomba katika hili. ni kweli haiwezekani kuboresha mazingira na malipo ya wafanyakazi wa sekta ya afya?


swali la 3. kwa maoni yako zomba ningependa kujua je demokrasia inakua au inadidimizwa nchini? na vipi kuhusu haki za binadamu je serikali ya kikwete inajali haki za binadamu? jibu swali hili kwa kutumia mifano hai
 
mimi naomba tu nimuulize zomba swali...je ameoa ? au ana mchumba.au g/f maana naona hayo mnayomuuliza ni kama kutafuta mashariki magharibi hapa copu &paste...loh!@mwali
 
Last edited by a moderator:
Mkuu First Lady,

There is only one mdahalo. This thread is for all those who want to comment in relation to the now ongoing mdahalo of the provided link in the first post of this thread.

This link is also intended to post comments from all members for questions intended for zomba or Matola in relation to the way they have commented on the subject matter.
 
Last edited by a moderator:
Zomba, hizo takwimu hazielezei hali halisi, masuala ya wazee bora hata usingeyacopy, yaache maana ukiacha wazee wanaoteseka wa iliyokuwa EAC, fuatilia kambi za funga funga na kule kigamboni uone namna gani ccm haijaweza kuhakikisha maisha ya wazee yanalindwa na mchango wao wakati wa ujana unathamini wakati hii
 
zomba katiririka vibaya kamwaga data mpaka PC ya matola imegoma...
 
mimi naomba tu nimuulize zomba swali...je ameoa ? au ana mchumba.au g/f maana naona hayo mnayomuuliza ni kama kutafuta mashariki magharibi hapa copu &paste...loh!@mwali
 
Last edited by a moderator:
lakini Matola nae majibu yake yamekuwa Shallow sana.
angejibu categorically kama mwenzake alivyofanya ila kwa kifupi.
nafikiri swala la internet limemzingua kwa kiasi fulani.
unajua nini mkuu.....kuongelea utawala wa jk hauhitaji uwe na div 1 point 3......kila mtu anaona....matola he's very smart compare to zomba......

pili hatuhitaji maelezo mareeeefu ya bajeti za mof na hotuba za mwisho wa mwezi.....

mfano....zomba atuambie utawala wa dr kikwete umefanya lipi kwenye slogan yao....maisha bora kwa kila mtanzania.....
 
Mwali swali langu ni kuwa...Kikwete amefanikiwa vipi kutekeleza kauli mbiu za "ajira milioni moja kwa vijana" "kilimo kwanza" ?
 
Last edited by a moderator:
7. Kuimairisha upatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu na wazee


  • Kukamilika kwa sera ya wazee
  • Kukamilisha sera ya watu wenye ulemavu
  • Kupitishwa kwa sheria ya walemavu 2010
  • Kukarabati nyumba za vyuo vya ufundi kwa watu wenye uelemavu.
  • Kukarabati majengo ya makazi ya wazee
  • Kuhamasisha jamii kuhusiana na utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kutoa nyenzo (vifaa) za kujimudu kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kuwajengea uwezo wazee na watu wenye ulemavu kwa kuwapa mitaji midogo midogo.

Zomba naomba kujua hapa mnaongelea nchi gani?

Ni tanzania hii hii au kuna nchi nyingine ya peponi inayoitwa Tanzania ambapo haya yanafanyika. Maana katika ncchi ambayo wazee hawathaminiki ni hapa kwetu. Sijui kama hiyo sera ya wazee unayoingelea huwa inafanya kazi au ishaanza kufanya kazi au may be ndio iko kwenye mchakato wa kuanzishwa na kupitiwa. Maana wazee hata matibabu kupata ni issue au huduma za afya au uangalizi wa karibu haupo waangalie wale wa kambi ya pale morogoro na tabu wanayoipata au sijui nyingine ya kigambboni.

Wazee wa Africa Mashariki mpaka leo wanazungushwa kulipwa mafao yao. Ni wazee gani hao anaoongelea Zomba ambao wana haya aliyoyasema.
 
Nilijua tu,mdahalo utakua hivi,aah ngoja niendelee kusoma nadharia!
 
mtaandika mengi 2015 tunataka majibu ya mawaziri na watumishi wezi wamewachukulia hatua gani pesa za uma ziko wapi? Ritz go back to school hujui kitu ni unazi wa ccm tu
zomba katiririka vibaya kamwaga data mpaka pc ya matola imepata imegoma...
 
Yan zomba wa hajabu sana ana shangaa mwenzie kujibu maswali bila ku copy
 
Mwali mimi nitaomba uwaulize washiriki kuhusu dhana ya udhaifu wa Kikwete. Je wanakubaliana nayo?

Kama ndiyo ni kwanini kama siyo ni kwanini? Nauliza hivyo kutokana na pamoja kuwa Marais waliopita kuwa na mapungufu mengi lakini haijapata kutokea Taifa kuwa kwenye hali ya mkanganyiko kama sasa, kuanzia sekta ya Afya na mgogoro wa madaktari.

Ukija kwenye Uchumi pia nayo utaona uhujumu uchumi mkubwa unaohusisha viongozi mbalimbali ambapo wanagusa nyanja zote Usafiri, elimu, ujenzi, utalii nakadhalika sasa ukijumuisha yanayotokea kiuhalisia naomba wainyambue hoja ya Udhaifu. Asante
 
zomba katiririka vibaya kamwaga data mpaka PC ya matola imepata imegoma...
katiririka nini? anagoogle na kukopy na kupaste fasta fasta ....hata hareview ....bana...hii debate sio kabisa...heri pc ya Matola imegoma maana navomjua matola hapendi upuuzi angeona tu huo .... angempiga tusi moja ale tu ban siku iishe
 
Last edited by a moderator:
zomba katiririka vibaya kamwaga data mpaka PC ya matola imepata imegoma...
katiririka nini? anagoogle na kukopy na kupaste fasta fasta ....hata hareview ....bana...hii debate sio kabisa...heri pc ya Matola imegoma maana navomjua matola hapendi upuuzi angeona tu huo .... angempiga tusi moja ale tu ban siku iishe
 
Last edited by a moderator:
Mwali swali langu ni kuwa...Kikwete amefanikiwa vipi kutekeleza kauli mbiu za "ajira milioni moja kwa vijana" "kilimo kwanza" ?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom