Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Ningetaka kujua toka kwa Zomba yafuatayo:
1. Inflation rate ilikuwa ngapi 2006 na sasa ikoje?
2. Gini Coeefficent ilikuwaje 2006 na sasa mambo yako vipi?
3. Miradi ya barabara iliyokuwa under pipeline 2006
4. Miradi mipya ya barabara iliyoanza (from scrach) tangu 2006
5. GDP growth rate na Inflation kwa hii miaka 1995, 2005 na 212.
 
Asante Mwali pamoja na wageni wetu zomba na Matola,

Mi napata tabu kidogo, ni kweli kwamba wakati wa utawala wa Nyerere ni kweli tulikuwa tuna export sana hasa mazao na tulifikia kuwa tunaongoza kwenye export ya zao la katani Duniani.

Sitaki kwenda mbali sana lakini kwa mtazamo wa sasa inaonekana sio tu kwamba hatuexport tena ila hata chakula tu cha kututosheleza hakipo (Tukumbuke miaka miwili iliyopita) Kwahiyo mkuu zomba je kwa mtazamo wako unataka kunambia leo hali ya kilimo nchini ni mbaya kuliko wakati wa Nyerere?

Mwali sina uhakika kama ulitualika na sisi but kama hukutualika sorry
 
swali langu kwa zomba na Matola-Hivi je nini umekuwa mchango wa vyama upinzani katika kuboresha utawala wa raisi kikwete? lijibiwe katika nyanja zote yaani elimu, afya ulinzi, kijamii nk. asanteni
 
Last edited by a moderator:
Swali kwa Zomba - Ndugu Kikwete alishawahi kutoa ahadi ya kutengenesha biashara na siasa (wakati wa mdahalo wa urais - 2010) ili kupunguza mgungano wa kimaslahi kwa mtu ambaye ni mfanyabiashara na anataka kuingia kwenye siasa. Aliahidi kuja na sera na sheria ya kutekeleza ahadi hiyo. Swali, unalizungumziaje suala hili? je, huoni hili ni pigo kubwa katika suala zima la uongozi bora na uwajibikaji kwa wanasiasa?!
 
Mkuu First Lady,

There is only one mdahalo. This thread is for all those who want to comment in relation to the now ongoing mdahalo of the provided link in the first post of this thread.

This link is also intended to post comments from all members for questions intended for zomba or Matola in relation to the way they have commented on the subject matter.

umeeleweka Thanks

Over and out ...
 
Asante Mwali pamoja na wageni wetu zomba na Matola,

Mi napata tabu kidogo, ni kweli kwamba wakati wa utawala wa Nyerere ni kweli tulikuwa tuna export sana hasa mazao na tulifikia kuwa tunaongoza kwenye export ya zao la katani Duniani.

Sitaki kwenda mbali sana lakini kwa mtazamo wa sasa inaonekana sio tu kwamba hatuexport tena ila hata chakula tu cha kututosheleza hakipo (Tukumbuke miaka miwili iliyopita) Kwahiyo mkuu zomba je kwa mtazamo wako unataka kunambia leo hali ya kilimo nchini ni mbaya kuliko wakati wa Nyerere?

Mwali sina uhakika kama ulitualika na sisi but kama hukutualika sorry
Mkuu, tafadhali jizuie kupost katika ile debate mpaka mjadala utakapo isha.
 
Asante Mwali pamoja na wageni wetu zomba na Matola,

Mi napata tabu kidogo, ni kweli kwamba wakati wa utawala wa Nyerere ni kweli tulikuwa tuna export sana hasa mazao na tulifikia kuwa tunaongoza kwenye export ya zao la katani Duniani.

Sitaki kwenda mbali sana lakini kwa mtazamo wa sasa inaonekana sio tu kwamba hatuexport tena ila hata chakula tu cha kututosheleza hakipo (Tukumbuke miaka miwili iliyopita) Kwahiyo mkuu zomba je kwa mtazamo wako unataka kunambia leo hali ya kilimo nchini ni mbaya kuliko wakati wa Nyerere?

Mwali sina uhakika kama ulitualika na sisi but kama hukutualika sorry

fuata utaratibu mkuu...Mods futa hii post,inazingua.
 
Ningetaka kujua toka kwa Zomba yafuatayo:
1. Inflation rate ilikuwa ngapi 2006 na sasa ikoje?
2. Gini Coeefficent ilikuwaje 2006 na sasa mambo yako vipi?
3. Miradi ya barabara iliyokuwa under pipeline 2006
4. Miradi mipya ya barabara iliyoanza (from scrach) tangu 2006
5. GDP growth rate na Inflation kwa hii miaka 1995, 2005 na 212.

Mimi ninataka kujua ni kwa nini mkate niliokua nanunua shilingi miambili hamsini 2005 leo naununua kwa shilingi mia nane
kwa nini niuziwe sukari shilingi 3000 leo wakati 2005 nilikuwa nanunua kwa 500.
 
Mwali swali langu ni kuwa...Kikwete amefanikiwa vipi kutekeleza kauli mbiu za "ajira milioni moja kwa vijana" "kilimo kwanza" ?

namsaidia zomba zije akakopi huko kwenye slogan zao za 2k5.......mwenyewe kakiri....

  • AKIRI TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA KUWA BOMU, ASEMA LISIPOTATULIWA LITALETA MACHAFUKO BARANI AFRIKA

Peter Saramba na Mussa Juma, Arusha | Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni tatizo kubwa na kwamba lisipotafutiwa ufumbuzi wa kudumu linaweza kusababisha vurugu, machafuko na uasi wa umma, hata kwa nchi zinaoongozwa kwa misingi ya kidemokrasia, kama inavyotokea sasa katika nchi za Kiarabu.

Onyo hilo la Rais Kikwete linafanana na lile ambalo limekuwa likitolewa mara kwa mara na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, lakini, linapingana na kauli ya Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka ambaye Machi 21 mwaka huu, alimjibu Lowassa akisema, "Kitendo cha wanasiasa kuendelea kusema tatizo la ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka, siyo kweli."

Jana akifungua mkutano wa mwaka wa Magavana wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Jijini Arusha, Rais Kikwete alisema moja ya sababu kuu ya machafuko yanayoshuhudiwa sasa kwenye ukanda wa nchi za Kiarabu, ni matokeo ya ukosefu wa ajira kwa vijana na watu kukata tamaa.

"Siyo kweli kwamba machafuko yanayoshuhudiwa kwenye nchi za Kiarabu ni matokeo ya Serikali za nchi hizo kukaa madarakani kwa kipindi kirefu kama wengi wanavyodhani. Ukweli ni kwamba hayo ni matokeo ya ukosefu wa ajira na watu kukata tamaa ya maisha," alisema Rais Kikwete.

Alisema bila kutafutia ufumbuzi wa haraka, tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana ambao wengi hukimbilia mijini kusaka hali bora ya maisha, hata nchi zenye kuongozwa kidemokrasia, zinaweza kukumbwa na machafuko na uasi wa umma.

Rais alitumia fursa hiyo kuishukuru Denmark kwa kutoa fedha za kusaidia Mfuko wa Ajira kwa Vijana barani Afika, akisema ni moja ya mapendekezo kadhaa yaliyotolewa na kamati maalum ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kiuchumi barani Afrika ambayo yeye na Rais wa AfDB, Dk Donald Kaberuka, walikuwa wajumbe.

Mapema Rais wa Ivory Coast, Allasane Ouattara aliyehudhuria mkutano huo aliunga mkono kauli hiyo ya Rais Kikwete kwa kusisitiza kuwa vijana lazima wawekewe mazingira mazuri na kuwezeshwa kukabiliana na kumudu changamoto za kiuchumi, kitamaduni na kiteknolojia wanazokabiliana nazo.



hayo kayasema 2k2......ona maana kashindwa kutatuz tatizo la ajira.....aliahidi..ndio.....akashindwa.....
 
Maswali mengine hayana msingi, Mwali ameuliza namna hii swali la Pili. Hili lilihitajika kweli jamani?

Swali langu la pili, ataanza kujibu mkuu Matola:

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, Rais Kikwete alitoa ahadi nyingi tuu ambazo alisema atazitekeleza kama angechaguliwa kuwa Rais. Baadhi ya hizo ahadi zimeonyereshwa Jukwaa la Siasa. Je, unafikiri anawea kutekeleza ahadi zote alizotoa kabla ya uchaguzi mkuu ujao?

Mkuu, una dakika kumi na tano kujibu swali hili, baada ya hapo nitamkaribisha Zomba. Karibu Matola.
 
Kama zomba anakopi na kupesti kwanini haonywi?Inakera!
 
Last edited by a moderator:
Kwenye swali la kwanza naona zomba kafunika na bila shaka anashangiliwa na umati wa watu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa matayarisho na mda uliotumika kwa ajili ya kutengeza huu mjadala, Zomba ungejaribu hata kidogo ku edit hizo desa. Umenikata "handas" siiwezi kufuatilia unachosema katika huu mjadala.
 
hii ndiyo source ya zomba sijachakachua kitu, hapa ni copy & paste
source: Afya | Kikwete 2010

AFYA

1. Kuongezeka kwa jitihada za kupambana na magonjwa ya mlipuko;
Elimu juu ya magonjwa ya kuambukkiza na yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii juu ya kujikinga na magonjwa mapya yanayojitokeza kama vilel ebola, marbug, Homa ya bonde la ufa na Homa ya mafua makali ya nguruwe.

Wizara imeendelea kuhamasisha jamii juu ya magonjwa milipuko kwa kutoa vipeperushi zaidi ya laki moja kwa nchi nzima pia imetoa elimu kwa umma kupiti vyombo mbalimbali vya habari kama vile radio, televion, magazeti na mabango ambayo yamebandikwa barabarani yakieleza mbinu za Kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

2. Kupungua kwa vifo vya watoto wachanga na Mama wajawazito;

Chanjo zimeendelea kutolewa kwa watoto wote bila malipo. Chajo mpya imeongezwa aina ya ‘HiB Vaccine' chanjo hii ianajumushwa na chanjo nyingine 4 zilizokuwa zinatolewa kwa pamoja sasa zimekuwa tano na kuitwa chanjo ya Pentavalent (DPT –HB-Hib). Katika mwaka 2009 watoto waliopata chanjo ya surua ni asilimia 93%, DPT-HB3 asilimia 85%, OPV asilimia 88%.
Huduma za kliniki zimeboreshwa kwa ununuzi wa vifaa vya kupima mimba, uzito, upatikanaji wa dawa, kufundisha watoa huduma
Huduma kwa wajawazito na huduma za kujifungua pamoja na huduma kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano zimeendelea kutolewa bila malipo aktika vituo vya Serikali.
Vifaa mbalimbali vya huduma ya uzazi na kliniki wakati wa ujazito vimepelekwa katika hospitali 86 na vituo vya afya 50 kwenye mikoa 20. Aidha machakato wa kupeleka vifaa vya uzazi na kuhudumia watoto katika vituo 200 vya vya afya unaendelea.
Ununuzi wa pikipiki za miguu mitatu (ambulance) kwa ajili ya usafiri wa kina mama wajawazito unaendelea na pikipiki 400 zitanunuliwa.
Ujenzi wa Zahanati katika kila kijiji unaendelea kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM). Kati ya mwaka 2008/09 hadi 2009/10 zahanati 400 na vituo vya afya 78 vimejengwa.

3. Kuimarika kwa vita dhidi ya UKIMWI na Malaria;

Hali ya maambukiza nchini kiwango cha asilimia 5.7.% ya watu wenye umri wa miaka 15 – 49 (THMIS 2007 – 2008). Hali hii ni pungufu ukilinganisha kiwango na kiwango cha 7.7.% cha watu wenye umri kama huo iliyotolewa (THIS 2003 – 2004). Hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na Kampeni ya upimaji iliyozunduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. Dr. J. K. Kikwete Julai 2007.
Hadi 2009 Disemba Kliniki 909 zinatoa Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI. Watu waishio na virusi vya UKIMWI 632,086 wamesajiliwa katika kiliniki hizo na 322,783 katik ya hao wanapata dawa za kupunguza makali ya viruasi vya UKIMWI.
Huduma za kupunguza maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto inatolewa katika vituo vya Tiba 3,626
Jamii inaendelea kuelimishwa kupitia vyombo mbali mbali vya upatikanaji habari ikiwa ni pamoja na machapisho, sinema vipindi vya radio, Televisheni na sanaa.
Ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu

Mwaka 2008 ni takribani 50% ya kaya hapa nchini zilikuwa na vyandarua vyeneye dawa ya kudumu (NGAO). Ili kuongeza kasi Serikali imeamua kugawa bila malipo ili ifikapo mwishoni mwaka mwaka 2011 killa sehemu ya kulaala iwe chandarua chenye dawa ya kudumu. Mwaka 2008 Serikali ilianzisha kampeni ya kugawa bila malipo vyandarua kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5. Hadi kufikia mwezi Aprili (2010) watoto takriban milioni 9 wamegawiwa vyandaru vyenye dawa ya kudumu. Kampeni hii imekamilika katika mikoa yote.
Kuanzia mwezi wa nane mwaka huu 2010 kuna kampeni ya pili ya kugawa bila malipo vyandarua 14.6 milioni kila kaya itapewa vyandarua viwili au zaidi,
Upuliziaji wa Viuatilifu Ukoko katika Kuta

(indoor Residual Spraying)
Kampeni hii imeanzia mkoa wa Kagera mwaka 2007 katika Wilaya ya Muleba, na Wilaya ya Karagwe 2008. Mwaka 2009, afua hii ilitekelzwa katika wilaya zote za mkoa wa Kagera kuanzia mwaka huu (mwezi Agosti, 2010 kampeni itaendelea itajumuisha pia mikoa ya Mara na Mwanza.
Kampeni hii imeanzia mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kuwa mikoa hii ndiyo inaongoza kwa maambukizi ya malaria ifuatatiwa na mikoa ya Kanda ya Pwani
Tiba ya malaria kwa dawa mseto

Dawa mseto kama Alu ndiyo dawa bora za kutibu malaria kwa sababu ufanisi wake wa kuponya uko juu (aslimia 95%)
Hapa nchini wagonjwa wa malaria wanaokwenda kutibiwa katika vituo vya huduma ya afya vya Serikali wanatibiwa bila malipo au huchangia gharama kidogo kama Sera ya uchangiaji ilivyo.

4. Kutolewa kwa huduma za upasuaji wa moyo nchini;

Wagonjwa 168 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo
Wataalam wa upasuaji wa moyo wameongezeka, WAUJ ilipelekea jumla ya wataalam 27, nchini india na Israel kusomea upasuaji wa moyo na sasa wote wamerudi nchini wakiendelea na kutuoa huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ujenzi wa kituo maalum cha matibabu ya moyo umeanza kaktika hospiotali ya Taifa Muhimbili, WAUJ inashirikiana na Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Mrisho J. Kikwete, na unatarajiwa kumalizika miezi kumi na nne ijayo. Kitakuwa ni kituo bora katika Afrika Mashariki na kati.

5. Kukamilika kwa ukarabati wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na upatikanaji wa vifaa vya kisasa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini

Karibu majengo yote ya Hospitali ya Taifa Muhimbili yamekarabatiwa na vifaa vya kisasa vimekwea vifaa hivyo ni CT Scan ya Kisasa, Magenet Resonance Imaging (MRI) ya kisasa, Digital, radiograph Sysytem, USS na Fluroscopy. Mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo zimeshafungwa.
Vifaa vya kisasa vimewekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Idara ya Huduma za magonjwa ya Dharura imeimarishwa kwa kuwa na wataalam na vifaa tiba vya kisasa
Vituo vingi vya kutolea huduma za afya hapa nchini vimepatiwa vifaa vya kutibu wagonjwa

6. Kuimarishsa upatikanaji wa haki za watoto

Kukarabati majengo na kutoa vifaa katika mahabusi za watoto na shule ya maadilisho Irambo.
Kukamilisha ujenzi wa mahabusu ya watoto Mtwara.
Kukarabati chuo cha Walezi wa Watoto Kisangara.
Kutoa mafunzo kuhusiana na haki za watoto katika jamii.
Kuimarisha utaratibu wa utojai huduma kwa watotot walio katika mazingira hatarishi.
Kutoa huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi
Kuweka viwango vya utoaji wa hududma kwa toto walio katika mazingira hatarishi.

7. Kuimairisha upatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu na wazee

Kukamilika kwa sera ya wazee
Kukamilisha sera ya watu wenye ulemavu
Kupitishwa kwa sheria ya walemavu 2010
Kukarabati nyumba za vyuo vya ufundi kwa watu wenye uelemavu.
Kukarabati majengo ya makazi ya wazee
Kuhamasisha jamii kuhusiana na utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu na wazee.
Kutoa nyenzo (vifaa) za kujimudu kwa watu wenye ulemavu na wazee.
Kuwajengea uwezo wazee na watu wenye ulemavu kwa kuwapa mitaji midogo midogo.
 
Back
Top Bottom