Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mkuu zomba, Matola

Kwanza mi nakubaliana na wewe kwamba kuna maeneo ambayo Kikwete amefanya vizuri kulinganisha na viongozi waliotangulia (Hasa kwenye sehemu ya miundombinu ya barabara) lakini pia siwezi kuacha moja ya udhaifu mkubwa ambao umetokea katika kipindi chake hiki cha uongozi (Utakumbuka last week tulikuwa tunadebate kuhusu ajali ya meli ya MV Skgt) ambayo ki uhalisia inaonyesha mapungufu ya kiuongozi ambayo siwezi kusita kumrudishia yeye moja kwa moja.

Katika kipindi chake pia ndipo tumeweza kushuhudia kitu cha ajabu kidogo, katika sakata la EPA kuna watu walituhumiwa kuchukua (kuiba) fedha zile lakini badala ya kuchukuliwa hatua za kisheria (kama kungekuwa kweli na utawala wa sheria kama tunavyosema) waliishia kubembelezwa na tena kupewa na uongozi huku ikisemekana wanabembelezwa ili warejeshe fedha hizo.

Hilo mnaliongeleaje mkuu zomba na Matola......

Mbona kwenye EPA wengine wameongezezewa kifungo juzi juzi Shaban Maranda na mwenzake Farijala. Au mzee huwa hufuatilii habari ?
 
Mbona kwenye EPA wengine wameongezezewa kifungo juzi juzi Shaban Maranda na mwenzake Farijala. Au mzee huwa hufuatilii habari ?
Na hasa hiyo ya kina Farijala na mwenzie Maranda, kwanini kuwe na uchaguzi wa nani anapelekwa mahakamani na nani haendi!

Umewahi kuchukua hata dakika sifuri kufikiria hilo?
Kwa mfano mtu mmoja amechonga mpango wa wizi na mwingine akaja akaiba. Lakini yule aliyechonga mpango ndo anapelekwa mahakamani lakini aliyeiba anaambiwa we ridisha tu kwasababu fulani fulani. Umewahi liona hilo?
 
Nani hajapelekwa mahakamani?

Naomba jina lake niwasiliane na Eliezer Feleshi sasa hivi.
 
Nani hajapelekwa mahakamani?

Naomba jina lake niwasiliane na Eliezer Feleshi sasa hivi.
Mkuu matumaini yangu ni kwamba wewe una akili ndefu kuliko hiyo, kwahiyo naomba niendelee kukufikiria hivyo
 
Nilikuwa kwenye Ban nimefuatilia hii Thread Leo Kumbe zomba hamna Kitu amecopy na kupaste kutoka kwenye miblog ya CCM na viongozi wao aondolewe hana jipya kwenye huu mdahalo hamuwezi Matola kabisa wala hamkaribii

Wewe ulitaka ni kopi kwenye mi blog ya chadema? Data zote zilizomo humu ni za uhakika na ndio zinazokubalika, hakuna hata mmoja aliyekuja kuzipinga hizo data. Eti copy na paste, unafikiri tunaandika kitabu hapa hata niwe na jipya? hapa tunamjadili Kikwete na mafanikio yake.
 
Wewe ulitaka ni kopi kwenye mi blog ya chadema? Data zote zilizomo humu ni za uhakika na ndio zinazokubalika, hakuna hata mmoja aliyekuja kuzipinga hizo data. Eti copy na paste. unafikiri tunaandika kitabu hapa? hapa tunamjadili Kikwete na mafanikio yake.
Mafanikio yapi? tupo kigoma tumesubiri ile ahadi yetu ya kuibadilisha kuwa Dubai ya Africa kwi! kwi! kwi! kwi!
 
Update:

Tumejaribu kufikiria namna ya kuendelea na Tathmini hii na zomba kakubali kuendelea kuhojiwa na Mwali peke yake, baadae ndugu Matola akiwa recollected na akipata muda wa kutosha tutam-hoji pia separately.
Asanteni wote kwa uelewa. Kongosho, gfsonwin Mr Rocky na wengine wote, mjadala unaendelea saa mbili kamili EAT
 
Last edited by a moderator:

Roulette thanks very much for the updates. I think now we can think of the best way to moderate this manake yesterday nimekaa had saa sita usiku.ila nimefurah kwamba leo tutaendelea nao.
 
Last edited by a moderator:
quote_icon.png
By M'Jr

Mkuu zomba, Matola

Katika kipindi chake pia ndipo tumeweza kushuhudia kitu cha ajabu kidogo, katika sakata la EPA kuna watu walituhumiwa kuchukua (kuiba) fedha zile lakini badala ya kuchukuliwa hatua za kisheria (kama kungekuwa kweli na utawala wa sheria kama tunavyosema) waliishia kubembelezwa na tena kupewa na uongozi huku ikisemekana wanabembelezwa ili warejeshe fedha hizo.

Hilo mnaliongeleaje mkuu zomba na Matola......

Kitu ambacho kinakufanya uone ajabu kuhusu EPA na kwanini wengine wametakiwa warudishe fedha na hawakushtakiwa na wengine wameshtakiwa ni kwa kuwa hujui dhanna nzima ya EPA. Nakushauri fanya ka research japo kadogo ili uelewe EPA ni nini na unaweza wapi ukawa na kosa la kushtakiwa na wapi usiwe na kosa la kushtakiwa. Hili swali nimeshalijibu kwa undani zamani humu JF.

Kwa faida yako naomba ujisomee kitu inaitwa "hedge foreign currency debt" baada ya hapo unaweza kuja na arguments nzuri, bila kuelewa ni nini EPA tunaweza kukesha hapa.

Kwa kifupi, EPA yenyewe sio haramu ila wapo waliofanya haramu na wao ndio wamechukuliwa hatua za kisheria. Na wapo ambao hawajafanya haramu na hao wameambiwa wazirudishe fedha na huo mpango umekwisha, umefutwa na haupo tena, sasa kwanini wachukuliwe hatua?
 
mkuu Matola pole sana mkuu kwa yaliyokukuta. Namtakia mama afya njema na kupona haraka pia mungu akujalie afya na moyo wa ujasiri katika kipindi hiki. Naamini utakuwepo kwa sehem ya mjadala iliyobakia. Kila la heri ma bro
 
Last edited by a moderator:
mkuu zomba ukumbuke kwamba tuhuma hizi ambazo kurugenzi ya ikulu humjibia mkuu wetu wa nchi nyingine huwa zinakuwa na sura mbaya sana machoni petu. Kumbuka mfano wa familia yake kuhusishwa na tuhuma za kufanya biashara wakiwa ikulu hii ilikuwa ni aibu sana kwa kurugenzi ya ikulu kujibu haya ilibidi mkuu wetu atuambie tena wazi na awachukulie hatua wale wanaochafua jina lake. sasa hivi ni kawaida huku msata kila sehem panaitwa kwa kikwete. hizi sheli magodown kweli hebu tuambie kwanini mkuu anakubali kuchafuliwa hivi?
 
Last edited by a moderator:
hapana zomba kama hilo ndo jibu mbona jamani tunazidi kuchafua chama? hivi swala la mheshimiwa rais kufanya biashara akiwa ikulu linahitaj uambiwe ni ufisadi gani? kwani kwanini yeye asiseme jaman hili halinihusu? mbona jamani zomba unataka tushindwe kirahisi kikwete has powers if real he is clean in that area.
 
Last edited by a moderator:
mkuu zomba ukumbuke kwamba tuhuma hizi ambazo kurugenzi ya ikulu humjibia mkuu wetu wa nchi nyingine huwa zinakuwa na sura mbaya sana machoni petu. Kumbuka mfano wa familia yake kuhusishwa na tuhuma za kufanya biashara wakiwa ikulu hii ilikuwa ni aibu sana kwa kurugenzi ya ikulu kujibu haya ilibidi mkuu wetu atuambie tena wazi na awachukulie hatua wale wanaochafua jina lake. sasa hivi ni kawaida huku msata kila sehem panaitwa kwa kikwete. hizi sheli magodown kweli hebu tuambie kwanini mkuu anakubali kuchafuliwa hivi?

Duh. Sijajuwa kama Tanzania kuna sheria inayosema ukiwa Rais basi familia yako hairuhusiwi kufanya biashara za halali.

Kwa Tanzania sehemu fulani kupewa jina la mtu maarufu ni kawaida, ukienda Sinza kwa Remmy haimaanishi kuwa hizo biashara zote za hapo ni za Remmy. Haikuanza leo, Kuna Mtoni kwa Azizi Ali, haimaanishi kila kitu hapo cha Azizi Ali. Nadhani tupo pamoja,
 
swali langu tena zomba kuna mambo mengi sana ambayo serikali ahii imefanya kama mazuri na ambayo pia yaliipitisha serikali kwenye changamoto nyingi sana. lakini je ni yepi ambayo serikalia iliyoko madarakani ilitaka kuyatimiza lakini mpaka leo hii miaka saba bado hayajafanikiwa kabisa? hapa nataka tuangalie hasa kwenye ilan za uchaguzi kwa vipindi vyote viwili vya hii serikali.
 
Duh. Sijajuwa kama Tanzania kuna sheria inayosema ukiwa Rais basi familia yako hairuhusiwi kufanya biashara za halali.

Kwa Tanzania sehemu fulani kupewa jina la mtu maarufu ni kawaida, ukienda Sinza kwa Remmy haimaanishi kuwa hizo biashara zote za hapo ni za Remmy. Haikuanza leo, Kuna Mtoni kwa Azizi Ali, haimaanishi kila kitu hapo cha Azizi Ali. Nadhani tupo pamoja,

kwani zomba kikwete alipaaokataa wafanya bisahara kuwa wanasiasa alilenga nini? na je tamko lililotolewa na kurugenzi ya ikulu likikanusha raisi kuwa mfanya biashara na kuseam kwamba yeye ni mkulima na mfugaji tu lililenga nini?
 
Last edited by a moderator:
zomba, pamoja na dhana ya ufisadi kuwa na mkanganyiko, lakini bado sijaona mantiki ya kurugenzi ya ikulu kumjibia hata masuala ya binafsi.

Wakati huo huo, majibu ya kurugenzi hiyo yamekuwa mepesi au yasiyokuwa na hoja za kulingana na issue iliyopo.
 
Last edited by a moderator:
kufanya biashara ukiwa ikulu huoni kama kutakuwa na conflict of interest?

Mfano, rais kufanya biashara na migodi huoni inamnyima nguvu ya kuwabana wamiliki maana na yeye anafaidika moja kwa moja na uwepo wa mgodi husika?

Hii inatakiwa kuwa kwenye sheria au maadili tu ambayo yako wazi?

Back
Top Bottom