Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

quote_icon.png
By Elizabeth Dominic

Mwali mimi nitaomba uwaulize washiriki kuhusu dhana ya udhaifu wa Kikwete. Je wanakubaliana nayo?

Unajuwa unapomuita mtu dhaifu, hususan Rais wa nchi, huo ni ukosefu wa heshima na adabu na nikujitafutia umaarufu bila kujiwekea mipaka ya maadili.

Upinzani siku zote unatafuta pa kutokea na tatizo linakuja pale ambapo wanakosa hoja na kuanza kurusha shutuma eti "dhaifu". Hiyo ni siasa majitaka na matusi. Ambayo imemshushia hadhi sana kijana Mnyika. Na amejiweka pabaya kisiasa.

Alikuwa anajaribu kum "provoke" Kikwete lakini alichoshindwa kupigia hesabu ni kuwa Kikwete ni mzoefu sana wa siasa na uongozi na Mnyika bado ni "mduchu" kisiasa. Natumai amejifunza kosa lake.
 
quote_icon.png
By Elizabeth Dominic


Kama ndiyo ni kwanini kama siyo ni kwanini? Nauliza hivyo kutokana na pamoja kuwa Marais waliopita kuwa na mapungufu mengi lakini haijapata kutokea Taifa kuwa kwenye hali ya mkanganyiko kama sasa, kuanzia sekta ya Afya na mgogoro wa madaktari.

Hili nilishalijibu nyuma huko:
Ndugu yangu unataka nicheke kwa swali lako. Sekta ya afya Tanzania wakati wa Kikwete, imeboreshwa kiasi hata "life expectancy" ya Mtanzania imeongezeka kutoka miaka 40 wakati wa Nyerere, miaka 48 wakati wa Mkapa mpaka kufikia miaka 58.2 wakati wa Kikwete na inazidi kupanda. Bila Kikwete kuwa na sera nzuri ya Afya ungeona life expectancy ya Mtanzania inapanda hivyo na kuwa record kwa Afrika Mashariki?

soma:

[TABLE="class: cms_table_contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: cms_table_contentheading"]Tanzania's life expectancy rises [/TD]
[TD="class: cms_table_buttonheading, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Thursday, 03 November 2011 22:59
By Ludger Kasumuni
The Citizen Reporter
Dar es Salaam. Tanzanians now have higher life expectancy fixed at 58.2 years at birth than the rest of the citizens of East African Community (EAC), the 2011 Human Development Report (HDR) released by the United Nations Development Programme (UNDP) shows.

Source: Tanzania
Mgomo wa madaktari Kikwete kaushughulikia vyema sana. Mwanzo mpaka mwisho na kila hatua alikuwa anawaeleza wananchi hatua iliyochukuliwa.
 
quote_icon.png
By Elizabeth Dominic

Mwali mimi nitaomba uwaulize washiriki kuhusu dhana ya udhaifu wa Kikwete. Je wanakubaliana nayo?

Kama ndiyo ni kwanini kama siyo ni kwanini? Nauliza hivyo kutokana na pamoja kuwa Marais waliopita kuwa na mapungufu mengi lakini haijapata kutokea Taifa kuwa kwenye hali ya mkanganyiko kama sasa, kuanzia sekta ya Afya na mgogoro wa madaktari.

Ukija kwenye Uchumi pia nayo utaona uhujumu uchumi mkubwa unaohusisha viongozi mbalimbali ambapo wanagusa nyanja zote Usafiri, elimu, ujenzi, utalii nakadhalika sasa ukijumuisha yanayotokea kiuhalisia naomba wainyambue hoja ya Udhaifu. Asante

Hili pia nimeshalijibu huko juu, inaonesha unauliza bila kupitia mjadala:
Utawala wa Kikwete haujagubukwa na shutuma za rushwa na ufisadi, utawala wa Kikwete unazishughulikia tuhuma za rushwa na ufisadi za tawala zilizopita na kung'oa mizizi iliyowachwa ikuwe kwa miaka 44. NDIO maana leo wakati wa Kikwete unaona kesi nyingi za ufisadi na zinajadiliwa wazi kwenye vyombo vya habari. Ukitazama kesi zote za rushwa na "ufisadi" utakuta ni za tawala iliyopita, mfano EPA, BOT, KIWIRA, MAHALU, RADAR, NDEGE YA RAIS, ATC. Yote hayo ni madudu ya tawala iliyopita. Kikwete anayaibuwa na kuyashughilikia ipasavyo ki kanuni na sheria bila kukiuka haki za mtuhumiwa na tunaona watu wakifikishwa mahakamani na wengine kufungwa na wengine kesi zinaendelea tena nyingi sana. Na bado anaendelea na kufumuwa madudu, tutayaona na kusikia mengi kabla ya muda wake kuisha. Huoni kuwa hiyo ni faraja kubwa kwa Watanzania leo hii?

Tunaona wakati wa Kikwete alivyobadili mfumo wa ukaguzi wa hesabu za Serikali na kumpa wigo mpana CAG na CAG kwa mara ya kwanza ukaguzi wake unajadiliwa kwa kina bungeni na kamati za udhibiti alizozianzisha bungeni. Hivi huuoni mfumo wake mpya unavyoibuwa madudu? na watu kufikishwa mahakamani na kukosa nyadhifa zao. Bado una mdomo wa kusema Kikwete ajiuzulu. Jiulize hao wa kabla yake walikuwa wapi? wakiyalea haya madudu?
 
Zomba anachangiwa na Lumumba kuanzia Nauli, Vitendea kazi, Airtime n.k kwakua anawatetea.

Matola tunamuachia mzigo wote, not fair at all.

Mkikosa hoja mnaanza viroja, jana kompyuta ilipata mchechetu, leo pancha. Kwi kwi kwi teh teh teh! mie InshaAllah nipo hapa iwe leo au kesho no problem.

Mimi nnaichangia CCM kwa mapenzi yangu kwa chama na Kikwete. CCM hainilipi wala hainilipii chochote. Kuwa makini na wacha kudanganya umma.
 
quote_icon.png
By matumbo

Mwali swali langu ni kuwa...Kikwete amefanikiwa vipi kutekeleza kauli mbiu za "ajira milioni moja kwa vijana" "kilimo kwanza" ?

Waliokuwa na ajira mwaka 2006 = 16,627,133

Waliokuwa na ajira mwaka 2011 = 19,783,648

19,783,648 - 16,627,133 = 3,156,515

Nadhani umepata jibu, ukipenda soma zaidi hapa: UNEMPLOYMENT ESTIMATES FOR THE YEAR 2011
 
quote_icon.png
By FJM
Ningetaka kujua toka kwa Zomba yafuatayo:
1. Inflation rate ilikuwa ngapi 2006 na sasa ikoje?
2. Gini Coeefficent ilikuwaje 2006 na sasa mambo yako vipi?
3. Miradi ya barabara iliyokuwa under pipeline 2006
4. Miradi mipya ya barabara iliyoanza (from scrach) tangu 2006
5. GDP growth rate na Inflation kwa hii miaka 1995, 2005 na 212.

Pitia hapa utapa figures zote; Bank of Tanzania: Publications and Statistics
 
quote_icon.png
By M'Jr

Asante Mwali pamoja na wageni wetu zomba na Matola,

Mi napata tabu kidogo, ni kweli kwamba wakati wa utawala wa Nyerere ni kweli tulikuwa tuna export sana hasa mazao na tulifikia kuwa tunaongoza kwenye export ya zao la katani Duniani.

Sitaki kwenda mbali sana lakini kwa mtazamo wa sasa inaonekana sio tu kwamba hatuexport tena ila hata chakula tu cha kututosheleza hakipo (Tukumbuke miaka miwili iliyopita) Kwahiyo mkuu zomba je kwa mtazamo wako unataka kunambia leo hali ya kilimo nchini ni mbaya kuliko wakati wa Nyerere?

Mwali sina uhakika kama ulitualika na sisi but kama hukutualika sorry

Nyerere alipokabidhiwa nchi tulikuwa tuna export mazao mengi ya shambani. Mwaka 1967 (miaka 6 baada ya Uhuru) Nyerere akataifisha mashamba mengi makubwa, baada ya hapo tu, tukashindwa kusafirisha nje mazao kwa sera zake za Ujamaa. Zilitumaliza mpaka tukawa omba-omba.

Usichanganye kuwa wakati wake tulikuwa tukisafirisha. Wakati wake ndio tuliharibu. Na hilo halina ubishi.

Sasa ndio tumeanza kusafirisha tena. Chakula sasa hivi ni asilimia 108 ya mahitaji yetu yaani tunaweza kuuza nje asilimia 8 na tusife na njaa.
 
quote_icon.png
By gfsonwin

swali langu kwa zomba na Matola-Hivi je nini umekuwa mchango wa vyama upinzani katika kuboresha utawala wa raisi kikwete? lijibiwe katika nyanja zote yaani elimu, afya ulinzi, kijamii nk. asanteni

Upinzani hauna mchango wowote wa maana. Upinzani ulikuwa unatakiwa uwe ndio "watch dog" wa Serikali iliyopo madarakani, badala ya kusimamia na kuhakikisha Serikali inatekeleza, wao ndio kwanza wanaleta siasa maji taka.

Kwa ufupi hakuna upinzani wa maana Tanzania.
 
zomba,
Naona majibu yako yapo sawa sawa data tupu hakuna porojo.
 
Last edited by a moderator:
quote_icon.png
By Nzi

Swali kwa Zomba - Ndugu Kikwete alishawahi kutoa ahadi ya kutengenesha biashara na siasa (wakati wa mdahalo wa urais - 2010) ili kupunguza mgungano wa kimaslahi kwa mtu ambaye ni mfanyabiashara na anataka kuingia kwenye siasa. Aliahidi kuja na sera na sheria ya kutekeleza ahadi hiyo. Swali, unalizungumziaje suala hili? je, huoni hili ni pigo kubwa katika suala zima la uongozi bora na uwajibikaji kwa wanasiasa?!

Hilo kama lilikuwa ni wazo na sio sera sina tatizo nalo. Ingekuwa ni ahadi ya kisera kama vile Mahakama ya Kadhi, hapo tungeenda vizuri sana. Lakini si kitu wacha nikupe darsa dogo la siasa na biashara;

Nadhani kulitekeleza hilo bila mikakati mizuri itakuwa unaturudisha kulekule nyuma tulikoshindwa (kwa Nyerere) badala ya kutupeleka mbele.

Mfanya biashara anaweza kuwa mwanasiasa mzuri kama vile ilivyo kwa fani zingine. Huwezi kutenganisha siasa na maisha ya watu. Ikiwa kuna mfanya biashara na anaona kuwa akiingia kwenye siasa atatowa mchango mzuri kuboresha maisha ya Mtanzania kwanini azuiliwe?

Kumbuka kuwa hata biashara yenyewe ni moja katika mambo yanayotiliwaa mkazo sana na Serikali ili yaendelezwe kwa manufaa ya nchi. Si busara kuitenganisha siasa na biashara na moja ya vigezo vya utawala bora ni pale utakaposimamia vizuri siasa kuendeleza biashara.
 
zomba,
Naona majibu yako yapo sawa sawa data tupu hakuna porojo.

Takwimu hazidanganyi, walitaka nilete porojo za kichwani kama wanavyoleta wao bila vielelezo wala takwimu. Wamezowea majungu hii ya data inawaudhi sana. Soma comment zao za "copy na paste".

Hapa ni nondo tu huwa sikisii!
 
quote_icon.png
By mwaJ

7. Kuimairisha upatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu na wazee

Maswali kwa Zomba:


  • Kukamilika kwa sera ya wazee

Je? Hiyo Sera inatekelezwa? Imewanufaisha wazee wa nchi hii? Toa mifano hai.



  • Kukamilisha sera ya watu wenye ulemavu

Je? Hiyo Sera inatekelezwa? Ni kwa nini mauaji ya walemavu wa ngozi yameongezeka kipindi cha Kikwete?



  • Kupitishwa kwa sheria ya walemavu 2010

Je? Hiyo sheria inatekelezwa? Ni kwa nini hata shule zenye watoto wenye ulemavu bado hazina mazingira rafiki kwa walemavu?



  • Kukarabati nyumba za vyuo vya ufundi kwa watu wenye uelemavu.

Toa mifano hai ukilinganisha na vyuo vya ufundi vilivyopo nchini.



  • Kukarabati majengo ya makazi ya wazee

Ni majengo ya wapi hayo yaliyokarabatiwa? Ni mwaka huu tumewaona na kuwasikia wazee wanaoishi katika kambi ya wazee Morogoro wakilalamika kuhusiana na mazingira magumu wanayoishi.



  • Kuhamasisha jamii kuhusiana na utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kutoa nyenzo (vifaa) za kujimudu kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kuwajengea uwezo wazee na watu wenye ulemavu kwa kuwapa mitaji midogo midogo.

Naomba utoe mifano hai kwa bullets 3 hapo juu.

Majibu ya swali lako yako kwenye MKUKUTA, unajuwa MKUKUTA ni nini?

Pitia hapa kwa majibu ya kina: http://www.povertymonitoring.go.tz/
 
quote_icon.png
By platozoom


Swali kwa zomba ukitilia maanani mabadiliko ya katiba yanayokuja ambayo pengine yakaongeza au kuondoa kikomo cha kugombe urais ......unafikiri JK anastahili kuongezewa kipindi kingine cha miaka mitano? na kwa nini?

Ingawa ningependa sana Kikwete aendelee kuongoza lakini sitaki iwe hivyo. Urais ni kazi ngumu sana. Unaambiwa ni bora kuongoza ng'ombe 1000 kuliko binaadam mmoja, sasa fikiri kuongoza binaadam million 40 kwa miaka 10.

Ni hatari sana Rais kuongoza kwa muda mrefu, mimi nigependekeza kwenye Katiba mpya Rais asizidi kuongoza zaidi ya miaka 8 na anachaguliwa mara moja tu. Na kila miaka minne anapigiwa kura ya "confidence" bungeni kama aendelee au asiendelee kuongoza. Hii itatu save sana gharama za uchaguzi za kila miaka 5.
 
quote_icon.png
By SnowBall

zomba alitakiwa aongee from his perspectives na ku'compare' na 'international standards'..sasa kuorodhesha asilimia tu pamoja na maelezo mengi hakuleti tija ya mjadala!..

Swali langu..na naomba Mwali ulichukue..ni hivi:

Kwa kuwa tumeamua kuwa na Kauli Mbiu ya Kilimo Kwanza..na kwa kuwa karibu watu wetu 80% wanategemea kilimo..na kwa kuwa Ukiinua Kilimo obviously utakuwa umeinua Uchumi wa Mtanzania..Je? Kwa karibu miaka mitano tangu hii Kauli Mbiu ilipoanzishwa nini Mafaniko yake na nini kiwango cha Utekelezaji wake??

Utaona kuwa mjadala umewekewa nyuzi mbili, moja ya mjadala na moja ya side comments za mjadala. Pale kwenye mjadala hakuna muda wa kujibizana posts. Kwa hiyo unashusha nondo pale halafu watu wanaozisoma kama haziwaingii akilini au wana maswali wanakuja hapa tunajibu na kufafanuwa. Si unaona maswali yenu yamebandikwa juu huko na kila yanayonihusu nayapitia na kuyajibu.
 
quote_icon.png
By platozoom


Mwali swali langu kwa Matola na zomba tena:

Katika miaka ya karibuni hasa katika kipindi cha JK kumekuwa na mijadala mikali sana ya udini (sio dini) miongoni mwa wanasiasa hata viongozi wenyewe wa dini juu ya mgawanyo wa madaraka na utoaji wa nafasi za elimu na ajira kwa vigezo vya dini ya mtu!

Swali: Mnafikiri ni kwa kiasi gani utawala wa JK umelishughulikia kwa namna ya kutoacha mpasuko katika Taifa?

Nini mchango wa Utawala wake katika mgawanyiko huu?

Kazi kubwa aliyoifanaya na anayoendelea kuifanya Kikwete kuhusu hilo ni kutoa fursa ya elimu kwa wote kwa kuongeza shule za sekondari kutoka chini ya 900 mwaka 2005 kufikia zaidi ya 4,000 mwaka 2011. Kuongeza idadi ya vyuo vikuu na kuongeza vyuo vya ufundi.

Hiyo ni njia muhimu sana ya kuondoa malalamiko, kwa sasa shule ni bidii yako na si kuchaguliwa kama ilivyokuwa awali. Ingawa bado huku kwenye elimu kuna maboresho makubwa yanatakiwa yafanyike ili kuondoa kabisa malalamiko, mfano mzuri ni madudu ya NECTS yaliyoibuliwa juzi ya kuwanyima watoto wa Kiislaam maksi zao wanazostahili eti kwa kuwa mtu wa IT kakosea. Haiingii akilini hayo ni madudu ya kurekebushwa.

Kutoa fursa ya elimu kwa wote ni njia kuu ya kutatua mgogoro wa udini. Kwa hili nampa pongezi Kikwete kwani elimu ndio kilio kikubwa cha Waislaam toka kabla ya Uhuru lakini sasa tunaona hilo likitatuliwa, Kikwete anstahili kila sifa kwa hili.
 
quote_icon.png
By FJM

Kwenye hoja ya ahadi za rais zomba amesema kuwa ahadi za rais zimetekelezwa. Ningetaka kujua ufafanuzi kwa haya yafuato:

1. Ahadi zote 69 ziligharimu kiasi gani?
2. Bajeti ya ahadi hizo ilipitishwa katiba kikao gani cha bunge?
3. Na hela hizo zilikuwa za ndani (domestic revenue) au misaada/loans? Na kama ni misaada/loans toka wapi?

Bajeti zote za Serikali kuanzia alivyoingia Kikwete madarakani ni za kutekeleza ahadi za sera za chama chake.

Hivi ulifikiri Rais anatekeleza ahadi kwa bajeti ya mshahara wake? kwi kwi kwi teh teh teh !
 
quote_icon.png
By Shark

Hivi karibuni kikwete alikaririwa akisema kua hajui hata umaskini wa watanzania unatokana Na nini?

Zomba, unafikiri ni sahihi hili??

Kikwete alikuwa ni sahihi na diplomatic sana alipojibu hivyo, mimi ningejibu "ni uvivu wao unawafanya wawe maskini, wale wote ambao wanaojituma ipasavyo hali yao kimaisha ni nzuri".
 
Back
Top Bottom