Wee omba weee mbona huna tofauti na JK mwenyewe. Lini Fisi akayaona mabaya ya fisi mwenzake ktk mawindo.Muulize Mkandara ananijuwa vizuri sana, ukiniona unaweza kucheka mpaka kuzimia, utasema "kizee chenyewe ndio hiki". Sipo Serikalini wala si kama unavyofikiria, mimi kweli ni CCM toka inaanzishwa na kabla ya hapo nilikuwa mmoja wa wana TANU youth league. Na u CCM wangu wote lakini kuna baadhi ya viongozi wa TANU/CCM sikubaliani na uongozi wao 98% na wengine nawakubali nusu nusu lakini Kikwete? huyu jamaa namkubali 100%. Eeeh bwana Kikwete anachapa kazi wacha mchezo, uliza waliopo karibu nae watakueleza. Muone vile vile anacheka-cheka jamaa ni mchapa kazi sana.
Mimi nilifuatilia kidogo sana mjadala huu kisha nikawa bored.Sintosema uongo kwani hapakuwepo na maswali ya kubana mbavu ila kujieleza zaidi kwa kutumia data na maelezo yetu. Nilitegemea sana Mwali kuuliza maswali katika ili tupate undani wa majibu maana unapoul;iza swali sii kila jibu linakubalika..
Nilitegema kitu kama kipindi cha Hard Talk cha BBC badala ya kuwa wapole sana ktk majibu rahisi sana.. Hii kufananisha watu na miaka ya zamani pia sikuupenda kwa sababu Jesse Owens alikimbia mbio za mita 100 kwa nukta 10 na amechukua medali hjiyo ktk wakati mgumu zaidi kuliko watu wote waliwahi kukimbia mbio hizo..Ati leo waja nambia hana mpango kwa sababu kuna mtu anakimbia mbio hizo hizo kwa nukta 9 bila kujali mazingira, vyenzo, vyakula na kikubwa zaidi msingi aloacha Jesse kwa watu weusi kushiriki mbio za Olimpiki...
Binafsi yangu hupenda kwenda undani zaidi, kujua nini chanzo na nini mategemeo ya mwisho na tumepata nini..Maana kuwa na shamba la hekari 1000 ukavuna magunia 10,000 inaweza kuonekana mengi sana lakini kama utajua kwamba hekari 1000 zinatakiwa kuzalisha magunia 100,000 hapo ndipo mjadala unapendeza zaidi. Kwa kutafuta kwa nini hayakuzalishwa magunia 100,000...
Last edited by a moderator: