Tani Elfu 50 za sukari kuingizwa nchini kukabiliana na upungufu uliopo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,300
9,727
Ndugu zangu Watanzania,

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Sukari nchini Tanzania Ndugu Kenneth Bengesi amesema kuwa katika kukabiliana na upungufu wa sukari hapa nchini, inatarajiwa kuanzia mwezi huu wa januari kuingizwa kwa Tani Elfu Hamsini za Sukari kutoka nje ya Nchi.

Mkurugenzi huyo ameelezea pia sababu ya upungufu wa sukari uliopo hapa nchini na njia au mikakati ambayo inaendelea kufanyika ili kumaliza tatizo hilo.ambapo amesema ya kuwa upungufu huo unatokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini ambapo zinakwamisha shughuli za uvunaji wa miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari.

Kwa hiyo uagizwaji na uingizwaji wa Tani hizi za sukari kutoka nje ya nchini kuja hapa Nchini ni katika juhudi za kuongeza kiasi cha upatikanaji wa sukari hapa nchini na kuweza kuendana na mahitaji ya Sukari yanayohitajika.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Sukari nchini Tanzania Ndugu Kenneth amesema kuwa katika kukabiliana na upungufu wa sukari hapa nchini, inatarajiwa kuanzia mwezi huu wa januari kuingizwi kwa Tani Elfu Hamsini za Sukari kutoka nje ya Nchi.

Mkurugenzi huyo ameelezea pia sababu ya upungufu wa sukari uliopo hapa nchini na njia au mikakati ambayo inaendelea kufanyika ili kumsliza tatizo hilo.ambapo amesema ya kuwa upungufu huo unatokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini ambapo zinakwamisha shughuli za uvunaji wa miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari.

Kwa hiyo uagizwaji na uingizwaji wa Tani hizi za sukari kutoka nje ya nchini kuja hapa Nchini ni katika juhudi za kuongeza kiasi cha upatikanaji wa sukari hapa nchini na kuweza kuendana na mahitaji ya Sukari.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Umeweka namba katika tani 50,000 wewe unataka tani ngapi🤔
 
Ni aibu kubwa kwa Taifa kama Tanzania sukari kuwadimika hadi kufikia kilo Tsh6,000.wakati jirani zetu kilo moja ya sukari inauzwa bei ndog o sana chini ya dollar1.
 
Hapa nagundua kwanin stars haipendwi na wananchi kumbe sababu ni team ya ccm
 
Ni aibu na upumbavu kuendelea kuagiza sukari, ngano, mafuta ya kula na wakati tuna maziwa, mito ya kutosha na mabonde mazuri ya kilimo, Utawala wa hovyo sn na unatia kinyaa.
 
Lucas unaupiga mwingi kuliko mama abdul
Usinifananishe mimi na Mheshimiwa Mama yetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita,nuru ya wanyonge ,nyota ya matumaini anayefanya kazi na kuchapa kazi mpaka kazi zenyewe zinapiga salute kwake. Mama Samia Ni Mpango wa Mungu Mwenyewe
 
Ni aibu na upumbavu kuendelea kuagiza sukari, ngano, mafuta ya kula na wakati tuna maziwa, mito ya kutosha na mabonde mazuri ya kilimo, Utawala wa hovyo sn na unatia kinyaa.
Mdogo wangu umeelewa lakini sababu zilizotolewa za kupungua kwa uzalishaji wa sukari kwa kipindi hiki? Au wewe umekimbilia kutoa maoni yako tu yanayokujia kichwani mwako humo😀😀😀
 
Usinifananishe mimi na Mheshimiwa Mama yetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita,nuru ya wanyonge ,nyota ya matumaini anayefanya kazi na kuchapa kazi mpaka kazi zenyewe zinapiga salute kwake. Mama Samia Ni Mpango wa Mungu Mwenyewe
Usinifokee!😂
 
Back
Top Bottom