Pre GE2025 Mjadala: Demokrasia Yetu, Viongozi Wetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
686
1,125
Wakuu,

MJADALA.jpg

Tunapoukaribia Uchaguzi Mkuu 2025, ni muhimu kutathmini changamoto za chaguzi zilizopita (2015 na 2020) na kushirikiana katika kutafuta suluhisho

Jiunge nasi kwenye mjadala maalum kupitia X Spaces ya JamiiForums tarehe 30 Januari 2025, kuanzia saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku.

Shiriki kwa kusikiliza, kuuliza maswali na kutoa maoni kuhusu hatma ya demokrasia yetu

Kushiriki, bofya : x.com

Soma hapa: Special Thread: Matukio ya Rafu za Uchaguzi na Malalamiko kwenye Zoezi zima Uchaguzi Serikali za Mitaa

========================================

MAONI YA WACHANGIAJI WALIOPO KWENYE MJADALA

AISHA MADOGA - Mwenyekiti wa CHADEMA, Dodoma

"Changamoto mama ya Uchaguzi ni usimamizi wenyewe wa Uchaguzi, hapo ndipo changamoto zote zinapoanzia

Ngazi ya Majimbo msimamizi ni Mkurugenzi ambaye ni Mteule wa Rais na Kada wa CCM, wanaomsaidia ni Watendaji wa Kata na wao ndio wanaosimamia taratibu zote kuanzia ngazi za awali, hapo uhalali unakuwa wapi?"

"Kada wa Chama anakuwa na jukumu la kusimamia Uchaguzi, huyo ndiye ambaye anapaswa kumsimamia Mgombea wa Chama cha Upinzani, ni vigumu kutenda haki. Hivyo hivyo ipo kwa Watendaji wa chini ambao nao asilimia 80 wanakuwa ni Makada wa Chama Tawala"

"Mawakala wa Uchaguzi nao wanakuwa wanadhibitiwa na Watendaji ambao wanasimamia Uchaguzi, hiyo haiwezi kufanya kuwe na matokeo ya Haki"

"Kanuni za Uchaguzi zinaeleza Tume ya Uchaguzi yenyewe ndio inatakiwa kuamua wapi pa kuweka Kituo cha Kupiga Kura, hiyo imesababisha waweke vituo katika Mazingira ambayo yanakuwa magumu kwa Wakala kuweza kufanya Kazi"

"Kada wa Chama anakuwa na jukumu la kusimamia Uchaguzi, huyo ndiye ambaye anapaswa kumsimamia Mgombea wa Chama cha Upinzani, ni vigumu kutenda haki. Hivyo hivyo ipo kwa Watendaji wa chini ambao nao asilimia 80 wanakuwa ni Makada wa Chama Tawala"

"Political Will (Nia ya kisiasa) ni moja ya kitu muhimu kwa kuwa kama wahusika hawajaamua hata kama Sheria zikiwemo hazitasaidia"

"Kuna wakati Wananchi wenyewe wanaweza kuamua kufanya maamuzi ya kuwalazimisha Wanasiasa au Serikali kuwa na nia ya mabadiliko ya Kisiasa"

"Sisi Viongozi au Wanasiasa hata kama tukiamua kusimama wenyewe bado haitasaidia lakini Wananchi wakiamua wao wenyewe itakuwa na nguvu na mabadiliko yataonekana "

Wakati nafanya kile kitu kilichotokea Dodoma na ikaonekana ni kama fujo, Wananchi walikuwepo wakawa wanashuhudia kinachoendelea, hawakuingilia kati, waliishia kutazama kupiga picha na baadaye kupongeza lakini hawakuchukua maamuzi wakati wa tukio"

"Vyama vya Kisiasa vinawajibu wa kutumia Mitandao ya Kijamii katika Chaguzi zinazokuja kwa kuwa ndipo Vijana wengi walipo na huko wanaweza kupatumia kupaza sauti zao na kuelezea changamoto wanazoziona"

"Uchaguzi wa Serikali za Mtaa ulikuwa wa ovyo kuliko Chaguzi nyingine zote, kulikuwa na uibaji wa Kura kwa njia rahisi. Kuna marekebisho makubwa yanatakiwa kufanyika kuboresha Mfumo mzima wa Uchaguzi"

"Kuna Watu bado wana matumaini na Serikali iliyopo Madarakani, wapo wenye matumaini hadi Asilimia 50 na wengine Asilimia 100 lakini mimi nina matumaini Asilimia 0 kwa haya yanayoendelea sasa"

"Kuna umuhimu mkubwa wa Wananchi kutambua wajibu wao na hali hiyo inaturudisha nyuma, kwa ufupi tunauhitaji umma kuliko wakati mwingine wowote"

MWANAISHA MNDEME: Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara – ACT

"Nimeshiriki katika Chaguzi na nimeona jinsi ambavyo hali huwa ngumu kwa Vyama vya Upinzani. Moja ya chanzo kinachoharibu ni matumizi ya nguvu ya Jeshi la Polisi"

"Ukifuatilia katika Chaguzi kadhaa imekuwa ikionekana kama Vyama vya Upinzani vinashindana na Jeshi la Polisi badala ya kushindana na Chama Tawala kama inavyotakiwa kuwa"

"Kifungu cha Uchaguzi 40 (5) kimekuwa kikitumiwa vibaya. Wasimamizi wa Uchaguzi hawakutambulisha Mawakala, wengine walichelewa kupata utambulisho na Wasimamizi wengine walidai kuwa hawajapewa Maelekezo ya kuwatambua Mawakali"

"Hicho ni moja kati ya Vifungu ambavyo tulipendekeza kibadilishwe kwa kuwa kinachangia kuathiri Uchaguzi"

"Changamoto nyingine ni ‘enguaengua ya Wagombea’, hali hiyo imetokea katika Chaguzi zilizopita na imekuwa ikiathiri kwa kiasi kikubwa Vyama vya Upinzani"

"Uzoefu unaonesha Wagombea wengi wanaoenguliwa, hawaondolewi kwa kuzingatia Katiba, badala yake wanaondolewa kwa makosa madogomadogo ambayo sio ya msingi"

"Tanzania iliamua kuingia katika Mfumo wa Vyama Vingi ili kuwapa Wananchi Mamlaka ya kuamua Viongozi inaowataka lakini kwa mwenendo unavyokwenda Nchini tunapoka Mamlaka ya Wananchi kuamua"

EUGENE KABENDERA - Msemaji wa Chaumma

"Uchaguzi kwa sasa umekuwa kama vita, hali hiyo inasababisha Wananchi kuwa na hofu. Tunapoelekea, itafikia hatua Wananchi watakuwa hawana Mamlaka ya kuamua, tutachekwa na Dunia"

"Pamoja na kuwa tunahitaji mabadiliko ya Katiba na Sheria yetu, kama hatutakuwa na dhamira ya Viongozi kututoa hapa tulipo mambo bado yatakuwa magumu"

"Hakuna Sheria inayosema kuwa Viongozi au Vyombo vya Dola vinaweza kuingilia lakini ndivyo ilivyotokea katika Chaguzi kadhaa zilizopitaViongozi wetu wasiwakatishe tamaa vijana wenzetu, hali ikiendelea hivyo ipo Siku wanaweza kuamua kupita njia nyingine"

"Kinachoendelea katika masuala ya Uchaguzi sio kwamba ni hofu pekee, bali inawezekana kukosekana kwa Haki katika Uchaguzi inaweza kuwa njia ya kutengeneza usugu kwa Watu"

"Tulifungua kesi 51 katika Wilaya mbalimbali tukipinga kesi zilizohusu masuala ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo hatukufanikiwa na Uchaguzi ukaendelea kama kawaida, hiyo ilionesha hakukuwa na nia ya Haki kupatikana"

"Hakuna Sheria inayosema kuwa Viongozi au Vyombo vya Dola vinaweza kuingilia lakini ndivyo ilivyotokea katika Chaguzi kadhaa zilizopitaViongozi wetu wasiwakatishe tamaa vijana wenzetu, hali ikiendelea hivyo ipo Siku wanaweza kuamua kupita njia nyingine"

"Pamoja na kuwa tunahitaji mabadiliko ya Katiba na Sheria yetu, kama hatutakuwa na dhamira ya Viongozi kututoa hapa tulipo mambo bado yatakuwa magumu"

"Uchaguzi kwa sasa umekuwa kama vita, hali hiyo inasababisha Wananchi kuwa na hofu. Tunapoelekea, itafikia hatua Wananchi watakuwa hawana Mamlaka ya kuamua, tutachekwa na Dunia"

"Tanzania iliamua kuingia katika Mfumo wa Vyama Vingi ili kuwapa Wananchi Mamlaka ya kuamua Viongozi inaowataka lakini kwa mwenendo unavyokwenda Nchini tunapoka Mamlaka ya Wananchi kuamua"

"Tumuongezee muda Rais ili tuweze kufanya mabadiliko ya mifumo ya Uchaguzi pamoja na Katiba, nchi mbalimbali wamefanya hivyo

"Kwa Watu wanaoshiriki Uchaguzi wanaona kinachoendelea ni uonevu, hatuna haja ya kukimbilia katika masuala ya Uchaguzi wakati hakuna kinachofanyika, CCM wameshika mpira kwapani wanasubiri mpira uanze"

"Rais Samia amekuwa na nyota na maono katika masuala ya kuboresha Uchaguzi, alikuwepo katika Bunge la Katiba Mpya, ana kila sababu ya kuliacha hili Taifa katika mikono salama na ataandikwa katika vitabu kuwa ameacha historia Tanzania. Akubali tumuongezee muda ili tupate Katiba Mpya na Bora ili Wananchi waamue wenyewe nini wanachokitaka"

MOHAMED NGULANGWA: Mkurugenzi wa Habari - CUF

"Mijadala mingi inaendeshwa na ninawapongeza wote wanaoandaa na kushiriki lakini ili tuweze kuwa na Uchaguzi wa Haki ni vema kukawa na mabadiliko ya Katiba pamoja na kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi inayotenda Haki na sio ambayo inabadilishwa jina lakini utendaji unakuwa ni uleule"

OBADIA NDANGA (Mdau)

"Taasisi nyingi zipo chini ya Serikali, ingekuwa zipo huru na zinazojitegemea ingechangia kuwa na Uchaguzi wa haki na huru"

"Kuna wakati nilienda Kupiga Kura, Wasimamizi waliokuwepo wakaniuliza kama ninajua ninayeenda kumpigia kura, wakaniambia wanijazie katarasi kisha mimi niwape wao waiweke kwenye boksi"

"Kwa kuwa nilikuwa najielewa sikufanya hivyo, lakini ninaamini kuna Watu wengi ambao inawezekana walirubuniwa na kufanya kile ambacho wale Watu walikuwa wanakitaka"

"Jambo lingine la muhimu ni kuwa Vyama vinatakiwa kuwa na umakini katika kuchagua aina ya Watu ambao wanaenda kuwa Mawakala wao, baadhi yao wakirubuniwa kidogo tu wanaacha kile kilichowafanya wawe hapo"

RC EVANGELIST GEORGE (Mdau)

"Kuna wakati ubinafsi umekuwa ukichangia kuwaangusha wapinzani wenyewe, wangekuwa wanaungana na kuwa kitu kimoja wakiwa na msimamo thabiti hiyo ingewasaidia, badala ya hii ya sasa kila mmoja kusimama upande wake"

RASHIDI CHIKAWE (Mdau)

"Kuna Vijana wameshakata tamaa na masuala ya Uchaguzi na Siasa, matokeo yake wapo ambao wanaona bora wabishane kuhusu mpira lakini sio Siasa"

"Ingetokea Vyama vya Upinzani vingeungana kisha kuna kuwa na pande mbili zenye nguvu kwa maana ya Chama Tawala na kile cha Upinzani ingesaidia wawe na uwezo wa kujenga hoja na kuisimamia"

DEDAN KAPONGO (Mdau)

"Inapotokea makosa madogo kama vile kukosea umri n.k kama inajulikana umri wake umekidhi vigezo vya Kupiga Kura haitakiwi kuwa sababu ya kumzuia kupiga au kupigiwa kura"

"Serikali inatakiwa kulitilia maanani hivi vitu ambavyo vinasababisha kuondoa usawa kwani vitu vya kuondoa watu katika sifa za kupiga au kupigiwa kura vinatakiwa kuchukuliwa hatua"

"Serikali inatakiwa kutilia maanani hivi vitu ambavyo vinasababisha kuondoa usawa kwani vitu vya kuondoa watu katika sifa za kupiga au kupigiwa kura vinatakiwa kuchukuliwa hatua"

OWEK DOZI (Mdau - Kenya)

"Uchaguzi umekuwa ukipata changamoto katika Nchi nyingi za Afrika kutokana na Serikali kuingilia michakato ya kuanzia mwanzo kuelekea katika Uchaguzi"

"Tanzania inaweza kujifunza kujiamini kutokana na kile ambacho kimekuwa kikitokea katika Uchaguzi wa Kenya. Hatutakiwi kuchagua Viongozi ambao wapo na tamaa binafsi, huku Kenya kama kuna kitu mbaya hatuwezi kunyamaza, tunazungumza ili Dunia ijue"

MR. JALOLE (Mdau)

"Naungana na alichosema Kabendera (Eugene Kabendera - CHAUMMA) kuwa Rais aongezwe muda ili tupate nafasi ya kufanya mabadiliko ya Katiba iwe bora na tuwe na Uchaguzi wa Haki"
 
Uchaguzi wetu unakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwa ni pamoja na ukosefu wa usawa katika uwanja wa siasa, udhibiti wa vyombo vya habari na matumizi mabaya ya vyombo vya dola.

Ili kuboresha demokrasia, ni muhimu kuwa na tume huru ya uchaguzi, kuhakikisha uhuru wa kujieleza na kukusanyika, na kusimamia haki za wapiga kura kwa usawa. Vilevile, ushiriki wa wadau wote, bila kubanwa
 
Wakuu,

Tunapoukaribia Uchaguzi Mkuu 2025, ni muhimu kutathmini changamoto za chaguzi zilizopita (2015 na 2020) na kushirikiana katika kutafuta suluhisho

Jiunge nasi kwenye mjadala maalum kupitia X Spaces ya JamiiForums tarehe 30 Januari 2025, kuanzia saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku.

Shiriki kwa kusikiliza, kuuliza maswali na kutoa maoni kuhusu hatma ya demokrasia yetu

Kushiriki, bofya : x.com

Changamoto kubwa ni CCM au nasema uongo ndugu zangu?🌚🌚🌚 johnthebaptist Malaria 2 FaizaFoxy ChoiceVariable Lucas Mwashambwa chiembe Tlaatlaah Mshana Jr Erythrocyte Muite Ngurukia Benjamini Netanyahu Kiranga Nyani Ngabu
 
Wakuu,

Tunapoukaribia Uchaguzi Mkuu 2025, ni muhimu kutathmini changamoto za chaguzi zilizopita (2015 na 2020) na kushirikiana katika kutafuta suluhisho

Jiunge nasi kwenye mjadala maalum kupitia X Spaces ya JamiiForums tarehe 30 Januari 2025, kuanzia saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku.

Shiriki kwa kusikiliza, kuuliza maswali na kutoa maoni kuhusu hatma ya demokrasia yetu

Kushiriki, bofya : x.com
Demokrasia nzuri zaidi, ni muhimu kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi, itapunguza malalamiko mengi hususani vyama vya upinzani
 
Demokrasia nzuri zaidi, ni muhimu kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi, itapunguza malalamiko mengi hususani vyama vya upinzani
Hapa ndio kuna kipengele, waache tume iwe huru ili wapigwe kipigo cha mbwa koko?
 
CCM pia ni kirusi wa taifa hili, ila huu ndio wakati wa kushikamana na kupaza sauti kuhusu mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi kwani muda bado unaruhusu hatujachelewa, bunge lipitishe mswada kisha kabla ya kuvunjwa, sheria zipitishwe na tukutane kwenye box Oktoba
 
Wakuu,

Tunapoukaribia Uchaguzi Mkuu 2025, ni muhimu kutathmini changamoto za chaguzi zilizopita (2015 na 2020) na kushirikiana katika kutafuta suluhisho

Jiunge nasi kwenye mjadala maalum kupitia X Spaces ya JamiiForums tarehe 30 Januari 2025, kuanzia saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku.

Shiriki kwa kusikiliza, kuuliza maswali na kutoa maoni kuhusu hatma ya demokrasia yetu

Kushiriki, bofya : x.com
Tume huru ya uchaguzi ndiyo msingi mzuri wa Demokrasia yetu katika kipindi cha uchaguzi, tumechoka kusikia kuenguliwa kwa wagombea wapinzani, ambao ni uchafu katika uchaguzi wetu kila nyakati. Na kukiwa na uchaguzi wa haki hata vijana watafanya vyema
 
Watanzania hasa usalama wa taifa angalieni mtu mwenye maono ya Magufuli!
Tulimkosea sana kwasababu hatukumjua vyema, hivyo akitokea wa aina yake tutampenda, tutamlinda na kumwombea muda wote ili tuweze kuheshimika hapa Africa na duniani hasa kwenye eneo la uchumi, utamaduni na kijeshi.
Narudia tena kuwakumbusha ninyi usalama wa taifa maana sisi wananchi hatuna maana yoyote mbele ya CCM wakati wa uchaguzi. Angalieni sana mtuletee Magufuli mengine awe anatoka ccm au nje ya CCM!

Tunataka mtu wa kutupeleka mchakamchaka huku akilinda rasilimali za nchi yetu.... Hata mkituletea mwanajeshi sawa tu itakuwa ni vyema.
 
Wakuu,

Tunapoukaribia Uchaguzi Mkuu 2025, ni muhimu kutathmini changamoto za chaguzi zilizopita (2015 na 2020) na kushirikiana katika kutafuta suluhisho

Jiunge nasi kwenye mjadala maalum kupitia X Spaces ya JamiiForums tarehe 30 Januari 2025, kuanzia saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku.

Shiriki kwa kusikiliza, kuuliza maswali na kutoa maoni kuhusu hatma ya demokrasia yetu

Kushiriki, bofya : x.com

========================================

MAONI YA WACHANGIAJI WALIOPO KWENYE MJADALA
AISHA MADOGA - Mwenyekiti wa CHADEMA, Dodoma

"Changamoto mama ya Uchaguzi ni usimamizi wenyewe wa Uchaguzi, hapo ndipo changamoto zote zinapoanzia

Ngazi ya Majimbo msimamizi ni Mkurugenzi ambaye ni Mteule wa Rais na Kada wa CCM, wanaomsaidia ni Watendaji wa Kata na wao ndio wanaosimamia taratibu zote kuanzia ngazi za awali, hapo uhalali unakuwa wapi?"

"Kanuni za Uchaguzi zinaeleza Tume ya Uchaguzi yenyewe ndio inatakiwa kuamua wapi pa kuweka Kituo cha Kupiga Kura, hiyo imesababisha waweke vituo katika Mazingira ambayo yanakuwa magumu kwa Wakala kuweza kufanya Kazi"

Kada wa Chama anakuwa na jukumu la kusimamia Uchaguzi, huyo ndiye ambaye anapaswa kumsimamia Mgombea wa Chama cha Upinzani, ni vigumu kutenda haki

Hivyo hivyo ipo kwa Watendaji wa chini ambao nao asilimia 80 wanakuwa ni Makada wa Chama Tawala
Halafu kwanini mijadala mingi CCM wanakimbia kuzungumza? Bila shaka wanajuwa madudu yao wanayoyafanya
 
Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ndivyo vitalikomboa taifa hili la maziwa na asali, bila wananchi kuungana na kupaza sauti zetu hakuna malaika atashuka kuja kutukomboa
 
Back
Top Bottom