Siku Ukraine ikipewa Lile Kombora za ATAMACS Lenye Range ya 200Miles (320km),Hilo Daraja la Kerch linalounganisha Cremea na Mainland Russia litakuwa matatani. Sema hi Vita Marekani anaipeleka taratibu TU. Walianza kutuma Rifles za Snipers(Majenerali wa Urusi wakapukutishwa Kama kuku wa kisasa),Wakatuma Stingers(Helicopter za Urusi zikadakwa Kama kumbikumbi angani),Wakatuma Javerine(Vifaru vya Urusi viliteketezwa Kama Uyoga). Sasa Wametuma HIMARS(Sasa tunashuhudia Temporary Commanding Centers za Urusi,Maghala ya Silaha na Maghala ya Mafuta yakisambaratishwa).
Hii Vita tukae TU kwa kutulia tutaona mengi. Wasipofikia Makubaliano ya Amani,Pande zote zitapata Matatizo. Sema Jeshi la Ukraine Ni dogo Sana (225,000) ukilinganisha na ukubwa wa Jeshi la Urusi (1.1M). Kwahiyo hata Wakifa kwa uwiano Sawa kila Upande,Ukraine itashindwa mwisho was siku.
KIUCHUMI
Kiuchumi mpaka Sasa Urusi imepoteza mapato mengi Sana. Kwa mjibu wa Takwimu,Urusi imeingiza $ 24B za kuuza Mafuta nchini China na India na $ 12B kwa kuuza Gesi barani Ulaya Tangu Vita vianze ( Miezi 5) Sasa. Kabla ya Vita,Urusi ilikuwa inapata $ 38B kwa mwezi tu kwa kuuza Gesi na Mafuta barani Ulaya. Lakini kwa miezi 5 imeingiza $ 36B TU.