Mizinga aina ya HIMARS (High Mobility Artillery Rockets System)

Kama wewe hujaweka legit source ya taarifa yako then unakuwa hauna tofauti na Mimi tu.

Tuishi
 

Nyie ndo mnalishwa matangopori na US ndo mnaamini yeye ndo kila kitu. US ni taifa linaloendeshwa kipropaganda na media ndo zinawabeba uhalisia ni weupe. Taifa unalolisifia linaongoza kwa tech mpaka sasa HYPERSONIC inamshinda kwa mara 4 mfululizo si aibu hizi.

Labda ndugu yangu utuambie tech alizonazo marekani kwenye silaha ambazo Russia hana. Mimi nimeanza na hyo Hypersonic, uwanja wako
 
Swali hili pia litajirudia hapa.
Wiki iliyopita Ukraine ilishambulia miundombinu ya Mafuta ndani ya Russia Kwa kutumia vile vidrone (quadcopter) vile vinauzwwa AliExpress na Alibaba Kwa Bei rahisi,je ilikuaje Russia yenye mifumo yenye nguvu ambayo mnaisifu kila siku humu kina S400,S300,Pantsir ishindwe kutungua vile vi-obsolete drone?!

Na mpaka sasa Ukraine hawajarusha hata jiwe kwenye hilo Daraja la Crimea waliishia kutoa vitisho tu sijui hizo habari umezitoa wapi

Lakini pia NI ukweli usiopingika na video zipo YouTube ammunition depot, command post zimepigwa Sana na hizo HIMARS Hadi kuna jamaa mtangazi wa Urusi (jina limenitoka) akawa anasema kwann Putin asiishambulie Marekani moja Kwa moja sababu silaha walizopeleka (HIMARS) zinaua watu wao.

NB:Hizo HIMARS si kwamba haziwezi kuharibiwa,La hasha! Ila NI kwamba ni ngumu kuzitarget sababu baada ya mashambulizi zinahama zinaenda mahali pengine. Warusi wakija kufanya counter attack wanapiga empy target sababu mtambo ushahamishwa. Pia mpaka sasa Ukraine iko outgunned na Russia kwenye kila mizinga 40 wao wanaweza kujibu mmoja (outgunned 40:1)
 
Javelin Sikh hizi hazitengenezwi au zimepigwa sanction? Vipi NLAW , stinger???
Vita ilishapita hiyo phase baada ya Russia kukimbia Kiev na kujikita kule Donbas. NLAW na Javellin zilitumika kulipua vifaru na magari ya warusi yaliyokua yakiingia mjini,au umesahau ule msafara wa 40km ulivyosambaratishwa wote?!

Kuhusu stinger,jiulize kwanini mpaka sasa Urusi harushi tena ndege zake kwenye anga la Ukraine anaishia kulauch expensive missiles tokea kwake au baharini.
 
Waasi wa yemen kwa kutumia home made drones jamaa huwa wanalipua mpaka battery za patroit Urusi maeneo mengi ya mipaka yake haina air defense cover ndo maana switch blade drone za USA zilivyo sumbua sana aka deploy laser na mchezo ukaisha sasa marekani hadi leo haina air defense yoyote itaweza ku counter houth drone jamaa. Kwa kutumia pantsir na buk Syria iliyashusha makombora mengi ya Tomahawk wakati patroit ya marekani imeshindwa kushusha fatah misseli za Iran huko Iran ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
 
Jamaa ana bahati ni job moja hivi napiga ila ninge waumbua ha ha ha ha ha ha mwingine anasema eti Urusi haija advance ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
 
Uzuri URUSI sio mtu maneno,iyo HIMARS hata wakipewa elfu 1000 msitegemee mabadiliko yoyote yale kwenye uwanja wa VITA. Kila siku wanapokea SILAHA mpya,wanaipa sifa kibao mwisho wa siku kimya.

Nawapa wiki 2 mtasahau hii mtakuja ni SILAHA nyingine
Ammunition depots na commanding post zinateketea kwa kasi ya ajabu.
 
We unasema expensive BBC wanasema Ni makombora ya kizamani yaso na shabaha imara. Yaani sio high precion kwahiyo Ni ya gharama ndogo. Na pia hii Ni kwasababu Russia wameishinda smart missile Kama iskander na kalibre.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Mimi siko upande wowote ule na nafuatilia toka mwanzo wa huu mzozo.

Sipendi huwo mzozo lakini endapo huyo mnaemtaka aingie (USA) hamjui kwamba kila kitu kitaharibika nikimaanisha hali za uchumi dunain kwasababu asilimia kubwa zimeshikiliwa na yeye.

Na vilevile ni vita vya tatu vya dania nahissi vitakuwepo vizazi vitaumia sana.


Anachokifanya usa labda ni msaada wa silaha tu kwa Ukraine ili awezekujilinda na sio kuingia. Tuacheni ushabiki maandazi wa kwamba urusi amesema hata usa aingie vitani. Hayo tunayo yafurahia tutayachukia ikitokezea kweli hapo mbeleni.


Huku afrika bado tuko nyuma sana kimaendelleo na kwa kila kitu. Mfano tu USA aseme azuiye kila kitu chake kila nchi ijitegemee ikiwemo kiuchumi kiteknologia itakuwaje mfano?? Sitoi ushabiki.


Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Haya ni mahaba tu. Impact za hizo HIMARS hazipo kama Russia ana advance. Pia ni uongo kudhani kuwa ziko mobile na haziwezi kulengwa. Scud iko mobile pia na technology ya zamani ya Russia tena ikiwa USSR. Lkn ziliweza kushambuliwa kipindi cha Saddam Hussein.
Kutumia GPS kwa nchi zetu si kwamba ni bora kuliko system zingine za aina hiyo. Hapo ni sawa na kusema pikipiki za SANLOG toka China ni more advanced kuliko Honda ya Japan au brand zingine, haina maana kuwa gari za japan ndio bora dunia eti kwa kuwa zipo zaidi Afrika. Huenda ni swala la Marketing na ukumbuke Afrika na dunia ni makoloni ya Ulaya kiaina hata sasa.
Ikiwa Kombola likuruka ving"ola katika mji vinaashiria kabla halijafika ishindikane vipi kuwa detected wakati linaruka toka gari ya HIMARS?
Lakini mwisho wa uzuri ni end product. Basi. Kama zinafanya manueverbility zooote hizo na hatusikii Russia wana retreat badala yake wanateka mji mwingine.ni ZERO
 
Hongera. Hongera. Hongera.
Nimesema mara 3. Anaweka ushabiki usio na maana. Hii natokana na ku google halafu anapewa docs yenye sifa za hizo HIMARS tu
Makombola hutunguliwa yakiwa on move , lkn cha ajabu anaaminisha kuwa Russia hana satellite ya kuziona.
Kingine cha ajabu zaidi anasema satellite za USA zinaona tena technology hiyo ndio hutumika tafiti za mafuta na gesi. Sasa swali utajiuliza Urusi yeye hana uwezo wa kugundua gesi na mafuta ardhini?.
Inshort Ushabiki tupu. Lkn nimpongeze kwa upendo alionao kwa USA na washirika wake
 
Kwa taarifa NASA ni ya kijeshi.
 
Ukipata watu wasioegemea upande wowote kama iliyokuwa mwanzoni mwa huu uzi unachota madini sana.
Inawezekana ikawa kweli lkn pia tukiwa wadogo tulidanganywa tulipokuwa wakubwa hata zile stori hawatuambii tena wanajua tunajua
 
Unataka uelewe hizo technology au unataka kujua uelewa wangu??...hapa hatupo kupimana uelewa wa mtu, you can find sources for your own benefit... By the way mada ni HIMARS , sio hizo technology, let's stick to the content
Issue ni HIMARS kuwa Game changer kwa sababu huwezi kuilenga ikipiga with short time inaondoka ilipokuwa wakati inapiga hivyo huwezi kuikuta.
. Je ni KWELI?
Je haipo teknolojia kudetect?
Je HIMARS tu inafanya hivyo?
Kujibu maswali hayo kunazua maswali mengine.
Je moving target zinapigwaje?
Je satellite zinaweza kuona?
Je kombola linaweza kuwa detected lini?
Tusipojihoji tupigwa propoganda ziwe za West au East. Vita pia ni pamoja na propaganda au kutisha.
Binafsi nimejilidhisha sio KWELI kile inafanya HIMARS ndio MRLS inafanya tofauti ni majina na utendaji mdogo mdogo, wa range, accuracy, lkn issue ya movement ziko sawa.
Satellite zinaona movement iwe ni ya USA au RUSSIA.
Mwisho ni matokeo ya ubora vitani. Je inazuia au kumpalalizi adui kuendelea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…