Mizigo yapungua bandari ya DSM

Mizigo yapungua bandari ya DSM

Kama bandari ilijaa mizigo isiyolipwa bora ikae kimya bila mzigo. Foleni zilitapakaa kila sehemu. ..malori yanaziba njia. Halafu hakuna kitu
 
Hizi ni story za vijiweni.[/QUTE]

Mussa Hizi siyo story za vijiweni. Alichosema Mpita njia ni kweli kabisa. Magari ya kutoka Japana (saloons au Haice) yamekuwa yakija yamepakiwa mizigo ndani ambayo haijawa declared kwenye bills of lading. Mara ya kwanza wafanyakazi wa bandari stevedores pamoja na askari wa bandari walikuwa wakiiba sana mizigo hii. Tatizo hili likawa kubwa kiasi kwamba likaleta mzozo mkubwa kati ya wateja, shipping lines pamoja na bandari. Lakini kilichosabaisha mzozo huu siyo tu hii loose cargo ambayo stevedores na askari wa banadari walikuwa wakiiba, bali walianda kuiba na vifaa vingine vya magari kama vile power windows, radio n.k n.k. kwa hiyo elewa kuwa hii michezo imekuwepo sana hapo bandarini.
Na alichokisema mpita njia ni kweli kabisa kwani wakati wa kutoa gari, askari wagetini walikuwa wakiangaria document inasemaje na wakiona gari lina mzigo ndani wakati huo mzigo haujawa declared lazima wakukomalie. Lakini ukitoa kitu kidogo unaachiwa unaenda zako.

Huu mchezo kwa taarifa yako bado unafanyika. Hasa mizigo ya backhresa wanaendelea kukwepa kodi. Mfano mwezi wa Feb mwaka huu, Bakhresa ameingiza container 15 za Laptops, document zinaonyesha kabisa ni laptops lakini transit zinaenda Kigali-Rwanda. Lakini ki-uhalisia Laptop hizi zilikuwa haziendi Kigali bali ulikuwa mzigo wa Local. Container hizi zilitolewa Ijumaa Jioni. zilipotolewa, gari zote zilizobeba containers hizi zilienda kwenye Yard ya Bakhresa iliyoko Mandela road, Container zikafunguliwa zote, Laptop zikatolewa na container kujazwa juice na Maziwa kwa safari ya kwenda Kigali. Wana mtaalamu wao wa kuforge seals za customs hivyo seal inarudishwa ile ile na kama siyo mtaalamu huwezi kujua kama hiyo seal imeishafunguliwa. Wanapofika Mipakani nadhani wanajua wanavyofanya kwa customs ya Rwanda.
Hiyo ndo Tanzania
 
Walikuwa hawalipi kodi..waondoke tu,ni bora tuwe na wachache wanalipa kodi
 
Hali si shwari kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) baada ya wafanyabiashara wa mataifa yanayotumia Bandari ya Dar es Salaam kutafuta sehemu nyingine kiasi cha kusababisha kiwango cha mizigo kupungua kwa asilimia 50.

Bandari hiyo, ambayo ni maarufu kwa usafirishaji wa mizigo inayokwenda na kutoka nchi za Malawi, Congo, Uganda, Burundi na Rwanda, imekumbwa na kadhia hiyo baada ya wafanyabiashara wa nchi hizo kuamua kutumia bandari nyingine za Beira, Msumbiji na Durban ya Afrika Kusini.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga alisema hali ya biashara kwa sasa si nzuri kwa kuwa mtiririko wa shehena za mizigo umepungua ikilinganishwa na miaka iliyopita.

“Miaka yote shehena ya mizigo bandarini ilikuwa ikiongezeka kwa kati ya asilimia 10 mpaka 11, lakini sasa imeshuka mpaka kufikia asilimia 50,” alisema Mhanga kwenye semnina ya wahariri iliyofanyika ofisi za bandari hiyo jana.

Mhanga alitoa mfano wa shehena iliyokuwa ikisafirishwa na wafanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), kuwa imepungua kwa asilimia 50 huku mizigo ya wafanyabiashara wa Zambia ikipungua kwa asilimia 46.

Alitaja sababu zilizochangia kuporomoka kwa biashara hiyo kuwa ni pamoja na wafanyabiashara hao kuanza kukatwa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Alisema tangu sheria ya ulipaji wa VAT ilipopitishwa mwaka jana, wasafirishaji wote wanaotumia bandari hata wale ambao mizigo yao inasafirishwa kwenda nchi jirani, wanalazimika kulipia kodi hiyo.

Sababu nyingine ni utaratibu wa himaya moja ya forodha kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema baada ya kuona mfumo huo unafaa, Tanzania iliamua kuutumia kwa nchi nyingine ambazo hazipo katika jumuiya hiyo.

Alisema katika utaratibu huo, nchi zote zinakuwa na mwakilishi katika ofisi za TPA na masuala ya kodi na mizigo yote inalipiwa ushuru nchini kabla ya kusafirishwa kwenda nchi zao.

“Hili limekuwa mwiba kwa wenzetu wa DRC, kwani nchini mwao mfumo wa ukusanyaji kodi unatoa mianya ya ukwepaji, kwa hiyo kwa kutumia njia hii ni wazi kuwa kila mzigo utalipiwa hapa nchini kabla haujasafirishwa, jambo wanaloona linalowaongezea gharama za uendeshaji,” alisema.

Mhanga alisema kutokana na hali hiyo, kwa sasa wafanyabiashara hao wameamua kutumia bandari za nchi nyingine kupitisha mizigo yao, akizitaja kuwa ni Durban na Beira.

Sababu nyingine aliyoitaja ni kushuka kwa thamani ya Randi dhidi ya Dola ya Marekani, kitu alichosema kinawafanya wasafirishaji kuona kwamba wakipitishia mizigo yao Dar es Salaam wanatumia fedha nyingi kuliko Durban.

“Ulipaji wetu unawalazimisha wafanyabiashara watumie Dola wakati wao wanatumia Randi ya Afrika Kusini na sasa imeshuka, hivyo njia rahisi kwao ni kutumia Bandari ya Durban kwa kuwa watapunguza gharama za usafirishaji,” alisema.

Alisema sababu ya nne ni kukamilika kwa ujenzi wa njia ya reli kutoka Malawi hadi Beira.

Alisema usafirishaji mizigo kwa njia ya reli ni nafuu kwa kuwa unapunguza gharama kwa asilimia 30 na pia hutumia siku chache hivyo wafanyabiashara wengi sasa wanatumia bandari ya Beira badala ya Dar es Salaam.

“Kutofanya vizuri kwa reli yetu ni kikwazo kikubwa kwa biashara ya bandari. Mfano hadi Desemba 2015, jumla ya tani 14.8 zilipita bandari yetu, lakini ni asilimia 0.01 pekee ndiyo iliyosafirishwa kwa njia ya reli na asilimia 99.9 ilisafirishwa kwa barabara,” alisema meneja huyo.

Meneja huyo alisema ili kunusuru hali hiyo, busara inahitajika zaidi, ikiwa ni pamoja na kupitia upya sheria hiyo ya VAT.

Alisema kwa upande wao wameshafanya maboresho ili kuvutia wawekezaji kuja nchini, ikiwa ni pamoja na kuimarisha matumizi ya teknolojia tofauti na awali.

Alisema kwa sasa wamezindua mfumo mpya unaojulikana kama ‘Habour View’ unaosaidia kupokea taarifa zote za meli, mizigo na ulipaji hivyo mteja anaweza kulipia kwa njia za benki na simu.

Alisema wamefupisha muda wa kushusha mzigo katika meli hadi kufika siku mbili tofauti na awali ilipokuwa inachukua siku sita.

Alisema kwa upande wa shehena ya magari, mwaka 2010 uwezo ulikuwa ni kushusha magari 200 lakini kwa sasa wana uwezo wa kushusha magari 700.

Awali, Mkurugenzi wa Masoko wa TPA, Fransisca Muhindi alishauri Serikali kuwekeza katika kutangaza bandari hiyo ili kuinusuru.

“Wenzetu hawalali, wanafanya biashara ya ‘door to door market’(nyumba kwa nyumba), wanawekeza kiasi kikubwa. Ni bahati mbaya sana sisi hatuwekezi. Kuna usemi unasema wekeza shilingi ili upate shilingi,” alisema.

Alisema kwa sasa mzigo wa shaba ambao awali ulikuwa asilimia 60 ya mizigo yote bandarini umeshuka hadi kufikia asilimia 15 huku sababu kubwa ikiwa ni reli
...wewe jipu, tena wa kukatwa hata mguu!!!!!
 
mpita njia povu ulilolitoa si bure mimi binafsi nimekuelewa sema nilitoka kidogo..poa poa mkuu.
 
Mi Na wewe tukae tu, Ila kuna watu wanajua kutumia mianya ya Kodi, kila siku wako ahead of time. Njia moja ikianza kuwekewa Shaka wao fasta wanaanza njia nyingine.

Ila suluhisho ni kupunguza kodi tu,
 
siasa na maigizo ziko wapi hapo....???
Msemo mmoja wa kiswahili unasema UKITAKA UIJUE NGOMA, UINGIE UCHEZE. ni rahisi kuona wenzako wanavurunda na ukalaumu, lakini haki ya Mungu ukipewa wewe utaona ugumu wake. Yawezekana kuna watu walitolewa bandarini kwa mapungufu yao kiutendaji lakini pia kwa ukosefu wa uadilifu, na hilo ni jambo jema. Shida inakuja kwa wachangiaji wengi wa JF wenye mizuka, wanafikiri kuwa wengi wa majipu walikua wabaya kiiivyooo, lakini yawezwkana siyo wote walikua wabaya. Hivyo Meneja mpya ameshaanza kukumbana na changamoto. Sasa hiyo ndo tunaita Jamaa yuko Field anakutana na mambo ambayo ni Real, siyo ya nadharia. Kiutendaji, mambo ya kuandika na kuongea ni rahisi, sasa put into practice, unakuja kugundua makosa kibao. So uvumilivu unahitajika sana kwenye mambo ambayo ni professional! Tuwavumilie wataalam wetu tulio nao, na kama wanataka kupotoka ni bora wakakumbushwa weledi
 
Watanzania ni wapuuzi sana.Kwa hiyo mlitaka mafisadi waendelee kutuibia TPA.Hovyo sana.

Hilo ndio tatizo Kubwa Na sio kwamba limeanzia kwa JK, tunayoyaona sasa ni matokeo ya ufisadi mdogo mdogo ambao ulikuwepo kwa Zaidi ya miaka 40.

40 years ago wazee wetu hawakuwa Na mahitaji makubwa ya pesa kama ilivyo sasa as dunia inavyogeuka ndio watu wanazidi kuhitaji pesa zaidi Na zaidi.

Halafu pia kuna mentality ambayo vijana wengi sasa wanao kwamba lazima awe Na gari simu nzuri avae vizuri, starehe kila weekend haya yote yanachangia katika uongezekaji.

Na sio kama ni kosa lao (vijana) ni system ya kifisadi ambayo wameikuta makazini Na wao wanaiendeleza.
 
mpita njia hapo nimekupata ndio maana nikakwambia izo nchi wazoshusha hasa South Africa wananyekea sana wateja na gharama ndogo kwetu kodi za ajabu ajabu mpaka za kujenga reli sijui ya wapi dola mia na upuuzi..ndio maana tuna mabasi ya ovyo..magari mengi tunayotumia ni ya ovyo pia mkuu wewe eti roli la mchanga mende kodi milion 40? wakati hatuna hata kiwanda cha kutengeneza hayo wanataka walete wao tuu..
 
Acha bandari ife tu!! Tuna watumiaji wa Pombe na sigara takriban million 4.3!! Na wamepokea kwa furaha ongezeko la bei!! Kwanza hao wafanyabiashara hatuna haja nao!! Hatuwezi kuendelea kuwanyenyekea Ebo!!! Hawajui kuwa serikali ya magufuli imejitosheleza kwa kila kitu? Wafadhili tumeshawatimua!! Sasa Hivi ni zamu ya wafanyabiashara, bora bandari yetu tuigeuze Beach!!

Ficha upumbavu wako.

Bora uwe msomaji.
 
Ila ilikuwa raha sana, unanunua gari mfano wa Hiace, unajaza mzigo. Gari Ile unaandisha kama Transit To DRC, kwenye Bill of Lading huandiki ule mzigo una weka gari tu.

Wakati wa kutoa unahonga kama laki pale getini mzigo unaachiwa kutoka.

Unakuja hadi kimara au mbezi unasimama sheli,Canter inakuja inafaulusha mzigo wote, gari tupu unaenda kulitelekeza Tunduma.
Halafu bado kuna watanzania wanabeza juhudi za serikali za kushughulika na uhuni kama huo kwa kuita ni maigizo.kama ni siasa na maigizo mbona wahalifu kama hao wameingia uvunguni na kufyata mikia?Unapotaka kurekebibisha uozo ambao ulikuwa unawanufaisha "wahuni"wachache na kuwaumiza wazalendo walio wengi changamoto ni lazima zitajitokeza,muhimu ni kukaza buti na belt anayesema ni maigizo yeye ndiye anafanya maigizo manake ni hakika kimoyo moyo anaisoma number ingawa mdomoni anaita maigizo-watu kama hawa ni kuwaacha wafe na tai shingoni.
 
Hivi huyu mwanahabari huru mzima kweli huyu? Angekuwa jirani yangu ningemuomba kumuuliza swali na ningemuuliza 'hivi wewe una akili kweli wewe?"
 
Na vipi sasa yule alieenda kujipachika kqenye chama lenu
Hili ndio tatizo la Tanzania, siasa imewekwa mbele. Siasa ndio inayodumaza ukuaji wa uchumi wa nchi.

Ni wakati sasa wa kuacha siasa Na kuwa wazalendo.
 
Kwenye kampeni walikuwa wanadanganya watu kuwa wakichaguliwa watejenga reli ya kisasa,baada ya kuchaguliwa wameruka kimanga kwamba kujenga reli ya kisasa ni ngumu na haiwezekani,kwa mapato ya serikali itachukua miaka 30 ili kukamilisha ujenzi.Sasa wanaanza kukiona kwa uongo wao
Kwa kweli naichukia sana ccm
 
Back
Top Bottom