Mizigo yapungua bandari ya DSM

Mizigo yapungua bandari ya DSM

Reli huwa inahujumuwa na Wamiliki wa Magari makubwa ya mizigo na mafuta , wanajua Reli ikifanya kazi watalala njaa hivyo huwatuma watu kwenda kuharibu reli na vichwa vyake .
Nakuunga mkono kwa 100% hao wamiliki wa hayo magari ndio wahujumu no 1wa miundombinu ya reli
 
Usafiri wa Reli umetushinda. Wa Anga pia umetushinda..... Na bado tunawapenda wenyewe na tunawachagua wenyewe. Acha tuisome namba. Hamna jinsi tena
Ccm ni nyonya damu
 
Wafanyabiashara wakubwa Wamiliki wa Magari ya mizigo na mafuta ambao wengi ni wafadhili wa ccm hawataki kusikia Reli inaanza kazi kabsa wanajua kuwa ikianza kazi wataathilika sana .
Umesahau pia na viongozi wengi wa serikali nikati ya wamiliki wakubwa wa hayo , magari makubwa ya mizigo
 
Naukumbuka sana Wimbo wa BAHATI BUKUKU, hakukosea. Unapoianza safari wanakupa matumaini, unapoonesha nafanikio wanaanza vikwazo, wewe mleta mada ni mmoja wa wale wanaonza vikwazo katika safari aliyoianzisha Magufuli.
Ccm ni ileile tu, dawa yenu ni kuwaondoa tu majizi wakubwa
 
Naona baadhi ya wachangiaji humu wana shutumu wenye malori ndiye wanahujumu kusiwepo huduma nzuri y a reli,nikisoma hii habari inelezea mizigo inayokuja bandari ya DSM, sasa hiyo mizigo huja wa meli sasa hawoa wenye malori wanahusika vipi kupunguza mizigo bandari ya Dar?
Mizigo kusafarishwa kwa reli au malori kwanza lazima yaje kupitia bandari ya Dar, ikashafika Dar ndipo husafirishwa kwa reli au kwa malori,hapo kiancho elezewa na mizigo kupungua banadirini ambaye mwenye mzigo ndiye option ya kupeleka atakako iwe kwa reli kama ipo kwa malori,sasa humu watu wamegana wenye malori !wenye mlori!Hata sielewei.
 
Bado magu hajamaliza mwaka mambo yote yanaharibika, kiuhalisia magu hana mvuto kibiashara kwa mengi tu, ukiachana na hao wafanyabiashara wakwepa kodi.nnachoona anapiga mikwara mingi sijui kwa sababu ya media au, na ukizingatia kwa staili ya watu wanavyosimamishwa bila kufata taratibu ni wazi sasa na hao wafanyabiashara wameona huenda wakatolewa chambo kua wanakataa kulipa kodi.mheshimiwa jitahid kutengeneza mazingira mazuri kwa wafanyabiashara huku msisitizo kua watoe kodi na kuiingizia serkali mapato
 
WAKATI Mamlaka ya Bandari (TPA) ikithibitisha ufanisi katika upakuaji na uondoshaji mizigo na usalama wa mali katika Bandari ya Dar es Salaam, imebainika idadi ya mizigo katika bandari hiyo, imepungua tofauti na matarajio.

Akizungumza wakati akifunga warsha ya Wahariri wa Habari mwishoni mwa wiki, Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga, alitoa mfano wa shehena ya magari yanayokwenda Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).

Kwa mujibu wa Mhanga, shehena ya magari yanayokwenda katika nchi hiyo kutoka Januari 2015 mpaka Januari 2016, imepungua kwa asilimia 50 huku shehena ya Zambia ikipungua kwa asilimia 46. Beira Mhanga alisema walipochunguza sababu ya kupungua kwa shehena hizo, walibaini sehemu ya shehena hiyo hasa iliyokuwa ikienda Zambia, DRC na Malawi, inashushwa katika Bandari ya Beira nchini Msumbiji.

Sababu za kushushwa katika Bandari ya Msumbiji, badala ya Bandari ya Dar es Salaam ambayo ndiyo yenye unafuu wa umbali kutokana na jiografia yake, Mhanga alisema ni unafuu wa kusafirisha shehena hiyo kwa reli ya Beira mpaka Malawi, tofauti na ilivyo kwa barabara.

Alisema usafirishaji wa reli ni nafuu kwa asilimia 30, ikilinganishwa na usafirishaji wa barabara na kwa kuwa Msumbiji wameshakamilisha ujenzi wa reli ya kisasa, wafanyabiashara wameona unafuu wa kupitisha mizigo katika Bandari ya Beira kuliko ya Dar es Salaam.

Athari hiyo katika Bandari ya Dar es Salaam, huenda ikawa mbaya zaidi baada ya kukamilika kwa reli ya kisasa inayoanzia katika Bandari ya Mombasa mpaka DRC, kwa kuwa itaongeza unafuu wa usafirishaji wa mizigo katika bandari hiyo shindani kwa Tanzania.

Katika warsha hiyo, ilifafanuliwa kuwa dunia nzima bandari zimekuwa na mafanikio, kutokana na kuwa na mfumo wa reli za kisasa unaotoa mizigo bandarini na kufikisha kwa mteja, jambo linalokosekana katika Bandari ya Dar es Salaam.

Durban Shehena nyingine iliyokuwa ikipitia nchini, imebainika kupelekwa katika Bandari ya Durban nchini Afrika Kusini kutokana na unafuu uliotokana na matumizi ya fedha ya nchi hiyo, Rand, katika utozaji wa gharama za kutoa mizigo, tofauti na Tanzania ambako gharama hutozwa kwa Dola ya Marekani.

Akifafanua hali hiyo, Mhanga alisema kwa sasa Rand imeshuka thamani na hivyo mfanyabiashara mwenye Dola ya Marekani, atatumia Dola chache za Marekani kulipia tozo hizo kwa Rand ya Afrika Kusini iliyoporomoka thamani.

Kutokana na hali hiyo, ingawa gharama za utoaji mizigo kati ya Bandari ya Dar es Salaam na Bandari ya Durban zinalingana, lakini mfanyabiashara akipitisha mzigo Afrika Kusini, atatakiwa kubadilisha Dola ili apate Rand ya kulipa gharama hizo; na kwa kuwa Rand imeporomoka thamani, atatumia Dola chache kuliko ilivyo kwa Tanzania.

Utambuzi wa mizigo Changamoto nyingine aliyotaja Mhanga ni ya mfumo wa kutambua shehena zilizoko katika meli, unaotumiwa kukadiria gharama za utoaji wa mizigo bandarini pamoja na kodi. Akifafanua, Mhanga alisema mzigo unapopakiwa katika nchi unakotoka, mpakiaji anapaswa kueleza aina ya mzigo katika fomu maalumu ya kutambulisha mzigo.

Fomu hiyo inayojazwa na mpakiaji, ikifika Dar es Salaam kabla ya kupakua mzigo, hutumiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kukadiria kodi. Hata hivyo Mhanga alisema fomu hiyo inapokosewa na mpakiaji, TRA wakati wa kuhakiki mzigo huhisi harufu ya ukwepaji kodi na hivyo utaratibu wa utoaji wa mzigo husika, huchukua muda kuliko kama fomu hiyo isingekosewa.

Mhanga alisema wakati utaratibu wa kurekebisha makosa hayo ya fomu ukichukua muda mrefu kabla ya kuruhusiwa na TRA, mzigo huo huchajiwa adhabu ya kukaa bandarini kwa muda mrefu na kama ni wa nje ya nchi, mteja hulazimika kukaa Dar es Salaam kwa kosa lililofanywa na mpakiaji wa mizigo.

Meneja huyo wa Bandari ya Dar es Salaam, alisema mteja huyo anaporuhusiwa na TRA kuchukua mzigo, wakati ameshaingia gharama ya kuishi Dar es Salaam kwa muda mrefu, akifika bandarini na kukutana na adhabu ya kuhifadhi mzigo ambayo hakuisababisha, wengi hukasirika na hajui wanapeleka ujumbe gani kwa wateja wengine katika nchi zao.

Ufanisi Pamoja na changamoto hizo, Mhanga alisema kama wadau wengine wakikamilisha taratibu za ukaguzi wa mzigo mapema, mzigo huchukua muda mfupi kupakuliwa katika meli na kuondolewa mapema bandarini, ili umfikie mteja katika muda mfupi zaidi.

Alitoa mfano wa mwaka 2011, ambapo mteja alitumia siku 4.7 kusubiri mzigo wake utoke bandarini, lakini leo mteja huyo huyo atasubiri siku 0.2 mpaka apate mzigo wake na hilo limesababishwa na uboreshaji wa utaratibu wa kupata vibali vya nyaraka, ambao kwa sasa unafanyika kwa mtandao.

Mhanga alisema bandari hiyo kwa sasa inakamilisha ujenzi wa jengo la ghorofa 35, ambalo litakuwa refu kuliko yote Afrika Mashariki na Kati, litakalohifadhi wadau wote wa bandari katika jengo moja, ili mteja akiingia katika jengo hilo, akitoka akatoe mzigo wake moja kwa moja.

Kwa sasa mteja anaweza kujikuta akihangaika na nyaraka zake kwa wadau mbalimbali wa Bandari ya Dar es Salaam kupata vibali, ikiwemo Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchikavu (Sumatra), Shirika la Viwango (TBS), Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Idara ya Uhamiaji, Idara ya Afya, Mkemi Mkuu na wengineo
Ushauri huo ulipashwa kuelekezwa kwa serikali kwa maana ya wizara ya mawasiliano. Prof Mbawalla namwaminia hilo atakuwa ameliona na atalifanyia kazi
 
Bado magu hajamaliza mwaka mambo yote yanaharibika, kiuhalisia magu hana mvuto kibiashara kwa mengi tu, ukiachana na hao wafanyabiashara wakwepa kodi.nnachoona anapiga mikwara mingi sijui kwa sababu ya media au, na ukizingatia kwa staili ya watu wanavyosimamishwa bila kufata taratibu ni wazi sasa na hao wafanyabiashara wameona huenda wakatolewa chambo kua wanakataa kulipa kodi.mheshimiwa jitahid kutengeneza mazingira mazuri kwa wafanyabiashara huku msisitizo kua watoe kodi na kuiingizia serkali mapato
Good point, Ila ku blame Serikali moja kwa moja its not fair.

Labda nnachoona wangeregeza kidogo hii ishu ya mizigo yote kuwa lazima ilipiwe hapa badala yake wangekuja Na system ambayo itawabana wafanya Biashara waliokuwa wanashusha mizigo njiani ambao kwa mwaka 2014/2015 walikwepa kodi zaidi ya bil 900.
 
Ccm ni ileile tu, dawa yenu ni kuwaondoa tu majizi wakubwa
Sioni kama chama kinahusu, kumbuka watu wa TPA ni civil servants, hata chama gani kishinde wanabaki hao hao.

Kikubwa ni kuwasaport ili mishahara yao yakidhi mahitaji hao ya kila siku, ili kuondoa wizi Na Rushwa.

Kwani hata chadema ikiingia Na kufukuza wafanya Kazi wote Bandari nzima still kama mishahara midogo watu wataiba tu.

Chama sio tija. Weka Siasa pembeni Fanya Kazi.
 
Naona baadhi ya wachangiaji humu wana shutumu wenye malori ndiye wanahujumu kusiwepo huduma nzuri y a reli,nikisoma hii habari inelezea mizigo inayokuja bandari ya DSM, sasa hiyo mizigo huja wa meli sasa hawoa wenye malori wanahusika vipi kupunguza mizigo bandari ya Dar?
Mizigo kusafarishwa kwa reli au malori kwanza lazima yaje kupitia bandari ya Dar, ikashafika Dar ndipo husafirishwa kwa reli au kwa malori,hapo kiancho elezewa na mizigo kupungua banadirini ambaye mwenye mzigo ndiye option ya kupeleka atakako iwe kwa reli kama ipo kwa malori,sasa humu watu wamegana wenye malori !wenye mlori!Hata sielewei.
Wamiliki wa Magari makubwa ya mizigo na mafuta hawataki kusikia Reli inafufuliwa kamwe Kwa sababu wanajua kuwa Reli ikibeba mizigo na mafuta hawana pa kupata pesa wataathilika sana, na endapo Serikali wanalazimisha Reli ifanye kazi lazima watakuwa wakiihujumu ili wateja waikatae Reli na kurudi kwao, huko Bandarini kuna Vioja vingi usumbufu mwingi usio wa lazima , mpangilio mbaya wa Ofisi za kutoa mizigo nk .
 
Jamani hacheni kudanganya, hizo gari za kwenda Cjui Zaire Zambia zimepungua kwa sababu ukweli zilikuwa haziendi huko, zinaishia kwny showrooms na yard za hapo hapo bongo.
Sasa wamebanwa wanaanza tafuta jinsi ya kukatisha watu tamaa, kwanza magari yanayopita kwenda nje ya nchi wanacholipa TPA Ni port fees tuu na gharama nyingine ndogo na sio kodi wala nn, sasa uchumi utatetereka vp kwa hivyo viport fees vyao???????
Vitu kama hivi vinanifanya nijiulize wasomi wetu wako wapi maana hii Ni total lies!!!?
 
Bandari ya Dsm imejaa mapungufu mengi sana 1- foleni za Meli kuingia bandarini 2- Ofisi za kutolea mizigo zimekaa shagalabagala zig zaga hawana mpangilio Kama kule Mombasa , Darban nk, 3- ucheleweshaji wa makusudi hasa Kwa wale wenye Bandari kavu lengo mteja alipe Storage pesa ambayo inaliwa na wajanja wachache na imesababisha wengi kutelekeza Mali zao huko na kuishia kufirisika huku wakidaiwa na mabenk nk 4- ukadiriaji wa Kodi bado ni Tatizo kubwa utakuta mizigo inafanana lakini kila mmoja kalipa Kodi yake 5- udokozi wa mizigo na wizi wa vifaa kwenye Magari Bado upo licha ya kujinadi kuwa imepungua , yapo mengi mapungufu ni vigumu kuyaainisha yote Kwa wakati mmoja .
 
Hizo Gari zenyewe zitakuwa chache mkuu , lakini Ukweli Bandari ya Dsm ina mapungufu mengi sana Serikali lazima ijipange kupunguza kero Sugu ambazo zimefugwa tokea awamu ya kwanza mpaka Sasa ,
 
Hii ni changamoto kwa serikali ila kuna kitu ameacha kukisema.. Watu wanakwepa kulipa gharama halali za kuingiza mzigo watu walizoea rushwa sasa hizi bandari za wenzetu bado staili ni ile ile ya rushwa mbele.
durban hamna rushwa mkuuu
wako vzuri@
 
Biashara ni changamoto.

Changamoto za kibiashara haziishi lakini kilicho cha muhimu ni kuwa na uwezo wa kuzitambua changamoto na kuzifanyia kazi kabla hazijatokea au hazijawa tatizo kubwa.

Aliyeua reli ya Kati na ile iendayo Kigoma alaaniwe katika maisha yake.
imekufa awmu gani mkuu?
 
Jamani hacheni kudanganya, hizo gari za kwenda Cjui Zaire Zambia zimepungua kwa sababu ukweli zilikuwa haziendi huko, zinaishia kwny showrooms na yard za hapo hapo bongo.
Sasa wamebanwa wanaanza tafuta jinsi ya kukatisha watu tamaa, kwanza magari yanayopita kwenda nje ya nchi wanacholipa TPA Ni port fees tuu na gharama nyingine ndogo na sio kodi wala nn, sasa uchumi utatetereka vp kwa hivyo viport fees vyao???????
Vitu kama hivi vinanifanya nijiulize wasomi wetu wako wapi maana hii Ni total lies!!!?
mkuu umeongea point sana
kwahiyo nan kadanganya mkuu?????
tupe point mkuu kuna kitu hujafunguka .........
 
Bandari ya Dsm imejaa mapungufu mengi sana 1- foleni za Meli kuingia bandarini 2- Ofisi za kutolea mizigo zimekaa shagalabagala zig zaga hawana mpangilio Kama kule Mombasa , Darban nk, 3- ucheleweshaji wa makusudi hasa Kwa wale wenye Bandari kavu lengo mteja alipe Storage pesa ambayo inaliwa na wajanja wachache na imesababisha wengi kutelekeza Mali zao huko na kuishia kufirisika huku wakidaiwa na mabenk nk 4- ukadiriaji wa Kodi bado ni Tatizo kubwa utakuta mizigo inafanana lakini kila mmoja kalipa Kodi yake 5- udokozi wa mizigo na wizi wa vifaa kwenye Magari Bado upo licha ya kujinadi kuwa imepungua , yapo mengi mapungufu ni vigumu kuyaainisha yote Kwa wakati mmoja .
duh
sasa ni kwanini lkn.,..
dah aisee kma nikweli bas tuko nyuma sana mkuu.........
 
Back
Top Bottom