Unachosema ni kweli, lakini kwa maana ya uzi huu, havina uhusiano wa moja kwa moja. Kinachotajwa ni meli kupungua baada ya waleta mizigo kuikacha bandari yetu, hicho ndicho nilichomuelewa mleta uzi na hata Meneja wa Bandari amezungumzia meli kupungua.Wamiliki wa Magari makubwa ya mizigo na mafuta hawataki kusikia Reli inafufuliwa kamwe Kwa sababu wanajua kuwa Reli ikibeba mizigo na mafuta hawana pa kupata pesa wataathilika sana, na endapo Serikali wanalazimisha Reli ifanye kazi lazima watakuwa wakiihujumu ili wateja waikatae Reli na kurudi kwao, huko Bandarini kuna Vioja vingi usumbufu mwingi usio wa lazima , mpangilio mbaya wa Ofisi za kutoa mizigo nk .
Ni kweli kwa muda mrefu kumekuwa na shutuma za wenye malori(ambao ashkumu si matusi wengi ni viongozi) wakitajwa kuhujumu jitihada za kuifanya reli iwe imara,hilo liko wazi!