Mizengo Pinda: Mwalimu alikataa kuwa 'dictated' na watu kutoka nje kwa sababu ya misaada

Mbali ya uchumi, Mwalimu alikuwa na kazi ngumu sana kuliunganisha Taifa kuwa moja na ukabila ukafutika, hiyo ilikuwa kazi ya kutukuka sana, Cha ajabu, ikaharibiwa ndani ya kipindi kifupi tu cha m iaka 6.
Labda hiyo tui ndio Kazi pekee ya kitukuka aliyoifanya..

Dhalimu shujaa wa Africa akapanda tena mbegu ya chuki ,ukabila,ukanda na migawanyiko mingine
 
Huo ndio ubaguzi?

Mbona chadema huwa mnasema tusichague ccm?
Chama kuvutia kwake ni sawa, lakini viongozi wanaosimamia uchaguzi kutishwa eneo lake akipita mpinzani ataona, haliko sawa. Chaguzi za CCM Sasa tunaziona ni 100%. Ndugai 100%, Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM 100%, uchaguzi wa Spika Tulia 100%, uchaguzi wa naibu Spika 100%. Mwenyezi Mungu mwenyewe hawezi kupata 100% kwa sababu mpinzani shetani yupo, Sasa tumejengewa utamaduni wa CCM 100%. Kupita bila kupingwa ni upuuzi wa awamu ya 5.
 
Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mizengo Pinda akiwa kwenye kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa Taifa, hayati Mwl. Nyerere ameongelea misaada na masharti yanayokuja nayo. Pinda amesema mwalimu alikataa katakata misaada yenye masharti yasioendana na Maslahi ya Taifa.

========

Mizengo Pinda: Kwenye uchumi pamoja na mambo mengine yote, vita ya Uganda na vinginevyo lakini wale mnaojua kilichokuwa kimetokea, nilipenda mimi binafsi, jeuri yake alikuwa anakataa kuwa 'dictated' na watu kutoka nje just because kuna misaada anataka akupatie. Mwalimu alikuwa mgumu sana, alikataa kabisa. Bora nikafe na umasikini wangu lakini hilo unalotaka nifanye siwezi.

Leo wangapi, tukibanwa na mambo hayo mazuri yanayotaka kuja na hili na lile, how many of us wako tayari kutoa masharti ambayo unaona hayaendani maslahi ya Taifa? Lakini yeye aliweza na nakumbuka mzee Mwinyi alipoingia kama Rais wa pili alikutana na hilo jambo, sasa ikawa ngombo. Mwalimu alikuwa na uwezo wa kulibeba hata kama hamjui litaishaje lakini tutafika huko.

=> Kuhusu Mkapa, Pinda amesema pamoja na kuleta 'Ukapa' alipomaliza miaka kumi watu walitamani aendelee.
Kwa Mwalimu👍,lakini kwa Mkapa simuungi mkono.Ila Pinda anajua yaliyomtokea Ndugai?Shauri yake.
 
Chama kuvutia kwake ni sawa, lakini viongozi wanaosimamia uchaguzi kutishwa eneo lake akipita mpinzani ataona, haliko sawa. Chaguzi za CCM Sasa tunaziona ni 100%. Ndugai 100%, Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM 100%, uchaguzi wa Spika Tulia 100%, uchaguzi wa naibu Spika 100%. Mwenyezi Mungu mwenyewe hawezi kupata 100% kwa sababu mpinzani shetani yupo, Sasa tumejengewa utamaduni wa CCM 100%. Kupita bila kupingwa ni upuuzi wa awamu ya 5.
Ni lini viongozi wa ccm hawajawahi kupita bila kupingwa,?

Ok.. Hiyo ni awamu ya tano vipi hii ni ya ngapi?
 
Back
Top Bottom