Mbunge Dkt. Mhagama: Wafanyabiashara wengi wanashindwa kufanya biashara nje ya Nchi kwa kuwa hawana Dola, hili ni tatizo kubwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464

Wabunge wamechangia kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2024/2025 pamoja na muongozo wa maandalizi ya Mpango wa Bajeti Mwaka 2024/2025, leo Novemba 7, 2023.

Akichangia hoja, Mbunge wa Jimbo la Madaba, Dkt. Joseph Kizito Mhagama amesema Wafanyabiashara wengi wakubwa wameshindwa kufanya biashara nje ya Nchi kwa kuwa hawana Dola na hilo ni tatizo kubwa sana Kiuchumi, hatuwezi kuichukulia kwa wepesi, lazima tulichukulie katika uzito mkubwa.”

Ameongeza kuwa kati ya Mwaka 2021 na 2022 nakisi imeongezeka kwa 54.8% ambalo ni ongezeko kubwa.

Amesema “Sitataja zile zilizo nje ya uwezo wetu kama vita ya Ukraine na Urusi, lakini sababu ambazo Kamati imezitaja ni kama uingizaji wa bidhaa za ujenzi kutoka nje ya Nchi kwa kuwa kuna miradi mikubwa tunajenga, pia kuna bidhaa nyingi tunaagiza kutoka nje ikiwemo mbolea, mafuta ya kula, ngano na mazao ya Petroli.”
 

Wabunge wamechangia kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2024/2025 pamoja na muongozo wa maandalizi ya Mpango wa Bajeti Mwaka 2024/2025, leo Novemba 7, 2023.

Akichangia hoja, Mbunge wa Jimbo la Madaba, Dkt. Joseph Kizito Mhagama amesema Wafanyabiashara wengi wakubwa wameshindwa kufanya biashara nje ya Nchi kwa kuwa hawana Dola na hilo ni tatizo kubwa sana kiuchumi, hatuwezi kuichukulia kwa wepesi.”
 

Attachments

  • 7670883B-139C-48C9-83D6-A5A34724E34C.jpeg
    7670883B-139C-48C9-83D6-A5A34724E34C.jpeg
    71.4 KB · Views: 1
Back
Top Bottom