Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amekiri kuwa Bunge Maalumu la Katiba, limeanza na changamoto, huku akihoji wanaotaka Serikali ya Tanganyika, wanakusudia ipi ya mkoloni au ya baada ya uhuru ya miaka mitatu.

Mbali na hilo, amesisitiza yeye na chama chake cha Mapinduzi wanataka mfumo wa serikali mbili na si tatu kama Rasimu ya Katiba ilivyopendekeza.

Amekiri kuwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo, utakuwa na misukosuko mingi, lakini utavuka salama.

Pinda aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya viongozi na watendaji wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye Makao Makuu ya chama hicho, White House mjini hapa.

Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alisema zipo hoja nyingi za msingi katika mchakato huo wa kutunga Katiba, lakini kubwa na litakalochukua muda mwingi ni muundo wa Serikali. Hata hivyo, alisema wazi msimamo wake na ule wa CCM kuhusu pendekezo lao la kuwa na Serikali mbili, kinyume cha Rasimu ya Katiba inayopendekeza Serikali tatu.

Hata ukiniamsha usingizini usiku wa manane, kwangu mimi bado Serikali mbili ni muundo mahsusi.

Mwalimu Nyerere hata wakati ule alikaa na Tanganyika kwa kipindi kifupi, mwaka 1961 Tanganyika ikawa huru, 1962 tukawa Jamhuri, 1963 Zanzibar ikapata uhuru (baadaye alisema Uhuru wa bandia), mwaka 1964 ikazaliwa Tanzania.

Tanganyika ya kikoloni ndiyo iliyokaa muda mrefu, hii nyingine ni kutoka mwaka 1961, 1962 na 1963. Ikazaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo hii miaka 50 tuko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunadai Tanganyika, alihoji Pinda na kuongeza:

Tanganyika ipi? Nikadai ile ya mkoloni? Kipi kimo katika Tanganyika ya miaka mitatu? Tanganyika wakati inazaliwa nilikuwa na miaka 13, Tanzania nilikuwa na miaka 16, naujua vizuri Muungano. Kuanzia pale sijui chochote kingine, kama ilivyo wengi wetu humu.

Au wale waliozaliwa miaka 50 iliyopita, wanaijua vizuri zaidi Tanzania. Tanganyika ipi mnazungumzia? Maana haikuwapo zaidi ya ile ya kikoloni iliyokaa muda mrefu.

Alisema njia bora ni kukaa chini na kuzungumzia matatizo ya muundo wa Serikali mbili na kuyaboresha kwa nia ya kusonga mbele kuliko kudai Serikali ya Tanganyika. Waziri Mkuu alisema si vyema kuanza sasa kujaribu muundo wa Shirikisho baada ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, huku akitolea mfano wa Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC).

Pale kuna Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini angalia mambo yanavyokwenda sasa wakubwa wakikutana. Utasikia wanazungumzia ardhi, mara pasipoti.

Haiwezekani miaka 50 baada ya Muungano tuanze majaribio ya Shirikisho. Aah, wapi tunataka kwenda. Tanzania Bara na Zanzibar wana historia ya udugu na ushirikiano. Ukaribu, lugha moja na kuoleana, alisema Pinda.

Huku akirejea kauli mbalimbali za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisema hata hilo Shirikisho linalopendekezwa litakwama, kwa sababu Rais wake hatakuwa na ardhi, na kama nchi wanachama zitakataa kutoa ardhi, atafanyaje kazi zake.

Alisema tatizo lililopo ni utambulisho wa Zanzibar na suala la umiliki wa ardhi kwa Tanzania Bara wakiwa visiwani, ambayo alisema ni mambo yanayozungumzika.

Suala hapa ni utambulisho wa Zanzibar ambalo hata hivyo si suala kubwa na tunaweza kulisahihisha. Pia liko suala la ardhi Zanzibar. Lakini wanaotaka ardhi huko, lazima wajiulize je, kweli iko ardhi ya kutosha, alieleza.

Akizungumzia Bunge Maalumu la Katiba alisema, Tumeanza mchakato wa kutunga Katiba, lakini tayari kuna changamoto zetu, lakini tumeanza kwa kuchagua Mwenyekiti wa Muda na kutengeneza Kanuni wiki ijayo zitakuwa tayari ili tulifikishe mwisho hili, alisema na kuongeza:

Bunge Maalumu la Katiba limeanza vikao vyake wiki iliyopita, lakini wiki ijayo linatarajiwa kuanza mijadala baada ya kupitishwa kwa Kanuni na kuchaguliwa kwa Mwenyekiti na hatimaye kuzinduliwa rasmi.

Hata hivyo, tayari kuanza hali ya sintofahamu kwa wabunge kuanzia kudai suala la nyongeza ya posho, hadi katika vikao vyao ya kazi ambako zimeshuhudiwa kauli zinazoashiria kazi nzito mbele na inayopaswa kuwa na udhibiti ili mijadala isitawaliwe na jazba na kutekwa na makundi yaliyowapeleka bungeni humo.

Aliwaomba wajumbe wa semina hiyo ya Jumuiya ya Wazazi kuwaombea wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, watimize majukumu yao kwa maslahi ya Taifa.

Kwa hisani ya Habari leo.
Watanganyika wenzangu kwa maneno ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, suala la Tanganyika litabakia kuwa historia.

Cc; Nguruvi3 Mag3 Mzee Mwanakijiji JokaKuu WildCard Mkandara Ngongo

Tutabaki kupambana kwenye forums tu, wako wapi Watanganyika watakaoweza kuirudisha Tanganyika yao.
 
Last edited by a moderator:
TRA, Uhamiaji, Polisi na JWTZ hawapo huko?
Hiyo TRA ni ile ambayo ukinunua gari Zanzibar na ukakadiriwa kodi na TRA znz , ukifika bandari ya Dar unatozwa kodi upya ? Kama umetoka nchi ya kigeni au unazungumzia ipi? Mbona ukipitisha gari Sirari au Holili hutozwi upya kodi na TRA za mikoa ya mara au Kilimanjaro ? Sasa unazungumzia TRA ipi hiyo?
 
Kila mtu ana msimamo wake juu ya hili. Pinda anaweza kuwa sahihi kwa maoni yake lakini pia wanaotaka serikali 3 nao wako sahihi kwa maoni yao. Kuhusu Tanganyika kwamba haikudumu kwa muda mrefu thats none sense kwa sababu historia inasema Tanganyika ilikuwepo hata kabla ya kuja lwa wakoloni wa Kijerumani japo walishi kwa makundi madogo madogo kama ntemiship na clanship
 
Watanganyika wenzangu kwa maneno ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, suala la Tanganyika litabakia kuwa historia.

Cc; Nguruvi3 Mag3 Mzee Mwanakijiji JokaKuu WildCard Mkandara Ngongo
Pinda ni waziri mkuu wa Tanganyika , ndio maana hana mamlaka Zanzibar , mamlaka yake inatisha Chumbe........hata wakuu wa mikoa na wilaya Zanzibar wanawajibika kwa Seif Idd na wanateuliwa na Shein ........sasa Pinda hajui hata anata wala wapi ........
 
Hiyo TRA ni ile ambayo ukinunua gari Zanzibar na ukakadiriwa kodi na TRA znz , ukifika bandari ya Dar unatozwa kodi upya ? Kama umetoka nchi ya kigeni au unazungumzia ipi? Mbona ukipitisha gari Sirari au Holili hutozwi upya kodi na TRA za mikoa ya mara au Kilimanjaro ? Sasa unazungumzia TRA ipi hiyo?

Mkuu tuzungumzie uwepo wake kwanza. Hilo la namna inavyooperate nalo lina sehemu yake! Hata hivyo, Zenz huwa wanapenda kuwa treated kama nchi jirani. Sasa malalamiko ya nini hapa?
 
Namuunga mkono moja kwa moja eti mtu ana miaka 25 eti kwa sababu kapata tiketi ya kuingia bungeni kama mjumbe unasikia anasema serikali Tatu wakati hata wakati Tanganyika inapata uhuru hakuwepo,Pinda nakupongeza kwa msimamo wako thabiti

Tanganyika yenu hamuitaki! maajabu haya.
 
Pinda ni waziri mkuu wa Tanganyika , ndio maana hana mamlaka Zanzibar , mamlaka yake inatisha Chumbe........hata wakuu wa mikoa na wilaya Zanzibar wanawajibika kwa Seif Idd na wanateuliwa na Shein ........sasa Pinda hajui hata anata wala wapi ........

Wakuu wa Usalama, JWTZ, TRA, Uhamiaji, nk wanateuliwa na wako chini ya nani?
 
Mkuu tuzungumzie uwepo wake kwanza. Hilo la namna inavyooperate nalo lina sehemu yake! Hata hivyo, Zenz huwa wanapenda kuwa treated kama nchi jirani. Sasa malalamiko ya nini hapa?
Nani kalalamika ? Nilikuwa na kuonyesha jinsi ambavyo Pinda ni waziri mkuu wa Tanganyika ila hajitambui , naye anahoji watu wanatak Tanganyika ipi kwani yeye ni waziri mkuu wa wapi? Tanganyika ikivua koti la Muungano hapo Muungano utaweza kuimarika na kuwa imara , sio kama sasa Muungano umeiva koti la Tanganyika
 
Nani muanzilishi Wa hoja ya serikali tatu na nini ilikuwa malengo yake? Nauliza tena
 
Naona kwa watawala na CCM uwepo wa serikali ya Zanzibar ni kitu hakina mjadala yaani hapo serikali moja tayari ipo ingawa bado kuna tafrani ni serikali ya aina gani (kimadaraka). Uwepo wa serikali ya Tanganyika ndio kitu wanaopenda serikali mbili hawataki kusikia, wakatupa kitu kinaitwa "Tanzania Bara'. Lakini ukweli hakuna serikali ya Tanzania bara bali tunategemea JMT kutawala Tanzania bara. Na tatizo liko hapa yaaani serikali ya JMT ambayo kwa muundo wa sasa ndio serikali ya Tanganyika (ipe jina linguine unalopenda wewe) na kiranja wake akiwa Mtanganyika (na huko mbeleni labda katiba ibadilike) ataendelea kuwa Mtanganyika itatawala Zanzibar kwa mambo ya Muungano. Hivyo kwa asili kubwa na unyeti wa mambo ya muungano wazanzibari wataendelea kulalamika kuwa wanatawaliwa na Tanganyika iliyovaa koti la Jamhuri ya Muungano. Na hii ndio sababu ya Mzee Karume kusema "Koti li kikubana unalivua". Na huu ndio msingi wa Katiba yao ya 2010? Cha ajabu watanganyika nao hawaelewi inakuwaje kwenye mambo yasiyo ya muungano wazanzibari wana sauti kule bungeni. Hili nalo litavumiliwa hadi lini? Na kama raisi wa JMT atatokea Zanzibar kama ilivyokuwa wakati wa awamu ya pili, je watanganyika watakuwa Tayari kutawaliwa na Mzanzibari kwenye mambo yasiyo ya muungano?
Cha ajabu wajanja wanatusemea au wanadai kutuwakilisha si wale wa serikali moja, mbili , tatu au zaidi. Mzee Jumbe alishughulikiwa kwa hili, G55/Malecela na Mwiyi wakapata joto la hili. Kisanga na Nyalali wakasema wakapuuzwa hata kama walikusanya mawazo ya wananchi. Warioba na tume yao wanasema. CCM wanasema mbili na wako tayari kutumia mbinu zozote kufanikisha hili. Kwa nini msiwaulize watanzania wenyewe tukate mzizi wa fitina?. Je unapenda muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar uwepo? Kama jibu lako ni ndio Unataka serikali ya namna gani?-Serkali moja, mbili, tatu, mkataba etc. Inaelekea kwa sababu watu wanaogopa majibu ya wananchi hili halitafanyika. Dhamira ya Muungano haiwezi kulazimishwa, muda utafika wananchi watazungumza tu kama sio leo ni kesho.
 
Wakuu wa Usalama, JWTZ, TRA, Uhamiaji, nk wanateuliwa na wako chini ya nani?
Umesoma katiba ya znz ya mwaka 2010 ? Jua znz ni nchi na ina vikosi vyake , sasa wewe unaulizia wakuu wa vyombo vya Tanganyika au vya Zanzibar? unaijua idara ya usalama znz inaitwaje ? Mkuu wake unamjua ?
 
Agreed.
 
Nani kalalamika ? Nilikuwa na kuonyesha jinsi ambavyo Pinda ni waziri mkuu wa Tanganyika ila hajitambui , naye anahoji watu wanatak Tanganyika ipi kwani yeye ni waziri mkuu wa wapi? Tanganyika ikivua koti la Muungano hapo Muungano utaweza kuimarika na kuwa imara , sio kama sasa Muungano umeiva koti la Tanganyika

Pinda hana mamlaka na ma-OCD, DSO na hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi, nk walio Zanzibar? Mbona unakwepa hoja?
 
Umesoma katiba ya znz ya mwaka 2010 ? Jua znz ni nchi na ina vikosi vyake , sasa wewe unaulizia wakuu wa vyombo vya Tanganyika au vya Zanzibar? unaijua idara ya usalama znz inaitwaje ? Mkuu wake unamjua ?

Naulizia Wakuu wa vyombo vya Muungano, sio vya Tanganyika! Zanzibar kuwa na vyombo vyake sio issue kwangu, hata CHADEMA wana Red Brigade, CCM wana Green Guard, CUF wana Blue Guard, nk!
 
Hivi jmn nani muanzilishi Wa hoja ya Tanganyika? Lengo lake ilikuwa nini?

Sio ungeuliza kwa nini mwanzo zilikuwa nchi mbili na zikaunganishwa????!!!
Sio swali la msingi kujadili sababu za muungano na kama bado zina hoja????!!
Kwa nini tusijadili lengo la kutaka kuendelea nao vis-a-vis kuuvunja!!!!!???
 
Hata wakoloni walikuwa na hoja kama yako once upon a time wako wapi leo??????!!!!

Wakoloni wapo mpaka leo, ndo maana mnakesha kutaka Tanganyika ya mkoloni kuliko nchi mliyoiunda wenyewe!
 
Pinda hana mamlaka na ma-OCD, DSO na hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi, nk walio Zanzibar? Mbona unakwepa hoja?
Hana, tume ya uchaguzi ya Zanzibar inaitwa ZEC sio NEC ......ndio maana Tanganyika ipo na DED ila Zenji hakuna hao MADED ila kuna Masheha ........kama hujui ombi ufafanuzi Acha ubishi , hujui mfumo wa SMZ ila sio tatizo lako bali ni la watanganyika wengi......Pinda ni waziri mkuu wa Tanganyika , mamlaka yake inatisha kisiwa cha Chumbe........hairuhusiwi kufika Nungwi...
 
Naulizia Wakuu wa vyombo vya Muungano, sio vya Tanganyika! Zanzibar kuwa na vyombo vyake sio issue kwangu, hata CHADEMA wana Red Brigade, CCM wana Green Guard, CUF wana Blue Guard, nk!
Mamlaka ya nchi ipo kwenye katiba soma kwanza katiba ya znz toleo la 2010 .....
 
Back
Top Bottom