Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 76,808
- 110,047
Pinda acha kupotosha umma wa Watanzania na kauli zenu za kisiasa kwenye jambo la kisheria...
Wananchi wanaotaka serikali tatu na kutaja kuwa wanahitaji Tanganyika huru maana yao ni kwamba wanahitaji mamlaka huru ya Tanganyika na kwa mantiki hiyo mamlaka huru ya watu wa Zanzibar.
Wasiwasi wa CCM katika jambo hili ni moja tu, uwepo wa serikali tatu utapunguza kwa kiasi kikubwa usultani wa chama chao ndio maana hoja yao haina mashiko ya kisheria bali inatetewa kisiasa zaidi.
Mwalimu Nyerere sio Mungu kiasi cha kuamua hatma ya Taifa letu, alichofanya kutuunganisha kinastahili pongezi.
Kwa sababu hiyo basi kwa nini CCM kupitia maono ya Nyerere wasipiganie serikali moja? Hii si ndio itamaanisha umoja zaidi?