Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Kama Tanganyika haitarudi na zikabaki serikali mbili baada ya kua moja nafikiria kudai Uhuru wa visiwa vya Ukerewe kutoka kwa wakoloni wa kitanzania. Wanaokubaliana nami wanipe like ili baadae tuweze kujadiliana jinsi ya kupata Uhuru wa UKEREWE.
 
Watawala kutoka chama chako cha CCM wameshindwa kusoma alama za nyakati kwasababu Tanganyika haizuiliki ni kama mafuriko. Mpaka sasa wanapinga bila hoja zozote za msingi ambazo wanaweza kutuonyesha wenye akili kwamba sasa tumepata mworobaini wa kero za muungano.

Ritz msaidie chama chenu kujiondoa ktk aibu ambayo itakuja kukiandama ktk uhai wake wote. Toka 1984 mpaka leo hakina majibu ya kero za muungano lakini bado wanalazimisha hata kutuchafulia Katiba yetu mpya!
Mimi sina chama, halafu hapa ndiyo watanzania tunaonyesha unafiki wetu, watawala ni wachache sana watanzania wamefanya jitihada gani kuidai Tanganyika yao, hili suala mpaka viongozi wa dini wanapingana nalo kwa maslahi yao haujamsikia Pengo?
 
Huyu kweli kadata na ccm yake, hivyo kweli Pinda una ubavu wa kuyakanyaga maoni ya wana nchi Watanganyika 61% na kutuletea ubabe wa kiccm kwa kulazimicha na kuchurudicha Sera zenu zipite? au ndio muna nguvu za Dola na Nec kuwabeba?.

Ccm inaonekana ina kibarua kikali ,maana ukiona wanalazimicha kitu basi uchuwe ngoma ngumu mitani , na hivi sasa inaonekana Chadema wamewakamata pabaya, maana ccm siku zote yeye ndio Criminal halafu anajita inosent.

Lakini ukweli uko wazi na Chadema wamewakamata pabaya ,Bila ya kutumia Dola na Tume ya Uchaguzi ,ccm hashindi.
 
MFUMO WA SERIKALI MBILI hauwezi tena kuendelea kutuongoza watanzania...la sivyo nchi kama anavyosema Mhe. Tungu Lissu "Nchi Itaparaganyika"
 
Last edited by a moderator:
Kama swala ni kupunguza gharama na kuimarisha umoja wetu, kwa nini tusiwe na serikali moja? Mbona ccm hawaongelei kuhusu serikali moja?

Serikari Moja inatosha huu Muungano wetu ndio muungano wa ghari yaani ni muungano wa gharama kubwa sana sana Ukiwa na Marais wawili wa Tanganyika na wa Zanzibar Pia makamu wa Rais watatu Mmoja anaishi Dsm na wawili wapo Visiwani huku Pia Dsm akiishi Waziri Mkuu ipo Wizara ya Muungano inapewa bajeti kubwa sana ili kuzifuta kero za Muungano Lakini Hadi Leo kero zipo na pesa inatumika bure Tujifunze kutoka Miungano mingine huko katika Mataifa Mengine yaliyoendelea Hawana Muungano wa aina hii ! Huu Muungano kwa kweli unafaa utizamwe kwa jicho la Tatu angalau sasa Tuwe na Serikari Moja tu Rais mmoja tu ili Misafara ipungue na Pesa za kuwahudumia hao viongozi na pesa za kuubembeleza Muungano nazo Zielekezwe kwenye Kujenga Hosptal kubwa ya Rufaa nje ya Mji wasibanane pale Mhimbili hapo italeta Maana kwani sasa huu Muungano umekuwa Janga la kumeza Mamilioni toka Hazina
 
Kama Tanganyika haitarudi na zikabaki serikali mbili baada ya kua moja nafikiria kudai Uhuru wa visiwa vya Ukerewe kutoka kwa wakoloni wa kitanzania. Wanaokubaliana nami wanipe like ili baadae tuweze kujadiliana jinsi ya kupata Uhuru wa UKEREWE.

dahhhhh......yani hadi hapo nimeona kuna haja ya pinda kukaa na kupitia upya alicho kisema.....baada ya hapo kama tutakuwa na serikali mbili ma pemba nao wakae kudai uhuru wao uliopotelea mikonini mwa unguja...
serikali tatu kiboko
 
Ulishasema Zanzibar siyo nchi, sasa ungetaka tukuelewe ungesema ni MUUNGANO wa serikali moja wala tusingekuuliza TANGANYIKA tunayoitaka
 
Nilichogundua mpaka sasa hivi viongozi wa tanzania (bara) na viongozi wa tanzania visiwani (zanzibar) wote kwa pamoja wanahofia kupoteza nguvu za kimadaraka na utawala.

Tanzania Bara wengi wao wanataka serikali tatu lakini viongozi wao hawataki wanataka serikali mbili.

Tanzania visiwani wengi wao wanataka serikali tatu lakini viongozi wao hawataki wanataka serikali mbili.

Kinachosikitisha hawa wananchi hawana nguvu za vitendo wana nguvu za maneno.

hapa umenena mkuu, na hizi chokochoko za serikali tatu zimesababishwa na zanzibar baada ya kudai mamlaka kamili tena kwa kuvunja katiba ya muungano bila viongozi wa muungano kukemea, leo na watanzania wamekuja na hoja yao ya kutaka mamlaka kamili hawa viongozi waliofumba macho wakati zanzibar wanavunja katiba ya jamhuri ya muungano na kutengeneza ya kwao yenye mamlaka huru, leo nasi watanganyika tunataka walichokifanya wanaona ni haramu, swali, je hawa viongozi hawakuona hili mapema!? Serikali moja ndo ilikuwa dawa ya muungano lakini hili kwa sasa haliwezekani it is too late kwa sababu wazanzibar hawatakubali.
 
Pesa inayotumika kulea na kuubembeleza Muungano ni Nyingi sana sasa inapaswa Hizo Pesa zipunguzwe ili zielekezwe kwenye Huduma za jamii kwani aina ya Miungano ya Gharama Kama hii haina nafasi katika Ulimwengu huu wa Sasa Muungano huu ulipaswa sasa uwe tayari ktk Serikari Moja tu na hizo kero wanazozipigia kerere zingebaki Kuwa Historia tu inatupasa Tutambue Kuwa ipo Siku Visiwa vitamezwa na Maji na wao watarejea huku Tanganyika kwao kuishi Wazanzibar wapunguze Vuvuzela pale Visiwani si kwao kiasilia wao walipelekwa Enzi ya Utumwa wa kiaraabu . Nyerere na karume waliunganisha Nchi wakiwa na nia Njema wakiamini Siku moja itakuwa Nchi moja Rais mmoja tu lakini imekuwa Kinyume na matarajio Yao sasa ni Miaka 50 bado eti kuna kero za muungano huku kukiwa na watu wajanja wanafurahia hizi kero ili waendelee kufaidi pesa inayotengwa kwa ajili ya kuzitatua kero za muungano zisizo na kikomo . Hakuna njia zaidi ya kuondoa Haya Majanga zaidi ya kuunda Serikari moja tu .
 
Tanganyika ni zao la Mjerumani (mambo ya Tanganyika Mandate na Baadaye Tanganyika Territory). Alipokuja Mwingereza akachukua hiyo kitu Tanganyika mpaka alipomkabidhi Julius, ambaye alipoona nchi "haitoshi" akaamua "kuiongeza" kidogo na kuipa jina jipya! Hongera sana Mwaaaaalim (RIP) kwa ubunifu! Wengine wanakuonea wivu tu, hamna lolote!

ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ah ah haaaaaaaah, mkuu umenichekesha sana hapa, kwa hiyo teacher hapa alikuwa mjanja sana, labda wenye kipande chao washagutuka ndo maana wamekomaa kukitaka
 
dahhhhh......yani hadi hapo nimeona kuna haja ya pinda kukaa na kupitia upya alicho kisema.....baada ya hapo kama tutakuwa na serikali mbili ma pemba nao wakae kudai uhuru wao uliopotelea mikonini mwa unguja...
serikali tatu kiboko

Huku Baharini kuna Visiwa kibao vikiwemo vya mafia kule lindi mtwara tanga nk vipo visiwa vingi wanaishi watanzania hata huko ziwa Victoria vipo Visiwa kibao zaidi ya Ukerewe na wanaishi watu lakini havina Baraza la wakilishi wala Rais hivyo haviwezi kupuliza Vuvuzela Kama la Zanzibar
 
Ulishasema Zanzibar siyo nchi, sasa ungetaka tukuelewe ungesema ni MUUNGANO wa serikali moja wala tusingekuuliza TANGANYIKA tunayoitaka

Muelezeni mzee wetu anaweza kubadili mawazo! Tatizo kubwa sana la Pinda ni kuwa "mkweli!" Kwenye siasa ukiwa mkweli sana unaweza kuleta madhara makubwa sana! Angalia kaingia mtaalam JK! Yeye kadai Zanzibar ni nchi "kwa jicho la ndani" ila kimataifa "Zanzibar sio Nchi!" Mzizi wote wa fitna ukakatwa! Chezea siasa weye!
 
ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ah ah haaaaaaaah, mkuu umenichekesha sana hapa, kwa hiyo teacher hapa alikuwa mjanja sana, labda wenye kipande chao washagutuka ndo maana wamekomaa kukitaka

Teacher alisoma Alama za Nyakati alijua ipo Siku Visiwa vitamezwa na Maji ya Bahari na wao kukosa pa kwenda akaamua Tuungane ili Siku Visiwa vikezwa na maji Wahamiaji wa Unguja na Pemba waludi kwao Tanganyika na Kuwa kitu kimoja Tambua hata hili jina la Tanzania ni jina lililotoka ktk ubunifu wa Teacher
 
Pinda kama unataka selikali mbili tuambie na majibu haya mbona zanzibar kwenye katiba yao wameainisha kuwa zanzibar ni nchi, wana wimbo wao, bendera yao, katiba yao inaruhusu wazanzibari ndio wanahaki ya kumiliki ardhi tu? Sasa tanganyika haina katiba, wimbo, bendera huu ni muungano gani? Hivi ni vizazi vingine tunahitaji majibu
 
Awaulize wa Scotch , ni Scotland ipi wanayoitaka. halafu atueleze kama wale wote waonadai uhuru wa scotland wawa umri sawa na muunganiko na Scotland na Great Britain
 
Hivi pale UN New York U.S.A wamelisajili jina la Zanzibar ? Hv Rais wa Zanzibar akija Dsm huwa anapigiwa Mizinga 21 ? Na endapo Tanganyika itarejea upya jina la Tanzania litabakia pale UN ? au itakuaje? Ni lini mchakato wa katiba ya Tanganyika pekee utaanza? Maana Zanzibar wao wana katiba Yao na itambulike kwamba waliunda katiba kinyemela kimya kimya kwa kukiuka vipengele vya muungano Zanzibar wao wapo kamili kwa kila kitu
 
Kung'ang'ania mfumo wa serikali mbili ni janja ya watanganyika kuitawala zanzibar kijanja! Mfano watanganyika wanatumia bunge la muungano kwa manufaa ya tanganyika badala ya tanzania! Watanganyika wengi wanajifanya kutetea serikali mbili kwa lengo la kuikandamiza zanzibar na si vinginevyo!
 
Pinda aache kupotosha wamanchi; Tanganyika ni jina la nchi iliyopata uhuru wake 9/12/1961 na tunaendelea kusherekea siku hii kila mwaka. Pinda anapoibeza Tanganyika na kuendelea kusherekea na kuienzi December 9 kila mwaka huu ni unafiki kwa sababu hakuna nchi juu ya uso wa dunia hii inayoitwa Tanzania iliyopata uhuru wake tarehe 9/12/1961. Kama kweli Pinda na ccm wanania nzuri ya muungano wangezungumzia muungano wa serikali moja hapo tungewaelewa. Pinda unaitwa waziri mkuu wa serikali ya JMT lakini huna hata chembe ya mamlaka yeyote Zanzibar; sasa huo wazari mkuu wako wa JMT uko wapi!! Hata Rais waJMT naye pia hana madaraka yeyote kwa serikali ya Zanzibar. Na vipi Rais wa Zanzibar naye hawezi hata kumkemea naibu waziri wa JMT. Tangayika anayoibeza Pinda na ccm ni sawa na kulikataa jina la baba yako la ukoo kwasababu kabatizwa au kaslimu akaitwa Joseph au Said jina la Kayanza ulikatee!!!
 
Pinda kama unataka selikali mbili tuambie na majibu haya mbona zanzibar kwenye katiba yao wameainisha kuwa zanzibar ni nchi, wana wimbo wao, bendera yao, katiba yao inaruhusu wazanzibari ndio wanahaki ya kumiliki ardhi tu? Sasa tanganyika haina katiba, wimbo, bendera huu ni muungano gani? Hivi ni vizazi vingine tunahitaji majibu

Tambua Wazanzibar ni wachache sana Lakini wanafaidi matunda ya Muungano kuliko watanganyika wengi kisha wakishashiba wanavulumisha Vuvuzela kuwachanganya watanganyika wasikumbuke Kuwa wanachunwa buzi kijanja . Pato la Taifa kwa 97% linatokana na Rasilimali zilizopo Tanganyika lakini 40% unatumika kulea na kuubembeleza Muungano yaani wanaofaidi matunda ya muungano ni watu wa Visiwani watanganyika wanalima wao wanavuna kisha wanapiga Mayowe kuwapumbaza kirahisi rahisi tu ! Kaa ukijia Zanzibar ni Eneo Dogo sana Lakini Lina Wabunge, Mawaziri, na Viongozi wengi kupindukia na wote wanagharamiwa na pesa inayotoka Tanganyika wao wamebuni mbinu nyingi za kuzifaidi pesa za Tanganyika lakini hadi sasa Tanganyika haijielewi
 
Back
Top Bottom