Hapa ni sebuleni kwangu, si mtandaoni.
Naongelea mtandaoni kwenye source iliyotolewa hapa, Deutsche Welle.
Najua Pinda ni tutusa, ila haya mambo kama kasema kweli atajipatia taji la ututusa zaidi. Wananchi wakikupa dhamana ya uongozi, ama unawatumikia mpaka mwisho, ama unasema kazi imenishinda unaachia wengine.
Kusema "kazi imenishinda lakini nitakuwepo kuwepo tu mpaka 2015" ni ujuha uso kifani.
Ndiyo maana napata tabu kuamini kwamba huyu Mizengo Pinda ni juha kiasi hicho kweli. Na kila nikiitafuta habari siioni ingawa imethibitishwa na "watu" wawili hapa.Mmoja akisema kwamba imetoka "Deutsche Welle".
Direct quote ni muhimu ili tupate maneno yake mwenyewe alivyoyapanga bila mtu kututafsiria, maana tafsiri inaweza kuongeza au kupunguza maana.