Pinda rais 2015?

Pinda rais 2015?

Nyangeta Marwa

Senior Member
Joined
Nov 10, 2014
Posts
136
Reaction score
60
Viko viashiria kuwa huenda Mizengo Pinda akawa Rais wa tano wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Pinda ambaye hakuwa na nia hiyo hapo awali, Inasemekana kuwa ameombwa na wazee na vigogo wastaafu waliowahi kushika nyadhifa za juu nchini. Hii inatokana na utulivu wake katika kupanga na kuamua mambo kwa hekima na busara, jambo ambalo linahitajika sana katika kipindi hiki ambacho siasa za dunia na hasa Afrika zinapitia katika wakati mgumu wa vuguvugu la mageuzi. "Hauhitaji mtu anayekurupuka katika kupanga na kuamua mambo wakati huu, Africa imekuwa na maadui wengi sana kutoka nje na ndani ambao wanatumia nafasi ya kuleta machafuko ili kupora rasilimali zetu . Hivyo unahitaji viongozi wenye busara na utulivu katika kuamua mambo. "Alinukuliwa mjumbe mmoja wa halmashauri kuu ya CCM taifa kutoka Mkoa mmoja ulioko kusini.

Kugunduliwa kwa gesi asilia huko Mtwara na tetesi za mafuta katika ukanda wa bahari ya hind kunatajwa kuwa ni moja ya sababu ya taifa kuhitaji mtu wa aina ya Pinda, mkomavu , anayejua vema misingi ya taifa, usalama wa nchi na makini katika kuamua mambo hasa nchi inapokuwa katika changamoto. Mabeberu wanatajwa kunyemelea rasilimali hii ya gesi na mafuta.

Uwezo aliouonesh waziri mkuu Pinda katika kukabiliana na joto la wabunge katika vipindi tofauti umezidi kumjengea sifa na heshima kubwa. Sakata la ESCROW, Operesheni TOKOMEZA na mengineyo ni mifano tosha ya uwezo wa Pinda katika kuhimili mambo mazito. Rais Jakaya Kikwete anatajwa kuridhishwa sana na uwezo wa Pinda kusimamia na kuivusha nchi katika kipindi kizito. Hii imesababishwa na umahiri aliouonesha waziri mkuu nyakati zote za masakata mazito kama TOKOMEZA na hata ESCROW ambapo wakati wote Rais hakuwepo nchini na mambo yalikwenda vema.

Pinda ametumikia ikulu kwa miaka 22, miaka 6 akifanya kazi kama msaidizi wa karibu wa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hivyo anaijua vizuri nchi. Pinda amejifunza uongozi kwa Mwalimu, Mwinyi na Mkapa akiwa ikulu. Hivyo anaelewa kwa upana uongozi ni nini. Ameanza kulitumikia baraza la mawaziri kabla hajawa waziri. Mwaka 1996 baada ya Rais Benjamin Mkapa kuingia madarakani, Pinda aliteuliwa kuwa afisa msaidi wa baraza la mawaziri, chombo kinachojadili mambo yote mazito ya nchi. Inasemekana mwalimu ndiye aliyeshauri Rais Mkapa afanye kazi kwa karibu na Pinda.

Rais mstaafu Benjamin William Mkapa anatajwa kumuunga mkono waziri Mkuu Mizengo Pinda katika mchakato wa mwakani 2015. Rais mstaafu Mkapa ambaye anatoka sehemu moja (Lindi) na waziri wa mambo ya nje Bernard Membe, anatajwa kutomkubali Membe kwa nafasi ya Urais . Mzee Mkapa aliwahi kusimama hadharani katika harambee kumsifu Pinda kuwa ni mtu makini na kiongozi anayefaa kupewa majukumu makubwa zaidi. Habari zisizo rasmizinasema waziri Membe anatajwa kwenda kuzungumza na Rais Mkapa na kumuomba amuunge mkono katika ndoto yake ya Urais, lakini mzee Mkapa alimwambia wazi kuwa haoni kama anafaa kwa nafasi hiyo. Mkapa alikwenda mbali zaidi kumwambia Membe kuwa yeye Mkapa akiwalinganisha Membe na Pinda kutokana na jinsi anavyowafahamu, anaona Pinda ana sifa kumzidi Membe.

Suala la Ukanda. Ukanda wa Pwani unaojumuisha mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es salaam, Lindi na Mtwara inatajwa kutoa Rais mara tatu. RAIS Ali Hassan Mwinyi licha ya kutokea Zanzibar, upande ni mtu wa Mkuranga. Rais Mkapa alitokea Lindi, Rais Jakaya Kikwete kadhalika anatokea Pwani . Hivyo ili kuleta umoja wa kitaifa ni lazima Rais ajaye atoke maeneo mengine ya nchi mbali na Pwani. Hili ni kaa la moto kwa Membe.

Kila nikitafakari kwa kina, simpuuzi Pinda. Namtazama kama mtu ambaye anaweza kufika mbali ya alipo sasa.
 
Hii analysis imekaa kiaina ........................ Anyway, napita tu! Lakini Mzee Mkapa ni mtu wa Mtwara ......................... Rekebisha hiyo!!
 
Waziri mkuu mzembe asie na maaamuz anaeishia kulia lia pale anapobanwa huku akitarajia huruma ya mamlaka yake ya uteuzi hafai hata kuwa PM.

Hili la escrow ndiyo limemmaliza moja kwa moja.

Anasema fedha si za umma huku mawaziri wake km mwandosya na vyombo vilivyopo chini yake vinaenda tofauti naye kuna cha kutumain hapo?

Kanisa katoliki tunajua linahaha sana kutaka kumweka mtu wake hapo 2015 kwa udi na uvumba...too bad hapa kwa pinda mmechemka.

Tafuteni mwingine.

No doubt ndio kwa maana mnamchukia lowasa maji yapo shingoni sasa.

Tutaelezana hapo mwakani insha allah.
 
Kama watanzania wakiridhika naye ni Rais atakayekuwa mchapakaz "GOD HELP PINDA"
 
Raisi ajae kakaa pembeni ya rahisi wa sasa leo kwenye gwaride.
 
Kama ni timu ya mpira basi hakuna mchezaji atakae leta matokeo mazuri,sio kocha wala wachezaji walio ndani hata wale wa substution,jahazi hili linazama labda wabuni mbinu mpya za kukokotoa matokeo!!
 
Kwa rekodi hiyo ya kufanya kazi ikulu na mwalimu Nyerere na marais waliofuatia kunaweza kuwa na mchango mkubwa katika kumuandaa Pinda kuwa kiongozi wa nchi. Mimi bado naamini kuwa urais ni kazi ngumu sana inayohitaji mtu aliyeandaliwa vizuri. Ukituliza kichwa unaweza kujua kuwa Pinda ana sifa za ziada
 
Pinda ni mtu muadilifu na mchapakazi asiye na majivuno na kujiona. Uongozi haujamvaa Pinda, bali yeye ameuvaa uongozi. Hii ni sifa muhimu sana kwa kiongozi yeyote anayetumikia watu.
 
Waziri mkuu mzembe asie na maaamuz anaeishia kulia lia pale anapobanwa huku akitarajia huruma ya mamlaka yake ya uteuzi hafai hata kuwa PM.

Hili la escrow ndiyo limemmaliza moja kwa moja.

Anasema fedha si za umma huku mawaziri wake km mwandosya na vyombo vilivyopo chini yake vinaenda tofauti naye kuna cha kutumain hapo?

Kanisa katoliki tunajua linahaha sana kutaka kumweka mtu wake hapo 2015 kwa udi na uvumba...too bad hapa kwa pinda mmechemka.

Tafuteni mwingine.

No doubt ndio kwa maana mnamchukia lowasa maji yapo shingoni sasa.

Tutaelezana hapo mwakani insha allah.

Pinda mwaka 2012 aliwafukuza kazi wakurugenzi 8 na kuwasimamisha kazi wengine kwa matumizi mabaya ya fedha, mwaka 2010 Pinda aliwavua madaraka mkurugenzi wa Bagamoyo, mweka hazina, afisa mifugo, kilimo n.k kwa ubadhirifu, ukitaka kujua uimara wa Pinda kawaulize wakurugenzi wa halmashauri za wilaya
 
U.S.E.L.E.S.S. ever PM in Tanzania for past and future years....!!!
 
Nyangeta mm sina tatizo na pinda kama angebaki pinda tunayemfahamu.huyu wa sasa mmmm....vibali vya sukari anatoa yeye badala ya waziri c.chiza. pia, kumpa masaburi akusanye fedha za kampeni yake is wrong. Huyu meya anafahamika kuwa kitovu cha uzembe na kielelezo cha ufisadi. Sasa pinda ndiye anamuona mtu anayefaa kumkusanyia fedha za asubuhi kampeni.nasikia ameahidiwa kupewa uwaziri wa fedha kwenye serikali yake....watanzania tumekwisha na huu ushabiki wa kijinga.
 
Back
Top Bottom