Mizengo Pinda for Pres 2015?

Status
Not open for further replies.
nadhan suala la pinda kua next president liko slightly straight forward na uwezo wake hata wapinzani wanaukubali toka yuko tamisemi! nadhan hata wapinzan wakijua pinda ndio mgombea wataishiwa nguvu! magufuli kwa kweli hafai kupewa highest office in the country kwani maamuzi yake mda mwingine sio yanatakiwa kufanyika hata kama ni sahihi! u need that leadership quality ambayo watu kama magufuli, mwakyembe hawana! jazba zao hazifai!
 
Kwa hapa Mh Pinda Kachemka ile vibaya! Hizi ni siasa za majitaka.....!!!!!!!!!!!!!!! Unajua tatizo la viongozi wetu siasa nyingi yaani watu badala ya kusimamia mipango ya nchi wanaanza harakati za uraisi kwa kweli wa Tz ni kichwa cha wendawazimu!!! Afu wengi wetu tutamuona amefanya la maana kumbe hakuna kitu!
 
BONA wewe ni kichwa cha wendawazimu....na mara nyingi nimegundua watu kama wewe mnakula na mafisadi.....Kuna vijisenti wanakupa!
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kuachia ngazi mara kipindi cha ubunge wake kitakapoisha mnamo mwaka 2015. Pinda amesema kazi yake ni ngumu na mara nyingi anashindwa hata kupata usingizi usiku, hivyo anawaachia wengine. Aidha amewaasa wote wanaokimbilia mbio za urais kwamba kazi hiyo siyo rahisi.

source: Pinda mwenyewe.

My take: 1. Good riddance.
2. Sijaona chochote cha maana alichofanya.
3. Jimbo hili litakua wazi kwa CHADEMA.
 
Inshalah Mungu atajalia

Why 2015 and not now? Kwa nini mzee avumilie hadi 2015 wakati hata usingizi unakua haupatikani jamani? Namhurumia mzee wa watu kwa kweli. Mimi sijui kuvumilia. Ningekuwa nishajitoa. Mwee!
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kuachia ngazi mara kipindi cha ubunge wake kitakapoisha mnamo mwaka 2015. Pinda amesema kazi yake ni ngumu na mara nyingi anashindwa hata kupata usingizi usiku, hivyo anawaachia wengine. Aidha amewaasa wote wanaokimbilia mbio za urais kwamba kazi hiyo siyo rahisi.

source: Pinda mwenyewe.

My take: 1. Good riddance.
2. Sijaona chochote cha maana alichofanya.
3. Jimbo hili litakua wazi kwa CHADEMA.

Baadaye atasema ameombwa na wapigakura wake kugombea
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kuachia ngazi mara kipindi cha ubunge wake kitakapoisha mnamo mwaka 2015. Pinda amesema kazi yake ni ngumu na mara nyingi anashindwa hata kupata usingizi usiku, hivyo anawaachia wengine. Aidha amewaasa wote wanaokimbilia mbio za urais kwamba kazi hiyo siyo rahisi.

source: Pinda mwenyewe.

My take: 1. Good riddance.
2. Sijaona chochote cha maana alichofanya.
3. Jimbo hili litakua wazi kwa CHADEMA.

Anajuaje? Lini amewahi kuwa Raisi?

Yeye aseme u-Waziri Mkuu siyo rahisi, kwa kiwango chake, na siyo kutoa nasaha kwa kazi ambazo hajawahi kuzifanya.

Kwa Peter Kayanda Mizengo Pinda, hata udiwani nadhani siyo rahisi kwani pia unahitaji kufikiri na ufumbuzi wa matatizo. Kulialia na kusema 'mimi nimeagizwa tu' siyo fikra za ufumbuzi wa matatizo.
 
deutche welle

Natafuta kitu verbatim sijakiona, na si kwa kukosa jitihada. Habari kubwa hii mbona haipo mtandaoni?

Kama ni kweli atajionyesha tu kwamba hakujua anaingia katika uongozi kufanya nini, na kuonyesha kwamba ushauri wa Mkapa kumtaka abaki Ikulu ulikuwa mzuri, na kwamba Kikwete ni mpuuzi kwa kumchagua mtu anayependa usingizi kuliko kulitumikia taifa lake.

Lakini pia atafaa kupongezwa kwa kujua kwamba kazi hawezi na kuachia ngazi. Nilitaka kusema kujiuzulu kwa sasa atakuwa hawatendea haki wapiga kura wake, but then again Pinda hakupigiwa kura hata na mtu mmoja na technically si mbunge (Tanzania ina Waziri Mkuu ambaye ubunge wake haujaainishwa kikatiba!) kwa hiyo hata akijiuzulu sasa sawa tu.

Kama kweli kashindwa kungojea 2015 kutangaza hili atajionyesha kazidiwa na hii kazi kweli kweli na kuthibitishia ulimwengu kwamba hamnazo.

Ndiyo maana natafuta sana a verbatim quote .
 
keshasoma alama za nyakati. Kauza sana ardhi huko kwao sasa kaona hilo litatumika kama fimbo
 
Natafuta kitu verbatim sijakiona, na si kwa kukosa jitihada. Habari kubwa hii mbona haipo mtandaoni?

Kama ni kweli atajionyesha tu kwamba hakujua anaingia katika uongozi kufanya nini, na kuonyesha kwamba ushauri wa Mkapa kumtaka abaki Ikulu ulikuwa mzuri, na kwamba Kikwete ni mpuuzi kwa kumchagua mtu anayependa usingizi kuliko kulitumikia taifa lake.

Lakini pia atafaa kupongezwa kwa kujua kwamba kazi hawezi na kuachia ngazi. Nilitaka kusema kujiuzulu kwa sasa atakuwa hawatendea haki wapiga kura wake, but then again Pinda hakupigiwa kura hata na mtu mmoja na technically si mbunge (Tanzania ina Waziri Mkuu ambaye ubunge wake haujaainishwa kikatiba!) kwa hiyo hata akijiuzulu sasa sawa tu.

Kama kweli kashindwa kungojea 2015 kutangaza hili atajionyesha kazidiwa na hii kazi kweli kweli na kuthibitishia ulimwengu kwamba hamnazo.

Ndiyo maana natafuta sana a verbatim quote .

Hapa unasoma wapi, si mtandaoni?
 
Hapa unasoma wapi, si mtandaoni?

Hapa ni sebuleni kwangu, si mtandaoni.

Naongelea mtandaoni kwenye source iliyotolewa hapa, Deutsche Welle.

Najua Pinda ni tutusa, ila haya mambo kama kasema kweli atajipatia taji la ututusa zaidi. Wananchi wakikupa dhamana ya uongozi, ama unawatumikia mpaka mwisho, ama unasema kazi imenishinda unaachia wengine.

Kusema "kazi imenishinda lakini nitakuwepo kuwepo tu mpaka 2015" ni ujuha uso kifani.

Ndiyo maana napata tabu kuamini kwamba huyu Mizengo Pinda ni juha kiasi hicho kweli. Na kila nikiitafuta habari siioni ingawa imethibitishwa na "watu" wawili hapa.Mmoja akisema kwamba imetoka "Deutsche Welle".

Direct quote ni muhimu ili tupate maneno yake mwenyewe alivyoyapanga bila mtu kututafsiria, maana tafsiri inaweza kuongeza au kupunguza maana.
 
Pinda mnafiki tu huyo keshajua wazi come 2015 hatoboi kwa hiyo anajihami mapema. Atakuwa anaiogopa Chadema siyo bure! Lol
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom