Miti ya aina ya mitiki inaweza kustawi Wilaya Mufindi?

Jenchede

JF-Expert Member
Jul 22, 2014
238
495
1681033531182.png

Habari za leo wanajukwaa. Heri ya siku ya pasaka.

Najua humu kuna wataalam mbalimbali, naomba kujua kwa mkoa wa iringa je miti ya mitiki inaweza kustawi?

Katika kupambana nimefanikiwa kununua shamba la hekari 20 katika Halmashauri ya Mafinga. Na malengo ni kupanda miti. Nimekua nikipitia jukwaa hili nikasikia mitiki nayo inathamani sana. Nilitamani kujua mazingira ya huko yanafaaa kwa kilimo hicho ili kwenye shamba hilo nichanganye miti yote milingoti, na mitiki

Kwa wenye ufahamu naomba kujuzwa juu ya hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma climatic condition ibayofaaa hapo, soil ph. Muone bwana miti wa mkoa atakupa ushauri.

Huko panda milingoti,mipaina, mipodo.
Ukitaka mitiki labda. Songea, Njombe ukanda wa Kuelleea Songea, Nyasaland nk.
 
... ila kilimo cha miti jamani; long term projects kwa ajili ya watoto na wajukuu.
Ni kweli ni uwekezaji wa mrefu. Maana tunaangalia changamoto ya ajira haya miaka hiyo itakuwaje kwa watoto wetu angalau tuwaandalie japo miti ikitokea wamekosa ajira basi wajikite hata kwenye biashara za mbao

Kama una miaka 40 utavuna ila hela utashindwa pa kuzitumia maana utakuwa na miaka 60.
Mti wa kuwahi ni mlingoti tu, ukifuatia mpaina ambayo miaka 10 unavuna. ila mitiki na miti ya asili ni miaka25+.
Hata hivyo mimi nimegundua kuna watu wanapanda miti kama hoby na si kwa ajili waje wavune.
Hivyo tupande miti kwa ajilu ya kutunza mazingira, maana wote tusipopanda vizazi vyetu vitaangamia.
Binafsi ninahobi ya kupanda miti ila muda haunipi nafasi.
 
Asante kwa ushauri mzuri. Binafsi nipo kwenye 30 's. Ni kweli tunapaswa kupanda kwa hobbie lkn pia maisha hayatabiriki. Binafsi nimenunua tu kwa ajili ya watoto wangu. Nitafatabushauri wako nitapanda mlingoti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri mzuri. Binafsi nipo kwenye 30 's. Ni kweli tunapaswa kupanda kwa hobbie lkn pia maisha hayatabiriki. Binafsi nimenunua tu kwa ajili ya watoto wangu. Nitafatabushauri wako nitapanda mlingoti

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko nasikia kuna mbegu ta Paina ya miaka 8. Jaribu kuitafuta hio. Hata mlingoti tafuta ule unao kimbia utastaajabu baada ya miaka 6.
Kitu kingine chagua heka chache ufanye kilimo cha miti zingine panda miti ila kama unauwezo wa kiuchimi basi shamba lote fanya kilimo cha miti.
Kunatofauti kati ys kilimo cha miti na kupanda miti.
Watu wengi tunapanda miti hatulimi miti.
 
Asante kwa ushauri naomba unifafanulie tofauti kati ya kilimo cha miti na kupanda miti ikoje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma climatic condition ibayofaaa hapo, soil ph. Muone bwana miti wa mkoa atakupa ushauri.

Huko panda milingoti,mipaina, mipodo.
Ukitaka mitiki labda. Songea, Njombe ukanda wa Kuelleea Songea, Nyasaland nk.
Vipi Kigoma?
 
... ila kilimo cha miti jamani; long term projects kwa ajili ya watoto na wajukuu.
sidhani kama ni sahihi tukisema ni kwa ajili ya watoto na wajukuu, unaweza mwenyewe ktk umri mkubwa kabisa miti ikakufaa sana, kuna watu wanafika 80yrs wakiwa na akili timamu na wanakula matunda ya kazi zao za ujanani. Na wengine wanatunzwa na kazi zao walizofanya wakiwa watu wazima. So usiangalie sana umri, kipato kikiwepo wewe otesha miti.

Msukuma mmoja alisema "' otesha miti maana haitakuacha, ila watoto watakuacha'", pia dunia inabadilika mno, Mchina anavuna miti hatari huko nyanda za juu, siyo muda mrefu ujao, miti itajipatia heshima yake.
 
Habari za leo wanajukwaa. Heri ya siku ya pasaka.

Najua humu kuna wataalam mbalimbali, naomba kujua kwa mkoa wa iringa je miti ya mitiki inaweza kustawi?

Katika kupambana nimefanikiwa kununua shamba la hekari 20 katika Halmashauri ya Mafinga. Na malengo ni kupanda miti. Nimekua nikipitia jukwaa hili nikasikia mitiki nayo inathamani sana. Nilitamani kujua mazingira ya huko yanafaaa kwa kilimo hicho ili kwenye shamba hilo nichanganye miti yote milingoti, na mitiki

Kwa wenye ufahamu naomba kujuzwa juu ya hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mitiki kwa Mafinga au Mufindi itakuwa tunadanganyana, ila ukienda kijiji cha Mpanga Tazara kule Mufindi kusini inaweza kumea na kufanya vizuri, changamoto ni namna ya kuitoa kule kijijini kuipeleka sokoni wakati ukifika.
 
sidhani kama ni sahihi tukisema ni kwa ajili ya watoto na wajukuu, unaweza mwenyewe ktk umri mkubwa kabisa miti ikakufaa sana, kuna watu wanafika 80yrs wakiwa na akili timamu na wanakula matunda ya kazi zao za ujanani. Na wengine wanatunzwa na kazi zao walizofanya wakiwa watu wazima. So usiangalie sana umri, kipato kikiwepo wewe otesha miti.

Msukuma mmoja alisema "' otesha miti maana haitakuacha, ila watoto watakuacha'", pia dunia inabadilika mno, Mchina anavuna miti hatari huko nyanda za juu, siyo muda mrefu ujao, miti itajipatia heshima yake.
Kuna mwalimu alistaaafu 2016 na akaanza kupanda pine, mpaka sasa aba afya nzuri na huenda akavuna na kupanda mipya.
 
Atavuna na kuotesha mipya, maana mara nyingi kifo kwa wastaafu wengi kipo kwenye vichwa vyao, hasa hofu inayosababishwa na kukosa kitu cha kufanya. Kama huyo kichwa kinamwelekeza kuwekeza kwenye miti basi ataishi sana.
 
Kwa Mufindi panda Pine na Mikaratusi maarufu kama milingoti. Mitiki inastawi ukanda wa joto kama Morogoro, Pwani, Tanga na Ruvuma.
 
kata ya kagongwa wilaya ya kahama mtaa wa ipyagula kuna mzee nasikia ni bwana misitu morogoro kaotesha hapa town kama heka 2 imestawi vizuri na inapendeza sana na inatunzwa sana ina miaka kama kumi hivi...
 
yap. Ukanda wowote ambao siyo wa baridi sana tiki inamea. Shida yake baridi. kwenye baridi inachelewa sana kukua. Ukanda wa Kahama hadi Biharamulo lazima inastawi vizuri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom