Mitandao isitumike kumchafua Rais

Mitandao isitumike kumchafua Rais

Mkuu, Mhariri kampongeza eti anasomesha watoto hapa nchini...hapo tuna jiuliza umakini wa mhariri..
Labda kwa kuwa huyu mwanaasha kasoma hapa tanzania....khalfan, khalifa, Rashid(chodo) na ali..wako nje ya bongo wanapiga kitabu...
 
Ni kweli kabisa hata mimi namwunga mkono Mhariri ingawa mimi si CCM na wala sifurahishwi na utendaji wa Rais wetu. Uhuru wa mmoja huishia uhuru wa mwezie unapoanzia, kwa kweli mimi nachukia "Personal attacks" ziwe kwa JK au yeyote. Lakini hapa ni lazima ieleweke kwamba kusema jambo fulani ni baya, linatuumiza, linakera, au linatuhujumu si dhambi hata kidogo, na kwa taasisi ya urais hilo ni sawa kabisa ila kuzungumzia juu ya mambo yake binafsi na familia (nje ya kujihusisha kwao na siasa za nchi) si ustaarabu hata kidogo.

Napenda kuwa wazi zaidi katika hili, kwa mfano kumekuwa na mijadala kadhaa ya jinsi baadhi ya wanafamilia wa Rais wetu kuutumia mgongo wake kulihujumu taifa - hapa si dhambi hata kidogo kuwakemea kuwajadili na hata kupambana nao kisheria pale hali itakaporuhusu maana kwa vitendo vyao wengi tunaumia. Watu walijadili mke wa Rais kutumia mali na amali za nchi kumpigia kampeni mumewe, ukifanyika uhalifu wa kubadili namba za magari ya serikali ili kufanikisha jambo lile, mtoto wake ambaye hajafanya kazi hata miaka kumi kumiliki mabilioni yanayohujumu utendaji wa serikali km uimarishaji wa reli ya kati ili makampuni ya kijana yule yapate tenda za kusafirisha mafuta n.k. huku si kumsema vibaya hata kidogo.
Mimi naamini kwamba mitandao hii inasaidia kuwafanya watu "wapumue" kero zao na kupooza hasira zao ambazo vinginevyo tungezishuhudia mabarabarani.
 
Tatizo ni baraza la mitihani na wizara ya elimu. Kama siyo wao hii mitandao ingepata wapi hayo matokeo. Huu ujinga wa kuanika majina ya watoto hadharani ukomeshwe. Matokeo ya mitihani ni private matter. Wanachofanya baraza/wizara ni kama vile upime afya halafu matokeo ya lab yatolewe hadharani. Sioni sababu ya Tz daima kulaumu mitandao

Mkuu sikubaliani na wewe kuhusu matokeo katika level ya sekondary. Ingekuwa level ya higher education tungekuwa ukurasa mmoja. Unachotakiwa kujua kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya wanafunzi wa sekondary kurudi chini na vyuo vya juu.

Wanafunzi wa sekondary wengi wao ni dependants na walezi wana haki ya kuyajua matokeo ya vijana wao bila kuficha. Tunaficha nini?, tena kwangu mimi hii ni motivating factor ya kuwafanya watoto wajitume sana kusoma kwani wasipofanya hivyo matokeo yao yatawaumbua. Mimi nina kijana wangu ninamlipia pesa nyingi sana, kila nikimuuliza matokeo ananiambia jina lake halipo. Kabla sijaenda kufuatilia nikaingia mtandaoni na kukuta amepata Div iv. Je si nimeepuka usumbufu?.

Hawa watoto ni wajanja sana. Hawasomi na kutudanganya wazazi. Mimi ninakubaliana kabisa na utaratibu huu wa kuanika majina public. Huko nyuma baraza walikuwa wanaweka namba tu, na matatizo waliyokutana nayo nafikiri ndiyo yamewafanya kuweka majina. Kuna wakati namba zinakosewa na kufanana ila kama kuna jina pembeni unaondoa utata.

Kuhusu mtoto wa JK kuwekwa mtandaoni that was unfortunate. Nilikemea sana kumshambulia mtoto kama mtoto kwa sababu tu baba yake ni mkuu wa nchi. Tupo wazazi wengi sana watoto wetu wamefanya vibaya sana. Uzembe hauna 'genes'. Ila kwa upande mwingine sioni kama kufanya hivi ni kumchafua rais, unamchafua kwa lipi?. Nafikiri nature ya kazi aliyo nayo Jakaya Kikwete, inamuweka kwenye spot light, hivyo kumzungumza vibaya au vizuri yote ni matokeo ya kazi aliyo nayo. Kama hutaki kuzungumwa vizuri au vibaya usijiweke kwenye Public spotlight (Ie usi-contest for public office)

Ukiingia katika mitandao ukaona jinsi Obama anavyoongelewa vibaya utachanganyikiwa. Ila kinachofanya hivyo si yeye bali ni ofisi aliyoishika. The only thing kujiweka kwenye good mood kama wewe si mvumilivu ni kutokuingia mitandaoni na kusoma criticism dhidi yako. Fanya kazi tu, waache watu waongee. Huwezi kuzuia watu kuongea/kuandika kwenye mitandao. Na ukifuatilia utakuwa mwendawazimu. Ndiyo maana mimi huwa nikiwasikia maafisa usalama wakitolea ufafanuzi maandishi ya kwenye internet huwa nawaona kama wamechanganyikiwa. Kazi yao ingekuwa ni ku-monitor maandishi yanayoweza kuhatarisha usalama wa mtu na kuyaangalia ukweli wake. Ila siyo kuangalia mipasho dhidi ya rais.
 
NIMEISOMA KWA MAKINI HII CHANGAMOTO KWA KWELI TANZANIA DAIMA WANAPASWA KUPONGEZWA... TUNAHITAJI SIASA ZENYE MUONA WA KITANZANIA NA SIO ZINAZO FANANA NA ZILE ZA JAMII YA KIARABU... lawama mwanzo mwisho kazeni TANZANIA DAIMA sasa muanze kuwakumbusha yale walioyaahidi na sio lawama
 
Kwa muda mrefu mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kumchafua Rais JAKAYA KIKWETE kwa mambo ambayo hayahusiani kabisa na majukumu yake ya kuongoza serikali.

Yapo mambo mengi ambayo watu kupitia mitandao wamekuwa wakimchafua Rais na hapa nitatoa michango michache tu:-

1) Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mtoto wake aitwaye MWANAASHA KIKWETE yametumika sana kumchafua JK.
2) Thread iliyoletwa hapa JF na kichwa cha habari "Maswali mia moja kwa Rais KIKWETE" yakiwemo yaliyohoji ana wake wangapi na mengine mengi yalioonekana ni ya kumchafua Rais zaidi na hayakuwa ya kiutendaji.

Yapo mengine mengi ambayo kiukweli hata kurudia kuyaandika hapa hayafai.


Katika gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 15/02/2012 katika ukurasa wake wa Tahariri (The Editorial page) mhariri ameandika kuhusu hili kwa kichwa cha habari "Mitandao isitumike kumchafua Rais". Amebainisha kwa uwazi na kuonya wanaomiliki mitandao hiyo wawe wanahariri na habari zinazotumwa kabla ya kuziandika katika mitandao yao.

Refference: Tanzania Daima la tarehe 15.02.2012


Kwa matokeo ya mwanao unaona wanamchafua sana.Je nahapa utasemaje mkuu??? https://www.facebook.com/photo.php?...66006044.14156.100002518337070&type=1&theater
 
Kwa bahati mbaya sana, matokeo ya mtoto huyo hayakuwa mazuri licha ya shule yake kufanya vizuri kitaifa katika mitihani hiyo na kuwa moja ya shule kumi bora

Hii ndio namna ya viwaandishi vinavyoandika kwa ajili ya tumbo. Kufeli bahati mbaya? Eboo!

Kufeli ni genetics, look at her father. Total failure. Kama kuchafuliwa basi kajichafua mwenyewe.

Pardon me please, huyu ndio ambaye mama yake ni ticha? Mweh! Mwalimu aliyesahau alikotoka
 
wanamchafua au wanasema ukweli?

Binafsi naona wao tanzania daima ndo wame mchafua kabisa
maana idadi ya watu wanao ingina mtandaoni ni chache kuliko wale wanao soma magazeti.

Kwa kuiweka habari hii gazetini ni sawa na ku-broadcast kwa ulimwengu kwamba
jamani kuna hili na hili,kama mnataka kujua kwa undani zaidi nendeni kwenye mitandao.

Tanzania daima wana tumia petroli kuzima moto,...wame kosea.
 
pole ila nafikiri magazeti au media inaripoti yale ambayo yameshatokea na hata kama hayataandikwa bado hayatafutika....yatajulikana tu...big figures ni target za media and somehow that is the prize they have to pay for being "big." It happens everywhere sio Tanzania tu......

Let them be targets but not for their personal and family issues which are merely private.
 
Mimi nadhani watoto wake ndio wanamchafua JK, mfano hili la Ridhiwani kudaiwa HESLB ni kashfa kwa Rais, kweli ameshindwa Ridhiwani ameshindwa kulipa bodi ya mikopo!? au ndio mambo ya kimjini mjini!! Sasa jamaa wakimshtaki maana kwa sheria ya HESLB wana nguvu hiyo watasema Rais anadhalilishwa!? Riz kafanya kazi IMMA Advocates na salary ni nzuri kiasi angeamua wamkate hata laki moja tu kwa mwezi saa hizi angemaliza huo mkopo!!
 
Binafsi naona wao tanzania daima ndo wame mchafua kabisa
maana idadi ya watu wanao ingina mtandaoni ni chache kuliko wale wanao soma magazeti.

Kwa kuiweka habari hii gazetini ni sawa na ku-broadcast kwa ulimwengu kwamba
jamani kuna hili na hili,kama mnataka kujua kwa undani zaidi nendeni kwenye mitandao.


Tanzania daima wana tumia petroli kuzima moto,...wame kosea.

Hawa jamaa wa Tanzania daima wamefanya hii makusudi, wamejifanya kuonesha sympathy lakini aim yao kubwa ni kuionesha jamii kuwa Mwanaasha Jakaya Kikwete nae kaambulia four!!
 
Huyu mtoto angepata div1 ya point saba nina uhakika kingeandaliwa kipindi maalumu kwa ajli yake ili awasihi wanafunzi wengine namna alivyokuwa anasoma ili na wao wafaulu.....lakini kwa kuwa amefeli na kupata four ya point 27 watu wakiuliza imekuwaje mtoto mwenye kila kitu nyumbani akapata daraja hilo wanaonekana ni wachochezi....tena ilifaa waandishi wamfate huyo mtoto na wamuulze imekuwaje akapata hivyo....nini kilipungua?

Lakini ukweli utabaki pale pale juu ya mwanaasha......huyu mtoto alikuwa mzito na wazazi wake hawakujua mapungufu yake toka alipotimuliwa kifungiro baada ya kushindwa kufikisha wastani na wakamuhamishia hapo Feza.... Wazazi walishindwa kujua kuwa binti ni mzito wa kuelewa na walikuwa hawafuatilii maendeleo yake ya shule...kama wote mjuavyo wazazi wa huyu binti wanashinda angani na kwenye bembea na wakirudi nyumbani badala ya kufatilia maendelea ya mtoto wao wao...wenyewe wazazi wanamchukua mtoto na kumpeleka kwenye shows kama inavyoonekana hapa chini...

Sasa hivi mama Salma na Kikwete waongeze nguvu na ufatiliaa kwa watoto wao wengine..kuna huyo mmoja anaitwa Ali nae ni mzito wa kuelewa tena sana.....kwa kuwa wako Botswana najua matokeo yao hayataonekana kama ya huyu Mwanaasha...ila ukweli utabaki kusemwa kuwa juu ya Mwanaasha, ni uzembe wake na uzembe wa wazazi wake...

Siku zote huwa nasema hivi:

Anayepata div one na anaepata div.iv wote msuli wao uko sawa ila in opposite direction.....wakati huyu anakomaa kupata div one huyu mwingine nae yuko bize na shows kama hizi :

LIONS%2BPRESIDENT%2BFRANK%2BGOYAYI%2B%2C%2BFIRST%2BLADY%2BSALMA%2BKIKWETE%2BAND%2BMWANAASHA%2BKIKWETE%2BFOLLOWING%2BTHE%2BEVNT%2BATTENTIVELY.JPG

Pongezi kubwa sana ziwaendee Balaza la Mitihani la Taifa na wasahihishaji wa mitihani hiyo kwa kutoangalia nyani usoni ila nini kimeaandikwa kwenye karatasi za mitihani.

Kuwa mtoto wa Rais si maana yake bongo lake kujipanga vizuri darasani, kwani ni dalili tosha uwezo wake umefikia hapo, na kama angekuwa mtoto wa kawaida au shule za huko Katani, basi kwa matokeo haya Divission "0" asingeikwepa, ujue hapa hiyo Divission "IV" ni kipangusa jasho tu kutokana na support kubwa ya mgongo wa mkuu wake vinginevyo tungeongea mengine.

Nusu ya kipindi cha uongozi wake anatumia kuwa nje ya nchi ni lini atakapokuwa na nafasi ya kuwa na familia yake?

Obama kipindi cha back to school utaona ameambatana na mabinti zake kwenda kuwanunulia vitabu na vifaa vingine vya shule, sisi tunawaachia watumishi washughulikie hayo ndiyo matokeo yake. Pomoja na utetezi lakini hawezi kukwepa kubeba lawama.
 
Tatizo nao wamezeoa sana kubeba habari za humu wanataka wazito kwenye magazeti yao, sasa hili wakaona litawatokea puaniii
 
Ni kweli kabisa hata mimi namwunga mkono Mhariri ingawa mimi si CCM na wala sifurahishwi na utendaji wa Rais wetu. Uhuru wa mmoja huishia uhuru wa mwezie unapoanzia, kwa kweli mimi nachukia "Personal attacks" ziwe kwa JK au yeyote. Lakini hapa ni lazima ieleweke kwamba kusema jambo fulani ni baya, linatuumiza, linakera, au linatuhujumu si dhambi hata kidogo, na kwa taasisi ya urais hilo ni sawa kabisa ila kuzungumzia juu ya mambo yake binafsi na familia (nje ya kujihusisha kwao na siasa za nchi) si ustaarabu hata kidogo.

Hiki ndicho hasa kilichomaanishwa na mhariri wa Tanzania Daima.
 
mwandishi yuko sahihi wengi tulitumia tukio hilo kisiasa badala ya ukweli.

Kwanza halikuwa swala la kujadili. Sikioni cha kujadili. Mtoto kufeli mtihani ujue inampa mzazi masikitiko. Rais pia ni mzazi kama mimi. Je mwanao akifeli utukanwae?
 
FEZA ni shule ya Private; ningemuona ni mzalendo kweli kama angelimpeleka katika shule za KATA zilizotapakaa kila kata. na ambazo anazisimamia MKULU AU HATA SHULE YA MSINGI ALIFELI HIVYO HAKUCHAGULIWA HATA KWENDA SHULE YA KATA??


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

sasa kama hakufaulu? Unalazimisha akasome kata,kata ni watoto waliofaulu,nampa big up raisi kikwete kwa kuwasomesha wanawe hapa hapa Tz
 
Mimi nadhani watoto wake ndio wanamchafua JK, mfano hili la Ridhiwani kudaiwa HESLB ni kashfa kwa Rais, kweli ameshindwa Ridhiwani ameshindwa kulipa bodi ya mikopo!? au ndio mambo ya kimjini mjini!! Sasa jamaa wakimshtaki maana kwa sheria ya HESLB wana nguvu hiyo watasema Rais anadhalilishwa!? Riz kafanya kazi IMMA Advocates na salary ni nzuri kiasi angeamua wamkate hata laki moja tu kwa mwezi saa hizi angemaliza huo mkopo!!

Baba ambaye ni Mkuu wa nchi yuko busy na misafara isiyoisha kutalii dunia utadhani yupo kwenye mashindano ya kitalii ili aibukie na tuzo ya dhahabu. Mama naye huyo kuzungukia mikoa sijui mama maendeleo au WAMA kama si WAWATA, nani yuko responsible na familia? Watumishi wa Ikulu ndio jukumu lao? TISS ndio wanaowajibika kwa kuwa ndio walinzi wa familia ya Mkulu?

Mama Obama baada ya mumewe kuapishwa aliulizwa na wanahabari shughuli yake itakuwa ipi mumewe awapo white house? Alijibu wajibu wake kwa sasa ni kutunza, kulea familia yake kwa kuwa mumewe atakuwa na majukumu mazito ya kitaifa.

Kwa Magogoni tofauti wote mitaani kusaka sitting allowances, yatokeayo kwa watoto na kupima maendeleo shuleni they don't care na haya yaliyotokea ndio ujira wao, hawana sababu ya kutetea zaidi ya kujifunika aibu. Wameshindwa kugawana majukumu katika familia watayaweza ya kitaifa?
 
Tatizo letu siku hizi tunataka kuugeuza huu mtandao wetu kama ni kijiwe cha kutunishiana misuli kati ya CDM na CCM, nakumbuka kuna member alisema kama CDm itshinda atatembea kwa miguu uchi wa mnyama. Alichoambiwa na jinsi alivyoshambuliwa na hali halisi ya kilichotokea ni kama mbingu na ardhi.

Hili la mtoto wa Kikwete niko upande mmoja na Tanzania Daima, haiwezekani sisi sote tujifanye kama vile ni wafaulu wa kiwango cha daraja la kwanza (Division 1) wakati wengine enzi zile za Mwalimu tulikuwa ni Ma - repeaters tuliokubuhu na hata majina yetu tunayotumia sasa tumeshayabadilbadili zaidi ya mara tatu. Hizi Private Candidate tumedunda nazo sana hadi Ndalichako hajui atupe adhabu gani, kama Supp watu tumefanya hadi deans wanajiuliza kwanini tupo vyuoni, kama Disco... basi tumecheza kwenye kila chuo tulichokwenda hadi sasa inatafutwa njia ya kutuzuia tusijiunge na vyuo vingine maana sasa inahitajika ngazi nyingine.

Sasa mtoto wa Kikwete tatizo lake ni nini, kwani kuishi Ikulu ndiyo uwe na uwezo wa kujibu kiikulu,
 
hapakuepo na sababu ya kushupalia kiushabiki huo mjadala,mimi nadhani tujifunze kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea kwamba maisha binafsi ya familia za viongozi wao na hasa watoto wanachukua tahadhari kubwa. kama huyo mtoto angekuwa amefanya mambo yasiyofaa ktk jamii angejadiliwa kwa kiwango kile lakini kufeli mtihani siyo dhambi ama kosa,hata watoto wetu na wadogo zetu wanafeli,na baadhi yetu humu kwa nyakati fulani tulifeli.

Huo ni ukweli na hata maprofessor wengine waliwahi kudisco kwa mfano prof.peter msorwa alidisco SUA lakini akaja kuwa mtu muhimu katika taifa
 
Back
Top Bottom