Mitandao isitumike kumchafua Rais

Mitandao isitumike kumchafua Rais

JK has to endure rain of abuses and criticism from the public as part of price he has to pay for his role in deepening this country's level of poverty.
 
1. Kumchafua mtu yeyote ni vibaya. Kwa hiyo kumchafua rais ni vibaya.Pia kumchafua mchuuzi wa samaki ni vibaya.

2. Wewe unachoona ni "kumchafua" mwingine atasema ni jambo la kusema sawa kabisa, kwa sababu huyu si mtu wa kawaida, ni rais.

3. Kurudia tusi ni kutukana. Kwa hiyo kuitoa hii habari kwenye "mitandao ya jamii" na kuipeleka kwenye magazeti ni kuikuza na kuwapa nafasi hata wale ambao hawasomi "mitandao ya jamii" waone "kumchafua rais" hivi.

4. Mwandishi anapoandika "Kwanza, lazima tutambue kuwa kufanya vibaya katika mitihani ni jambo la bahati mbaya ambalo kimsingi linamuumiza mtahiniwa na vile vile wazazi au walezi wake" analazimisha kwamba kufanya vibaya katika mtihani ni jambo la bahati mbaya. Ingawa inawezekana kufanya vibaya kukatokea kwa sababu ya bahati mbaya (mtu kajiandaa lakini kaumwa siku hiyo, ka panic, etc) hili halimaanishi kufanya vibaya automatically kunatokana na bahati mbaya. Moja ya outrage ya watu - justified or not- ni kuona kwamba mtu mwenye resources zote za taifa kupitia Ikulu, anafanya vibaya kwenye mtihani. Muandishi asitake kuhalalisha kufanya vibaya automatically kuwe "bahati mbaya". Kwa kufanya hivyo atamaanisha kufanya vizuri ni "bahati nzuri". Na mambo yote yanakwenda kibahati bahati tu,hivyo hamna responsibility, hamna merit wala remorse.

5. Inabidi tuangalie mambo kwa undani zaidi ya "kumchafua rais". Tumeongelea mambo mapana zaidi ya "kumchafua rais" hapa. Tumeongelea utamaduni na sheria za privacy kwa Watanzania wote. Waandishi wa habari kwa kushikia bango swala la mtoto wa rais na kuacha kuongelea swala kubwa zaidi la faragha za Watanzania wote wanajionyesha walivyo na ufinyu wa mawazo. The bigger story here should be whether the results should be made public or not. Hatutaki leo hii tuwape faragha Watanzania watoto wa marais wakati wenzangumie watoto wa Baba Kabwela hawapewi haki hiyo. Haki sawa kwa wote.

6. Ingawa "Noblesse oblige" na "Ukubwa mzigo" na mambo mengine wenzetu wanasema "it comes with the territory", I feel for Mwanaasha because she did not choose for her father to be the president. Waungwana hawatajihusisha na kashfa za kifamilia zisizo msingi. Lakini sitaki kulifanya hili swala kuwa la "familia ya rais". Inabidi kila Mtanzania apewe heshima hiyo hiyo.
 
Nakubaliana na wewe katika hili 100%.‎؛Lakini naomba niseme kitu kimoja,si busara pia kutojiuliza kwa nini jambo hili linatokea.Kwa mtizamo wangu mimi ni kwamba kuna sababu,tena sababu ya msingi kabisa.

Rais Kikwete amewaangusha watanzania,tena kwa kiwango cha kutisha kiutendaji. Hakuna Raisi wa Tanzania, ambaye utendaji wake unaweza kulinganishwa na wakwake.

Ni utendaji ambao ni mbovu na duni sana.Nisisitize kwamba Watanzania wana-express hasira yao kwa kusema mambo mabaya against him.Wanafanya hivyo kwa vile they cannot confront him physically. Kama anataka haya yasitokee aboreshe utendaji wake.

Hivi unajua kwanini mwamke ukimuudhi silaha yake ya kwanza nikuku-chafua katika jamii?Ni kwasababu hawezi kuku-confront physically.
Kwa muda mrefu mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kumchafua Rais JAKAYA KIKWETE kwa mambo ambayo hayahusiani kabisa na majukumu yake ya kuongoza serikali.

Yapo mambo mengi ambayo watu kupitia mitandao wamekuwa wakimchafua Rais na hapa nitatoa michango michache tu:-

1) Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mtoto wake aitwaye MWANAASHA KIKWETE yametumika sana kumchafua JK.
2) Thread iliyoletwa hapa JF na kichwa cha habari "Maswali mia moja kwa Rais KIKWETE" yakiwemo yaliyohoji ana wake wangapi na mengine mengi yalioonekana ni ya kumchafua Rais zaidi na hayakuwa ya kiutendaji.

Yapo mengine mengi ambayo kiukweli hata kurudia kuyaandika hapa hayafai.


Katika gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 15/02/2012 katika ukurasa wake wa Tahariri (The Editorial page) mhariri ameandika kuhusu hili kwa kichwa cha habari "Mitandao isitumike kumchafua Rais". Amebainisha kwa uwazi na kuonya wanaomiliki mitandao hiyo wawe wanahariri na habari zinazotumwa kabla ya kuziandika katika mitandao yao.

Refference: Tanzania Daima la tarehe 15.02.2012

 
Hakuna anayepinga hilo, lakini si kiasi kilichofikiwa kwa sasa cha kumuondolea hata utu wake kwa matusi na kashfa zisizo na maana. Katika hali ya kawaida hata wewe usingekubali haya. To be a public figure is not the reason for this.
Inaonekana huyu VGL ndo kamlipa mhariri wa TZ Daima atoe tahariri hii, halafu kaileta na thread huku, inaonekana huna kazi,we huyu rais kakusaidia nini mpaka leo?watoto wa kawaida wakifaulu wameiba mtihani,eti majibu yanafanana,malipo hapahapa duniani,unasoma academia,unapata kila kitu na unapata four vilevile.
Hao baraza wanaowaonea ndugu zetu,waziri anawahukumu watoto walio innocent eti wezi wa mitihani,kila mtihani una marking scheme,inakuwaje wanafunzi waliofundishwa na mwalimu mmoja wajibu tofauti wakati wote tumekuwa tukikariri?

Huyu rais lazima asemwe,amezidi,na wewe hapa unatwanga maji tu,kaemwa fb, blogs,email n.k,watu wameshamchoka,hata huyo wa tz daima mbona kaongelea four ya huyo first baby?mbona haongelei kashfa nyingine?hana maana,mngehoka baraza wampasishe ili tusiseme,tuna hasira sana na huyu prezidaa wa kichina
 
Kwani mara hii mmeshasahau? c ni nyinyi mliosema DR amepora mke wa mtu? mkasema ameacha upadri na mambo mengi binafsi.Hizo ni sera zenu na dhambi sasa inawarudia na bado.
Pamoja na maza kuwa ticha na jitihada za wasimamizi kuubeba mzigo ndio ikapatikana hiyo 4 isingekuwa hivyo tungesema mengine.
 
Kwa muda mrefu mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kumchafua Rais JAKAYA KIKWETE kwa mambo ambayo hayahusiani kabisa na majukumu yake ya kuongoza serikali.

Yapo mambo mengi ambayo watu kupitia mitandao wamekuwa wakimchafua Rais na hapa nitatoa michango michache tu:-

1) Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mtoto wake aitwaye MWANAASHA KIKWETE yametumika sana kumchafua JK.
2) Thread iliyoletwa hapa JF na kichwa cha habari "Maswali mia moja kwa Rais KIKWETE" yakiwemo yaliyohoji ana wake wangapi na mengine mengi yalioonekana ni ya kumchafua Rais zaidi na hayakuwa ya kiutendaji.

Yapo mengine mengi ambayo kiukweli hata kurudia kuyaandika hapa hayafai.


Katika gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 15/02/2012 katika ukurasa wake wa Tahariri (The Editorial page) mhariri ameandika kuhusu hili kwa kichwa cha habari "Mitandao isitumike kumchafua Rais". Amebainisha kwa uwazi na kuonya wanaomiliki mitandao hiyo wawe wanahariri na habari zinazotumwa kabla ya kuziandika katika mitandao yao.

Refference: Tanzania Daima la tarehe 15.02.2012


bata ni bata huwa hachafuliwh bali anachafua mwenyewe
 
mbona wakati wa uchaguzi mtoto wa rais Ridhiwani na mke wa rais walikua mstari wa mbele kumpigia kampeni baba yao na ikawa kama vile kampeni ya familia badala ya chama mbona nyie hamkusema hilo?Mtoto yeyot yule anayefeli mitihani mzazi ndo huwa anbebeshwa msalaba maana yy ndo anayetakiwa kumtengenezea mazingira mazuri ya mtoto kufaulu.
Pili mtoto aliyefanya vizuri kila mwaka huwa anaitwa kwenye tv hasa ya taifa na kuulizwa ilikuaje hadi akafanikiwa moja ya sababu ni familia yake kumpa ushirikiano na wazazi huwa wanasifiwa sana hata kupewa zawadi,je anayefanya vibaya wazazi wake hawatasemwa?hapa tutofautishe kumtukana mtu na kumsema hasa pale anapofanya vibaya.
 
Rais anahusika vipi na matokeo ya mtoto wake? uzumbukuku huu.

Mama Porojo,

..ukizingatia kwamba huyo binti ni mtoto wa sekondari ambaye hajafikisha umri wa kujitegemea basi wazazi wake wanahusika ktk suala zima la elimu yake, and particularly matokeo yake ya mitihani.
 
Baba yangu angekuwa Rais angesemwa vilevile.....kuna watu hawakanyagi baa baada ya watoto wao kufeli kwa kuogopa maneno sembuse Rais?

Mkuu samahani utakuwa unachanganya habari mzee wako kushambuliwa na maneno sio mpaka awe Rais na hata wasio kanyanga baa hatuwezi kujua kwanini hawakanyangi labda yawezekana waliwatambia hapo baa watoto wao ni vichwa na wakaahidiana kuonyeshana ktk matokeo! Kikubwa mkuu hapa si kumkashifu Rais kwa maneno ambayo hata ukiambiwa wewe naamini hutayafurahia bali ni kumwomba aitizame sasa secta yetu ya elimu!
 
Mwandishi alikuwa anataka kuwaeleza watanzania ambao hawatumii mitandao ya kijamii kuwa mtoto wa rais yaani mwanaasha amepata DIV 4, kwani heading na content viko tofauti kabisa. Mwandishi huyo ndio aache kumchafua rais
 
wenze2 wazungu wenye akili mara nyingi kabla hawajagombea nafac hizi za kisiasa.. wanakaa na familia zao kwanza.. wanaelewa unapoingia kwenye siasa ni sawa na kuamua kuvua nguo hadharani.. so hauwi uamuzi wa wake binafc.. ila unakuwa ni uamuzi wa baba na mama na watoto.. Jenerali Collin Powell alishawishiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais marekani.. lakini baada ya kukaa na familia yake.. alikataa kabisa kujiingiza.. ukishakuwa mwanasiasa unakuwa sawa na taulo..
 
Wanajamiii, kimsingi tunakubaliana kuwa public figure ni vigumu kutojadiliwa - kwa uzuri au ubaya- na jamii. Hiyo ndiyo faida na hasara (au gharama) ya ukubwa. Hata hivyo tukubaliane vile vile kwamba matusi yamezidi katika michango yetu na wakati mwingine tunakosa dira. Na mashambuluzi personal dhidi ya Rais yamevuka hata mipaka ya uhuru wa kupashana habari. Tujaribu kuwa waungwana katika michango yetu. Huyu binti tunazidi kumwongezea simanzi; tulitegemewa kumpa moyo kwamba kateleza tu hajaanguka. Asikate tamaa na akijaribu tena atafanikiwa. Hili liwe jamvi la kuelemishana na kuonyeshana njia ya mafanikio, siyo matusi na kukatishana tamaa.
 
Angepata Div.one wangesema amependelewa au kupewa paper..Watanzania kwa kuongea ni mwisho..
 
JK angeweza hata kumpeleka mtoto wake nje na tusingejua yote haya. Amesoma shule za ndani kwa nini tusimpongeze kwa hilo.
Kwani mtoto wa raisi akisoma shule hapa au nje mtanzania wa kawaidi kama mimi na athirika vipi?
 
Mkuu, wewe ni mkongwe humu JF lugha unayotumia wala aipendezi, new members unadhani watajifunza nini kutoka kwa wakongwe kama nyie!
ritz wakati mwingine sijui huwa unakuwa na akili ya jinsi gani, kweli nyani haoni kundule!
 
Sisi huku vijijini tunaambiwa kuwa ili mtoto aweze kufaulu mzazi lazima afuatilie, asimwachie mwalimu peke yake. Sijui kama nadharia hii inaapply hata huko Feza. Kama inaapply then nani alaumiwe kwa suala hili?
 
Hahitaji kuchafuliwa. Kesha jichafua mwenyewe kwa masafari ya kwenda kuomba omba.

Nchi tajiri kama TZ inanuka umaskini. Kwa nini?
 
Back
Top Bottom