Mitandao isitumike kumchafua Rais

kama kweli wote tulipitia posts baada ya tukio matokeo ya mwanaasha tunakubaliana kwamba mjadala ulihama kutoka kwa mtoto kwenda kwa baba.

hapakuepo na sababu ya kushupalia kiushabiki huo mjadala,mimi nadhani tujifunze kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea kwamba maisha binafsi ya familia za viongozi wao na hasa watoto wanachukua tahadhari kubwa. kama huyo mtoto angekuwa amefanya mambo yasiyofaa ktk jamii angejadiliwa kwa kiwango kile lakini kufeli mtihani siyo dhambi ama kosa,hata watoto wetu na wadogo zetu wanafeli,na baadhi yetu humu kwa nyakati fulani tulifeli.
 
suala hilo ni binafsi lakini likahusishwa na siasa chafu dhidi ya JK. Haipendezi hata kidogo.
 
Kufeli kwa mtoto wake kuna uhusiano gani na urais wake? na je wewe kwenu hakuna waliowahi kufeli mitihani na pengine ukiwemo wewe, je nani alimsema Baba yako?

Baba yangu angekuwa Rais angesemwa vilevile.....kuna watu hawakanyagi baa baada ya watoto wao kufeli kwa kuogopa maneno sembuse Rais?
 
Kikwete ni public figure. Definition ya "public figure" kwenye answer.com ni

"A famous person whose life and behavior are the
focus of intense public interest and scrutiny."

Hawezi kukwepa haya especially kwenye kipindi hiki cha utandawazi
 
Kwa hiyo mnataka TUMSIFU RAIS WETU...............MILELE DAIMA?


Hakuna anayekulazimisha umusifu, tunachozungumzia hapa ni kwa nini atukanwe hata kwa mambo yasiyo na tija kwa taifa na hayahusiani? Kasome Tanzania Daima la leo unaweza kupata mantiki ya hii thread!
 
Tanzania Daima kwa mara ya kwanza nawapongeza kuliona hili. Mitandao inatumika vibaya ingawa sio wakati wote.

Ni nini kilichokufanya kufungua mtandao huo unaochafua. Na Tanzania Daima wanatafuta nini kama siyo kihelehele. Wameshindwa kutoa taarifa ya watuhumiwa wa kesi za EPA zimeishia wapi siku hizi Kimya. Vyombo vya habari tunasikia mambo ya migomo, mafuriko, maandamano.

Lakini mambo yanayolihusu Taifa kama wezi wa EPA, RICHMOND, IPTL; akhaaaa siku hizi hawaandiki tena.

Sasa wanaamua kuchunguza yasiyo wahusu, au ni kujipendekeza ili wachaguliwe katika Baraza Jipya la Mawaziri linalotegemewa kutangazwa karibuni na Mh. Raisi??

ACHENI HIZOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

FANYA KAZI YENU.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
hakuna anayekulazimisha umusifu, tunachozungumzia hapa ni kwa nini atukanwe hata kwa mambo yasiyo na tija kwa taifa na hayahusiani? Kasome tanzania daima la leo unaweza kupata mantiki ya hii thread!

si lazimiki kukisoma tanzania daima.........hoja hii ya huyu mtoto imejadiliwa kirefu hapa labda hukusoma.......ni kuwa mtoto kama huyu mwenye kuishi katika mazingira bora pengine kuliko watoto wote wa tanzania hii kwanini anashindwa kupita mitihani yake?
 
Kikwete ni public figure. Definition ya "public figure" kwenye answer.com ni

"A famous person whose life and behavior are the
focus of intense public interest and scrutiny."

Hawezi kukwepa haya especially kwenye kipindi hiki cha utandawazi

Hakuna anayepinga hilo, lakini si kiasi kilichofikiwa kwa sasa cha kumuondolea hata utu wake kwa matusi na kashfa zisizo na maana. Katika hali ya kawaida hata wewe usingekubali haya. To be a public figure is not the reason for this.
 
Kikwete ni public figure. Definition ya "public figure" kwenye answer.com ni

"A famous person whose life and behavior are the
focus of intense public interest and scrutiny."

Hawezi kukwepa haya especially kwenye kipindi hiki cha utandawazi

whose life na whose family ni sawa?
 
Rais anahusika vipi na matokeo ya mtoto wake? uzumbukuku huu.

Kama unadhani hahusiki na matokeo ya mtoto wake, nani aliyekuwa akimsomesha? Hujui kuwa watoto na wake za viongozi huheshimiwa kwa sababu ya viongozi wenyewe? Imetokea hata wakuu wa wilaya husoma taarifa za wilaya zao mbele ya mke wa rais. Hivyo utendaji mbovu wa rais au hata wa mke na/au watoto wake unahusihusishwa na viongozi kwa jinsi wao wanavyojihusisha na masuala ya wazazi au waume/wake zao.
 
sikubali wala kukataa kinachojadiliwa, ila najaribu tu kuwaza,

Kama Mwanaasha Jakaya Kikwete angepata Division 1 na au angeongoza katika kumi bora ingekuwaje?

Maana lazima watu tungemsifu kuwa mtoto wa raisi kapasua kwenye mitihani yake, je, mngelalamika pia kwamba tuna'mkashifu' mtoto wa raisi?

At the end of the day as long yeye ni raisi hakuna cha maisha binafsi, tutamjadili kwa jema au baya, awe tayari kukubali tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom