Nimeshuhudia misiba mingi ya watu wa kaskazini mwa nchi hii. Kama safari inaanzia Dar, basi safari hiyo hugeuka kuwa tour kwa baadhi yao hasa wale wasindikizaji wasiokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na wafiwa.
Utakuta watu wapejipachika na vistarehesha kibao, ndani ya magari kumesheheni vilevi na vitu vinginevyo.
Siku hizi Njia Panda ya Himo huko Moshi ndio mahali pa kutia break wanapofika Moshi kabla ya kukucha vizuri watu huweka kambi pale ili waingie msibani baada ya kupambazuka. Pale Njia Panda club za starehe hufurika waombolezaji walioamua kugeuza msiba wao kuwa starehe, watu wanapotezea vibaya pale, hawataki simanzi hata moja. Watu hawa humwagilia mioyo yao bila kujali ni saa kumi na moja asubuhi ilhali tu wawe freshi. Na wengine huruka majoka na vibenteni vya pale usiku kucha!
Wakiingia msibani huko milimani utawaona tu nyuso zao, utafikiri wameleta harusi nyumbani!
Huzuni huwa ni kwa sekunde chache tu pale marehemu anapopumzishwa na kurudishwa mavumbini. Sekunde chache baada ya hapo watu wanapiga cheeers!!! Wanavunja vyupa!
Ni mwendo wa kumwagilia na kama msiba ni wa kitajiri ndio usiseme, watu huagiza kama wapo Copa Cabana na wengine hujisahau kama wapo kwenye msiba na hata kuanza kucheza nyimbo za kwaya msibani kwa raha zao! Kweli msiba ni wa wafiwa tu na sio wasindikizaji!