Misheni kubwa za taasisi ya upelelezi MOSSAD!

Misheni kubwa za taasisi ya upelelezi MOSSAD!

Tuendelee....

UNYONGAJI NDANI YA BAGHDAD

Sehemu ya tatu.

Reuven Shiloah, miaka arobaini(40), mpole na mstaarabu, msiri, alikuwa ni mtu aliyejaa mafumbo. Alitokea kwenye tamaduni tajiri, akiwa na ubongo mwepesi kwa uchambuzi, mwenye uelewa mpana wa Uarabuni ya mashariki ya kati, mila zake za kikabila, koo zinazoongoza, ushirikiano wa mashaka na ugomvi uliopelekea umwagaji wa damu.

Moja kati ya watu waliomhusudu sana alimwita "malkia katika mchezo wa chess wa Ben- Gurion" wakati akifanya kazi kama mshauri wa kisiasa wa David Ben- Gurion. Baadhi walimfananisha na Kadrinali Richelieu wa Ufaransa; wengine walimuona kama mtu 'mjanja mjanja', 'mpiga pupa' mzamivu, mtu aliyejua namna ya kuendesha matukio nyuma ya pazia bila kujihusisha moja kwa moja. Shiloah alikuwa akijihusisha moja kwa moja, katika maisha yake yote, katika misheni za siri na kazi za uaskari kanzu.

Akiwa mchangamfu, aliyejiamini, muadilifu na mtoto wa mwalimu wa sheria za kiyahudi (rabbi), Shiloah alizaliwa katika iliyokuwa Jerusalem ya zamani. Kila wakati akiwa amevalia nadhifu na kunyoa ndevu vizuri, akinyemelewa na upaa - Shiloah alikuwa amejiwekea misheni huko Baghdad, muda mrefu nyuma kabla ya kuzaliwa kwa taifa la Israel.
Alishakaa kwa miaka mitatu ndani ya Iraq, akijifanya kama mwandishi wa habari na mwalimu huku akijifunza siasa za nchi hiyo.

Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia (wwii) alifanya makubaliano na Uingereza ili kuanzisha kikosi cha makomandoo cha wayahudi ili kuhujumu operesheni za wa-Nazi waliokua wakiitawala Ulaya.Alisaidia katika kutengeneza vikosi viwili vya makomandoo: Kimoja kikiwa ni Battaliani ya wajerumani, waliokua na silaha na sare za Ujerumani, ambao walitekeleza operesheni za hatari nyuma ya maadui huko Ulaya; Kingine kilikuwa ni Battaliani ya waarabu, ambao washiriki wake waliongea kiarabu, walivalia kiarabu, na walipewa mafunzo kwa misheni ndani kabisa Uarabuni. Aliwashawishi pia waingereza kuwaingiza kwa miavuli ya upepo - parachute, wayahudi waliojitolea kutokea Palestina ili kuingia Ulaya, ili kupangilia upinzani wa ndani wa wayahudi dhidi ya wa-Nazi.

Shiloah alikua wa kwanza kuanzisha mawasiliano na OSS (Office of Strategic Service), taasisi iliyokwuwepo kabla ya CIA. Wakati wa vita ya uhuru wa Israel, alisafiri kwenda makao makuu ya nchi jirani ya Kiarabu kwa siri na akarudi na 'kombe la thamani kubwa': mkakati wa uvamizi wa majeshi ya kiarabu. Uhitaji wa Shiloah kufanya kazi chini ya wingu kubwa la usiri ulikuwa chanzo cha shujaha huyu wa ajabu.
Marafiki zake waliwahi kutania kuwa, wakati alipokodi teksi na kuulizwa,"unaelekea wapi?". Shiloah alijibu: "Hiyo ni siri ya serikali".

Itaendelea......
 
Kuna kitu sijaelewa, wadau mko kimya sanaaa...
Au story inaboa tuiache...
Au naandika sana mpaka mnashindwa kucomment...
Nichukue lipi?
Ukweli hatu comment sana kwakuwa iko poa so hatutaki comments nyingi ila tunataka story tu
 
Tuendelee...

UNYONGAJI NDANI YA BAGHDAD

Sehemu ya nne.

Wakati wa vita ya Uhuru, Shiloah alikuwa kiongozi wa kitengo chahuduma za taarifa za kisiasa za nje. Kilikuwa moja kati ya vikundi vilivyoonekana kuwa huru vilivyoanzishwa kabla ya kuzaliwa kwa Israel. Ila Desemba 13, 1949, Ben- Gurion alitoa agizo la kuanzishwa kwa "taasisi (Kiebrania, Mossad) kuunganisha taasisi za usalama wa Taifa", ikiongozwa na Reuven Shiloah.

Ila ilichukua miaka miwili zaidi ya ucheleweshaji na migogoro kabla ya Mossad kuanzishwa. kitengo kimoja cha kijasusi, kilichoitwa 'Kitengo cha siasa', ambacho wanachama wake walikua wakikusanya taarifa kutoka mataifa ya nje, wakiwa na akaunti nono za matumizi na maisha ya kifahari, kiligoma na kukataa kufanya kazi ya ushushushu kwa Israel waliposikia mikakati ya kuvunja kitengo chao na kukiunganisha ndani ya Mossad.
Ni baada tu ya kukaripiwa - na wengi kufukuzwa kazi - ndipo Shiloah akaanzisha Mossad.

Jina lake lilikuja kubadilishwa na kuwa taasisi ya ujasusi na operesheni za kipekee, na msemo wake wa hamasa ukachaguliwa kutoka Mithali, 11:14 : "
Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka, bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika". Ila sio jina jipya wala kauli mbiu ya hamasa iliyofanya Mossad kuwa ya kipekee. Shiloah alikuwa na nia ya dhati ya kuipatia muonekano wa kipekee. Mossad ilikuja kuwa si mkono mrefu tu wa Israel, Ila pia mkono mrefu wa jamii yote ya Kiyahudi.

Katika mkutano wake wa kwanza na maafisa wa mwanzo kabisa, kiongozi huyu wa Mossad (ramsad) alisema :" Ukiachilia mbali majukumu yote ya taasisi ya kijasusi, tuna jukumu lingine kubwa: kulinda wayahudi wote, popote pale walipo, na kupanga utaratibu wa kuwarudisha Israel." Na kweli, katika miaka iliyofuata Mossad ilikuja kusaidia kuanzisha vikosi vya ulinzi binafsi katika sehemu ambazo jamii ya kiyahudi ilikuwa katika harakati ya kuteketea : Cairo, Alexandria, Damascus, Baghdad, na baadhi ya miji kusini mwa Amerika.
Vijana wakakamavu wa kiyahudi waliletwa Israel na kupewa mafunzo na jeshi pamoja na Mossad, silaha zilivushwa katika mipaka ya nchi zenye migogoro na nchi maadui na kufichwa, wayahudi wenyeji walipangwa katika vikosi vya ulinzi ili kutengeneza nguvu ya kuweza kulinda jamii ya wayahudi dhidi ya magenge au vikundi vya kijeshi visivyo rasmi - angalau mpaka msaada uje kutoka vikosi vya serikali au taasisi za kimataifa.

Katika miaka ya hamsini (50's), Mossad iliwapeleka Israel makumi ya maelfu ya wayahudi waliokua wakiishi katika hatari kutoka nchi za kiarabu huko mashariki ya kati na Morocco; na miaka baadae, miaka ya themanini (80's), ilikuwa ni Mossad tena aliyepanga uokoaji wa wayahudi waliokwama katika Iran ya Khomeini na kutekeleza kuhama kwa wayahudi wengi waliokuwa Ethiopia kuelekea Israel.
Ila katika operesheni yake ya kwanza ya siri Iraq, balaa lilitokea.

Katika maduka makubwa ya bidhaa huko Baghdad, Orosdi Bak, mtaa wa Rashid, kijana mmoja aliyeitwa Assad alikuwa akiuza kauta ya duka la tai za shingoni. Kama mkimbizi wa Palestina, alikuwa....

Itaendelea.....
 
Special mention kwa Morgan Ande...
Nimeona buku mia nne..
So kutiririka ni uhakika..
Ubarikiwe sana
 
Tuendelee...

UNYONGAJI NDANI YA BAGHDAD

Sehemu ya Tano.

..... amekimbia nyumbani kwao Acre ambako jeshi la Israel lilikuwa limeteka jiji. Kitambo kidogo kabla ya kukimbia Israel, alikuwa ametoa msaada kwa binamu yake aliyekuwa mgonjwa, kwa kushika nafasi yake kama mhudumu katika kefu karibu na makazi ya gavana wa jeshi. Kwa wiki nzima, Assad alikuwa akitembea katika viunga vya makazi ya gavana, akiwa amebeba trei la shaba lililopambwa vizuri akihudumia vikombe vidogo wa kahawa kali ya Uturuki kwa maafisa wa kijeshi wa Israel. Nyuso za baadhi ya hawa maafisa vijana zilibaki katika kumbukumbu zake.

Siku hiyo, May 22, 1951, alikua akiwaangalia wateja waliokua wakiingia na kutoka dukani, kisha akatambua uso usiokua mgeni. Haiwezi kuwa, alifikiria kwanza, haiwezekani! Ila alimkumbuka mtu aliyemuona - sio katika katika shati na bukta (nguo za msimu wa joto) kama ilivyo leo, ila katika sare za kaki. Haraka, Assad akawajulisha polisi. "Nimemuona ofisaa wa jeshi la Israel! Hapahapa Baghdad!"

Mara moja Polisi wakamkamata huyu mtu aliyefanania mzungu, aliyekuwa ameambatana na kijana mwembamba, mwenye sura isiyorahisi kufananisha, aliyevaa miwani na myahudi wa Iraq. Aliitwa Nissim Moshe, na alowaambia polisi kuwa alikuwa mtumishi wa uma katika kikundi cha jamii ya wayahudi. "Nilikutana na huyu mtalii jana katika kongamano," alielezea, "na akaniomba nimuongoze kwenye maduka".

Walipofika makao makuu, hawa watu wawili walitenganishwa. Wapelelezi wa Iraq walimuhoji , Moshe na mtu aliyetambulika kama Muisrael, kikatili. Moshe akakomaa na stori yake: alikutana na huyu mtalii jana tu, na hakumjua. Katika sero zenye giza kwenye makao makiu ya polisi, wapelelezi walimfunga Moshe miguu na mikono, wakampiga na kutishia kumuua. Ila mfungwa wao jeuri alionyesha kutojua chochote. Baada ya wiki ya mateso, wairaq wakakubaliana kwamba Nossim Moshe hana umuhimu na wakamuachia.

Yule mfungwa mwingine aliendelea kurudia kuwa alikuwa raia wa Iran, anaitwa Ismail Salhun, na akawaonyesha waliomkamata pasi ya kusafiria ya Iran; ila waliendelea kumtesa. Hakuonekana kama muiran, na hakuweza kuzungumza neno moja la kipersia. Mwishowe, walimkutanisha na Assad, yule mpalestina aliyemtambua. "Damu yangu iliganda kwenye mishipa mara nilipomuona,"mfungwa alisema baadae. Alizidiwa na mateso na akaungama: aliitwa Yehuda Taggar (Yudke Tadjer),muisrael na kepteni wa IDF. Wapelelezi wakamzoa mzobemzobe hadi kwenye makazi aliyofikia, wakavunja thamani, wakatoboatoboa ukuta, na ndipo wakagundua akiba ya nyaraka - faili kubwa lililogundishwa chini ya droo la dawati.

Hapo kizungumkuti kikaanza. Sio tu kwa Taggar, bali kwa jamii yote ya kiyahudi ndani ya Baghdad.
Taasisi kadhaa za siri za kiyahudi na za Israel zilikuwa zikifanya operesheni ndani ya Baghdad, ikiwa ni pamoja na kikosi cha uhamiaji ambacho hakikuwepo kisheria, kikundi binafsi cha ulinzi, na vyama vichache vya wanaharakati vya kizayoni na vya vijana. Vingine vilianzishwa hata kabla ya kuzaliwa kwa taifa la Israel. Ndani ya Baghdad, katika mahandaki kadhaa, silaha na nyaraka zilikua zimehifadhiwa, baadhi ndani ya sinagogi la kati la Mas'uda Shemtov.


Itaendelea...
 
Tuendelee....

UNYONGAJI NDANI YA BAGHDAD

Sehemu ya sita.

Ongezeko la karibuni kwenye hivi vikundi ilikuwa mitandao michache ya kijasusi, iliyoratibiwa harakaharaka kabla ya kuanzishwa kwa Mossad; muunganiko na ushirikiano wa pamoja ni kama havikuwepo, na anguko la moja ya hivi vikundi lingeweza kupelekea kirahisi kabisa maanguko ya vikundi vingine vyote. Wayahudi wa Iraq walikaa katika 'bakuli la unga': Iraq alikuwa adui hatari zaidi kwa taifa changa la Israel, na ambaye peke yake alikataa kuweka saini makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kila mwanachama wa mitandao ya siri ya Kiyahudi alifahamu kuwa Iraq isingeonyesha huruma na maisha ya yake yangening'inia kwenye kamba.
Kwa sababu hiyo, Yehuda Taggar alitumwa kutenganisha mtandao wa kijasusi kutoka kwenye ile mingine. Akiwa afisa wa zamani wa kikosi maalum chenye umahiri mkubwa cha Palmach, Taggar alikuwa na miaka ishirini na saba (27) akiwa na muonekano wa uasi na tabasamu la kila wakati.

Hii ilikuwa misheni yake ya kwanza nje ya Israel, na kabla ya kukamatwa alitumia juhudi zake zote kutenganisha mtandao huo kutoka kwenye makundi mengine, ila baadhi ya watu wake , bila kujali, bado walishiriki katika shughuli nyingine za siri; muisrael mwingine mwenye pasi halali ya kusafiria ya uingereza, Peter Yaniv (Rodney - mhindu), aliendesha mtandao uliojitenga ila akiwa na mawasiliano na Taggar.

Mawasiliano ya Taggar kwenda Tel Aviv yalipitia kwa kamanda wa ngazi ya juu wa vikundi vyote vilivyokuwa vikifanya operesheni ndani ya Baghdad: mtu msiri sana ambaye utambulisho wake ulifahamika na wachache. Jina lake la bandia aliitwa Zaki Haviv, ila ukweli alikuwa Mordechai Ben - Porat, muisraeli aloyezaliwa Iraq, afisa wa zamani katika vita ya uhuru ya Israel. Hakupenda kurudi Baghdad na alikuwa katika hatua za mwisho za kumuoa msichana waliyekutana jeshini, ila baadae akakubali msukumo wa jamii ya kijasusi na akakubali misheni hii ya hatari.


Katika siku zilizofuata baada ya kukamatwa kwa Taggar, taasisi yote ya ujasusi iliparanganyika vipande vipande. Kikosi cha kipekee cha polisi cha Iraq kilikamata wayahudi wengi. Kuna walioshindwa kuvumilia kwenye mateso na mahojiano, wakatoa siri zilizowapelekea polisi kujua sehemu zao za kificho. Wairaki waligundua nyaraka zilizowahusisha wayahudi na ujasusi. Chini ya jiwe la bendera la sinagogi la Shemtob, polisi waligundua hifadhi kubwa ya silaha. Jiwe hili lilijengwa miaka mingi nyuma, kuanzia baada ya umwagaji wa damu wa kimbari mwaka 1941 ambapo wayahudi 179 walichinjwa, 2118 waliumizwa, na mamia ya wanawake kubakwa.

Idadi ya silaha zilizopatikana iliwashangaza Wairaq : mabomu 436 ya kurusha kwa mkono, bastola 33, rivolva 186, Bunduki 97, majambia 32 ya makomandoo na viboksi 25,000 vya risasi.
Katika mahojiano makali ya wairaq, kuna jina lilitajwatajwa mara kadhaa : Zaki Haviv, kiongozi wa ajabu wa hivi vikundi vya siri. Ila alikuwa ni nani? Na alikuwa wapi?
Mwishowe, mpelelezi, kijana makini, akafanya muunganiko : Zaki Haviv asingeweza kuwa mwingine zaidi ya Nissim Moshe, huyu mtu aliyeonekana wa kawaida alikuwa amekamatwa pamoja na Taggar na kuachiwa.

Watu kadhaa wa usalama wakavamia nyumba ya Moshe ila hawakukuta mtu. Moshe aliwindwa kote ndani ya Baghdad katika operesheni ya ukubwa wa kihistoria, ila Zaki Haviv alikuwa ametoweka.

Itaendelea....
 
Nyie mkiweka bando kama hivi.. mimi nashusha vitu..
 
Tuendelee...

UNYONGAJI NDANI YA BAGHDAD

Sehemu ya saba.

Ila kimsingi alikuwa sehemu pekee ambayo polisi hawakuota kumtafuta. Alikuwa jela.
Siku chache baada ya kuachiwa mara ya mwanzo akiwa na Taggar, Ben - Porat aliamshwa na kelele za kugongwa kwa mlango wake. "Fungua, polisi!" Maafisa walikua wakifoka. Ben - Porat akadhani huo ulikua mwisho wake. Nyumba haikuwa na mlango wa nyuma wa kutokea, na hakukuwa na yeyote ndani ya Baghdad ambaye angeweza kumuokoa kwa sasa. Na alifahamu - kwa mtu wa nafasi yake, kungekuwa na hukumu moja tu katika mahakama za Iraq : Kitanzi.

Alikubali mwenyewe na akaamua kufungua mlango. Maafisa wawili wa polisi walikua nje. "Uko chini ya ulinzi", mmoja akasema. Ben - Porat akajifanya kushangaa:" kwani nimefanya nini?" "Ah, hakuna kitu 'serious' ", yule askari akasema,"ni ajali tu ya gari. Sasa, kavae".
Ben - Porat hakuamini masikio yake. Alishasahau kuhusu ajali aliyohusika miezi kadhaa iliyopita. Alipuuza wito wa mahakama, na sasa alipaswa kwenda kwenye kesi. Kesi ilikuwa fupi, haukizidi saa moja. Jaji akamhukumu wiki mbili jela. Na hivyo, wakati jeshi la maafisa wa Iraq likiwa katika hali ya juu ya tahadhari, wakimtafuta, Zaki Haviv alikuwa akilipa deni lake kwa jamii kwenye jela ya Baghdad.

Kabla ya kuachiwa wiki mbili baadae, alikuwa akipelekwa makao makuu, kuchukuliwa alama za vidole na kupigwa picha. Alifahamu kama hili lingetokea basi ingekula kwake. Wangeweza kumtambua kama Zaki Haviv, na wakati huu isingekua humumu ya wiki mbili. Alitembea na walinzi wawili katika mitaa ya Baghdad kuelekea makao makuu, yaliyokua mbali kidogo. Njiani walipitia eneo lenye msongamano wa watu la Shurja Souk, soko la watu wengi lililojaa maduka yenye mwanga hafifu, wafanyabiashara wakipiga kelele kusifia bidhaa zao, na likiwa na chochoro nyembamba zenye konakona.

Alipoona ni muda sahihi, Ben - Porat aliwasukuma walinzi pembeni, akajichanganya katikati ya watu, na kutoweka. Askari wala hawakujaribu kumkimbiza. Maana, alikuwa aachiliwe chini ya lisaa mbele, usumbufu wa nini?
Ila waliporipoti hilo tukio, milango yote ya jehanam ikafunguka. Walikua wamemuachia Zaki Haviv, mtu alijetafutwa zaidi ndani ya Iraq!
Vyombo vya habari vya upinzani vikapata hiyo taarifa na kushambulia uzembe wa serikali na vichwa vya habari. " Yuko wapi Haviv?" liliuliza gazeti moja, na kujibu : "Haviv - yuko Tel Aviv!"

Huko Tel Aviv, wakubwa wa Ben - Porat kwa umakini waliandaa njia za yeye kutoroka Iraq. Wakati amejificha katika nyumba ya rafiki yake, mkakati wa maana ulianza kutekelezwa. Wakati huo zoezi kubwa la usafirishaji wa jamii za Kiyahudi kutoka Iraq kwenda Israel lilikuwa likiendelea, kwa kupitia Cyprus.
Kama wayahudi laki moja walikimbia Iraq, kwa ndege kubwa zilizokuwa zikiruka karibu kila usiku.

Usiku wa June 12, Ben - Porat alivaa nguo zake maridadi kabisa na kusimamisha teksi. Rafiki yake alikuwa amemwagia arrak - pombe ya kienyeji - na, ....

Itaendelea.....
 
Wakuu MB za buku voda ni masaa 24 tu!
Jie wekeni MB.. mimi nashusha
 
Tuendelee....

MAZISHI NDANI YA TEHRAN

Sehemu ya pili.

Mauaji ya wanasayansi wa nyuklia wa Iran ilikuwa sehemu moja tu katika vita kubwa. Gazeti la 'Daily Telegraph' la London liliandika kuwa, Mossad chini ya Dagan ilipandikiza mshushushu waliowapa Iran taarifa za uongo zinazofanania na kweli ila kuchukua taarifa za kweli za Iran, ilitengeneza timu za wauaji, timu za kuharibu miundombinu inayohusiana na programu za nyuklia, ilisajili kampuni za uongo zilizoiuzia Iran vifaa feki na hivyo kudhoofisha sana nguvu za Iran kwa miaka na miaka ya operesheni za siri dhidi ya programu ya silaha za nyuklia za Iran.

Reva Bhalla, mkurugenzi wa uchambuzi taasisi ya Stratfor aliwahi kunukuliwa akisema: "Kwa ushirikiano na Marekani, operesheni za siri za Israel zilijikita kwenye kumaliza rasilimali watu waliojihusisha na programu ya nyuklia na kuhujumu utaratibu mzima wa Iran kupata malighafi". Mwanamama huyu alisema, Israel iliwahi kutumia mbinu hizohizo kwa Iraq miaka ya mwanzo ya themanini (80's), wakati Mossad ilipowaua wanasayansi watatu wa nyuklia wa Iraq hivyo kukwamisha kumalizika kwa kinu cha 'atom' cha Osiraq, karibu na Baghdad.

Katika vita hii dhidi ya programu ya nyuklia ya Iran, Mossad chini ya Dagan kwa ukamilifu kabisa ilikua inachelewesha utengenezaji wa bomu la nyuklia la Iran kwa muda mrefu itakavyowezekana, na hivyo kufurusha tishio la kuifuta Israel katika uso wa dunia kama ambavyo Ahmadinejad alivyokua akitishia.

Lakini hata hivyo haya mafanikio madogo hayawezi kulipia makosa makubwa zaidi yaliyofanywa na Mossad katika historia - kushindwa kugundua na kuanika mradi wa siri wa nyuklia wa Iran toka mwanzo wake.
Kwa miaka kadhaa sasa Iran imekua ikiimarisha uwezo wake kinyuklia - Na Israel haikuwa na habari.

Iran imewekeza kiasi kikubwa cha fedha, kufundisha wanasayansi, kujenga ngome za siri, kufanya majaribio ya kisasa yaliyofanikiwa- na Israel haikujua kitu. Kutokea wakati Iran chini ya Khomeini ilipoamua kuwa taifa lenye nguvu ya nyuklia, ilitumia udanganyifu, hila na mikakati iliofanya vyombo vya ujasusi vya magharibi na Israel kwa pamoja waonekane wapumbavu.

Shah Reza Pahlavi wa Iran, alianza kujenga kinu cha nyuklia, kwa matumizi ya amani na ya kivita. Mradi wa Shah ulianza miaka ya 1970 na Israel hawakushtuka; wakati huo, Israel alikuwa rafiki wa karibu wa Iran. Mwaka 1977, jenerali Ezer Weizman, waziri wa ulinzi wa Israel, alimkaribisha jenerali Hasan Toufanian, aliyekuwa akisimamia zoezi la kugeuza jeshi la Iran kuwa la kisasa, katika wizara ya ulinzi Tel Aviv- kama marafiki, Israeli ilikua ikiwapatia Iran vifaa vya kijeshi vya kisasa.

Kutokana na agenda zilizorekodiwa za mazungumzo yao ya siri, Weizman alitoa ofa ya kuwapatia Iran mfumo wa kisasa zaidi wa kurusha makombora ardhini kwenda ardhini (Surface- to - surface missiles), wakati huohuo katibu mkuu wa wizara ya ulinzi, Dr. Pinhas Zusman, akimhamasisha Toufanian kwa kusema, mfumo wa makombora wa Israel unaweza kufanyiwa marekebisho kidogo ukabeba bomu la nyuklia.

Ila kabla hawa maafisa hawajafanyia kazi mipangilio yao, mapinduzi ya Iran yakabadili mahusiano ya Israel na Iran. Serikali ya Kiislam ya mapinduzi iliwaua wafuasi wa Shah na kubadili mahusiano na Israel. Shah aliyekuwa mgonjwa kipindi hicho alitoroka nchi yake na nchi ikawa chini ya Ayatollah Khomeini na Mullah waliokua watiifu kwake.

Itaendelea....
Siti ya mbele mkuu

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Tuendelee...

MAZISHI NDANI YA TEHRAN

Sehemu ya nane.

Mwaka 2008 na 2010, gazeti la New York Times liliripoti kuwa 'Tinners', familia ya uswisi ya mainjinia, ilisaidia CIA kuweka hadharani programu ya nyuklia ya Libya na Iran na walilipwa dolla millioni kumi na CIA ($10 million). CIA pia ilisaidia kuwalinda dhidi ya mashtaka ambayo wangeweza kufunguliwa na mamlaka za Uswisi kwa kutorosha vifaa vya ki-nyuklia. Baba yao, Frederic Tinner, na wanawe wawili, Urs na Marco, waliiuzia Iran vifaa feki katika ufungaji wa umeme kuelekea kituo cha Natanz, vilivyowezesha kuharibu vizungushi vya kasi hamsini (50 centrifuges). Kina- Tinner walinunua pampu za presha kutoka, Pfeiffer Vacuum Company, ya Ujerumani? Na wakazifanyia mizengwe huko New Mexico na kisha kuziuza kwa Iran.

Gazeti la Time lilieleza kuwa, Mossad ilihusika katika utekaji wa meli kwenye bahari ya Arctic, ambayo ilisafiri kutoka Finland kwenda Aljeria na mabaharia wa Urusi huku ikipeperusha bendera ya Maltese, ikibeba 'mzigo wa kuni'. Julai 24, 2009, siku mbili baada ya kuanza safari, chombo kilitekwa na watekaji nane. Ilichukua mwezi mzima kwa Urusi kusema kuwa kikosi cha makomandoo wa Urusi kimeikomboa meli hiyo.
Gazeti la Times la London na Daily Telegraph vilidokeza kuwa Mossad ndio waliopiga kengele ya hatari. Watu wa Dagan, walisemekana, waliitaarifu Urusi kuwa meli ilikuwa imebeba mzigo wa Uranium, uliouzwa kwa Iran na afisa wa zamani wa Urusi.Ila admirali Kouts, aloyeongoza mapambano dhidi ya maharamia katika umoja wa Ulaya alitoa mtazamo wa peke yake kwa gazeti la Times. Maelezo pekee yaliyonyooka, alisema, ni kiwa meli ilitekwa na Mossad ili kuzuia Uranium kufika Iran.

Ila pamoja na haya mashambulizi yaliyoendelea, Wa-Iran hawakukaa tu bila kufanya kitu. Kati ya 2005 na 2008, kwa usiri mkubwa,walijenga kituo kipya karibu na Qom. Walipanga kuweka vizungushi vya kasi elfu tatu (3000) kwenye kumbi mpya chini ya ardhi.

Hatahivyo, katikati ya 2009, Iran ilitambua yakua, taasisi za ujasusi za Marekani, Uingereza na Israel walikuwa na taarifa zote kuhusu kituo cha Qom.Iran ikachukua hatua mara moja. Septemba 2009, Tehran ilishangaza dunia kwa kuwahi kuwataarifu waangalizi wa kimataifa wa masuala ya atom (IAEA) juu ya uwepo wa kituo cha Qom.

Baadhi ya vyanzo vya taarifa vilieleza kuwa Iran ilimdaka mpelelezi kutoka magharibi ( ilidokezwa huenda ni mpelelezi wa MI6 ya Uingereza), ambaye alikwishakusanya taarifa za muhimu na za kuaminika juu ya Qom; hivyo waliweka wazi uwepo wa kituo hicho ili kupunguza aibu.

Mwenzi mmoja baadae, mkurugenzi wa CIA, Leon Panetta aliliambia gazeti la Times kuwa taasisi yake ilifahamu juu ya Qom kwa miaka mitatu na Israel ilihusika katika kuigundua. Ugunduzi wa Qom ulionyesha kwa mbali ushirikiano uliotengenezwa kati ya taasisi tatu zilizohusika na mapambano dhidi ya Iran: CIA, MI6, na Mossad.
Kutoka kwenye vyanzo vya taarifa vya Ufaransa, taasisi hizo tatu zilifanya kazi pamoja, ambapo Mossad ilikuwa ikitekeleza operesheni ndani ya Iran, CIA na MI6 wakiwasaidia waisraeli.

Itaendelea.....
Noma

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Tuendelee...

UNYONGAJI NDANI YA BAGHDAD

Sehemu ya nane.

...akinuka harufu ya pombe, alianguka kwenye siti ya nyuma na kuvunga kusinzia. Dereva akamsaidia kumtoa kwenye gari katika mtaa mmoja nyuma ya uwanja wa ndege na akaondoka. Alipoona kuwa yuko mwenyewe, Ben - Porat akakimbilia uzio wa kutokea - alijua kwa hakika sehemu ulipokatwa - na akapenya ndani. Kwenye njia ya kurukia, kuna ndege iliyokwisha jaza abiria wanaoondoka Iraq na mdogomdogo ilianza kushika njia. Mara rubani akaelekeza mwanga mkali kwenye mnara wa kudhibiti hapo uwanjani, na kwa muda kuwatia upofu wadhibiti kwenye huo mnara. Ndege ikaongeza kasi na mlango wa nyuma ukafunguka.Ikiwa urefu wa futi kumi kutoka usawa wa ardhi, kamba ikarushwa kutoka kwenye ndege. Akitokea gizani, Ben - Porat aliikimbilia ndege na kukamata kamba, kisha akavutwa kuingia ndani ya ndege na mara ndege ikapaa. Hakuna muongoza ndege waliobaki uwanjani, wala abiria aliyetambua hili tukio, lililoonekana kuchukuliwa katika filamu ya mapambano.
Wakati ndege ilipokuwa inaruka juu ya jiji, ilizima na kuwasha taa zake mara tatu. "Mungu asifiwe," walitamka watu wachache waliokuwa juu ya paa la nyumba. Rafiki yao alikuwa salama kuelekea nyumbani.

Masaa machache baadae, Haviv, kweli kwa sasa, alikuwa ndani ya Tel Aviv. Akamuoa mpenzi wake, na kwa miaka iliyofuatia akajiunga na siasa, akawa mbunge, waziri, na leo ni kiongizi anayeheshimiwa sana wa wayahudi wa Iraq ndani ya Israel. Wale walioachwa nyuma hawakuwa na bahati sana, wayahudi kwa makundi walikamatwa, walioigwa na kuteswa. Taggar na wengine ishirini na moja walishtakiwa kwa kudharau mamlaka.

Wayahudi wawili maarufu wa Baghdad, Shalom Salach na Joseph Batzri, walituhumiwa kwa kumiliki vilipuzi na silaha na hivyo kuhukumiwa kifo. Muda kidogo kabla ya kesi yake, Taggar aliamshwa usiku wa manane, sero yake ikiwa imejaa maaskari. "Unaenda kunyongwa usiku wa leo", kiongozi wa upelelezi akasema. "Ila hamuwezi kumnyonga mtu bila kesi yake kusikilizwa!" Alisema Taggar. "Hatuwezi? tunajua yote kuhusu wewe tayari, wewe ni afisa wa Israel, wewe ni mpelelezi - hatuhitaji kitu kingine cha ziada".
Mwalimu wa sheria mwenye ndevu nyingi akaingia na kukaa kando ya Taggar, akimsomea zaburi.

Saa tatu na nusu asubuhi, kuna afisa akampeleka Taggar sehemu ya kunyongea. Alitembeya katikati yao akiwa amepagawa. Ni wiki chache tu nyuma alikuwa akitembelea familia yake Jerusalem, na katika safari yake kuja Baghdad alifurahia starehe za Paris na Roma. Na sasa anaenda kuning'inia katika mwisho wa kamba.

Wairaq wakamlazimisha aweke sahihi kwenye fomu kadhaa - urasimu kazini, hata katika wakati huo - na kisha mnyong'waji akatoa pete na saa yake. Taggar akawaomba mwili wake upelekwe Israel. Mnyongaji akamsimamisha juu ya mtego na kumfunga mifuko ya mchanga miguuni. Akalazimishwa ampe mgongo mnyongaji 'asimuangalie', ambaye....

Itaendelea...

Wekeni MB
 
Back
Top Bottom