Tuendelee...
UNYONGAJI NDANI YA BAGHDAD
Sehemu ya tisa.
....aliweka kitanzi kwenye shingo yake na kukamata mshikio wa kudhibiti mtego. Taggar alikataa mfuko mweusi waliojaribu kumvalisha kichwani. Mnyongaji sasa akamtazama afisa anayetoa amri, akiwa amesimama na wengine wachache mbele ya mtu anayeenda kufa.
Taggar aliwaza juu ya familia yake, juu ya nyumbani kwake Jerusalem, na juu ya maisha ambayo angeweza kuwa nayo kama asingechagua hii njia. Hivi, shingo yangu itavunjika? Alitafakari, na kuhisi hofu kuu ikimtafuna.
Na mara, ghafla, maafisa wakaondoka. Taggar akatolewa kwenye mlango wa mtego. Yule mnyongaji akaondoa mifuko ya mchanga kwenye miguu na kitanzi kwenye shingo yake, akilalamika kuwa amekosa malipo yake kwa siku hiyo. Taggar akagundua, kwa mshangao, kuwa hangekufa siku hiyo! Kila kitu, kwa mpangilio wote kilikuwa mtego. Walidhani wangemfanya akiri na kutoa taarifa zaidi juu wa watu alioshirikiana nao. Ila kwa sasa, akijikongoja kurudi kwenye sero yake, akiwa hai, Taggar alikuwa na hakika kuwa asingeweza kufa ndani ya jela ya Iraq. Rafiki zake wangemtoa ije mvua, lije jua.
Wakati kesi ilipoisha, alihukumiwa kifo, ila,mara, hukumu yake ikabadilishwa na kuwa atumikie maisha yote jela. Batzri na Salach walinyongwa. Walitumia siku yao ya mwisho na Taggar, aliyejaribu kuwafanya wawe wenye furaha.
Kisha ikaanza "Yudke - Mungu asifiwe" kama njia ya Yesu kule Jerusalem kuelekea msalabani, ila alifanikiwa kushinda. Katika kampuni ya wauaji, wafungwa wa kisiasa, na mabwana jela wenye roho mbaya katika jela kadhaa ndani ya Iraq, ila Taggar aliamini asingeweza kufa mateka. Siku moja atakuwa huru!
Alikua amesubiri kwa miaka tisa. Mwaka 1958, jenerali Abdul Karim Kassem alikamata madaraka kwa mapinduzi na kumuua waziri mkuu wa Iraq na familia yake yote. Miaka miwili baadae, wasaidizi wake wa karibu wakatengeneza mkakati wa kumuua ( ambao walikuja kufanikiwa miaka michache mbele). Mosad wakapata hizo habaro, na kiongozi wa Mossad mara moja akatengeneza mawasiliano na watu waaminifu wa Kassem, na kukubaliana dili : Angewapatia majina ya wasaliti waliopanga kumuua Kassem - kwa kubadilishana na uhuru wa Yehuda Taggar.
Taggar alikuwa kwenye sero yake iliyochoka na yenye giza, wakati mabwana jela walipomfuata na nguo za Khaki. "Vaa hizi" walimuamuru. "Unaenda Baghdad".
Gari ya Polisi ilimpeleka Taggar mpaka kwenye jengo la ikulu. Wanajeshi kadhaa wakamsindikiza mpaka kwenye ofisi kubwa. Nyuma ya dawati la thamani alikaa mtu aliyemfahamu - rais Kassem mwenyewe. Taggar aligundua mara: anaachwa kuwa huru! Kassem akatumia muda kidogo kumtizama huyu muisrael.
"Niambie", kisha akasema,"kama vita ikitangazwa kati ya Iraq na Israel, utapigana dhidi yetu?"
"Nitakaporudi nchini kwangu", Taggar akajibu, "Nitajitahidi nitakavyoweza kuleta uelewa na amani kati ya Israel na mataifa ya kiarabu. Ila kama vita itatokea, nitapigania Israel, kama ambavyo wewe umepigana mara nyingi kwa nchi yako".
Itaendelea...