Misheni kubwa za taasisi ya upelelezi MOSSAD!

Misheni kubwa za taasisi ya upelelezi MOSSAD!

Tuendelee....

MAZISHI NDANI YA TEHRAN

Sehemu ya kumi na moja.

...mashinikizo ya kidiplomasia, vikwazo vilivyowekwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa; mbinu za kukwamisha kasi - kuwazuia wairan kupata malighafi zilizohitajika kutengeneza bomu; vita vya kiuchumi - Kukataza mabenki katika nchi zinazoendeshwa kidemokrasia kufanya biashara na Iran; Kuchochea mabadiliko ya kiutawala, Kwa kutoa misaada na kuimarisha vurugu za kisiasa na kuchochea mipasuko ya kikabila ndani ya Iran, ambapo wakurd, waazeri, wabeloshi, waarabu na wa-Turkmen walichangia asilimia hamsini (50%) ya idadi yote ya watu; na zaidi sana, hatua za siri, operesheni maalum na za 'giza' dhidi ya mradi wa Iran.

Ila pamoja na ubora wao wote, hawakuweza kuusimamisha mradi moja kwa moja, hata pamoja na ushirikiano wao wote."Dagan ndiye 'James Bond' wa ukweli",mchambuzi wa hadhi ya juu wa Israel alisema, ila kwenye huu mradi, hata James Bond hakuweza kuiokoa dunia. Alifanikiwa tu kuwapunguza kasi wairan. Ni au maamuzi ya serikali ya Iran au shambulio kubwa kutoka nje ya Iran, ambavyo vingeweza kabisa kusitisha ndoto ya Iran ya kuwa taifa lenye nguvu ya nyuklia mahali ambapo, kabla, ilisimama Hima ya Persia.

Hata hivyo, wakati Dagan anachaguliwa kuwa kiongozi wa Mossad (ramsad - kifupi cha rosh hamossad), wataalam walibashiri kuwa Iran itafikia uwezo wa kinyuklia mwaka 2005; tarehe hii ilisogezwa mpaka 2007, baadae 2009, kisha 2011. Na Dagan aliposimama kazi, Januari 6,2011, alikuwa na ujumbe kwa nchi yake: Mradi wa Iran umecheleweshwa angalau mpaka mwaka 2015. Hivyo alishauri muendelezo wa matendo yaleyale, yaliyofanikiwa sana kwa miaka nane iliyopita, na kuachana na shambulio lolote la kijeshi dhidi ya Iran. Ni pale tu makali ya kisu yatakapoanza kutukata, hapo ndipo tutashambulia; makali hayo yamebakiza miaka minne kuanza kutukata.

Dagan alihudumu kama kiongozi wa Mossad (ramsad) kwa miaka nane na nusu - miaka mingi zaidi kuzidi viongozi wengi wa Mossad. Aliachia kiti kwa Tamir Pardo, afsa mkongwe wa Mossad aliyeanza kazi za operesheni kama msaidizi wa karibu wa Yoni Netanyahu, shujaa wa uvamizi wa 1976 wa Israel kule Entebbe, na baadae akajitanabaisha kama jasusi mwenye uthubutu mkubwa, mtaalam wa tekinolojia mpya, na mpanga mikakati mbunifu kwenye operesheni zisizo za kawaida.

Wakati wa kumkabidhi Pardo tochi, Dagan aliongelea mazingira magumu ya upweke ya majasusi wa Mossad wanaofanya operesheni katika nchi maadui, wakati hawana mtu wa kumgeukia, hawana mtu wa kuwaokoa inapohitajika. Kwa unyenyekevu alikubali baadhi ya madhaifu yake; kubwa zaidi ikiwa kushindwa kufahamu sehemu ambayo Hamas walimficha mwanajeshi wa Israel, Gilad Shalit, aliyetekwa miaka mitano iliyopita. Ila hata pamoja na madhaifu hayo, mafanikio ya Dagan yalimheshimisha kama kiongozi bora zaidi wa Mossad kuwahi kutokea.

Waziri mkuu, Benjamin Netanyahu alimshukuru "kwa niaba ya waisraeli wote" na kumkumbatia kwa upendo. Katika tukio la ghafla na lisilotegemewa, baraza la mawaziri lilisimama na kumpigia makofi kiongozi huyu wa Mossad aliyekuwa na miaka sitini na tano (65). George W. Bush alimsalimu katika barua binafsi.
Ila sifa za kipekee kabisa kwa Dagan zilitolewa mwaka mmoja kabla, kutoka kwenye chanzo cha habari cha nje, gazeti la kila siku huko Misri, Al- Ahram, lililofahamika kwa uadui na upingaji mkali wa Israel.
Januari 16, 2010, lilichapisha makala iliyoandikwa na mwandishi aliyefahamika vizuri, Ashraf Abu Al- Haul. "Bila Dagan," Al- Haul aliandika,"mradi wa nyuklia wa Iran ungekuwa umekamilika miaka mingi iliyopita.... wairan wanajua ni nani aliyehusika na mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia Masud Ali Mohammadi. Kila kiongozi wa ngazi za juu Iran anajua kuwa neno la msingi ni 'Dagan'.

Ni watu wachache wanaolifahamu jina la mkurugenzi wa Mossad. Anafanya kazi kimyakimya, mbali kabisa na vyombo vya habari. Ila kwa miaka saba iliyopita ametoa mapigo yenye maumivu makali kwa mradi wa nyuklia wa Iran na kuzuia muendelezo wake.
"Mossad inahusika na operesheni kadhaa zilizohitaji uthubutu wa hali ya juu Mashariki ya jati," Al - Haul aliongeza, na kutaja baadhi ya mafanikio ya Dagan dhidi ya Syria, Hizbollah, Hamas, na Islamic Jihad.. (tutaona katika sura ya 18 -20).
"Yote haya," alimalizia," Yamemfanya Dagan kuwa mtu wa kutukuka sana ndani ya taifa la Israel."
Hakukuwa na watu wa kutukuka sana ndani ya shirika la kijasusi la Israel wakati linazaliwa May 1948, ukiacha wakongwe wachache wa 'Shai', waliokua wamepata uzoefu katika operesheni za siri na za kuhujumu kutoka kwenye shirika la kijasusi la Haganah, shirika la jeahi la siri la jamii ya kiisraeli ndani ya Palestina.

Na katika miaka yao ya mwanzo, hawa wapiganaji wa viwango vya kawaida ila waliojituma, wa taasisi changa ya usalama ya kijeshi, walitingishwa na fujo, misuguano ya ndani, ukatili na mauaji ya, iliyokuja kujulikana kama "jambo la Be'eri".

Mwisho wa sura ya pili.. ila ni mwanzo wa sura ya tatu - UNYONGAJI NDANI YA BAGHDAD.

Hivyo usiende mbali...
Tutaendelea...
 
Wadau mimi naendelea kushusha mzigo kama mnavyoona, hivyo kama ikikupendeza, unanirushia buku ya MB na mimi naendelea kutiririka..
Unaweza kurusha kwa namba 0759-84-16-85. Jina ni hilihili nalotumia..

Note: ni hiyari kuchangia MB, hamna lazima na sio kigezo cha mimi kutiririka au kutotiririka.
 
Wadau mimi naendelea kushusha mzigo kama mnavyoona, hivyo kama ikikupendeza, unanirushia buku ya MB na mimi naendelea kutiririka..
Unaweza kurusha kwa namba 0759-84-16-85. Jina ni hilihili nalotumia..

Note: ni hiyari kuchangia MB, hamna lazima na sio kigezo cha mimi kutiririka au kutotiririka.
Naipenda sana Mossad. Iko biyee ase
 
3. UNYONGAJI NDANI YA BAGHDAD.

Sehemu ya Kwanza.

Isser Be'eri, aliyejulikana pia kama 'Bigi'- "Big Isser", alikua mtu mrefu, mwenye muonekano wa mshiriki wa magenge ya kihalifu, na aliyekuwa na nywele zenye mvi za mbalimbali. Nyusi zake nyingi na ndefu zilifunika kidogo macho yake meusi yaliyoingia ndani na mara nyingi akiwa na tabasamu la sardoni juu ya mdomo wake.

Alizaliwa huko Poland, alikuwa ni mtu wa kiasi mwenye uadilifu usio na mashaka; ila washindani wake walimuelezea kama mtu hatari na mkali aliyependa madaraka.
Akiwa mwanachama wa muda mrefu wa Haganah, Big Isser alikuwa mkurugenzi wa kampuni binafsi ya ujenzi huko Haifa. Alikuwa ni mtu mpweke, mkimya na asiyechangamana na watu, akiishi na mke na mtoto wao wa kiume katika nyumba ndogo iliyokuwa eneo lenye upepo mkali katika kijiji kilochokua pwani, cha BatGalim.

Miaka michache kabla ya kuundwa kwa taifa la Israel, Be'eri alikua amechaguliwa na makamanda wa Haganah kuongoza taasisi ya Shai. Wakati uhuru ulipotangazwa, May 14, 1948, Israel ilishambuliwa kutoka kila upande na majirani zake, na Be'eri ndio aliyekuwa kiongozi wa taasisi mpya ya kijasusi ya jeshi. Be'eri alijihusisha na mrengo wa kushoto wa harakati za wafanyakazi na mahusiano mazuri na wanasiasa. Marafiki zake na watu wake wa karibu walisifu jinsi alivyojitolea kwa ulinzi wa Israel.

Vita ya uhuru iliendelea mpaka April 1949. Ila, mara tu baada ya Be'eri kuwa kiongozi wa taasisi hiyo ya kijasusi, matukio ya ajabu, ya umwagaji wa damu - yaliyoonekana kutohusiana - yalianza kutokea.

Baadhi ya wapandamilima walifanya ugunduzi wa kushtusha juu ya mlima Carmel. Katika maporomoko marefu chini ya mlima, waliona mwili wa mtu ulioungua nusu huku ukiwa umeshona marisasi kibao. Ulikuja kutambuliwa kama mwili wa mwarabu aliyefahamika vizuri, aliyekuwa shushushu wa Shai kwa jina la Ali Kassem.
Wauaji wake walimpiga risasi kisha wakajaribu kuuchoma mwili wake.

Wiki kadhaa baadae, katika kikao cha siri na waziri mkuu Ben-Gurion, Big Isser alimtuhumu Abba Hushi, kiongozi mwenye ushawishi ndani ya Mapai - chama cha siasa cha Ben - Gurion - kwa kuwa msaliti na shushushu wa Uingereza.
Ben-Gurion alipigwa na mshangao.

Uingereza ilikuwa taifa tawala la Palestina kabla ya kuanzishwa kwa taifa la Israel; Haganah ilikuwa ikiendesha mapambano ya chini kwa chini kinyume na mipaka yake ndani ya jamii ya wayahudi. Taasisi ya ujasusi ya Uingereza ilijaribu mara kadhaa kuchomeka mashushushu wake ndani ya uongozi wa wayahudi. Ila Abba Hushi, moja ya nguzo katika jamii ya wayahudi na kiongozi mwenye upendo na watu - awe msaliti?
Ilionekana haiwezekani. Mwanzoni, viongozi wa Israel waliokuwa wakifahamu hizi tuhuma za Be'eri walizitupilia mbali. Ila Be'eri alifanikiwa kupata telegramu mbili za siri zilizotumwa na...

Itaendelea...
 
1.MFALME WA VIVULI

Sehemu ya kwanza

Wakuu naomba niwatafsirie kitabu kilichoandikwa na Michael Bar-Zohar na Nissim Mishal 'The greatest mission of the Israel secret service Mossad'.

Natafsiri kitabu hiki kama shukrani kidogo kwa makala nyingi nilizosoma hapa kwenye jamii intelligence... watu wametumia muda wao na vipaji vyao kunipa taarifa na kupanua uwezo wangu wakuona mambo hivyo sioni vibaya kama nami nikijita kuandika kidogo...

Story zinazoelezwa katika kitabu hiki ni za kweli kabisa na hata rais wa Israel - Shimon Peres alisema, 'ni mambo ambayo ulimwengu ulipaswa kuwa umeyajua kwa muda mrefu'.

Moja kwa moja nitaanza na sura ya kwanza- King of the shadows au mfalme wa vivuli kwa kiswahili...

Ilikua ni mwishoni mwa majira ya joto, mwaka 1971, mawimbi makali yakipiga katika ufukwe wa Mediterranean na mawimbi makali zaidi yakionekana kuushinda ufukwe wa Gaza. Kwa busara kabisa wavuvi wadogowadogo wa Kiarabu walikaa mbali na fukwe; hii haikuwa siku nzuri ya kushindana na bahari iliyoonyesha kuchanganyikiwa.

Walitazama kwa mshangao wakati boti moja ilipojitokeza katika mawimbi yaliyokua yakinguruma ilipotua kwanguvu katika mchanga ulioloana maji ufukweni. Wapalestina wachache, nguo zao na shungi zao zikiwa zimeloana maji, waliruka kutoka kwenye boti na kukimbilia ufukweni. Sura zao zilizokua hazijanyolewa ndevu zilionyesha uchovu wa safari ndefu baharini, ila hawakua na muda wa kupumzika, walikua wakikimbia kuokoa maisha yao.

Kutoka kwenye bahari iliyokasirika, boti ya kivita ya Israeli ilitokea, ikiwakimbiza kwa speed kali ikiwa na wanajeshi waliovalia kivita. Iliposogelea ufukwe, wale wanajeshi waliruka kwenye maji madogo na kuanza kumimina risasi kwa uelekeo wa wale wapalestina waliokua wanakimbia. Vijana kadhaa wa Gaza waliokua wakicheza kwenye ufukwe waliwakimbilia wale wapalestina na kuwaelekeza sehemu salama kwenye shamba la matunda; wanajeshi wa kiisrael wakapoteza uelekeo wa wale wapalestina ila wakaendelea kuwatafuta ufukweni.

Baadae kabisa usiku huo kijana wa kipalestina aliyebeba bunduki ya Kalashnikov aliingia kwenye shamba la matunda kuchunguza.
Akawakuta wale wapalestina wamejikusanya pamoja kwenye moja ya kona za shamba."Nyie ni akina nani, ndugu?". Aliuliza.
"Sisi ni wanachama wa chama cha ukombozi wa wapalestina- PFLP" likawa jibu."Kutoka katika kambi ya wakimbizi ya Tyre, Lebanon." "Marhaba, karibuni," yule kijana akasema. "Mnamjua Abu-Seif, kamanda wetu? Alitutuma tukutane na kamanda wenu Beth Lahia (kambi kuu ya magaidi kusini mwa ukanda wa gaza).Tuna hela na silaha, na tunataka kuunganisha oparesheni zetu.”"Nitawasaidia kwa hilo", yule kijana akasema.

Asubuhi iliyofuata, magaidi kadhaa wenye silaha wakawasindikiza wageni kwenye nyumba iliyojitenga pembezoni ndani ya kambi ya wakimbizi ya Jabalia. Wakaongozwa katika chumba kikubwa na wakakaribishwa kukaa mezani. Muda kidogo baadae, kamanda wa popular front waliyetegemea kukutana nae akaingia. Wakabadilishana salamu za upendo na ndugu zao wa Lebanoni, na wakakaa kwa kwa kuangaliana.

"Tunaweza kuanza?" Aliuliza kijana mwenye mwili uliojengeka aliyevalia ushungi mwekundu, ambaye alionekana kuwa kiongozi wa lile kundi la walebanoni.
"Kila mtu yupo?"
"Watu wote wapo!". Yule mlebanoni akanyanyua mkono wake kuangalia saa. Hii ilikua ishara waliyokubaliana kabla. Ghafla, 'wale wageni wa Kilebanoni' wakatoa bastola zao na kuanza kumimina risasi. Ndani ya dakika moja, magaidi wa Beth Lahia walikua wamekufa.

'Walebanoni' wakakimbia kutoka kwenye nyumba, wakapita katika viunga vya kambi ya Jabalia na mitaa iliyojaa watu ya Gaza na muda mfupi wakawa ndani ya ardhi ya Israel. Jioni ile, kijana aliyekua na ushungi mwekundu, kapteni Meir Dagan, kamanda wa IDF (Israel Defense Forces) na kikundi cha siri cha makomando (Rimon Commando unit), Akaripoti kwa jenerali Ariel (Arik) Sharon kuwa operesheni 'kinyonga' imefanikiwa. Viongozi wote wa Popular Front Beth Lahia, kikundi hatari cha kigaidi, wameuawa.

Itaendelea....
Uzi umenyooka balaa
 
Ila watanzania ni wagumu hatari..
Zaidi ya watu elfu tatu wanafuatilia story ila hamna anayetaka kutoa buku ya MB..

Nimewanyooshea mikono..
Wadau tumen basi MB kijiwe kisije kutawanyika
 
Ila watanzania ni wagumu hatari..
Zaidi ya watu elfu tatu wanafuatilia story ila hamna anayetaka kutoa buku ya MB..

Nimewanyooshea mikono..
3,000 X 1,000 = 3,000,000/=
Bro ukipiga hesabu kama hiz ki bongo bongo biashara yako itakufa siku chache.
Ofcz watu watatuma tu wala usijal wewe endelea kushusha vitu
 
Vyuma mazee ...mtoa mada fanya kama unatoa SADAKA hazina utaikuta mbinguni..
 
Tuendelee...

UNYONGAJI NDANI YA BAGHDAD

Sehemu ya pili.

.... majasusi wa Uingereza kutokea ofisi za posta za Haifa May 1948. Akaziweka juu ya dawati la Ben- Gurion kama ushahidi usiopingika wa usaliti wa Hushi.
Wakati huohuo, Be'eri akaagiza kukamatwa kwa Jules Amster, rafiki wa Hushi. Be'eri aliagiza Amster apelekwe katika machimbo ya chumvi huko Atlit, nje ya Haifa, na akaamuru apigwe na kuteswa kwa siku sabini na sita (76), na akamlazimisha akubali kuwa Hushi alikuwa msaliti wa hovyo.
Amster alikataa kukubali, na mwishowe akaachiwa, akiwa amepigika kwelikweli.
Walimtoa meno yote, miguu yake ilijaa vidonda na makovu, na akawa akiwindwa na zimwi la uoga kwa miaka mingi.

June 30, 1948, akinunua bidhaa katika soko la Tel Aviv, Meir Tubiansky, kepteni wa jeshi, alikamatwa na kupelekwa Beth Giz, kijiji cha Kiarabu kilichokua kimetekwa siku za karibuni. Tubiansky alishukiwa na majasusi wa jeshi ya kuwa, wakati akiwa Jerusalem, alitoa siri muhimu za jeshi kwa raia wa Uingereza, ambaye naye alizigawa kwa shushushu wa jeshi la Jordan.
Kikosi cha makombora cha Jordani kwa msaada wa hizo taarifa, walishambulia vikali vituo kadhaa vya kimkakati kote ndani ya Jerusalem.
Kwenye kesi fupi ndani ya mahakama ya kijeshi iliyochukua chini ya lisaa limoja, Tubiansky alishtakiwa kwa kuwa mpelelezi wa waarabu, akakutwa na hatia na kuhukumiwa kifo. Kikosi cha walenga shabaha kilichokusanywa kwa haraka kikamuua mbele ya wanajeshi wa Israel waliobaki na bumbuwazi. (Tubiansky anakuja kuwa mtu pekee aliyeuawa kwa amri ya mahakama ndani ya Israel ukimuacha Adolf Eichmann.)

Uchunguzi katika kifo na mateso vilipelekea wapelelezi kwa muhusika : Big Isser. Alimshuku Ali Kassem kwa kuwa jasusi wa pande mbili (double agent) na akaamuru mauaji yake. Kisha akamtegea msala Abba Hushi. Kulingana na wapelelezi kadhaa, Big Isser alikuwa na ugomvi binafsi na Hushi. Anaweza kuwa alifanikiwa katika kudanganya ndani ya kazi yake katika taasisi, ila akitafunwa na roho ya dhulma, aliungama kwa wakubwa zake kwamba alitengeneza telegram zilizomtia hatiani Abba Hushi, kwa kufuata amri ya moja kwa moja kutoka kwa Be'eri. Na Be'eri ndiye aliyekuwa ametoa amri za kukamatwa na kuuawa kwa haraka kwa kepteni Tubiansky.

Waziri mkuu Ben- Gurion alichukua hatua za haraka. Be'eri alipelekwa mbele ya mahakama ya kijeshi, halafu kwenye mahakama ya kiraia, akanyang'anywa vyeo vyake, na akafukuzwa bila heshima katika jeshi la Israel (IDF) na akakutwa na hatia katika vifo vya Ali Kassem na Meir Tubiansky.
Viongozi wa Israel walipigwa na mshtuko mkuu.Mbinu za Be'eri zilionekana kuchukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye shirika lisilokuwa na maadili mazuri la Urusi (KGB); muonekano wake uliotisha, amri zake za kutengenezea watu tuhuma, na mauaji vilitia doa kubwa katika maadili na kanuni za kibinadamu kwa ambazo Israel ilijengwa.
Hili suala la Be'eri liliacha makovu yanayouma katika taasisi hii ya kijasusi na lilikuwa na mchango mkubwa katika mageuzi yake.

Kama, ni katika vita, viongozi wa kiraia walijaribu kufikiri , kwa kupinga matendo ya Be'eri, taasisi ya kijasusi ya Israel itakuwa imebadili kabisa sifa yake. Kama wangekaa kimya bila kuyakemea, taasisi hii ingeweza kuwa kama KGB ambako ku'mfremu' mtu, udanganyifu, mateso na mauaji zilikuwa kanuni za kila wakati. Ila kinyume chake kabisa, mbeleni hizi mbinu za Be'eri zilikuja kukatazwa
Taasisi hii ya kijasusi iliweka mipaka kwa matumizi ya nguvu na ikahakikisha operesheni zilizofuata zinakuwa kwenye misingi ya kisheria na ya kiutu ambayo itaweka msisitizo katika haki za watu. Kwa kuondolewa kwa Be'eri, mtu mwingine aliingia katikati ya dimba la ulimwengu wa vivuli wa Israel, kinyume kabisa cha Be'eri: Reuven Shiloah.


Itaendelea.....
 
Back
Top Bottom