Tuendelee...
"AHH, HIYO? HIYO NDIYO HOTUBA YA KHRUSHCHEV.."
Sehemu ya tatu.
.....kuwa amepasuapasua, bila uoga na bila huruma, hadithi ya imani ya Yosif Vissarionovich Stalin. Khrushchev aliweka wazi kwamba Stalin, katika miaka yake kwenye uongozi, alikuwa ametenda jinai za kinyama na kuamuru mauaji ya mamillioni ya watu. Aliikumbusha hadhira yake kwamba Lenin, baba wa mapinduzi ya Bolshevuk, alishakionya chama dhidi ya Stalin.
Khrushchev alilaani imani kwa nafsi ya mtu ambaye alisifiwa kama, " Jua la mataifa".Akaelezea juu ya uhamisho wa nguvu wa vikundi vya kikabila ndani ya umoja wa kisovieti, uliopelekea vifo visivyo na idadi; juu ya mauaji makubwa ya watu waliodhaniwa kupingana na uongozi wa Stalin (1936 - 1937), ambapo wajamaa millioni 1.5 walikamatwa na laki sita na themanini (680,000) kati yao kuuawa. Kati ya wajumbe 1,966 wa mkutano wa kumi na saba (17) wa chama, kwa amri ya Stalin wajumbe 846 waliuawa, vivyo hivyo pia wagombea 98 kati ya 138 wa ujumbe wa kamati kuu waliuawa.
Khrushchev pia aliongelea njama dhidi ya madaktari, tuhuma zilizopikwa dhidi ya madaktari wa kiyahudi ambao walituhumiwa kula njama ya kumuua Stalin na viongozi wengine wa Kisovieti.
Maneno ya Khrushchev yalimuanika Stalin kama muuaji wa halaiki ya watu, aliyewaua mamilioni ya warusi na watu wa mataifa mengine, wengi wao wakiwa wajamaa watiifu. Ndani ya masaa manne, masiha alikuwa amebadilishwa kuwa shetani.
Hotuba ya Khrushchev iliondoa imani ya uongo aliyokuwa amebakiwa nayo Victor juu ya ujamaa. Na akagundua kwamba, mikononi mwake amekamata bomu ambalo lingeweza kutikisa kambi ya kisovieti mpaka kwenye msingi wake. Aliamua kukirudisha hiki kipeperushi chekundu kwa Lucia. Ila njiani kuelekea kwa Lucia, akapata mawazo mengine, na miguu yake ikampeleka sehemu nyingine - kwenye ubalozi wa Israel.
Akatembea kwa kujiamini, na ukuta wa polisi wa Poland na mawakala wa kijasusi wakampisha na kumuacha apite. Dakika chache baadae, alikuwa ndani ya ofisi ya Yaacov Barmor, kiofisi ni katibu wa kwanza wa ubalozi, ila kiuhalisia, ni mjumbe wa Shabak huko Poland.
Grayevski akampatia kile kipeperushi chekundu. Yule muisrael akakipitia na akapigwa na mshangao. Unaweza kusubiri dakika moja, akauliza, akakichukua kile kipeperushi na kutoka hapo ofisini. Akarudi lisaa limoja baadae. Grayevski aligundua kuwa Barmor alikuwa ametoa nakala za kile kipeperushi, ila hakuuliza swali. Akakichukua, akakificha kwenye koti lake na kuondoka.
Alifika ofisini kwa Lucia kwa wakati, na Lucia akakiweka kwenye 'safe'. Hakuna aliyemsumbua au kumuuliza juu ya safari ya ghafla kwenye ubalozi wa Israel.
Siku ya Ijumaa, April 13, 1956, mapema mchana, Zelig Katz aliingia ofisini kwa mkurugenzi wa Shabak, Amos Manor. Katz alikuwa msaidizi binafsi wa Manor. Makao makuu ya Shabak yaliwekwa katika jengo la kiarabu la kizamani huko Jaffa, karibu na soka la kuvutia la flea. Manor akamuuliza Katz swali la kawaida la kila Ijumaa : "Kuna habari yeyote kutokea mashariki ya Ulaya?"
Ijumaa ndiyo siku ambayo, kontena la kidiplomasia lisilo na ukaguzi, lilileta taarifa kutoka kwa mawakala wa Shabak nyuma ya pazia la chuma.
Itaendelea...