Tuendelee....
MAZISHI NDANI YA TEHRAN
Sehemu ya tisa.
Mossad ilihusika na milipuko kadhaa ndani ya October 2010, ambapo wataalam 18 wa Iran waliuawa katika kituo kimoja kilichokua katika milima ya Zagros, kikiunganisha makombora aina ya Shehab.
Kwa msaada wa marifiki zake, Uingereza na Marekani, Mossad ilifanikiwa pia kuwaua wanasayansi watano waliojihusisha na nyuklia.
Urafiki huu uliimarishwa kiasi kikubwa kwa juhudi za Meir Dagan. Kuanzia siku amekuwa mkurugenzi wa Mossad, aliongeza presha kwa watu wake kujenga ushirikiano wa karibu na taasisi za nje za kijasusi.
Wasaidizi wake walimshauri kutoanika siri za Mossad kwa wageni, ila alipotezea huo ushauri."Achaneni na huo ujinga", alifoka,"na muende mkafanye nao kazi!"
Ukiacha Uingereza na Marekani, Dagan alikuwa na rafiki mwingine wa muhimu aliyeleta taarifa za thamani kubwa kutoka ndani ya Iran: Kiongozi wa upinzani Iran. Katika mkutano usiokua wa kawaida na vyombo vya habari uliofanyika nje ya Iran,Kiongozi wa baraza la upinzani la kitaifa alitaja jina la mwanasayansi kiongozi katika mradi wa Iran. Mpaka kufikia hapo, utambulisho wake ulikua umefanywa kuwa siri.
Mohsen Fakhri Zadeh, akiwa na miaka harobaini na tisa, alikuwa profesa wa Fizikia katika chuo kikuu cha Tehran. Alisemekana kuwa mtu wa ajabu na aloyeishi kwa kupoteapotea.
Upinzani uliweka hadharani taarifa nyingi kumhusu, ikiwa ni pamoja na uanachama wake kwenye jeshi la ulinzi wa mapinduzi kutokea umri wa miaka kumi na nane (18), anwani yake - mtaa wa ShahidMhallalti, Tehran, namba za paspoti ya kusafiria - 0009228 na 4229533, na hata namba yake ya simu ya nyumbani, 021 - 2448413.
Fakhri Zadeh alikuwa na taaluma iliyojikita katika mchakato wa kugeuza bomu la msingi kuwa na ujazo na uzito wa kutosha kuanzisha mnyororo wa matukio ambao unapelekea mlipuko wa nyuklia. Timu yake pia ilikuwa ikifanya kazi kupunguza ukubwa wa bomu, ili liweze kubebwa katika kichwa cha kombora la shehab.
Kufuatia ufahamu wa mambo haya, Zadeh alikataliwa kuingia Marekani na katika nchi za jumuiya ya Ulaya, na akaunti zake za benki katika nchi za magharibi zikazuiliwa.
Upinzani walieleza hatua kwa hatua matendo yake yote, wakaweka bayana majina ya wanasayansi wengine waliokua wakishirikiana naye na hata sehemu zilipo maabara zake za siri.
Huu wingi wa taarifa na namna zilivyotolewa, zinampelekea mtu yeyote kuamini kuwa, kwa mara nyingine, "taasisi fulani ya ujasusi" iliyowahi kushukiwa na mataifa ya magharibi kwa kuwa na ajenda yake peke yake ya siri, ilikusanya hizi taarifa kwa shida juu ya huyu mwanasayansi wa Iran na kuwapatia Wapinzani ndani ya Iran, ambao waliziwasilisha kwa mataifa ya magharibi.
Kumuweka 'uchi' kulikua na maana ya kumuonya kuwa anaweza kuwa "ndiye anayefuata katika mstari" wa kuuawa na kumchagiza kujificha au kuchagua suluhu bora zaidi: kukimbilia kwenye mataifa ya magharibi.
Jenerali AliReza Asgari, waziri wa ulinzi msaidizi aliyepita wa Iran, alipotea Februari 2007 akisafiri kwenda Istanbul. Alikuwa amehusika kwa undani sana kwenye mradi wa nyuklia. Majasusi wa Iran walimtafuta kila mahali, ulimwengu mzima, ila hawakuweza kumpata.
Kama miaka minne baadae, Januari 2011, waziri wa mambo ya nje wa Iran, AliAkbar Salehi, akamgeukia katibu mkuu wa umoja wa mataifa na kuituhumu Mossa kwa kumteka na kumfunga kwenye magereza ndani ya Israel. Ila kwa mujibu wa gazeti la Sunday Telegraph la London, Asgari alikuwa ameasi na kukimbilia magharibi; Mossad ilipangilia uasi huo na walihusika kumlinda akiwa Uturuki. Vyanzo vingine vilidai kua baadae alihojiwa na CIA na akawapatia taarifa muhimu sana juu ya programu ya nyuklia ya Iran.
Mwezi mmoja baada ya kupotea kwa Asgari - March 2007 - afisa mwingine wa ngazi za juu wa Iran naye alipotea. Amir Shirazi aliyetumikia katika kikosi cha "Al Quds", kikosi mahiri sana ndani ya jeshi la ulinzi wa mapinduzi, kilichojihusisha na operesheni za siri nje ya mipaka ya Iran.
Chanzo kimoja cha habari kutoka ndani ya Iran kililiambia gazeti la London Times kuwa, ukiacha kupotea kwa Asgari na Shirazi, afisa mwingine wa ngazi za juu pia alipotea: kamanda wa jeshi la ulinzi wa mapinduzi kwenye ghuba ya Persia, Mohammad Soltani.
Julai 2009, mwanasayansi wa nyuklia, Shahram Amiri alijiunga kwenye orodha ya wasaliti. Amiri aliyekuwa ameajiriwa Qom, alipotelea Saudi Arabia alipoenda kuhiji Mecca. Iran iliwataka wasaudia kuchunguza kilichompata Shahram. Amiri alijitokeza miezi michache baadae huko Marekani, akahojiwa vyakutosha, akapewa dolla millioni tano ($5 million), kitambulisho kipya, na makazi mapya huko Arizona.
Vyanzo vya CIA vilieleza kuwa Amiri alikuwa mtoa taarifa kwa miaka mingi kwa vyombo vya ujasusi vya magharibi na alikiwa akiwapatia taarifa 'halisi na iliyochakatwa vizuri'.
Amiri alieleza kuwa chuo cha Tecknolojia cha Malek - Ashtar, alipowahi kufundisha, kilikuwa tu kama geresha kwa kutoa elimi. Ila ukweli ni kuwa kilikuwa kituo cha utafiti wa kuunda vichwa vya kubebea mabomu yatakayorushwa na makombora ya masafa marefu ya Iran; Fakhri Zadeh alikuwa mkuu wa hicho chuo.
Itaendelea...
Usikae mbali.