Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,346
- 9,846
- Thread starter
- #21
Tuendelee....
MAZISHI NDANI YA TEHRAN
Sehemu ya pili.
Mauaji ya wanasayansi wa nyuklia wa Iran ilikuwa sehemu moja tu katika vita kubwa. Gazeti la 'Daily Telegraph' la London liliandika kuwa, Mossad chini ya Dagan ilipandikiza mshushushu waliowapa Iran taarifa za uongo zinazofanania na kweli ila kuchukua taarifa za kweli za Iran, ilitengeneza timu za wauaji, timu za kuharibu miundombinu inayohusiana na programu za nyuklia, ilisajili kampuni za uongo zilizoiuzia Iran vifaa feki na hivyo kudhoofisha sana nguvu za Iran kwa miaka na miaka ya operesheni za siri dhidi ya programu ya silaha za nyuklia za Iran.
Reva Bhalla, mkurugenzi wa uchambuzi taasisi ya Stratfor aliwahi kunukuliwa akisema: "Kwa ushirikiano na Marekani, operesheni za siri za Israel zilijikita kwenye kumaliza rasilimali watu waliojihusisha na programu ya nyuklia na kuhujumu utaratibu mzima wa Iran kupata malighafi". Mwanamama huyu alisema, Israel iliwahi kutumia mbinu hizohizo kwa Iraq miaka ya mwanzo ya themanini (80's), wakati Mossad ilipowaua wanasayansi watatu wa nyuklia wa Iraq hivyo kukwamisha kumalizika kwa kinu cha 'atom' cha Osiraq, karibu na Baghdad.
Katika vita hii dhidi ya programu ya nyuklia ya Iran, Mossad chini ya Dagan kwa ukamilifu kabisa ilikua inachelewesha utengenezaji wa bomu la nyuklia la Iran kwa muda mrefu itakavyowezekana, na hivyo kufurusha tishio la kuifuta Israel katika uso wa dunia kama ambavyo Ahmadinejad alivyokua akitishia.
Lakini hata hivyo haya mafanikio madogo hayawezi kulipia makosa makubwa zaidi yaliyofanywa na Mossad katika historia - kushindwa kugundua na kuanika mradi wa siri wa nyuklia wa Iran toka mwanzo wake.
Kwa miaka kadhaa sasa Iran imekua ikiimarisha uwezo wake kinyuklia - Na Israel haikuwa na habari.
Iran imewekeza kiasi kikubwa cha fedha, kufundisha wanasayansi, kujenga ngome za siri, kufanya majaribio ya kisasa yaliyofanikiwa- na Israel haikujua kitu. Kutokea wakati Iran chini ya Khomeini ilipoamua kuwa taifa lenye nguvu ya nyuklia, ilitumia udanganyifu, hila na mikakati iliofanya vyombo vya ujasusi vya magharibi na Israel kwa pamoja waonekane wapumbavu.
Shah Reza Pahlavi wa Iran, alianza kujenga kinu cha nyuklia, kwa matumizi ya amani na ya kivita. Mradi wa Shah ulianza miaka ya 1970 na Israel hawakushtuka; wakati huo, Israel alikuwa rafiki wa karibu wa Iran. Mwaka 1977, jenerali Ezer Weizman, waziri wa ulinzi wa Israel, alimkaribisha jenerali Hasan Toufanian, aliyekuwa akisimamia zoezi la kugeuza jeshi la Iran kuwa la kisasa, katika wizara ya ulinzi Tel Aviv- kama marafiki, Israeli ilikua ikiwapatia Iran vifaa vya kijeshi vya kisasa.
Kutokana na agenda zilizorekodiwa za mazungumzo yao ya siri, Weizman alitoa ofa ya kuwapatia Iran mfumo wa kisasa zaidi wa kurusha makombora ardhini kwenda ardhini (Surface- to - surface missiles), wakati huohuo katibu mkuu wa wizara ya ulinzi, Dr. Pinhas Zusman, akimhamasisha Toufanian kwa kusema, mfumo wa makombora wa Israel unaweza kufanyiwa marekebisho kidogo ukabeba bomu la nyuklia.
Ila kabla hawa maafisa hawajafanyia kazi mipangilio yao, mapinduzi ya Iran yakabadili mahusiano ya Israel na Iran. Serikali ya Kiislam ya mapinduzi iliwaua wafuasi wa Shah na kubadili mahusiano na Israel. Shah aliyekuwa mgonjwa kipindi hicho alitoroka nchi yake na nchi ikawa chini ya Ayatollah Khomeini na Mullah waliokua watiifu kwake.
Itaendelea....