Misheni kubwa za taasisi ya upelelezi MOSSAD!

Misheni kubwa za taasisi ya upelelezi MOSSAD!

hongera mkuu hakika uzi umetulia.
 
Tuendelee...

"AHH, HIYO? HIYO NDIYO HOTUBA YA KHRUSHCHEV.."

Sehemu ya nne.

Zelig alojibu kwa kutulia kuwa dakika chache zilizopita alipokea kutoka Warsaw "hotuba fulani ya Khrushchev huko kwenye kongamano..." Manor aliruka kitoka kwenye kiti chake. "Nini?" Aliunguruma. "Ilete mara moja!" Manor, kijana mzuri mrefu, alihamia Israel miaka michache tu iliyopita.

Alizaliwa akiitwa Arthur Mendelovitch huko Romania, kwenye familia inayojiweza, alipelekwa Auschwitz, ambako familia yake yote - wazazi, dada, na kaka zake wawili - waliuawa. Yeye alinusurika, akiwa na uzito usiofika pound themanini (80) wakati hiyo kambi ilipokombolewa. Aliporudi Bucharest, aliajiriwa na 'Aliya Beth', akisaidia kuingiza kinyemela, wakimbizi wa kiyahudi, Palestina iliyokuwa chini ya Uingereza. Alitumia jina la Amos la wakati wa vita, na majina mengine kadhaa kuficha mienendo yake. Wakati nafasi yake ilipofika kuhamia Israel, mwaka 1949, mamlaka ya Romania haikumruhusu kuondoka. Alifanikiwa kutoroka kwa kutumia pass ya kusafiria ya Czech ya kubumba, kwa jina la Otto Stanek. Marafiki zake walianza kumuita 'mtu mwenye majina elfu moja'; akiwa Israel, akabadili na kuitwa Amos Manor.

Alipanda ngazi haraka haraka katika taasisi ya usalama. Isser alivutiwa nae. Manor alikuwa kinyume chake. Isser mdogo, Manor bonge la mtu. Isser mbabe na mwenye kuongea kwa sauti ya chini ya kukwaruza, Amos mchangamfu na mwenye tabia tulivu. Isser hakucheza mchezo wowote, wakati Manor alikuwa muogeleaji, na alicheza mpira, tennis na volleyball. Isser aliongea kirusi na ki-yiddish, Manor aliongea lugha saba. Isser alikuwa mwanachama aliyejitoa wa chama cha wafanyakazi, Amos hakujali kuhusu siasa. Isser alivaa kawaida tu, Amos alipendelea fasheni, muonekano wa kiulaya.

Ila ukiacha hayo yote, Amos alikuwa na akili nyingi na mtu wa kutumainiwa. Isser alimsajili Shabak mwaka 1949; karibu miaka minne baadae, aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa Ben - Gurion kwa mapendekezo ya Isser. Alifanywa pia kuwa kiongozi wa mahusiano ya jamii ya kiintelijensia ya Israel na CIA.

Ijumaa hiyo iliyokuwa na mvua, Manor alijirusha kwenye rundo la nakala za karatasi. Hakuwa na tatizo la kuisoma - moja kati ya lugha zake saba ilikuwa ki-rusi. Akiwa anasoma kurasa, aligundua umuhimu mkubwa wa hotuba ya Khrushchev. Alirukia kwenye gari yake na kukimbilia kwenye nyumba ya Ben- Gurion.
"Lazima uisome hii", alimwambia waziri mkuu. Ben - Gurion aliejua ki-rusi, akaisoma hotuba. Asubuhi iliyofuata, siku ya Sabato, haraka akamwita Manor. "Hii ni nyaraka ya kihistoria", alisema, "na pamoja na mambo mengine, inashuhudia kwamba, mbeleni Urusi litakuwa taifa la kidemokrasia".
Isser aliipata hotuba April 15, na maramoja akaona inaweza kuwa bonanza kwa Israel. Ndani yake kulikuwa na namna ya kuboresha mahusiano kati ya Mossad na CIA, yaliyoanzishwa kwa mara ya kwanza 1947. Mwaka 1951, alipokuwa akitembelea Marekani, Ben -Gurion alimpigia jenerali Walter BedellSmith, ambaye walikutana Ulaya mwishoni mwa vita kuu ya pili ya dunia -WWII. Bedell Smith alikuwa mkurugenzi wa CIA ( na karibu....


Itaendelea....
 
Back
Top Bottom