kibavu
Senior Member
- Oct 15, 2008
- 136
- 82
Jamani kwa mliomaliza kidato cha sita kuanzia mwaka 2003 kurudi nyuma mtanielewa kirahisi katika hili.
Mnaweza kukumbuka jinsi ilivyokua shida kupata nafasi ya kusoma degree unapopata haya division two HASA KWA MASOMO YA ARTS, kwan wakati huo vyuo vilikua ni UDSM, MZUMBE, SUA, MUHIMBILI na UCLAS, ukiacha vyuo vya uhasibu na usimamizi wa fedha ambavyo vingi vilikua vinatoa diploma na advanced diploma. Hakukua na bodi ya mikopo kama sasa ukienda huko kwingine wajijua mwenyewe kwa kila kitu. Nina ushahidi wa rafiki zangu waliokosa nafasi mlimani kwa kuwa walikua na division 2.
Lakini leo hii kuna wanafunzi wapo TEKU wana principal 1 (moja tu) tena ambayo ni E! Je unaweza kwenda University of Dar es Salaam kwa principal moja? Hapo ndipo dharau kwa vyuo inapoanzia, i.e. aina ya wanafunzi wanaopelekwa huko. WANAJAMVI TUWE WAKWELI, NA TUWEKE UNAZI NA VYUO VYETU PEMBENI......Je huyu mwalimu aliyepata S.S.E kwenye mtihani wa kidato cha sita hata baada ya ku-reseat atakua na uwezo wa kuwapa watoto kile kinachostahili? Kuna watu wanasoma degree kwenye baadhi ya vyuo sasa hivi, wakati siku za nyuma hata nafasi ya kusoma diploma wangehaha kupata. Hapa ndipo unapokuja utata.
Jingine ni aina ya walimu, kabla ya TCU kuja na sera za kuweka kiwango cha GPA kwa walimu wa vyuo vikuu kuna vyuo vilikua vinaajiri watu wasio na sifa kuwa wahadhiri wa vyuo vikuu. Sasa mwalimu kilaza lazima azalishe mhitimu kilaza, na kama mwalimu wako ni kilaza. Unakuta mwanafunzi wa chuo kikuu hajawahi kufundishwa na mwalimu mwenye PhD au aliyefikia ngazi ya Profesa hata mmoja mpaka anamaliza chuo, sasa unategemea ataongea nini mbele ya mwenzake aliyefundishwa na maprofesa wenye machapisho ya kutosha?
Njooni mashuleni mtaona vituko kuna walimu wanakataliwa madarasani na wanafunzi tena kwenye shule za sekondari kisa wapo shalo....ni weupe! Pia, hawa vijana wakija field mashuleni hakika utaona tofauti miongoni mwao hata uwezo wa kujiamini na kujichanganya. Nadhani hata makazini huko kwenye sekta zingine pia unagundua tofauti baina ya hawa vijana kutokana na vyuo wanavyosoma.
LAKINI hii haimaanishi kwamba kila aliye TEKU au chuo kingine cha binafsi ni kilaza, LA HASHA. Kuna watu wanatoka kwenye hivyo vyuo na wako safi...na pia kuna walimu wa kutoka UDSM na campus zake ni vilaza wa kutosha tu.
HATA HIVYO tofauti ya vyuo haikwepeki bandugu, na ndio maana hata entry points zipo tofauti. Hii sio kwa bongo tu hata kwa wenzetu waliotutangulia prestigious colleges zipo. Huwezi kuwa kilaza ukaingia Yale, Harvard, Stanford au Columbia University kwa Marekani. Au ukawa mbugila mbugila halafu utegemee kuingia Oxford au Cambridge kwa UK...no way!